ULINZI WA AKILI YAKO;
Unapoona huyu amekuwa wa kwanza na huyu wa mwisho,
unapoona ona huyu kajenga na huyu kapanga, wote wana virusi vya ukimwi huyu
anaishi kwa uhuru na huyu anaishi kama kifungoni, huyu ana afya na huyu hana
afya, huyu ndoa yake inaimarika zaidi katika changamoto na mwingine ndoa yake
imevunjika, wakati mwingine huyu anaomba kwa uchungu na huyu anaomba kwa furaha
yote haya yana jumuisha matumizi ya akili.
Akili inaitaji afya njema mbali na mwili japo wengi
hawawezi kukupongeza unapokuwa na afya ya akili kuliko ya mwili, lakini ukweli
ni kwamba akili inahitaji afya ili iweze kutekeleza utendaji wake kwa ufasaha
pasipo upingamizi wowote kama vile ili utembee vizuri kuwa na mwili ulio vizuri
lakini katika yote akili isipo kuwa na afya njema kuna shida itatokea katika
maisha.
Katika maisha ndani ya dunia ya leo tunaona umakini
mkubwa unapewa namna ya kutunza mwili wako ili kujikinga na magonjwa yanayoweza
kukuathiri na kuleta mateso katika mwili wako na hatimae kudhoofika, lakini
ulinzi katika akili yako ni kitu cha msingi sana ambacho unahitajika sana ukipe
kipaumbele
Kwa kiasi kikubwa sana mateso ya watu yanasababishwa
na kukosa ulinzi katika akili yako mimi nilikuwa na rafiki yangu ambae matokeo
hayakuwa mazuri japo hakutarajia alijipa moyo na maisha yakawa yanaendelea
lakini maneno yasiyo faa yaliyokuwa yakisema juu yake kutokana na kutofanya
vizuri katika matokeo yake ya kidato cha nne kuwa ni mzembe, mbona ndugu
wengine walifaulu haya maneno yalikuwa yakijirudia kichwani mwake hatimae
mwisho wake akapata ugonjwa wa akili na mpaka sasa anaendelea na matibabu
muhimbili.
Ni akili pekee inayoweza kukutambulisha kuwa uko
wapi na unafanya nini au una hali gani? Majibu yote yanatokana na akili sio
masikio au kitu chochote, na ni jambo la kawaida mtu anaweza akakusuma
ukadondoka na baadae ukarudi tena katika
hali ya kawaida lakini pindi tu utakaposhindwa kuweka ulinzi katika akili yako
kuna maneno mengine unayoambiwa yanaweza sababisha shinikizo kubwa katika
maisha yako.( kutokana na maneno na sio matendo/kitendo).
Kile kinachokubalika katika akili yako ndicho
kinachopelekea utekelezaji, wako watu waliojinyinga kutokana na maneno tu au
waliokimbia na hata kujitenga na jamii zao kutokana na maneno tu yaliyoweza
athiri akili yake kwa kiasi kikubwa,mathalani baba yako anakwambia neno
gumu(nimekuchoka sasa unaweza kwenda, umenichefua sina radhi nawe au najuta
kwanini nimekulea) haya ni maneno ambayo yanaweza kuathiri akili yako kwa kiasi
kikubwa hata ukakosa maana ya jambo lolote zuri linaloendelea katika maisha
yako.(kama kweli unajipenda basi hauna budi kuulinda akili yako isi haribiwe na
majanga mbalimbali) na ni vizuri utambue kuwa kila mtu anaakili yake hivyo kila
mtu anawajibika kuilinda akili yake na sio ya mtu mwingine.
Akili ni ufunguo unaoweza ruhusu jambo liingie
katika moyo na jambo lisiingie katika moyo kwa maana uamuzi wa jambo hili
limebebwa na akili na sio jambo lingine.
Hakuna kitu kizuri kama kufanya jambo katika akili
iliyotulia kwa maana inaleta ufasaha na umairi katika utendaji wako, na akili
isipotulia inapelekea mwili kukosa ufanisi na umairi wake katika utendaji wako
ni bora uishi katika utumwa wa mwili kuliko kuwa mtumwa wa akili unakuwa zaidi
ya kichaa,teja au mtu asiye jitambua.
Kila kitu ilikiedelee kuwa bora na cha maana sana
hakina budi kitunzwe katika hali stahiki na isiyo na mwendelezo usiofaa, hivyo
akili ni kitu muhimu sana tunaona watu wakiheshimika kutokana na namna
wanavyotumia akili yao na wako watu ambao wanazalaurika kutokana na matumizi ya
akili zao.
Nailindaje akili
yangu?
Kila mtu upenda kuona ustawi wa akili yake siku
baada ya siku ila japokuwa ili akili iweze kustawi na kuwa bora siku hadi siku
kupenda pekee yake au kutamani haisaidii sana bali ni lazima utambue kuwa ni
nalo tatizo hili na ni wajibu wangu kuhakikisha akili yangu inastawi kwa
kutambua kuwa ustawi wa akili yako ndio ustawi wako.
I.umakini
katika kile unachokisikia
Unasikia nini kinaweza kukutengeneza nawe ukawa vile
sawa na unachokisikia, ni seme wazi sio kila unayo yapenda basi yanaleta afya katika
akili yako bali ni yale yaliyoshihi ambayo unatkiwa kuyasikia kwa ufasaha ili
kuimarisha ufahamu wako kuhusu Mungu.
Wakrito tumekuwa huru kusikia kitu chochote pasipo
kujua matokeo yake na pindi matokeo yake yanapokuwa mabaya tunajiraumu au
kurahumu watu wengine pasipo kujua kuwa ni zao ya kile tunachopenda kusikia.
Yesu alisema;…..jiangalieni sana jinsi msikiavyo!!!!!
Namna unavyosikia ni muhimu sana kwakua kinakujaza
na hatimae inaweza kukupeleka sawa na maneno hayo yanavyotaka.
II.changamko
la kweli ndani ya moyo wako(furaha isiyo na mipaka)
Biblia inasema;…changamko la moyo ni dawa ya mifupa!!!
Hakikisha furaha inakuwa ni maisha yako katika ajira
yote ahuitaji kuogopa bali unahitaji kuzidi katika kumwamini Mungu pasipo
kuchoka wala kukata tamaa.
I wathesalonike 5: 16-18
Kwa kila jambo linalokutokea jifunze kumuona Mungu
sana kuliko zaidi kuliko shetani maana ndivyo Mungu anataka uone.
Tamani kuona furaha yako ikawa nguvu katika maisha
yako na hata wengine utakiwi kuchoka katika kuzidi kumwamini Mungu.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
MUNGU
AKUBARIKI SANA……….!!!!!!!!!!