NAFASI YA KUPOTEZA;
Hapa duniani katika mambo ambayo wanadamu wote
wangeungana kwa pamoja katika kupiga vita ni kupoteza(loose) hakuna mtu
anapenda kupoteza wala kutegemea kupoteza kwani katika kupoteza kumeleta
maumivu mateso na ukiwa miongoni mwa watu wengi, hili neno ni neno ambalo
alitarajiwi sana na watu wngi kutamkwa kwani ni neno ambalo aliinui moyo bali
linafanya moyo kuwa chini.
Hata mfanyabiashara yeyote anapotoa mtaji wake uwa
hatarajii kama kuna kupoteza kwakua ni matarajio yake katika kuongezeka, na
hili neno la kupoteza uwa linatokea katika hali ya kujua au kutojua kulingana
na hali iliyopo husika mathalani mtu anafanya shughuli pasipo na maarifa ya
kutosha.
Japo katika kupoteza kuna husika sana na nini
unapoteza ingawa yako mengine yakipotea yana kuwa na upande wa kukusaidia zaidi
au kuudhihirisha ule uwezo ulionao na mengine yanaweza kuacha pengo ambalo
litaweza kukusumbua kulingana na uelewa wako.
Unaweza ukajitaidi kuziba kila kona lakini kama kuna
upande umehusahau huo upande utachangia katika upande wa kukurudisha nyuma
mathalani unaweza kujenga nyumba nzuri sana lakini ukasahau kuweka mlango hivyo
hali hii inaondoa usalama wa mali ulizonazo na kuruhusu wezi kuweza kuchukua
mali zako na kupelekea kukurudisha nyuma jitiada zako katika kujiletea
maendeleo.
Japo kila mtu upenda aendelee ila usipo iangalia
mianya hiyo inayo sababisha usiendelee inaweza kukurudisha nyuma tofauti na
ulivyofikiri.
Katika makanisa mengi hasa wale wanao mwamini Mungu
wa kweli tena katika usahihi wamekuwa wanamalengo mazuri yenye kuinua ufalme wa
Mungu na kuaibisha ufalme wa shetani………..
Yesu alisema…….juu ya mwamba huu
nitalijenga kanisa langu ambalo milango ya kuzimu haitalijenga.
Uimara wa kanisa lake litajengwa katika misingi ya kristo mwenyewe ambacho
hakuna cha kumshinda na hii aliidhihirisha pale alipotoka msalabani na kukaa
katika ardhi siku mbili baadae ardhi ilimtapika kwa kua haikuweza kumzuia.
Lakini tunaona ndani ya kanisa la leo kunamambo
ambayo hayasadifu maneno maneno haya kwa kua ndani ya kanisa la leo kuna
udhihirisho mkubwa wa tabia za mwilini ,paulo
anasema kama ninyi watu mnaenenda kwa kufuata mwili ninyi si watu watabia za
mwilini ninyi…..
Ndani ya kanisa la leo kuna uasherati,uzinzi,uongo,
ubinafsi, choyo, maslai binafsi na mengine mengi……….( wagalatia 5; 19-21).
Ili kanisa tuweze kupona hatuna budi kurudi katika
misingi ya yesu tukiona na namna yeye alivyoishi na hatimae alishinda….!!!
I.ukamilisho
wangu unamtegemea mwingine
Japo biblia inasema tunayaweza yote katika yeye
atutiaye nguvu (wafilipi 4: 13)
haina maana maisha ya peke yako tu yataleta kuyafanya yote. Hata yesu
aliiwahitaji watu ili kuacha msingi wake uzidi kutawa katika dunia nzima.
Kama hauta tambua basi utakuwa ukipoteza atakama
unatuia nguvu nyingi kiasi gani kwani hauwezi kuyafanya yote mwenyewe.
Japo kunawakati ambalo unaweza ukahisi naweza
kufanya lolote hata bila ya kumwitaji mtu kutokana na vile unavyojiona lakini
ukweli tunahitajiana tena kwa muda wote sio wa kipindi fulani tu. (wafilipi 2:3). Mathalani mtu mwenye
hela anaweza jua kuwa anaweza fanya jambo lolote ila kuna mambo mengi atatambua
kuwa mimi na hela zangu bado sijitoshelezi katika kujikamilisha.
Kanisa ni kama mwili unategemeana mdomo ili kula una
mtegemea mkono na tumbo linaitegemea. Ni kweli kuna wakati unaweza usivione
vitu vikidhihirika katika muonekeno wako unaoutaka lakini katika yote tambua
vyote vipo ila shida inakuja katika kuvitambua na kuvipa nafasi mathalani mtu
asipotembea haina maana hana miguu kunawakati ana amua kuto tembea, na mtu
asipo ongea haina maana hana mdomo au yeye ni bubu…………!!!
Hili ni tatizo ambalo linakuwa ni shida kwa watu
wengi kuona kwamba wenyewe wanaweza tu maadamu wanafanya kazi pasipo kujali
kuwa paulo anasema kuwa ….pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.( 1wakorintho 12: 4-7 ) wote wanatenda
kazi lakini katika namna mbalimbali kadili ya Mungu alivyojalia na sio nani
zaidi. Mathalani katika ujenzi wa nyumba kunautendji kazi tofauti tofauti
lakini wote wanakusudi moja tu kuwa nyumba isimame.
Imeandaliwa na ;
Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
MTAMBUE MWINGINE NAYE AKUTAMBUE?
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni