MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU!
Kama bahari inavyo hifadhi vitu vingi na hata kufanya viumbe
viishi na kuimarisha mzunguko wao pamoja, kwakua ndani ya ulimwengu viko vitu
mathalani viumbe vinavyoishi nchi kavu kama vile binadamu, wanyama( samba,tembo,swala,nyoka
n.k) na viumbe vinavyoishi ndani ya maji(samaki,mamba, papa, nyangumi n.k)
kwakifupi ukiangalia ulimwengu unaweza kuona imesheeni vitu vingi sana, lakini
uzuri wakevitu vyote vina nafasi yake ya kuishi ukiachilia mbali na mwingiliano
usiokuwa rasmi.
Ni kibinadamu tu, kutambua kuna watu na wako watu wanahusika
na maisha yako katika hali zote kwa maana binadamu anataka awe na watu katika
kuendelea shughuli zake, lakini shida inakuja pale utakapoona jambo linalo
kugusa wewe wengine aliwagusi wanaona ni lako na wala sio la wote.
Niseme tu kuna wakati unaweza kuona watu wanakuwa na wewe,
kuna wakati utakuta watu kama hawako tena nawe, hali hii inakuwa shida sana kwa
mtu ambaye ameweka akili zake katika matarajio ya watu, japo kwa ukweli unaweza
kuweka akili kwenye matarajio ya Mungu tu lakini bado utaona faraja ya wanadamu
inahitajika katika maisha yako kwakua unaishi katika ulimwengu uliobeba watu.
“ MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU” hii ni sauti inayo nenwa na moyo
wa mtu husika baada ya hali ya fulani katika maisha ya mtu husika inaweza kuwa
hali njema au mbaya! Japo kwa kiasi kikubwa inaonekana sana katika hali mbaya.
Niseme tu hali hii hakuna anapenda impate ila inapotokea uwa
hakuna namna nyingine ya kuikwepa zaidi ya kuikabili na kusubiri namna itakavyo
kuwa kwakua ni wewe na ndilo limekukuta
uwezi kuomba mzigo ulionao umpe mwingineza zaidi ya Mungu ajuaye kesho
maana ndio aliye iruhusu iwe.
Nikutie moyo hali hii inawakuta watu wa namna zote walio weka
imani yao kwa Mungu kwa asilimia zote na kwa wale wanaotumia hadhina zao katika
akili (elimu na maarifa) lakini inafika wakati wana jikuta wako wenyewe, kwa
hali halisi katika maisha husika muda mwingi unakuwa katika maongezi yako
binafsi ambayo utaki mwingine ahusike.
Katika kipindi hiki unapojiona “ MWENYEWE KATIKA ULIMWENGU”
ni kipindi cha kudhihirisha wewe ni nani? Kutoa ile hadhina ambayo Mungu
amekupa kuona mkono wake katika namna yake kwakua yeye ndiye ajuaye mwisho
kabla ya yote.
Kipindi hiki usipokuwa makini unaweza kuchukua maamuzi
yanaweza kuharibu hatima yako au kuifanya iwe bora, wako watu wanapojiona wako
pekee yao katika ulimwengu kutokana na hali aliyokuwa nayo uweza kuwaza hata
kujiua, kwenda sehemu mbali ambako anahisi nafsi yake itapata pumziko na
mwingine kujiingiza katika mtindo mwingine wa maisha ambayo uta hatarisha zaidi
maisha yake badala ya kuleta mwanga wa matumaini.
Lakini ni muhimu kutambua hichi kipindi kina muhusu kila mtu
kwa muda wake maadam anaishi katika ulimwengu ambao wewe unaishi na hivyo
usione kuwa wewe ndio hali hiyo imekukumba kama umeonewa kumbe kila mtu
anapopita hapo ila kuvuka hapo inategemea imani yake ameiweka wapi na utayari
wa kuingia mazingira mapya.
Usipoteze muda wako katika kutafuta mbaya ni nani? Mpaka ni
mekuwa hapa maana kwa kufanya hivyo utakuwa umeliongeza tatizo na sio utatuzi
wa tatizo kwa maana utafanya ufahamu wako kulikuza tatizo zaidi na kuzidi
kukita mizizi katika moyo wako na mwisho wake unaweza kuibua kisasi kisichokuwa
na faida yoyote katika maisha yako.
Hapo lazima utulie na Mungu mwenye dira nzima ya maisha yako
maana yeye alikujua tangu ulimwengu ujakuweko!
Yeremia 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Katika kuzidi kwa Mungu ndio unaleta wepesi wa kutoka hapo
ulipo, mbali na hapo utazidi kukaa katika muonekano usio na tija katika maisha
yako.
ANAITWA MUNGU! BARIKIWA
Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………………0764
018535