MUNGU ASHUGHULIKI NA
MAMBO MEPESI bali ushughulika na
magumu;
Yoshua
4: 19-24
Yoshua
6:1-2
Wakati yeriko imefungwa kwa ajili kuwazuia israel hapo Mungu anasema” Tazama nimeutia yeriko
mikononi mwako”Mungu anaonyesha kuwa mahali ambapo yoshua alikosa ufumbuzi
bwana anaonyesha kuwa hakuna uwezo utakao pingana na uwezo wake.
Ni wazi swali hapo linakuja kichwani mwako nikutaka
kujua yapi mambo mepesi na yapi mambo magumu na kwanini yamekuwa magumu na
kwanini yameitwa mepesi ni katika vipimo gani vimetumika katika kupima hili,
ondoa shaka kama bado unaendelea kusoma basi utapata maana ya haya maneno haya
kwa ufasaha tu.
Kwanza nichukue fulsa hii kukushukuru kwa muda wako
katika kuutumia katika kusoma ujumbe huu, naamini utakubariki sana na kuwa
maisha yako katika kuongeza maarifa na kuuimarisha imani yako hatimae kuujenga
ufalme wa Mungu na kuushangaza ufalme wa giza.
Kama binadamu unapitia mambo ambayo akili yako
inapata changamoto na kwa wakati fulani unahisi akili yako inazidiwa au
kushindwa kumudu ilo jambo ambalo linakukabili au lililokukabili.na hata
kukupelekea kwa akili yako kuchushwa sana hatimae nafasi kufikia hatma ya
kutoendelea kwa vile ilivyokuwa au ilivyo.
Katika dunia tunayoishi ni kawaida jambo ambalo
limekuwa uwezo wa akili wa nje wa akili yao binafsi imepelekea kuabudu hata
kuita eneo hilo kuwa maaalumu kwa ajili ya ibada mathalani eneo ambalo maji
yanapanda mlima, maji kuwa na moto kwa muda wote hata pasipo kuona moto
unaoleta uo moto na vitu vinavyoendana na mambo hayo.
Mambo yaliyo ndani ya uwezo wa kibinadamu hicho ni
chakula cha binadamu bali yale mambo yaliyo kuwa magumu ni chakula cha Mungu.mambo
magumu yanaonyesha uwezo wa akili ya Mungu na mambo mepesi yanaonyesha uwezo
mdogo wa akili ya kibinadamu.
Ni wazi tu kuwa Mungu anaweza yote na anafanya yote
ila yako mambo ambayo yanamdhihirisha sana na yako mambo ambayo hakuna kitu
kitakachoonyesha watu wamuone Mungu zaidi kuliko yoyote.
Wakati ugumu unapotawala hapo sio wakati wa kuuliza
maswali mengi ambayo unafikiri hayana majibu bali ni wakati wa kufurahi ili
kumpisha Mungu aweze kutenda. Tangu mwanzo wa biblia hadi ufunuo hakuna jambo
ambalo Mungu alilikusudia likashindwa kutendeka HAIJAWAI TOKEA HAITAKAA
ITOKEE!!!!!!!!!!
Mungu anasifa ya kujitukuza hivyo mambo ambayo akili
yako inashindwa kuyapatia ufumbuzi au kuyabeba ndipo hayo ya kuonyesha utukufu
wake kwa namna yake na kwa nguvu yake lazima wanadamu ashangae ili Mungu
aonyeshe uwezo wake sio wa kuigwa na kitu chochote. Agawani na mtu utukufu kwa
lolote kwakua utukufu wake unamtosha yeye na mwanadamu anakusudi lake.
Ni kweli kibinadamu tunapenda kuona Mungu
ashughuliki na mambo yote lakini ukweli sio kila jambo analolifanya Mungu akili
yako itatambua ni Mungu na kumpa heshima kama Mungu.
Yako mambo anayoyafanya Mungu lakini katika mambo
hayo bado unaweza kuktotambua kuwa ni Mungu kwa ufasaha wake mathalani
uhai,ulinzi,kuamka salama mambo madogo japo ni muhimu sana lakini wanadamu
wengi hawamuoni Mungu na kumpa heshima ambayo aliyokusudia.
Mathayo
6: 25-34
Yako mambo mengine yanakuwa ni magumu sana lakini
Mungu anayaweza kuyadhihirisha na kuyachia kwako hana lengo la kukukatisha
tamaa bali anakupenda sana lakini
anahitaji kuona namna unvyomshirikisha katika mambo yako.
Japo yako mambo ni magumu katika maisha yako ya
wanadamu ingawa yanatofautiana yaliyo magumu kwako sio yaliyo magumu kwa wenzio
ugumu kwa mtu unategemea akili yako umempa nafasi kiasi gani na sio ukubwa wa
jambo linalokukabili.
Mambo kuwa magumu ni ishara ya ubinadamu lakini sio
ishara ya Mungu, yeye ufanya yaliyo magumu kuwa mepesi.kwakua ndivyo alivyo na
ndivyo anavyo yaona mambo mbalimbali anayapima kwa kipimo chake na sio kipimo
cha jambo lolote.
Katika ubinadamu huwa atumuoni Mungu sana katika
mambo kama haya mathalani kuponywa mafua,kuponywa vidonda na mengine yaliyo
chini ya uwezo wa akili yako katika hali ni ngumu kumuona Mungu zaidi bali tuna
muona Mungu katika yale yaliyo zaidi ya uwezo wa kibinadamu.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
Mungu
anafanya yaliyo nj’e ya uwezo wa akili ya kibinadamu ili uweze kumwelewa katika
mapana mengine ( zaidi unavyoelewa) sio vile tu watu wanavyomuelewa……….
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni