NENO LA KINYWA
Wako watu katika dunia
ya leo wamekuwa machizi, wamekosa mwelekeo,wanashindwa kuzaa,maisha hayasongi,
hawajielewi maisha yanavyokwenda zaidi ya kuona miaka inakatika tu! Lakini yote
haya yanaweza kusababishwa na NENO LA KINYWA.
Na ni ukweli
usiopingika kuwa wako watu wanafika mbali kutokana na neno linalotoka kinywani,
wanapokea uponyaji,wananawiri na
kushamiri kwasababu ya NENO LA KINYWA, na ukumbuke kuwa neno lenye misingi ya kweli uwa linadumu siku zote
ata kama mtamkaji wa hilo neno amesha fariki au hayupo tena lakini lile neno
linaweza kuishi na kumshikilia au kuwashikilia. Kwa kusema hivyo unaweza
ukamkimbia mtu na kuama sehemu nyingine lakini kamwe hauwezi kulikimbia neno
linatoka kinywani mwake.
Na ukumbuke kuwa neno
alikuachi kwasababu umeteseka sana au umelia sana bali linaondoka au kukuacha
kutokana na kubadilisha mfumo au mtu kuja kulitengua hilo neno alilolitamka.
Naweza kusema moja ya laana mbaya ni laana zinatokana na neno lenye uhalisi(sababu
za kweli) , mathalanii mtu anaweza kusema kwamba kama hauta mweshimu mzazi wako
basi hautatoka katika maisha haya mabovu unayoishi sasa na kweli iwe
ujamuheshimu mzazi wako basi laaana hiyo itakuwa maisha yako.
Ujenzi wa maisha ya
rohoni katika upande wa GIZA na NURU uwa yanajengwa au kuumbwa kupitia neno la
kinywa cha mtu husika au kunenewa na mtu ambaye moyo wake umemlizia au
haujamlizia, na mwisho hayo maneno tutayaona ya kidhihirika katika ulimwengu wa
mwili.
Ni kweli neno la kinywa
chako linakuwa na nguvu sawasawa na hadhina iliyoko ndani yako lakini sio
tofauti na kile kilichomo ndani yako, japo kuna vitu viwili kuna kuwa na
hadhina katika moyo wako na kuliamini lile neno unalolitumia kuwa lina nguvu na
linaweza kufanya kazi.
Kinywa chako lazima
kiwe ni kisima kinachotoa maji matamu ambayo mtu akiyanywa atataka kunywa hayo
maji na pindi atakapo kunywa hayo maji basi yatajenga afya katika maisha yake
na sio kumdhuru katika afya yake, japo watu wengi tumekuwa tukishindwa
kujitambua kwamba kwa uhakika sisi ni watu tulibeba aina gani ya maji kutokana
na mchanganyo wa maji matamu na machungu.
Uwezi kuwa katikati
alafu ukawa na nguvu kubwa lakini pindi utakapo kuwa katika upande mmoja
unaoeleweka ndio nguvu itakuwa ya uhakika maana Mungu katika neno lake anasema
ukiwa vugu vugu nitakutapika kwakua kila upande unagharama zake na una mambo
yake hivyo pasipo kujua kuwa unahitaji kuwa na nguvu moja ambayo nitawezesha
maisha yako.
Ni ukweli kwamba
ukombozi wa kinywa usihanishwa kwa karibu na ukombozi wa mawazo na fikra kwa
ujumla wake kwakua tuna jua katika fikra kunajenga au kunatoa tafsiri ya mambo
na hatimae ndio kunazaliwa na tamko(maneno ya kinywa).
Siku zote siraha ambayo
ni hatari ufichwa na kuwa katika uangalifu wa hali ya juu sana kwasababu
inaaminika kuwa ni siraha ya ushindi na inatumika katika mazingira muafaka na
sio kila wakati na kila mahali, hivyo lazima utambue kuwa kinywa ni siraha ya
ushindi na hatari sana basi inapaswa kuitunza kujilinda kuhakikisha inatumika
katika mazingira muafaka ilikuleta matokeo sahihi.
Nikweli mtua anaweza
akaongea mengi lakini yako maneno yalibeba athari katika maisha ya mtu husika
na katika hayo unaweza kuona ni ngumu kutoka hapo ulipo, hivyousikubali kuishi
maisha ambayo kila mtu ataweza kuona anasababu ya kunenea neno baya katika
maisha yako.
Kila
neno linalotamkwa katika maisha yako linakuwa na nguvu pindi tu litakapopata
nafasi!!!
Imeandaliwa
na;
Cothey Nelson…………………………………………..0764
018535