TULIZO LA MOYO
Kuna
vitu vingi ukikosa unaweza ukavumilia na maisha ya kaendelea lakini kamwe sio tulizo la Moyo, nimeona watu wengi
wakifikia maamuzi mbalimbali kwasababu la kukosa tulizo la moyo!!!
Ni
kwli mtu unaweza ukakosa fedha,watoto,elimu na mengine mengi lakini bado maisha
ya kaendelea japo katika hali ya kuvumilia na baadae ukazoea, lakini kamwe sio
tulizo la moyo kwani katika hali hii moyo unakuwa haujielewi maana hauna
furaha, ujui ufanye nini au usifanye nini? Unaweza kukaa ukaona bora usimamame
na hata ukisimama bado utaona haitoshi unaweza ukaona bora ukimbie na hata
ukikimbia bado utaona haitoshi utaona bora utambae na utamaliza mambo yote
lakini kamwe hauta weza kupata jibu la swali la moyo wako!
Najua
hali hii sio ya wote kwakua wako watu wanaweza wakaishi maisha ambayo hayaleti
burudiko au tulizo katika moyo lakini
bado akaona wacha maisha yaendelee maana nitavumilia na baadae ndio yatakuwa
maisha yangu.
Niseme
mtu anayeishi katika hali hii ukweli anaishi maisha ya utumwa na ya ukiwa japo
anaweza kuwa na mali nyingi familia bora iliyoelimika na maendeleo .
Kitu pekee kinachoweza
kuleta tulizo la moyo ni SEHEMU SAHIHI
Nje
ya hapo uwezi kuwa na tulizo la moyo, kwakua unaweza kuwa sehemu nzuri
inayopendeza macho na inayofurahisha na kugusa hisia zako lakini isiwe sehemu
sahihi!
Kwa
kawaida ukuaji wa binadamu ili uweze kwenda katika ubora wake kila jambo lina
wakati wake pindi mtoto anapozaliwa sehemu sahihi kwake ni mikononi mwa mama
yake japo anaweza kulelewa katika taasisi na hata watu wengine tofauti na ndugu
zake na kila hatua atayopiga ina sehemu yake sahihi mathalani katika mfumo wa
elimu kuna hatua anayotakiwa kuwa shule
ya awali na baadae kuingia chuo kikuu.
Ni
napozungumzia sehemu sahihi na zungumzia sehemu ambayo itakayokupa mwanga
katika maisha yako uliojaa ushindi na ubora na ushujaa na mwendo wenye kishindo
ulio jaa mamlaka. Na ninapozungumzia sehemu hapa na zungumzia ni zaidi ya
nyumba nzuri iliyo jaa malumalu na kumetameta au aina ya kanisa ambayo iliyojaa
nguvu ya Mungu au yenye taratibu zenye kuheshimika na kukubalika katika nchi.
Sina
tatizo na nyumba nzuri, kanisa lako nzuri bali ninashida na tulizo la moyo wako
kweli lipo? niseme kusema kunatofauti kati ya matumaini ya akili na tulizo la
moyo na niseme tu kwamba hakuna mtu ataleta tulizo la moyo wako zaidi ya Mungu
mwenyewe katika moyo wako kwani katika yeye ndio linapatika tulizo la kudumu.
Unaweza
kuwa sehemu yoyote hata iwe bora kiasi gani lakini ukweli kwamba kama tulizo
alipo hata kama ikiwaje na kamwe tulizo la moyo aliwekewi katika kutamkiwa bali
linachipuka ndani yako!
Unaweza
kuwa sehemu sahihi katika mazingira lakini usipo itambua nafasi ya Mungu katika
maisha yako iliyojaa kwa ukamilifu utaweza kufanya jambo sahihi.
N.B;
tulizo alitegemei namna unavyokaa na mtu wa Mungu vizuri tu bali namna
unavyokaa na Mungu vizuri kwani yeye ndio mtoaji tulizo la Moyo kwako na
mtumishi wake,
Kwakua
hivi sasa watu wamekuwa makini sana namna ya kukaa na mtu wa Mungu kuliko namna
ya kukaa na Mungu na watu wa namna hii wamekuwa wakiangukia katika maumivu
makali kwakua walimuamini Mtumishi wa Mungu kama Mungu mwenyewe!
Sisemi
usiwasikilize watumishi ambao Mungu amewaweka uwaheshimu sana kwakua Mungu
amewaweka kwa kusudi lake na Mungu anawaheshimu sana maana amesema
mwenyewe…..mtu akinitumikia nami nitamuheshimu,
Kubwa
sana nataka kusema ni muhimu kutambua nafasi ya mtumishi wa Mungu na Mungu
mwenyewe ili ufanye jambo katika ustawi mzuri wa maisha yako.
Sehemu
sahihi ya kukaa wakati mwingi kwa macho haya ya nyama inaweza isivutie bali
sehemu nzuri na kuvutia lakini niseme sehemu
sahihi ni mahali wewe ulipo na Mungu
Nasio
mahali ambapo watu wengi wanakimbilia na kupasifia bali ni mahali ambapo Mungu
anakuwa tulizo la moyo wako na sio mazingira au maneno ya mtu yenye ushawishi
au yenye kutisha , kwakua hakuna mwenye hatima ya maisha yako zaidi ya Mungu
mwenyewe yeye mwenye kujua kabla ujatoka duniani na baada ya kutoka yeye
anaijua hatima yako na kujua namna ya kukufikisha.
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson…………………………………………………………0764 018535
SEHEMU SAHIHI KATIKA HATIMA NJEMA!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni