BADO UNAYO NAFASI
Maumivu
ya mtu yanaongezeka sana sio kukosa nafasi tu bali pindi anapotambua kuwa
hakuna nafasi nyingine ya kuweza kufanikiwa tena!
Haijarishi
upo katika kipindi kigumu kipi elimu,kazi,mausiano au huduma jibu langu kwako
ni kusema kuwa BADO UNAYO NAFASI!
Machozi
ya mtu unaweza kuyaona hapa katika hatua hii pindi mtu anapo ona sasa sina
nafasi tena kinachopaswa sasa niangalia kitu kingine kabisa.
Ni
jambo kubwa na ni mateso pindi unapogundua kuwa katika mtu mliyependana sana
inawezekana alikuwa rafiki tu au mchumba na hata mke pindi inapojua sasa ndio
mwisho wa mausiano yangu naye katika maisha yako!
Kinacho wa umiza watu wengi sio kukosa katika
yale wanayoyatarajia tu bali ni kuona kuwa hawana uwezekano tena kuyapata yale
waliokuwa wakitarajia! Ndo mana mtu anaweza kulia mara mbili kwakumkosa mtu
anaye mpenda na kuwa hata onana nae tena hivi vinakuwa ni vilio viwili katika
moyo wa mtu.
Ni
kitu kizuri pindi unaposikia kuwa bado unayo nafasi kwakua unajua kuwa kumbe
naweza fanya kitu bora au kizuri zaidi kwakua ninayo nafasi tena!
Kutoona
nafasi tena kunaweza kusababishwa na namna unavyojiona au mazingira au hali
halisi inayoonekana mathalani binti anaona umri unaenda na mwili unazidi kuwa
katika hali ya uzee basi nafsi yake inaweza kusema sasa nitakufa bila mume wala
mtoto. Kitu ambacho wanawake wanalia sio tu kupoteza watoto au kutoshika mimba
kwa sababu mfumo wa kimwili kutokuwa sawa bali maumivu hayo yanazidi pindi
anapopewa jibu kuwa hakuna uwezekano wa yeye kushika mimba au kupata mtoto.
Katika
hali hii na maumivu haya mtu uweza kujikuta kufanya maamuzi ambayo kiukweli
yanaweza kusababisha matatizo katika maisha yake na sio kuleta pumziko au
suluhisho la kudumu katika maisha yake.
Niseme
katika yote bado unayo nafasi ya kufanya lolote na kufika popote na kuwa yeyote, la msingi tu
limepata kibali kwa Mungu na kwa neema zake basi unaweza kuwa mtu wa tofauti
sana, niseme watu wengi wanalia kwasababu maarifa yao yameshafika kikomo hivyo
anakuwa anajibu linguine zaidi ya kusema SAWA! Lakini kumbuka kuwa maarifa yako
sio ya Mungu.
Ni
seme kuwa watu wengi wanafika katika hatua hii kwasababu wanakuwa wanalazimisha
mambo yao yaweze kufanikiwa kwa maarifa yao kwa mawazo yao na mwisho inavyokuwa
tofauti basi hapo kilio kinachukua nafasi na kilio kinakuwa na nafasi kubwa na
hali ya mtu kupenda kuwa katika hali ya mwenyewe tu! Upweke uzaliwa hapo.
Niseme
katika maisha jambo baya sana ni kikwazo katika maisha ya watu wengi ni kuona
ubaya aliotendewa kuliko wajibu wake sikuzote ubaya unapozidi wajibu wako basi
kinachofauta hapo ni maumivu na mateso na kujikataa.
Jua
anayeweza kukupa raha sio mchungaji, mpenzi au wazazi wala watoto ni kweli
wanaweza kukupa furaha furaha tu! Lakini sio raha kama chimbuko la matumaini
katika maisha yako ya sasa naya baadae.
Niseme
tu kweli yanayotokea yanaweza kuwa mshangao kwako au surprise lakini sio
mshangao kwa Mungu kwakua hakuna jipya kwa Mungu hivyo unachopaswa kuona kama
bado huko kwa Mungu basi ujue yeye atarekebisha tu na utakuwa salama.
Ni
vizuri kuwa na mipango mizuri katika maisha tulionayo yaani kuwa na mke au mume
mzuri na mengine mengi lakini pindi Mungu anapoingilia ili kuyaboresha usiwe
kikwazo kwake katika kukusaidia kuyafanya kuwa katika mtazamo wake Mungu
uliojaa matumaini ya kweli.
Usikubali
kuonekana sawa na vile watu wanavyo kuona kuwa umeshindwa au umeaibika au
hauwezi tena yaani usiishi katika mtazamo wa watu bali kubali kuishi katika
mtazamo wa Mungu mwenyewe anaeijua kesho yako na kuitunza kwa ajili yako.
Niseme
tu hakuna mtu anamwamini Mungu katika hali sahihi akawa ana kesho mbaya hayupo
hii inakuwa ni fikra zetu tu na hofu za maisha kikubwa ni kumwamini Mungu
katika kila hatua….kwakua Mungu anafanya jambo kwa Yule anaye mwamini.
Unahaja
ya kuchoka maana Mungu ajachoka, unahaja ya kushindwa maana Mungu ajashindwa
kufanya jambo litakalo leta mwanga katika maisha yako.
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson………………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni