Jumanne, 4 Agosti 2015

KILA KIU KINA UJAZO WAKE



KILA KIU KINA UJAZO WAKE!!!


 Sote tunafahamu kuwa kunywa maji wakati unakiu ni burudiko la nafsi inaloleta usawa wa akili… ingawa wako watu wanapenda kutumia maji ya moto (maji yasiyo ya baridi) na wengine watapenda kutumia maji ya baridi lakini katika yote la msingi ni kazi ya hayo maji katika kuleta burudiko katika mwili wa binadamu na afya………….japo wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa kunywa maji sio mpaka uone kiu bali ijengeke kama utaratibu wa maisha yako!

Ni kweli hata kama utaamua kunywa maji kwa kufuata utaratibu wako au kunywa maji kwa kufuata utaratibu wa wataalamu lakini hauta kunywa zaidi ya kiu yako, na kwa kufanya hivyo itakuwa tofauti katika ujazo kati yako na mwingine japo wote mnaweza kuwa na kiu lakini bado mtakuwa tofauti katika utoshelevu au katika kukidhi matakwa ya kiu.

Na pindi unapojua ujazo wa maji utakao tosheleza kiu yako basi bila shaka utachukua maamuzi sahihi katika kujipimia ujazo unaostahili na wakati mwingine hali hii inaweza ikaokoa upotevu wa fedha, muda na hata matumizi mabaya ya maji kama vile kiasi kinachobaki ukawaza kuyamwaga na wakati ungejipimia kiasi chako hicho kiasi kitakachobaki kingewafaa wengine.

►Ninapozungumzia kiu na zungumzia jambo lilo zaidi ya hili, sio kiu cha maji tu bali hali sahihi katika utekeleza wa jambo liwe gumu au jepesi  hama liwe jema au baya basi tunapaswa kuangalia na kulitatua katika hali stahiki au katika mazingira stahiki.

Pindi unapoamua kuukata mti na ukaweka bidii katika kuyakata matawi yake tu ukijua utauangusha huo mti na hatimae usiote tena pasipokuangalia tabia za huo mti na uwezo wa mizizi katika kujikita katika ardhi…………….unaweza kuonekana kuwa unaakili sana pindi utakapo kuwa unaukata matawi ya mti lakini pindi matawi yatakapo anza kuota tena basi utaonekana kumbe juhudi yako yote ilikuwa bure!

Ni wazi jambo linaloumiza kichwa na hata moyo pindi utakapoona tatizo ulilonalo hakuna njia sahihi katika kutoka hapo baada ya kujaribu kila njia ya kutoka pale ulipo……tatizo kama tatizo uwa hakuna mtu analipenda na lipo katika kila mazingira na katika maeneo mbalimbali mathalani kanisani,shuleni na katika familia.

►Tatizo lolote liwe mahali popote ukubwa wake na udogo wako utegemea nguvu maarifa yako na zaidi sana utayari wa ufahamu kukubali kuenenda na wimbi la kimbingu ambalo Mungu atakuagiza katika utekelezaji katika kuliondoa tatizo.

Watu wengi wanapenda kuchukulia kuwa tatizo na kuona kuweza kulitatua kwa njia moja mathalani ukali, ukimya au kupotezea hasa jambo linapokuwa uwezo wa akili yako!! Niseme kuwa hali hii sio stahiki kwa kila utatuzi wa kila tatizo.

Yako matatizo ambayo yanaisha kwa mtu kukutana na mshirika mwenzake,rafiki na mwengine kueleweshwa vizuri na mwingira kujaliwa na mwingine kukutana na uongozi wa kanisa na mwingine kukutana na mchungaji wake!

Lazima kila tatizo lipatiwe utekelezaji unao stahili ukikosea kufuata utaratibu wa kulitatua tatizo ni wazi kabisa alitaisha litadumu kwa muda wote hata tatizo lilikuwa dogo au kubwa…..kama ilivyo katika hesabu nyingi uwezi kupata jibu sahihi kwanza formulary (kanuni) iwe sahihi na uweze kuitumia iyo kanuni basi bila shaka utapata jibu lililo sahihi.

►Yapo matatizo kutokana na namna lilivyo linahitaji kiongozi au mchungaji fulani ajishushe au amue tu kuwa mkweli alafu mambo mengine yatakuwa sawa hata bila kuomba sana au kuwaza vibaya.

