IKO WAPI THAMANI?
Torati
24:19-22(22).
Unaposikia neno thamani ni neno lenye radha ya
tofauti sana yenye kuvutia ambayo kila mtu anataka awe nayo kwani ndani ya
thamani kuna heshima, kupendwa na hata kupewa nafasi unayo stahili ……………………………………………………………………………
niko hapa kuchukua nafasi hii kwa ajili ya shukrani kwa kutumia muda wako
katika kusoma kwa kadili ya Mungu atakavyo kusaidia. Tumeona ustawi
ulioambatana na neno hili na furaha pamoja na majonzi ya kitokana na neno hili.
Ni neno ambalo limebeba maana zaidi ya vile unavyojua na kuamini bali neno hili
limekuwa na ujazo wa maana iliyo kamili ambayo sio rahisi kutambua kwa maana
moja bali ni zaidi ya vile unavyofikiria.
Neno hili kwa sasa limepoteza maana yake hile halisi wako kwani
Mungu alitoa thamani yake kubwa kwa mwanadamu kuliko ardhi na Mungu ameonyesha
thamani hiyo kwa kumtoa yesu kwa ajili ya wanadamu. Mungu akufanya kitu
chochote akakipa thamani kuliko kuliko mwanadamu. Lakini sisi wanadamu sasa
tumegeuza kinyume kile alichopewa thamani na Mungu sasa hivi akina thamani tena
bali kile kisichopewa thamani kimepewa. Hivi sasa katika dunia ya leo vitu
visivyo na stahili vimekuwa na thamani kuliko vinavyotakiwa mfano sasa
ardhi(mavazi, nyumba, na magari) imekuwa na thamani kuliko mtu/mwanadamu. Sasa
hizi sio ajabu mtu kusikitika kwa kupote gari au nyumba kuliko binadamu.
Mwanzo
1:1-31
Yohana
3:16
Ni wazi maana ya neno hili linategemea na mtu husika
katika uelewa wake na sio kitu kingine mbali na yeye kuna mgawanyiko wa thamani;
i)kitu
kinacho shikika mathalani furniture za nyumba, gari na mali kwa ujumla.
ii)kitu
kisicho shikika mathalani utu, afya na muonekano.
******************************************************************************
Japo katika dunia tuliyonayo
hakuna kitu kibaya kama kuishi uku akijitoa thamani au akiwa hana thamani,
unaweza kukaa mahali popote penye kila kitu lakini mahali hapo patakuwa pazuri
au pabaya pindi utakapo tambua tu hapa nilipo hakuna thamani haipo. Hili neno
ambalo limeleta shida sana katika dunia ya leo,hakuna mahali utapenda kukaa
kama tu unajua hapa thamani yangu imepotea au haipo.kwani thamani ni zaidi ya
fedha au jambo lolote kwa maana nyingine hakuna mbadilishano wa chochote
ukaendana sawa na jambo hilo, unaweza weza ukapewa fedha nyingi sana lakini
pindi utapo tambua hapa sina thamani basi hapo utakuwa huna amani. Wapo wengine
kwa kutokana kujua thamani yake hapo imeisha mahala fulani upelekea kufanya
hata yasiyo faa katika jamii mfano mtu uweza kuingia katika ulevi wa kupindukia
mbali na yote alikuwa anatakiwa afanye. Tumeona mahali ambapo mtu anapotambua
kuwa thamani yake hipo hata kama akiwa mgonjwa basi uweza kupona hata kabla
hajaanza matibabu, usiombe uwepo mahali ukatambua mahali hapa ulipo sina
thamani utakuwa kama umemebebeshwa mzigo zaidi ya chochote na uhuru hapo
unakosekana kabisa hivyo uimara wako ukosekana kabisa. Mahali ambapo utajua
hapa nimekosa thamani utaweza kuishi maisha ya utumwa usiyo ya penda. Katika
dunia tuliyonayo wako watu wana kesha mchana na usiku kutafuta heshima(thamani)
katika kupigana kwa njia yoyote pasipo kuangalia matokeo yake ya jambo hilo
anaweza kudanganya hata kuiba ili mradi tu aendelee kuthaminika mathalani wako
watu hata wajaribu kutoa miili yao kwa kusudi waendelee kuwa na thamani pasipo
kujali kama anaweza kupata maradhi ya kuathiri afya yake. Watu wengine
usianisha thamani katika familia bora, afya njema , mavazi na mausiano mema.
Katika mambo hayo lazima tukubali kuwa kuna thamani
ambayo inatokana kwa wanadamu na thamani ambayo inatoka kwa Mungu, hizi ni
thamani tofauti sana kwani thamani ya wanadamu inakuwa pale tu unapokuwepo au
unapohitajika lakini thamani ambayo haitokani na wanadamu hii ni thamani ambayo
upo au haupo bado unakuwa nayo na uwa haitaji watu wakusemehe bali ile thamani
yenyewe inajidhihirisha na kuwa mwanga katika giza lolote.
Wakati mwingi watu wamekuwa wakiusihanisha thamani
na KIBALI kinatoa mwanga katika giza nene kwa thamani inapodhihirika basi
kibali kinafuata, hivyo kibali na thamani ni mapacha wasioachana. Thamani
ikishuka basi kibali kinapungua na thamani ikipanda basi kibali kinapanda.hivyo
ukiachana na thamani basi umeachana na kibali moja kwa moja.
Kila mtu anafurahi sana pindi anapoona thamani yake
inajengwa katika misingi ya utu na sio vile analivyonavyo, japo ki ukweli
katika dunia tuliyonayo tuna thaminiana pale tuna potoa kitu au tunapokuwa na
kitu mbali hapo thamani inakuwa ya mashaka au yawasiwasi kwani tumeona
mmomonyoko wa mausiano kutokana kushuka au kupungukiwa kifedha.
Ndani ya jamii kuna njia au kanuni ambazo
zinazofanya thamani ya mtu ipande au ishuke ndani jamii kuna hatua za kufuata
mathalani mfumo wa elimu kwa ukamilisho wake, kiwango cha elimu ndicho thamani
yako lakini kanuni hii inavunjwa mtu anapokuwa na hela (biblia imesema hekima ya maskini haisikilizwi). Na pia ziko mila
ambazo ukizifuata basi katika jamii fulani basi thamani yako inapanda mathalani
jando na unyago ( kutoka hatua fulani kwenda hatua nyingine iliyo bora). Pamoja na hayo pia
kuna namna ya thamani inaweza kuongezeka kwa namna ya Mungu iliyo sahihi na
iliyo bora na ndio njia muafaka.
Ni kweli huko usemi usemao kwamba watu tuko thamani
sawa mbele za Mungu hiyo haimaanishi tu kwa namna unavyofikiria tu bali ina
maanisha kuwa wote tuna nafasi sawa lakini namna unavyoitumia hiyo nafasi
ndivyo utakuwa na hiyo thamani katika kuongezeka au kuipoteza na hii inaendana
sawa wote mnana nafasi ya kusoma pamoja lakini matokeo yanatoka katika madaraja
i ii iii iv inamtegemea mwanafunzi husika na sio usawa tena.
Ni vizuri kutambua kuwa thamani sio vile ulivyonavyo
bali ni vile ulivyo wewe binafsi pasipo kuhusishwa na chochote, wewe kama
ulivyozaliwa na sio ulivyokuwa navyo mara baada ya kuzaliwa kwa kua hivyo vipo
pia vitatoweka.
MUHIMU;
Yako mambo mawili ya msingi katika kuelewa na
kuthamini katika usahihi ulio sahihi ulio na manufaa kwa Mungu na kwa ustawi
wako.
I.Elewa thamani ya mwanadamu kwa misingi ya kimungu
Mwananadamu chimbuko lake ni Mungu hivyo kumwelewa
Mungu ni kujua thamani ya mwanadamu kutokana na yeye na sio dunia inavyotoa
thamani. Wakati wote dunia utoa thamani kwa maslai( kama hauna kitu hauna
chako). Kama wakristo japo tunaenenda katika dunia hii lazima tusamini na
kuweka misingi ya mwanadamu inasimama katika misingi yake.
Japo duniani yeye Mungu anaweka miguu yake anahitaji
usalama uweze kudumu katika wanadamu kuthaminiana katika msingi yake na sio jingine.
Hatumfurahishi Mungu kwa kuishi tu bali kufuata na kuheshimu utaratibu wake.
Tambua gharama yote ambayo Mungu ameiweka katika
kuitengeneza dunia ni kwa ajili ya makazi bora ya mwanadamu, hivyo ujue kwamba
Mungu kwa jinsi ya ajabu anayompa thamani mwanadamu kwa misingi yake.dunia ni
kazi yake na mtu yeyote mwenye akili hayuko tayari kuona kazi yake inapotea
mbele yake.
Ni vizuri kutambua kuwa misingi hii ya thamani
inajengwa na neno la Mungu na sio maneno ya watu yanayobadilika. Mpaka pale
thamani ya Mungu itoke ndani yako kwa nguvu na kwa ukamilisho wake katika namna
yake.
Thamani ya Mungu ni Pendo la Mungu
Uelewa ulionao wa kuhusu Mungu unadhihirika sana
katika utendaji unaendana katika neno la Mungu( usiishi kama mbingu unataka
kwenda mwenyewe hata wengine wasipoenda haina shida)
Tamani sana kuona unashamiri katika misingi ya
kimungu katika uelewa wa thamani ya mwanadamu maana hali hiyo italeta uimara na
umaana wa jambo la kimungu katika utendaji wako.
II. Dhihirisha uelewa wako katika utendaji
Wafilipi
2: 3-11(9)
Pasipo
udhihirisho katika utendaji hatuoni umaana wa wewe kujua au utofauti wa kati
anaye jua na asiye jua unakuwa uko wapi. Watu hawamuoni Mungu katika ufahamu
wako bali kile kinachotoka katika ufahamu ndicho hatari na tishio katika katika
ulimwengu wa nyama na wa roho.
Watu
ujifunza sana mahali ambapo unapoonyesha katika utendaji wa kuonyesha thamani
ya mwanadamu mwenzako kujua iko juu kuliko chochote.
Furaha
yako iwe mwendelezo na sio kucheka kusipo kuwa na uhusianishwa na moyo katika
dhamira njema iliyobeba Mungu.
Mathayo 15:8
Tamani sana watu wajifunze katika mwenendo ulio safi
na wakujenga thamani ya UTU kuliko chochote.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
THAMANI YAKO INAKUWA MBELE ZA MUNGU SAWA NA VILE UNAVYO
THAMINI
Kwa
vile nakujali muda si mrefu nitaachia audio ya fundisho
hili……barikiwa!!!!!!!!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni