NGUVU YA JICHO
Japo mwili wa binadamu una viungo vingi na kila kiungo kina
umuhimu wake na hiyo inatokana na kazi yake katika kuendesha gurudumu la mwili.
Lakini mimi nimeona bora ni zungumzie jicho kama moja ya kiungo chenye umuhimu
wa kipekee katika mwili japo si zaidi ya viungo vingine.
Tunapozungumzia jicho kila mtu anatambua umuhimu wake kwani
kupitia macho unaweza kufanya uchaguzi, kufurahi na kujisikia vizuri na hata
kutambua hisia za mtu kwako. Naweza
kusema jicho ni moja nyenzo ambayo imetumika katika watu kufanya maamuzi.
Hivyo Jicho linasafishwa,
linatunzwa na linatengenezwa ili liwe na muonekano unaofahaa ili liweze kufanya
kazi inayopaswa…….!
Sote tunajua kazi ya jicho iliyokuu kuwa ni kuona japo
inakazi nyingine kama kuwa ni sehemu moja ambao mwili utumia katika kutoa taka
zake, tunajua katika sehemu ambayo mojawapo inaumakini sana katika maisha ya
mwanadamu basi ni jicho au macho…………..unaweza kuwa mtunzaji wa mwili wako
lakini usipo tunza jicho lako na ikatokea jicho likapoteza nguvu yake ya kuona
basi maana ya wewe kupendeza hutaiona bali itakuwa kwa wengine hivyo itakunyima
uhuru wa wewe katika kuwa na changamko la kweli na kuamini kile wanachokisema
kuwa ndicho kweli au sicho kweli.
Pindi unapokosa macho basi yako mambo mengi utakosa kupata
radha iliyokamili kwakua utakuwa unaishia katika kutumia milango ya fahamu
iliyobakia. Kwakusema hivi hakuna mtu namtenga au namdharau kwakua kila kiungo
cha mwili ukikosa kunasuluba yake….lakini neema ya Mungu inatosha sana.
Ni jambo la kawaida kwa mtu ambaye aliyepoteza uwezo wa kuona
au tunaita ulemavu wa macho mtu huyu anakuwa anatumia sana hisia na umakini
katika kusikia (sikio), ni jambo jema kwakua ni njia iliyobaki kwa yeye katika
kuleta uelewa wa mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa yeye alipo,
Nipende kusema kuwa jicho ni moja njia inayotumika katika
mawasiliano katika kuleta uwelewa wa mtu na mtu hivyo ni seme kuwa jicho
linatafsiri kwakua linaweza weza kuonyesha hali ya kufurahi, hatari au hali ya
kuvutiwa na hata hali ya kushawishi hizi ni kazi zisizo rasmi sana japo
zinaongoza katika matumizi hasa kataika ulimwengu wa sasa wakiongozwa na
vijana.
Ni pende kusema kuwa jicho linatoa tafsiri, majibu na lina
ishara maalum katika kuonyesha kwendelea mbele au kubaki palepale au kuacha
kabisa!!
Nipende kusema tafsiri
ya jicho inabebwa na;
i.uelewa wa ufahamu
wako
ii.imani yako kwa Mungu
iii.nafasi ya jambo
lililotokea katika moyo wako
Ni kweli jambo linaweza kuwa ni moja lakini kila mtu pindi
anapoliona anatoa tafsiri yake ilibebwa na macho yake katika hiyo tafsiri ndio
inaweza kumpa kushinda au kushindwa………mathalani daudi wakati anaenda kumkabili
goliati japo wote Israel walimuona na kila jicho la kila mmoja lilitoa tafsiri
yake lakini daudi alipomuona naye macho yake yalitoa tafsiri yake ambayo kiukweli
ilikuwa tofauti na tafsiri na watu wengine kutokana na uelewa kile kitu
anachokiamini.
Uwezi kushinda kama macho yako hayajabeba tafsiri sahihi ya
jambo linalokukabili kwa maana nyingine tafsiri ya macho yako katika jambo
ambalo litakalo kukabili ndio limebeba kushindwa kwako au kushinda kwako.
Wengi wanatafsiri katika macho yao ambayo sio sahihi
hazijaambatana na uelewa katika fahamu zao bali wao wana amini kwakua kilisha
fanyika basi wanaamini hivyo na wala sio kitu kingine hivyo wanashindwa kubeba
nguvu na ujasiri wa kudumu katika utendaji wao.
Macho yako yakikosa kukupa tafsiri basi ni rahisi kila kitu
kiwe na nafasi katika maisha yako kwakua ujui kuwa hiki ni haki yako na kile si
haki yako. Hakikisha macho yako yanakupa tafsiri ya Mungu kwa usahihi iliikupe
kuyakabili mambo katika uvuvio na uweza wa Roho mtakatifu.
Unaweza kufa kabla ya wakati wako au kuishi katika hali ya
mateso kwakuto kuwa na tafsiri ya macho yako katika jambo linalo kuzunguka,
Ukitafuta ushindi katika maisha yako lazima uwe na tafsiri
iliyo sahihi katika kila linalokukabili!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………………………0764
018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni