AHADI YA MUNGU
Kama kuna kitu ambacho utakiwi kuweka mashaka
atachembe!...wala moyo wako kushuka chini na hata fahamu kupoteza muelekeo ni
hiki kitu kinaitwa AHADI YA MUNGU! Nitangulie kusema tu maadamu unaishi ndani
ya dunia hii jua ahadi ya Mungu juu ya maisha yako ipo kama isingelikuwepo
isinge likuwa ya maana ya wewe kuwepo duniani, hivyo uhitaji kuomba ahadi ya
Mungu jua zipo na zitakuja kwa namna yake kutokana na mfumo na utaratibu wake.
Yeremia 1:5
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni,
nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Haya ni maneno ya Mungu yanaishi na yana
nguvu mpaka leo! Ni akili yako ni kutambua tu.
Ni pende kusema tu ahadi ziko nyingi…..ziko
zinazo toka kwa wanadamu, miungu na MUNGU lakini kamwe haziwezi kufanana lakini
nikubaliane tu kuwa kila ahadi ina taratibu zake na ili uzipate ahadi zake basi
hauna budi uzifuate hizo kanuni zake kwakua ndani ya taratibu zake huko ndiko
ahadi upitia.
Najua yako malengo mengi ya ahadi lakini
mimi niseme malengo machache tu:
i.
Kufanya uwe na furaha
ii.
Kufanya uzidi kuimarika
pasipo kuchoka
iii.
Kudumu katika mwenendo mzuri
iv.
Kufanya usahau mengine na
kuweka bidii katika jambo husika
Nikubaliane tu ahadi imetumika sana
katika maeneo mbalimbali mathalani ofisini bosi anaweza kukuambia ukiifanya
vizuri kazi hii kuna zawadi nitakupa au kukuongeza kima cha mshahara wako na
nyingine nyingi, katika familia wazazi wengi wamekuwa waki waahidi sana watoto
wao zawadi ilikuwafanya watoto wasome
kwa bidii au wabadilike kutoka katika tabia fulani ambayo wazazi/mzazi
afurahishwi nayo.
Nipende kusema tu kuwa ahadi ya Mungu
juu ya maisha yako ni zaidi ya kukopa salio katika mitandao ya mawasiliano
(voda,tigo,zantel,airtel) na pindi utakapoongeza salio kwa njia ya kawaida
utaona meseji watakayokuandikia “asante kwa kurudisha deni lako” japo kuwa
tunaona ni mtandao uliotengenezwa na hiyo program kuanza kufanya kazi…..lakini
ahadi ya Mungu kumbukumbu yake ni zaidi
ya hapo kamwe haiwezi kuwa rahisi kusahaulika!
Ahadi za Mungu ni nyingi katika maisha
yako na katika mwendo wako na Mungu bila shaka utaona mambo mengi wala usijue
haya mambo mbona sikuyajua wala sikuwai kumuomba bali yatakuja kwakua yeye kama
baba anajua wajibu wake kwako na atatoa kwakua
hilo ni jukumu lake.
Mathayo 6: 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa
mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.
Na wakati mwingine unaweza kujua baadhi
ya ahadi ya Mungu katika maisha yako, Ni ukweli usiopingika kuwa hivi ni vitu
viwili tofauti sana kati ya kutambua ahadi ambayo Mungu amekuwaidi na kuipata
ahadi hiyo, kwani kuna mchakato mrefu sana(majira sahihi) na hapo ndipo kuna
kuwa ni kipindi kizuri cha kupima PENZI LAKO kwa Mungu.
Warumi 4:18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa
baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
19
Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha
kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo
lake Sara.
20
Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa
imani, akimtukuza Mungu;
21
huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.
Tunaona ibraham japo Mungu
mwenyewe alimuahidi lakini alihitaji kutiwa nguvu na Mungu mwenyewe ili
kuifikia ahadi yake.
Kama nilivvosema hapo awali kuwa kila mtu maadamu
uko duniani unayo ahadi ya Mungu katika maisha yako hasa mtu uliye okoka
unapata kibali kuishi katika maisha yanayoambata na ahadi ya Mungu kwa asilimia
mia, lakini kutokana na mabadiliko ya dunia imekuwa ni changamoto sana acha mbali
na sayansi na teknolojia bali hasa injiri ya sasa imekuwa ikiwapa watu njia
fupi katika kuwapatia mapumziko ya shida zao mathalani maombezi kwa wagonjwa
kwa namna ya kimwili fedha imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa.
Pamoja na hilo wa kristo wengi wanashindwa kudumu
katika imani zao za kweli kutokana na misingi waliyo ibeba sio imara imara
zaidi.
Mathayo 7: 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya,
atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
25 mvua
ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa
maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na
mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba
ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa
Nipende kusema ahadi ya Mungu ni amina
na kweli na kamwe awezi kusahau ila uzidi kudumu katika yeye kwa majira yake
atakutoa na kuchomoza!
Sina maneno mengi zaidi ya kusema!
Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani;
Ndivyo mema yatakavyokujia.
Imeandaliwa na:
Cothey
Nelson………………………………….0764 018535
BARIKIWA SANA RAFIKI