Jumanne, 31 Januari 2017

SIKU YANGU!



SIKU YANGU


Kama kuna kitu ambacho thamani yake haiwezi kupimwa ili uipate hama kisichoangalia uwezo wa mtu kuwa huyu anavyo vingi na huyu ana kidogo hama kwa maana pawepo na kitu kishawishi uweze kuipata ukweli HAKUNA, hicho kitu kinaitwa SIKU

 Inapotokea watu kumi  wakapewa zawadi zinazo fanana, kama imeamliwa kutolewa gari kwa kila mmoja basi  watapewa gari zinazofanana, lakini kila mmoja baada ya kupewa gari basi atashukuru kwa nafsi yake ( kwakua yeye atakuwa ndio mmiliki) na sio kwa ujumla kwakua kila mtu kapewa  na ana namna yake ya kushukuru,

Ni tabia nzuri ya kushukuru pindi unapoona nawe umepata zawadi miongoni mwa wengi kwakua ni jambo jema kukumbukwa au kutambulika na wala usiwe na kinyongo kuwa wewe kutaka kupewa zaidi ya wengine, ni bora kupata hata kidogo kuliko kukosa kabisa.

 Ni muhimu kutambua lolote linaloendelea katika siku linakuwa ni kwa ajili yako, mvua, jua na kwa ujumla hali ya hewa yote vinakuwa ni kwa ajili ya kuwezesha maisha yako yawe vizuri. (ila inategemea tafsiri ya akili yako), maana unaweza kukuta mtu analalamika ikiwa mvua anaona mafuriko na jua likiwaka anaona kiangazi.

Ni vizuri kutambua Mungu baada ya kuumba dunia katika kuhakikisha maandalizi yanakuwa mazuri kwa ajili ya mwanadamu aweze kukaa na kumfurahia Mungu kwaku mwandalia mahala pazuri, hivyo Mungu aliingia gharama katika kuitengeneza kuanzia siku ya kwanza mpaka anafikia kumtengeneza mwanadamu katika siku zote hizo Mungu alikuwa ana hakikisha mazingira yawe mazuri ambayo mwanadamu( kipenzi chake) aweze kuifurahia kwakua kila kitu cha kuhakikisha kila kitu cha kumwezesha kuishi kinapatikana. 

Maadam umepata kuona siku nyingine naam katika wachache waliopewa neema na wengi walikosa kuiona lazima ujue umepita katika hatua nyingi sana na hatimaye kupata kibali cha kuona hiyo siku mathalani mtoto tangu mimba inapotungwa hadi mtoto anapozaliwa sio kitu chepesi ukipata neema ya kuangalia mchakato wake wa hatua ya awali mpaka hatua ya mtoto anazaliwa, kwakua wako watoto wana kufa katika kila hatua ya kufanyika kuwa mtoto ni yule tu mwenye uwezo wa kuimiri katika hali zote na hatimaye kutokea duniani.

Hivyo uone thamani kubwa sana ya wewe katika kuona siku nyingine haijarishi umeona ukiwa katika hali njema au mbaya bado uone katika yote uone neema ya Mungu iliyokupa heshima ya kukupa siku na kama zawadi iliyo kuu ya kufanya uweze kuifurahia zawadi zingine mathalani chakula, marafiki na ndugu pamoja na wale unaowapenda maana vitu vyote hivi vinakuwa na maana sana pindi unapopata neema ya kuona siku,

Ni muhimu kutambua kuwa furaha ya mtoa zawadi ni kuona unaifurahia na kuitumia sawa na vile au na lile kusudi analolitaka ulifanye atajisikia vibaya sana pindi anapokupa zawadi anapoona inakutesa, inapunguza upendo wake kwako, yaani inaondoa ibada mbele zake kwakua tumeona baadhi ya watu wanavyoitumia tofauti ya na lile kusudi alilokusudia, wako watu wanatamani siku isiishe kabla hajatimiza hazma yake inawezekana kuua, kuiba, kumfanya mtu ajute! Hama kulewa sana na mengine mengi yasiyo ufurahisha moyo wa Mungu.

Lazima utambue japo wote mmepewa siku tambua kila mtu atafaidika sawa na namna atavyoitumia mathalani inawezekana wote mnasoma kitabu kimoja lakini kila mtu anaweza kuondoka na kitu chake na akakitumia katika maisha yake kikawa msaada kwake na mwingine aliyesoma kitabu hichohicho akamaliza na akawa kama ajasoma kitu na mbaya zaidi kesho yake ikawa mbaya kuliko leo.

Ni muhimu kuwa na mtazamo sahihi katika siku yako maana siku ina maana kwakua wewe upo maana wewe ndio inaipa kuwa leo ni siku fulani, sawa na mtoto wako unapo mpa jina, lazima aishi vile uwezo wako ulivyo ndivyo ilivyo siku lazima uifanye kuwa siku yako na kuweza kuitawala na niseme kuitawala siku hahitaji fedha tu, bali akili inayojielewa na kuitumia,

Hivyo huna sababu kusema siku yangu ni mbaya kwakua ni wewe pekee unaweza kuifanya iwe unavyotaka mathalani kama njaa, shida, misiba, kusalitiwa, kuachwa na mambo mengine hiyo ni kawaida ya wanadamu na amini ingeweza kutokea mambo makubwa zaidi hapo hivyo lazima ujifunze na kuona uone upendo wa ajabu wa Mungu katika kila siku,

Ni muhimu kutambua siku inakuja kwa kusudi jema ila inategemea namna unavyoitafsiri mambo yanayotokea katika siku hiyo  kwakua ndani ya kuitafakari kuna ruhusu moyo wako kukamatwa na unaweza kuufanya moyo wako kuwa chini bila sababu yoyote.

SIKU NI NZURI IPENDE ITAKUPENDA NAAM UTAIFURAHIA!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………0764 018535

Jumanne, 24 Januari 2017

NAKAZA MWENDO.



NAKAZA MWENDO.


Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu;  ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. (1 Wakorintho 10:13)

Ukubwa wa jambo unakuwa pale unapolitazama katika hali ya kulikuza!

Pindi unapoingia ulingoni na utakapo muona mpinzani wako namna alivyo na maandalizi yake uliyo yasikia akiyafanya katika kujiandaa kupambana na wewe unaweza ukajikuta unazimia hata kabla pambano kuanza.

Kulitazama jambo hakuna shida maadam linaonekana lakini kubwa ni namna unavyolitazama ndio linaweza kutoa picha ndani ya moyo wako katika hofu hama ujasiri katika kuliendea ili kulikabili,
Katika mashinadano mengi kuna changamoto nyingi sana hadi kufikia kwenye hatima au kuibuka kuwa mshindi na kama wangeweka MKAZO katika kutazama dhoruba zitakazo wakabili basi bila shaka kushinda ingekuwa ngumu sana,

Moja ya dalili ya mtu kuliweka na kulikuza jambo linalo mkabili ni kulia, unaweza kukuta mtu analia mpaka anazimia zimia na kumwagiwa maji napengine hata kuwekewa watu wakumwangalia wakati wote.

Ni muhimu kujua kuwa chochote utakachokipa nafasi kitachukua nafasi na kutoa matokeo yake katika maisha yako katika upande ulio wa faida au hasara, na katika ulimwengu tulionao wako watu ambao ni lazima watiwe nguvu ndio wa hamishe mawazo kutoka katika hali ya inayowakabili na kupata mwanga au njia katika maisha yanayo wakabili na wako watu walivyo pekee pasipo msaada mwingine wa nje wanapoona jambo wanaona njia ya kupita,

Ni muhimu kutambua unapoliangalia tatizo katika ya wasiwasi hapo unaweza kujikuta hali ya hofu inatanda katika moyo wako na giza litayafunika macho na miguu itakuwa mizito na kukuta unasimama njia panda usijue uende au ubaki hapo.

Atakama unajua sana na uzoefu pindi utakapo weka mkazo mkubwa katika jambo linalokukabili na kuona katika mapana yake na sio madogo hapo hofu na kuona tayari umekuwa mdogo na kamwe kutoka hapo itakuwa ngumu kwakua ndivyo unavyojiona naam ndivyo utakavyo kuwa.

