UIMARA WA MIZIZI YENYE UBORA;
Mathayo
7: 24-27
Hapa atuzungumzii tu mizizi bali tunazungumzia
iliyoimara iliyonauwezo umkubwa katika kukiwezesha kitu hicho kiendelee kua
mahala pale.Ni jambo la kawaida kwa usalama wa mtu au kitu utegemea wapi
umegemea au uwezi wa mtu anayekukinga, wako watu wanaitwa wanajeuri ya
fedha,waliojizindika au wenyekujuana na watu wenye uwezo au mamlaka hivyo uona
yuko salama katika vigezo hivyo.
Unapoona uimara wa kitu chochote kimedumu kwa muda
mrefu tena katika mafanikio mafanikio makubwa jua kuna uimara katika
utawala,hivyo unapoona maafa yoyote jua sio muonekano wa nje wa kitu bali ni
vile ndani kulivyobomoka.uimara wa nje hauna shida sana bali unategemea sana
uimara wa ndani( mtu anaweza akaharibika sana katika muonekano wa nje lakini
kama ndani pakiwa na uimara basi kuendelea kupo lakini ndani pakiwa apaeleweki
nje hata paking’ara vipi muda si mrefu mpolomoko utatokea muda si mrefu.
Mti unapokuwa umenyauka matawi lakini mizizi bado
imara basi hapo panakuwa na matumaini ya matawi kustawi lakini ikitokea mizizi
ikatwe basi tambua hapo matawi yatanyauka hata kama sasa yanaonekana
yanaonekana yanavutia ila kwa sababu tu kinachofanya ustawi wa tawi na shina
akipo basi kinachofuata hapo ni anguko la tawi.
Sipo hapa kuelezea sayansi ya mizizi kwenye mti la
hasha! Bali niko hapa kuleta somo hili
UTENDAJI WA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YA MWAMINI
Vile unavyoelewa utendaji wa Roho mtakatifu katika
ufasaha mzuri ndivyo inakupa kibali na nguvu katika maisha ya ukristo.
Utendaji(Operation) ya Roho mtakatifu ndio uimara wa mkristo pasipo hilo
hauwezi ukawa na ukristo wenye nguvu na kibali kwa Mungu. Uwa ninapozungumzia
nguvu na kibali kwa Mungu ni vitu viwili tofauti kwani uanapozungumzia nguvu ya
Mungu inadhihirisha katika fundisho na hata kuponya wagonjwa lakini hivi
vinauweza kosa kibali kwa Mungu, maisha yenye kabali kwa Mungu yanaweza yasiwe
na kibali na watu ila hicho cha Mungu kimebeba utoshelevu ulio timilifu.
Utendaji huu hupo katika nguvu ya kumsikia Roho
mtakatifu na kumwelewa ili kuleta utendaji wako ufanane au uwe sawasawa na yeye
atakavyotaka sio vile unavyojisikia bali vile alivyopanga kwa kusudi lake.
Katika biblia Roho mtakatifu kapewa nafasi kubwa
sana katika ulimwengu wa sasa yesu anasema naenda ili aje msaidizi ( yohana 15:
26-27).
Wote wanaoongozwa na Roho mtakatifu hao ndio Mungu
uwatambua kama watu wake. (
warumi 8: 14).
Watu wengi wanaposhindwa kuendelea mbele tu ni vile
mizizi yao haina uchambuzi ulio imara katika Roho mtakatifu,kwani namna unavyo
endelea kutumika na Roho mtakatifu ndivyo unavyozidi kuwa imara na kuimalika
katika yeye kwani kumtambua Roho mtakatifu katika mapana zaidi ndio ushindi wa
kuzidi kutembea nae pasipo.
Isaya 66: 2(b)
Mtu anaposhindwa kutembea katika maisha ya ushindi
na hatimae kukata tamaa ni vile mizizi yake katika Roho mtakatifu sio imara
yenye nguvu iliyojikita sio katika mazoea bali kwa hofu na kutetemeka mbele za
Mungu siku zote.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
NURU YA BWANA IKUANGAZE………………!!!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni