NGUVU
ILIYOPO KATIKA UTULIVU
Wepesi wa macho sio
uzito wa mizizi!
Usione mti umetulia tu ukadhani ni rahisi nitauangusha! Usipokuwa makini unaweza kuchukua miaka mingi pasipo kupata jibu…….na kubaki na swali pasipo muafaka kuwa mti huu hivi utaanguka lini?
Iko misemo mingi mizuri
na ya kushawishi masikio ya watu na kivutio cha macho ya watu na kuna wakati
mwingine misemo/methali hizo zinakuwa na uhalisia katika jamii yetu mathalani
harakaharaka haina Baraka, polepole ndio mwendo, mvumilivu ula mbivu na nyingine
nyingi na zote ziki husisha hali sahihi
katika kuamua maamuzi yoyote na nyingi zikilandana na methali hii fikiri kabla
ya kutenda bado ikilalia sehemu inayoitwa tatua jambo katika njia muafaka na
sio kwa kukulupuka.
Ndomana maamuzi ya
vijana wengi hayathaminiki kama ya wazee kwani haya maamuzi yana aminika kuwa
ndani yake hakuna umakini kama ya wazee na pia yana amini kuwa hayajakomaa au
hoja zao hazina shibe/mshiko kwa kiufupi hoja zao hazina uhalisia katika maisha
wanaoishi na moja ya sifa kubwa ambayo inaaminiwa sana na maamuzi ya wazee ni
kuwa na hekima yanaangalia mbali sana, japo pamoja na hayo kunaweza kuwa na
kasoro katika upande wa mawazo ua wazee mathalani yakawa ni mawazo yasioendana
na mabadiliko ya sasa( mawazo mgando) bila shaka iliutambue hili unahitaji
mawazo mapana yaani mawazo yenye utafiti wa uhakika.
Japo kuna mazingira
mengine maamuzi ya haraka yanahitajika na hasa katika jambo la haraka
linalohitajika utatuzi wa haraka mathali katika vita bila shaka hapo maamuzi ya
haraka na yenye akili yanahitajika sana ili kujiweka katika nafasi nzuri ya
kuweza kuwa salama na hata kuleta ushindi kwani utambue kuwa makosa yako ndio
fursa ya mwenzako!
Na kubaliana kabisa
kuwa unaweza kuwa katika hali ya utulivu lakini bado unaweza usiamue jambo la maana
kutokana na sababu mbalimbali migandamizo ya mawazo(stress), mshauri wako,
nguvu za hisia zako na hasa pindi unaposhindwa kuzitawala.
Pamoja na hayo nipende
kusema kuwa maamuzi sahihi na yenye utendaji wa nguvu kubwa pamoja na kishindo
yanayoweza kuleta mabadiliko makubwa ya ajabu sana kusababisha mafanikio
makubwa katika maisha yako!
Mwanzo
1:2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa
vilindi vya maji; Roho ya Mungu
ikatulia juu ya uso wa maji.
3 Mungu akasema, Iwe nuru;
ikawa nuru.
Tunaona katika utulivu
wa Roho ya Mungu ndio ilikuwa ni hatua ya kwanza ya Mungu kabla ya uumbaji wa
kitu chochote japo dunia haikuwa na sura nzuri wala muonekano usio faa, lakini
katika utulivu ndani yake ilikuwako nguvu ya kuleta mageuza ambayo ndio
imefanya sisi wanadamu tuweze kukaa na kuona fahari ya dunia tuliyonayo.
Tunaona Mungu anatumia
siri kuu katika utulivu kufanya mambo makuu atuoni Mungu akiamua tu jambo kwa
sababu lipo tu na anaweza kuliamua tu maadamu anayo nafasi na uwezo huo bali
alitulia katika hali ya kujua mwisho kabla ya mwanzo na katika hilo tunaona
Mungu kushindwa hakutajwi kwake…………….ndomana mwisho tunaona akisema
Mwanzo
1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana………
Ukweli Mungu
anatufundisha siri kubwa hapa na inadhihirika katika hali ya ushindi wake
katika kila alichokifanya!
Kiubinadamu hali hii
inakuwa ngumu sana unaweza ona mtu kuwa ni mtulivu sana katika muonekano wan je
lakini ukweli ndani anafurukuta moto unaotaka kulipuka kwa hiyo muda wowote unaweza
kulipuka ni sawa sawa na dumu la petro kupita
mahali ambapo moto unaweka na dumu
likiwa wazi.
Katika mambo yote
ningependa kusema utulivu uliobeba akili ya kutosha na dhamira njema ni jambo
muhimu sana katika maisha yako kama mkristo inawezekana watu wakakuona
unachelewa sana, niseme ni bora wakuone unachelewa sana kuliko uwai badala ya
kutengeneza ukajikuta unaharibu.
Nikubaliane kusema
ukweli hasira wakati mwingi isipoongozwa na akili iliyo sahihi mwisho wake ni
uharibifu au mtokeo yake yakawa chini ya kiwango au hali inayotakiwa.
Niseme utulivu wa
kibinadamu hauna matokeo mazuri kwani ni kweli unaweza ukatoa maamuzi ya
kuangalia kesho lakini uhakika wa hiyo kesho kuwa sawa na unavyosema au
anavyoamini lakini uko utulivu wa kimbingu ambao ukiiwaza kesho kamwe haiwezi
kuwa tofauti na vile alivyowaza kwani yeye anaitwa jana leo kesho hata milele na
neno lake hakuna kinachoweza kutengua.
Isaya
55:10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi
huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye
mbegu, na mtu alaye chakula;
11 ndivyo litakavyokuwa neno
langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza
mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma
Anavyosema
ndivyo inavyokuwa na sio kitu kingine!
Umaana
wako mbele za Mungu unaanza pale utakapoamua kumbeba Mungu!
Imeandaliwa
na:
Cothey
Nelson…………………………………………….0764 018535
BARIKIWA!