Mbaya zaidi hata kama mtu mke na mme kamwe hamuwezi kurithishana namna ya kutazama jambo japo unaweza kumwambia na kumuamasisha lakini kamwe hauwezi kumpa ufahamu wako uwe kwake bado atakuwa na utayari wake wa kuamua kuchukua hama kuitikia tu.

Unapolitazama tatizo kwa maana ya tatizo ni ngumu kutoka hapo lakini ukilitazama tatizo katika ufumbuzi basi hapo utaona njia ya kupita,

Lazima ujipende na kujithamini kwa kuona kila jambo linalo kukabili ujue kuna namna la kuliangalia ili lisiwe mzigo kwako bali funzo na kuimarisha imani yako,

UKIONA VYEMA UTAPITA VYEMA LAKINI UKIONA VIBAYA UWEZI PITA SALAMA!
INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 17 Januari 2017

NENO ZURI.



NENO ZURI

Kama kitu hiki kingekuwa bidhaa basi soko lake lingekuwa kwa haraka sana, tena kwa kasi ya ajabu! Naam kama angekuwa mtu basi kila mtu angetamani awe rafiki yake na kama angekuwa mtoto basi kila mama angetamani awe wake hama awe rafiki wa mwanae……..linaitwa NENO ZURI (USIOGOPE).

Masikioni mwa watu wengi wangependa kusikia kitu/jambo hama neno zuri ili aweze kufurahi na kuzidi kufarijika na inawezekana kuwa sababu ya yeye kwenda mbele, japo maneno mazuri utegemea mtu husika namna alivyo au hali aliyonayo napia  naamini unaweza kuongea neno moja lakini likapokelewa tofauti, kwani wako watu ukiwaambia POLE wanaweza kuona una wakashifu na kuna wengine wanaweza kujisikia vizuri na kuona fahari ndani yao kwa sababu yako.

Nakuna watu wengine ukiwaambia HONGERA wanaweza kusema ona huyu naye anajipendekeza lakini wengine ukiwaambia HONGERA watajisikia vizuri watakupenda sana na kuona wewe ni mmoja kati ya watu wanaothamini kile wanachokifanya.

Hivyo neno zuri utegemea mtu/ watu husika namna watakavyolipokea!

Yako maneno mengi mazuri ambayo kwa ukweli binadamu yeyote angependa kusikia akiambiwa kila siku mathalani UNAWEZA, SONGA MBELE, UNAJUA!, USIOGOPE, JITIE NGUVU UTAFIKA, KAZA BUTI, USICHOKE BADO KITAMBO KIDOGO! Na mengine mengi.

Lakini mimi leo ningependa kuliongelea neno hili USIOGOPE!

Naamini katika maneno ambayo yanapendwa na watu wengi ni hili neno kwa kuwa tunajua kama binadamu kuna kipindi unafika uwoga unaweza kukuingia katika jambo lolote linalo kukabili na hapo unaweza kuwa na kiu ya kutaka kusikia neno USIOGOPE likitamkwa na mtu unayemwamini au kumtegemea, unayempenda na hatimae moyo wako ukainuka tena.

Nimeona hali za watu zikibadilika ghafla mara baada ya kuambiwa neon hili “USIOGOPE NIKO NA WEWE” walipokuwa wanalia ghafla machozi yakakoma, mioyo ilipokuwa imeinama ghafla ikainuka, walipokuwa wamechoka mara wakapata nguvu, alipokuwa ametendwa ghafla amani ikaingia ndani yake na kuona inawezekana kuishi na mambo yakasonga.

Uwa na penda kusema kuwa maadamu unaishi huna haja ya kuona kuna mambo yanawezekana na mengine unayo yaona hayawezekani maadamu uko na Mungu anayeweza basi atakukuwezesha nawe utaweza.