Yako matatizo mengine ni lazima upoteze thamani yako kwanza ili uweze kuungamanika tena na hatimae kulitatua tatizo.
Ni pende kusema kwamba tatizo lolote lina sifa kuu mbili

i.kukua
usipoamua kulichukulia kwa umakini na kutaka liishe kabisa kwa gharama yeyote bila shaka litakuwa kubwa na hatimae unaweza kushindwa hata kulitatua na ukajuta hata kusema kwamba ningelijua ningelimaliza mapema.
Tatizo linaachwa pasipo kuangalia kuwa jambo hili linaisha au linaendelea kuwa kubwa kwa kutokua makini unaweza ukakuta jipu likapusa hata usijue limepasukia wapi na namna ya kulitibu lisiwezekane tena.
Ushauri wangu kila tatizo linategemea utatuzi sahihi ili liweze kuisha na sio bora utatuzi tu kwakua sio kila tatizo linatatulika katika njia moja!

ii. kupungua
hili ni jambo jema sana tatizo linaweza kuisha kwa ukimya, kuongea au kupeana zawadi na ndio hatua nzuri ambayo inahitajika kwa waliotofauti katika jambo lolote.

Lazima ujue kuwa tatizo linapungua kwa kudhamiria kulipunguza na hatimae kulimaliza kabisa hilo ni jambo jema kuwa mnaweza kulimaliza japo katika kulimaliza mnaweza msiendelee katika kufanya jambo moja.

Kwa Mungu ni jambo la hatari sana……..ole wake akwazikae na ole wake asabishae makwazo!!!

Tatizo linakuwa sio tatizo tu ukiipata njia sahihi ya kulimaliza tatizo na sio kila njia inatakiwaitumike katika kutatua maadam ni njia! Sio kweli.

Kutafuta njia sahihi ya kumaliza tofauti zenu hapo ndipo tunasema hapo ndipo kutafuta kwa bidii kuwa na amani na watu wote.

►Tatizo kubwa linakuwa pale ambapo hakuna mtu anajihesabu kuwa ni mkosaji wote wanaona wamefanya vizuri hivyo wanapaswa kuombwa msamaha.

Kiu ya maji haiwezi kumalizwa na juisi!! Hizi kiu mbili tofauti kamwe hazina mbadala……!!!!

Tafuta njia sahihi huku ukiwa tayari kujishusha na kukubali kosa na hakika utakuwa salama katika yeye………….zaidi sana Roho mtakatifu atakujulisha moyo watu na kukupa utatuzi wake bila ya kukosea.
Nikisema siku njema nitakuwa sijakosea!!!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………….0764 018535

Jumanne, 28 Julai 2015

JICHO LANGU NDIO MAAMUZI YANGU



JICHO LANGU NDIO MAAMUZI YANGU



 Kile ninachokiona ndicho nitakachoamua sio kile ninakachokisikia!

Hakuna kitu kigumu kama maamuzi na hakuna kitu chepesi kama maamuzi ila inategemea maamuzi haya yamebebwa na nini na yanahusu nini?

Katika uwanda wa mwanadamu kuamua jambo ni dhana pana kuna maamuzi yanatokana na kushawishiwa na maamuzi yanayotokana na busara za mtu husika………..mwisho wa siku yote yanajulikana ni maamuzi yaliyo amliwa na mtu kwa utashi wa mtu husika.

Wako watu wameacha kazi,rafiki,jamaa na hata kugombana na wazazi kwasababu ya kuambiwa maneno na kuyaamini na hatimae kuchukua maamuzi ya kuacha hama kuendelea, maamuzi yanayotokana na kuambiwa yamekuwa na nguvu sana kwakua tunaishi katika dunia ambayo hatujui yote hivyo tunahitaji kusikiliza wengine katika kuchukua maamuzi na tunahitaji kuishi kwa amani na ndugu wanaotuzunguka,

Niseme hata kama wewe mwenyewe  uliwai kuamua maamuzi pasipo kushuhudia mwenyewe ila katika ushawishi wa maneno nikutoe hofu wewe si wa kwanza……hata adam alipoulizwa na Mungu kwanini umekula tunda alisema ni huyu mwanamke uliyenipa…..!!!

Japo matokeo yake yamekuwa ni athari si kwao hata katika ulimwengu sasa na mengi yanatupata kutokana na maamuzi ya hawa watu wawili.

Hakuna kitu kizuri kama kuamua maamuzi yaliyobebwa na ushuhuda wa macho yako na sio ushawishi wa upande wanje! Kwakua maamuzi yanakupa nguvu na kukupa ujasiri katika mwenendo wako, ukweli maamuzi mengi tunayo yafanya kiukweli sio katika maamuzi yaliyobebwa na ushuhuda wa macho yetu. Usipende kuwa na maamuzi yakushinikizwa usio na muono wako binafsi kwamba hivi nasikia au kuambiwa mambo ambayo ya na ushuhuda wenye nguvu katika macho au wakimazingira! Pasipo uhakika wako mwenyewe.

Wako watu waliopoteza Baraka zao na ushindi wao kwa kuambiwa na kushawishika na watu wengine pindi mtu husika anapoamua kumshilikisha mtu jambo lake………….mathalani biashara imeenda vibaya wanaokuzunguka au uliomshirikisha anaweza kusema kuwa uliyenaye sio mwaminifu hivyo vunja nae huo mpango kwani hata kuzidi kukurudisha nyuma maendeleo yako na wewe kutokana na usadifu wa mazingira na nguvu ya ushawishi kwa mtu ukaweza kuamua sasa mimi basi acha niangalia upande mwingine!

Maamuzi yaliyobebwa na macho yako…. kiukweli yanakuwa hayana unafiki wala ushawishi wa mtu au chochote kwakua unakuwa na ushahidi wa kutosha sana ambao moyo wako unakushuhudia kuwa uko salama na sifa kubwa katika maaamuzi haya uwa haya ambatani kabisa na uzushi kwakua kile unachokifanya unakiamini.

Haya ni maamuzi yanakufanya kuwa mkweli na kuwa halisi sana katika kile unachoamua na bila shaka dhamira yako inakuwa haina hatia kwakua kile unachokiamua ni kwa ajili ya kujenga wakati wako katika uzuri.

Nipende kusema kuwa hakuna maendeleo ya kweli kama ukiwa unaamuliwa mambo yako nawe kisha unafuata na kamwe hawezi kwenda mbele japo utaongeza miaka!

Maamuzi ya kuaamliwa yanakuweka katika maisha ya utumwa ambao hutaweza kutoka katika utumwa huo kama utachukua maamuzi bila ya kuheshimu maamuzi yako binafsi kwakua wewe ndio unatakiwa kuonyesha unaijali na kuithamini kesho yako.

Bila shaka ukiwa unaendelea na utumwa wa maamuzi sio rahisi kuungamanishwa na Mungu hata kama ahusiki mkumbuke adamu hata alivyojitahidi kujitetea lakini hakusikizwa tena kwakua Alisha kula tunda ambalo Mungu aliigiza lisiliwe lakini yeye katika ushawishi wa mwanamke ambaye Mungu mwenyewe aliluhusu awe nae.

Mungu amekupa akili akaweka wazo na akakupa kuamua hivyo mtendee haki Mungu kwakuendeleza kile alichokianzisha ndani yako!!!

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………..0764 018535

Jumatano, 15 Julai 2015

CHAKULA CHAKE NI MAUMIVU YA.......................



CHAKULA CHAKE NI MAUMIVU YA MUNGU


 Sote tunajua kuwa chakula ni kitu muhimu sana kwani pasipo chakula uhai uweza kutoka hivyo tunavyokula chakula inasaidia kuustili uhai ambao Mungu ameweka ndani yetu uzidi kuwepo  chakula ni kitu kizuri na muhimu sana  kwani katika hiki tunapata uwezesho wa kuishi na kuona fahari ya maisha yetu katika kukizi mahitaji ya mwili (katika hili mwili unakuwa na nguvu) na kujisikia kuwa ni mtu kama watu wengine!!

Nazungumzia chakula kama kitu cha msingi katika maisha ya mwanadamu kwani mtu anaweza kukosa mavazi, malazi akaishi lakini kamwe sio chakula kinachoweza kusababisha viungo vya mwili kufanya kazi na hata kufanya utendaji wa mwili kuwa mzuri!

Kwa utafiti wangu mdogo binadamu anaweza kukaa siku nyingi bila nguo akawa salama na kuendelea kuishi lakini sio kushindwa kula katika siku hizo na kuweza kuendelea kuishi ila yesu pekee ndiye aliyeweza kukaa siku arobaini bila kula!

Ni kubali wazi kuwa binadamu hatupo kwa ajili ya chakula ila chakula kipo kwa ajili yetu….hivyo hatuna budi kukitumia kwa ajili ya kujenga afya njema ya miili yetu.

Kisayansi wanasema muonekano wa mtu uonyesha au udhihirisha kiwango au ubora wa chakula anachokula.

Ukweli kwamba mambo mengi ambayo yanafanyika katika dunia, yawe mambo mema na hata yasiyo mema mwisho wa yote yanakamilishwa na jambo au kitu kinaitwa chakula kwa ajili ya kuridhisha mwili katika kuupa matumaini ya kuendelea kuishi!!

Wako watu wanashughulika katika maisha yao ya kila siku kwa ajili yao na wengine kwa ajili ya familia zao, na hata kwa ajili ya ndugu na jamaa wanao wangalia…..ukweli ni seme kuwa katika mambo yanayoweza kuumiza kichwa sana kwa mtu mwenye majukumu ya kuwa hudumia jamii inayo mzunguka na hasa familia inayo mtegemea ni pale anapokosa uwezo wa kuwapa chakula!
Mambo mengine yanaweza yaka simamishwa kwa mtu baada kugundua kwamba uhakika wa chakula haupo au ni mdogo…..hata mzazi anapotaka kumpeleka mwanae shule jambo ambalo linampa furaha sana ni kuona kwamba mtoto wake ana uhakika wa kula vizuri tena katika hadhi anayopaswa!

►Ni seme hili ni jambo muhimu sana lakini katika jamii yetu imekuwa ni tatizo hasa pindi uwezekano wa chakula hicho kutopatikana na ijulikane wazi ninapozungumzia chakula rafiki yake mkubwa ni fedha.

Katika kukidhi mahitaji yake binafsi au familia yake mtu anapokosa kuona uwezekano wa kupata fedha kwa njia iliyo sahihi na kukidhi mahitaji ya familia yake lolote linaweza fanyika!

Wamekuwa watu wakiuana kwa ajili ya kupata fedha na kukidhi mahitaji ya familia zao hasa  wenye uwezo huo lakini kwa wengine wamekuwa wakijiingiza katika shughuli zingine kwa ajili ya kupata fedha katika kukizi mahitaji yake na familia yake kubwa ni chakula moja wapo ya shughuli hizo ni ujangili, ujambazi, utapeli na hata ukahaba!

Wengi wanaofanya shughuli hizi sio kama wanapenda bali yote ni katika mbio katika kufanikisha mahitaji katika familia yake na yeye muhusika.

Watu wamekuwa wakiuuza miili yao ili wapate fedha kujikimu katika maisha yao watu hawa wanafanyakazi kama wanapenda lakini ukweli ni mateso katika maisha yake!

Japo wako wengine wanafanya shughuli hii pasipo kuwa na uhitaji huu hasa hawa si wazungumzii kwakua hawa wanahitaji kitu kingine ili kiwasaidie lakini katika wale ambalo hawanauchaguzi hayo yamekuwa maisha yao na zaidi sana yamekuwa ni maumivu ya Mungu!

Katika makusudi ya Mungu katika kumuumba mwanadamu hajawai kufikiria kusudi la mtu kuuza mwili wake ili kujikim mahitaji yake na familia yake….bali yote haya kwasababu mwanadamu ana utashi wa kufanya chochote ila matokeo yake kamwe huwezi kuyabadili yanakuja sawa na ulivyofanya.

Ni pende kusema kuwa bado unanafasi ya kufanya vizuri na kuwa bora kwa Mungu kwa mtu ambaye anaye husika maisha yake katika kuuza mwili wake bado unaweza kuwa bora na kuwa wa maana hata kuliko unavyofikiri.

Chukua nafasi hii kwa wewe unayesoma kuwa mwema kwa watu wa jinsi hii kufanya kuwa duniani ni mahali salama ambapo yeye anahitajika sana na sio kumuonyesha UPENDO tu! Bali aweze kuona YESU kuwa ndiye mtoshelevu wake na sio kitu kingine!

Mungu hajawai choka, hata choka na kamwe hawezi kuchoka kwa mtu anayempenda bila shaka ni wewe!

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………..0764 018535

Baraka za Mungu zipo kwa ajili yako!!

Jumatano, 24 Juni 2015

NAOMBA JANA RUDI



NAIOMBA JANA

Unaweza kuzani kuwa ni kama ndoto au kitu ambacho akiwezekana kwani sio kawaida mtu kuomba jana irudi! Lakini ni jambo ambalo watu wanaomba ila wakati mwingine inakuwa ngumu sana kuirudisha jana ikawa leo au kesho ikawa jana kwakua imeshapita na mbaya zaidi inakuwa imepita na mambo yake ila inaacha alama ambayo kuonyesha kuwa ilishapita!