Unaweza kukuta mtu ameanza safari ya jambo lake na akakuta njiani kuna hali ya kutoeleweka na mawazo yake yakaanza kuwaza kuona bora  arudi nyuma ili ajipange vizuri lakini hapo akikutana na neno USIOGOPE likabadilisha akili yake nakuona kuwa ninaweza endelea mbele, na ni vizuri kutambua hakuna safari isiyo na vikwazo na vikwazo ndio ishara ya uimara wako.

Na niseme wazi tu kuwa hata mtu uwe unajiamini kwa kiasi gani bado utalihitaji hili neno USIOGOPE kusikia kutoka kwa mtu mwingine na pindi unapolikosa uwa unakuwa na hali ya mashaka hata kama moyo wako unajua kuwa utashinda, maadamu Mungu amekuweka na watu basi tambua wapo watakutia moyo (watafanyika Baraka) na wengine wataona bora uangamie tu lakini hatima yako haiku mikononi mwao.

Ndani ya kitabu ninachokipenda yaani BIBLIA neno hili USIOGOPE limeandikwa mara nyingi na wataalamu wanasema ukiliangalia neno hili katika biblia limeandikwa zaidi ya mara 360 kwa kusema kwamba kila siku neno hili usiogope liwe kinywani mwako katika jambo lolote hama hali yeyote uone kutoogopa ndio sehemu yako.

Ili neno liwe na nguvu kwako lazima uyajue mambo ya msingi:

i. maana ya neno USIOGOPE

II. na mamlaka anayekuambia USIOGOPE

Ni vizuriutambue kuwa Mungu amekuweka duniani sio kuishi maisha ya kuogopa na ukweli maisha ya kuogopa hayawezi kumpendeza Mungu na kamwe uwezi kuishi maisha unayopaswa kuishi kama uoga utatatawala maisha yako.

Usijali inapotokea hakuna mtu atakwambia USIOGOPE unaweza kujiambia mwenyewe na Mungu akalithibisha na amini utakuwa salama!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 10 Januari 2017

KUJUA KWA FAIDA!

                                                                KUJUA KWA FAIDA


Katika dunia ya sasa ni nadra sana umuulize mtu jambo alafu akakujibu AJUI labda jambo hilo ameona alina faida kwake lakini mbali na hapo lazima na yeye aonyeshe kuwa anajua na sio kujua tu! 
Bali kujua vizuri sana kana kwamba alitabiri hicho kitu/ jambo kabla alijatokea hata kama anajua nukta moja ya picha nzima bado atataka kuonyesha anajua vizuri akionyesha kuwa yuko “updated” issue mbalimbali kwake ndio kisima………ukimtazama sana mtu huyu utakuta anapenda sana sifa alafu mbaya zaidi ajui kiunaga ubaga.

Katika sayari ya sasa watu wengi upenda kujua vitu vingi na hasa vipya hama vinavyoonekana kuwa watu wengi wanahitaji kuvijua ili na yeye aonekane kuwa ni wa kisasa na mwisho naye apatesifa kuwa katika watu naye yupo na kwa bahati mbaya ukimwangalia mtu huyu ukimweka katika maisha yake unaweza usione tofauti yake na mtu asiyejua kabisa,

Nipende kusema kwamba ni kweli KUJUA ndio ukumbozi wa kwanza katika maisha ya mwanadamu kwakua katika kujua uweza kupelekea kuamua/ utendaji uweze kuwa wa maana na wenye tija katika maisha ya mtu,

Napenda kusema KUJUA kunakuwa na maana:
i.mazingira ya utendaji kazi kwa yale unajua
ii.hali ya kuchukua hatua
iii.wakati sahihi

haya ni mambo machache ambayo yanaweza kuleta tija ya wewe kujua na kuwa faida kwako na wengine wanao kuzunguka hivyo kicheko chako kinakuwa kicheko cha wote.