Mtu anaweza kuomba ombi hili endapo tu atakapo ona leo yake imekuwa ni tofauti na vile alivyotegemea yamkini aliona kutakuwa na manufaa zaidi lakini mwisho akaona hakuna unafuu wowote zaidi ya majanga na mateso tu wala hakuna unafuu wowote hivyo utamani kuona jana mrudie tena ili aweze kufanya tena maaamuzi yatakayo mmletea mwanga mzuri!

Sio jambo jema sana kwa mtu kukumbuka watu waliotangulia (kufariki) kuona kama wangekuwepo leo nisingekuwa hivi nilivyo japo uwezi kuzuia hisia za mtu kutokana na kukosa mahitaji fulani na hivyo kupelekea katika hali duni au isiyopendeza macho pake!

Katika swala hili wako watu ambao wanaiomba jana irudi kutokana walicheza/awakufanya vizuri pindi alipokuwa shule,au akumthamini mtu fulani na hatimae akawa bora kuliko yeye…pia wako watu wanalia juu ya viungo vyao baada ya kupoteza kwasababu mbalimbali mathalani ajari katika kazi au safari za kawaida wengine wamepoteza miguu,mikono na hata macho na wengi wao wanatamani sana kama siku zao zingejirudia tena wangefanya vizuri zaidi ya vile walivyofanya.

Katika jana kuomba irudi kuna wako watu walio wakimbia wenzi wao kwasababu mbalimbali zikiwemo umaskini, wakizamani, hana muonekano wa kuvutia au hajakizi vigezo vyake hivyo awezi kuendana nae na pindi baada ya kumwacha yule na kwenda kwa wengine hali huko ikawa mbaya sana na kutamani yule wa mwenzi wa mwanzo arudi tena kwake na wakati mwingine inakuwa ni ngumu tena kuirudia jana kwani mazingira yanaweza yasiruhusu tena katika kurudiana………….ikabaki kilio tu na kujilaumu tu na zaidi sana kuwa na maisha ya majuto siku zote.

Unaweza kuona kuwa ni kitu rahisi ukikaa na kutafakari kwa haraka pasipo kina basi bila shaka lakini ikifika kipindi jana yako ikawa mbaya na usione mwanga wa kutokea ndipo hapo utaanza kuyakumbuka yote ya jana pasipo kujali mapungufu yake na unaweza ukaishia kutamani tu lakini usiweze kuibadilisha jana ikawa leo au sasa!

Bila shaka kilio cha mtu au huzuni ya mtu uongezeka sana pindi anapoona ubora wa jana ulivyo tofauti na leo yake kwani ule utoshelevu wa jana haupo tena………lakini inakuwa ni furaha kwa mtu ambaye hakika jana yake ilivyokuwa ngumu sana na sasa leo yake imemjaa kicheko ambacho akina kikomo kamwe

Ni kweli walio wengi wanacheka leo inategemea sana maandalizi yao ya jana lakini sio wote wanalia leo jana yao hawakujiandaa inawezekana walijaandaa lakini hawakufikia lile lengo walilo kusudia au changamoto ikaibuka katikati akashindwa kutimiza ndoto yao.

Ni kweli maisha yako ya nyuma yana mchango mkubwa sana katika maisha yako ya sasa kwani yanaweza yakaweka nuru au giza… hivyo kusema kila dakika unayo itumia ni mbegu matunda yake utayaona pindi muda wa kuchipua utakapofika!

Utakiwi kuishi maisha ya hofu sana ilikutaka kuwa na kesho isiyoihitaji leo irudi tena bali katika yote unachohitajika kuwa na maarifa sahihi katika kila jambo unalo lifanya acha kufuata mkumbo haijalishi nani yupo katika huo mkumbo bali heshimu maamuzi yako na kuyazingatia kwani huo ndio utambulisho wako…………kwakua kila kitu kitakachokutokea kitafanyika furaha kwako au hasara kwako kwanza kabla ya kutokea kwa mtu mwingine au katika jamii husika.

Unaweza kuwa wa maana kama ukisimamia kitu cha maana na unaweza usiwe wa maana kama hauta simamia kitu kisicho cha maana yote inakutegemea wewe na sio jirani yako! Tengeneza ajabu yako kuwa kweli na halisi sana.

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson………………………………………………0764 018535