Msukumo wa kutaka kujua kitu nacho kitu muhimu sana katika kukupa matumizi sahihi wa kile utakachokijua
a)unaweza kutamani kujua kitu kwa ajili ya kuongeza/kuimarisha maisha yako na hatimaye kukupa hatua moja katika kufikia hatua bora ya maisha yako.

b)maumivu/hasira/uchungu hali hizi zikikupelekea kujua kitu hakika kujua huku hakuta kuwa na maana sana kwako na hata kwa wengine kwaku katika hali hii hapo kiburi na kisasi ni sehemu yake

c)kutaka na wewe utambulike kanisani/mtaani/jamii ni kweli watu watajua unajua lakini hawatafaidika na hayo unayo yajua kwakua utafanya kwa masharti yasio na utu ndani bali yanayo kutambulisha wewe pasipo faida yoyote.

Isaya 66:2 Maana mkono wangu ndio uliofanya hivi vyote, vitu hivi vyote vikapata kutokea, asema Bwana; lakini mtu huyu ndiye nitakayemwangalia, mtu aliye mnyonge, mwenye roho iliyopondeka, atetemekaye asikiapo neno langu.

Tambua Mungu ili ahusike na maisha yako atufuti mtu mwenye kujua tu! Japo kujua ni vizuri lakini sifa kubwa ambayo Mungu utamani kuiona kwa mtu:
i.mtu aliye mnyonge

ii.mwenye roho iliyopondeka

iii.atetemekaye asikiapo neno lake

jua ujuavyo pasipo kuwa na msingi huu kujua kwako hakuta kuwa na maana kwa Mungu sana kwakua unaweza fanyika daraja kwa wengine lakini wewe usiwe na faida kwa hayo.

Umuhimu wako katika kujua kwako hutumie kwa wakati sahihi, penye kusikiliza basi sikiliza, penye kuongea basi ongea na penye kujifunza basi ni vizuri.

Dhahabu haina haja ya kujitengeneza ili ionekane ina thamani uwa ikionekana basi watu huitaka kuwa nayo, kwakua wanajua wanapokuwa nayo nini kinatokea katika maisha,

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:


Cothey  Nelson………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 3 Januari 2017

TAFSIRI ILIYO BEBWA NA JICHO!

TAFSIRI YA JICHO


Niseme kuna tofauti ya kuwa na macho na kuwa macho yenye tafsiri sahihi!
Japo kila jicho linapoangalia kitu uwa linakuwa na tafsiri ila sio kila jicho linaloweza beba tafsiri sahihi.
Moja ya fahari ya mwanadamu ni MACHO! Kwakua kupitia macho uwezesha vionjo vya mwili kufanya kazi kwa wepesi na kwa hali stahiki, kwa maana baadhi ya watu kwakukosa kuona uweza kupelekea baadhi ya hali kushindwa kufanya kazi inavyotakiwa mathalani kucheka, kutabasamu,kuhuzunika na hata hali kufikiri kwa wepesi uweza kupungua.

Naamini katika JICHO kuna makundi makuu mawili kundi linalo ona alafu likwenda mbele na kundi linarudi nyuma, yote haya ni makundi  yanafanya kazi kutegemea na mtu husika…….kwakua kila jambo linapotokea ushindi au kushindwa utegemea NAMNA UNAVYOONA!

Tafsiri sahihi ya jicho ukupa:

i.kuwa na bidii kwa kile unachokifanya,kwakua wewe pekee unakiona
ii.kuwa na imani thabiti isiyo yumbishwa
iii.kuwa na amani katika hali zote
-utofauti wako na watu wengine unao onekana ni sawa kwa kuwa mnaona tofauti hivyo maamuzi hayawezi kufanana.

Tukubaliane tu kuwa maamuzi mengi yanafanywa baada ya JICHO KUKUPA TAFSIRI kwani kupitia kuona unaweza kuona kuwa hili jambo lina nihitaji mimi peke yangu au watu zaidi ili liweze kutendeka na wengine wengi jambo linapokuwa gumu sana kuzidi kimo cha akili yake hapo uona haja ya kuwa na Mungu kuhusika kwa watu wote wameshindwa.

Niseme unapokosa tafsiri sahihi ya macho hapo inakuwa ni rahisi kuona upendeleo baadhi ya watu na kuona wewe unanyimwa haki kwa tafsiri rahisi wanakuzibia riziki yako au hawataki maendeleo yako na mwisho kuona wanakukomoa, nawe hapo utajipanga kupambambana ili uwakomoe na sio kutoka hapo,

Tatizo kubwa kwa watu wengi pindi tunapoona mtu anainuka katika hatua fulani katika maisha yake kwa kuona tafsiri sahihi ya jambo fulani au hali fulani katika maisha yake, tuna anza kumpa siku kama atadumu katika maisha yake baada ya ya wewe kutafuta siri nawe uchomoke katika hali uliyoko.

Niseme kwa dhati ukubwa wa tatizo na udogo utegemea TAFSIRI YA JICHO, wote mnaweza kupata shida moja lakini matokeo yakawa tofauti kutokana na tafsiri binafsi uliolipa hilo jambo ukiona litakutesa maisha mwako nalo litachukua nafasi katika maisha yako na kuhakikisha jambo hilo linakuwa sawa na vile ulivyo liamini.

Na niseme tu, katika kitu kigumu sana katika maisha ya mtu ni kubadilisha tafsiri inayotolewa na macho yake, maana bila hapo unaweza ukafanya yote kama macho hayaja badili tafsiri yake mabadiliko kuyaona hapo ina kuwa ngumu ni kama kuona chozi la samaki akiwa majini.

Na inawezekana tatizo likachukua siku moja , wiki moja, mwezi, mwaka hama miaka ishirini, ambalo limeshawai kukutokea katika maisha yako yote utegemea na tafsiri ambayo jicho lako litatoa kutokana na hali inayokuzunguka mathalani.kufukuzwa kazi, kuachwa hama kutengwa na mambo mengine mengi

Niseme unapokuwa na jicho lililobeba tafsiri unaweza kuona vitu tofauti na wengine wanavyoona maana unaweza kuona maisha mengine pindi unapoona jalala la uchafu wewe ukaona maisha ya utele na ustawi wa mambo mengi.

Na msimamo unao zalishwa baada ya kuona/ kupata tafsiri sahihi ya jicho kamwe hauwezi kuyumbishwa kwani unaweza kuona mwisho kabla ya mwanzo kuanza unajua kupitia hapa na utafika wapi! Hivyo utajali kule unako kwenda kuliko vile wanavyosema,

Kukosa tafsiri sahihi ya macho unaweza kuishi maisha ambayo kiukweli hakupaswa kuishi hivyo unaweza kujikuta unaishi maisha ya kujikunyata hata kama hakuna baridi, hata mtu akikushauri bado unaweza usimwamini kwakua wewe ndivyo unavyoona na sio vile unavyotakiwa kuona.
Uwezi kupata tafsiri sahihi ya kuona kama tu kama ujampa nafasi ya kutosha yeye aliyekupa macho uwe  nayo naam yeye ndio anajua matumizi sahihi hayo macho,

Niseme unapoona watu mbali waliomwamini Mungu wakitumia vizuri tafsiri ya macho yao na hata kufanikiwa katika maisha yao hayo yote ni matokeo ya wana wa Mungu kutotumia nafasi zao, kwa hiyo wamechukua nafasi zote katika upande huo nasi tumebaki kwenda kanisani tu,

Na Mungu amewaachie watu wengine mbali na watoto wake katika matumizi sahihi ya tafsiri ya macho yao ili kuonyesha kuwa tunatakiwa tuishi vipi ilikuweza kuitawala dunia katika misingi yake, kwani hakuna mzazi ambaye anaweza kuruhu mwanae anayempenda kuteseka wakati uwezo wa kufanya aishi maisha ya utele na furaha anao uwezo.

Kama kunavitu unahitaji upambane navyo sana ni hali ya kuapata tafsiri sahihi ya jicho katika mambo yanayokuzunguka,yanayokutokea,yanayokunyimaraha,yanayofanya usiwe na amani, kwani tafsiri sahihi ya macho upelekea kuamua mazuri yaliyo jaa hekima na yenye ubora yanayo kutengenezea kesho yenye matumaini bora yasiyo kwamishwa na mtu.
INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:


Cothey  Nelson……………………………………………………..0764 018535