Jumatatu, 21 Julai 2014

THE POWER OF CHOICE




NGUVU YA UCHAGUZI,

Kila uchaguzi uliotokana na maamuzi uwa kuna misingi inayojijenga ndani ya mtu yanayopelekea kufanya UCHAGUZI. Hiki ni kipindi ambacho hakina mfano na wala hakina tabia ya kujirudiarudia kwakua matokeo yake katika maisha ya mtu yanaweza kujenga hatima mpya ya mtu ambayo hakuwazwa wala kufikiriwa yaani inatoa mwelekeo mwingine tofauti na kule uliko kusudia. Ila uzuri wa uchaguzi huu uwa hakuna msukumo wa mtu unaoweza kukupelekea bali ni MSUKUMO TOKA NDANI YA MTU HUSIKA.

Hakuna kitu kibaya duniani kama nguvu ya uchaguzi, kwani uchaguzi ni mpasuko wa kitu kimoja na mwingiliano wa kitu kingine ambacho knajikita kwenye misuli,nyama na hata damu na kuishi ndani ya mtu kwa utayari wa mtu husika. Jambo hili linaleta giza katika mambo mengine na kupelekea nuru kwa ule uchaguzi alioufanya na aijarishi nyinyi mnaona giza yeye ataona nuru iliyo kali zaidi ya jua kali lisilo na mfano na hata ikitokea mnaona mabonde miporomoko na mito mikubwa yaani mambo yasio na matumaini kwa macho bado yeye ataona barabara iliyonyooka isiyo na kikwazo chochote na ikitokea watu wengi wanaona kucheleweshwa kwa safari yao lakini yeye ataona ni karibu saaaana kama sebuleni na chumba cha kulala. 

Ukitaka kuona mtu haogopi hata kufa ni pale tu utakapokwenda kinyume na uchaguzi wake hali hii uweza kuwa tayari kukabiliana na chochote pasipo kuangalia nguvu alizonazo kulingana na kile kitu ambacho anakwenda kupambana nacho uwezo aliokuwa kutokana na uchaguzi alioufanya uweza kuona anaweza kumuua simba kwa sekunde chache.

Ni kweli watu wanafanya uchaguzi kila mara na kubadilisha lakini hapa na zungumzia uchaguzi katika hatua ya juu saaana mathalani maamuzi yaliyo katika kilele cha mbingu maamuzi yanafanya mtu kubadili muonekano wake kabisa na wakati mwingine unaweza ukaona afadhari kichaa kwakua anaweza akapona lakini si kama mtu aliyefanya maamuzi thabiti ya kuchagua mtu huyu inakuwa bora ukutane na simba anaweza akaacha alama watu wakajua kutoka na damu au masalio ya nyama au mifupa basi wanaweza sema kuwa hapa kuna mtu kauwawa kuliko kusimama kinyume na mtu katika uchaguzi wake kwakua anaweza akakumaliza asibakishe ata ishara yeyote wala watu wasijue kama kuna tukio limefanyika.

Kusimamia jambo kwa mtu ndio ishara ya nguvu ya uchaguzi wa mtu juu ya jambo fulani kwaiyo uchaguzi wa mtu uimara wake unategemea kiwango cha uchaguzi. Sio kila jambo unatakiwa ufanye uchaguzi wa kiwango cha juu kama hiki lakini ni vyema utambue kuwa uimara wa uchaguzi uweza kukupelekea uthabiti wa mafanikio unayo yatamani na wengi wa watu uwa tunashindwa kutimiza ndoto zetu kwakua hatuja fanya maamuzi ya kula kiapo cha kutorudi nyuma na akili zetu pamoja na damu zetu zikakubaliana na hilo kuwa ndio maisha yako sasa ulio ya chagua pasipo kushurutishwa na mtu yeyote. Nguvu ya uchaguzi sio jambo la kuamua tu bali ni nguvu uliyonayo katika kuhakikisha uchaguzi ulioufanya unakuwa wa kufanikiwa katika maana iliyo bora na iliyo ya mwendelezo wa kudumu.

Hili ni jambo mtu anaye amua kufanya uchaguzi wa namna hii uwa anakuwa ni mtu aliyeamua baada kukaa chini na kuhesabu gharama zake za uchaguzi huo na kisha akachukua huo uchaguzi akiwa ana akili timamu akijua anafanya nini na yuko tayari kupambana na chochote ambacho akitakuwa rafiki wa kile anachokiamini au alicho kichagua muhusika. Watu wenye aina hii ndio rahisi kuabiliana na bahari halafu bahari ikapisha njia. Kwa maana nyingine nguvu ya uchaguzi ndio umekuweka leo mahali ulipo kwakua uchaguzi wako pamoja na juhudi zako zikakupelekea kuwa katika mazingira mengine ambayo ndipo ulipo leo.

Hili swala aliitaji sana maombi bali ubinafsi wa uliochukua uchaguzi wa kujitoa sadaka ili tu aweze kufanikisha uchaguzi wake kama vile alivyopanga kwa uhakika zaidi pasipo kuona haina ya shaka. Uchaguzi huu haujui asilimia ya kushindwa bali unatambua uko uwezo wa kushinda tu hivyo faili la kushindwa uwa linakuwa limetupwa nje na wala hakuna ushawishi wowote wa ishara ya kushindwa ni kama mnyama mkali aliyejeruhiwa saaana na baada kutoka hapo na kuta kulipiza kisasi huwa haoni kama kunauwezekano kushindwa kutimiza hazma yake kwakua alichokiamua anajua kuna kushinda tu wala hakuna jambo lingine.

Kwa watu wapembeni mnaye muona mtu huyo mnaweza kuona mtu huyu kwa uchaguzi alio ufanya ana hatarisha sana maisha yake hivyo mngeona ni bora ahuache lakini yeye uwa haoni vile mnavyoona bali anaona vile sawa na uchaguzi wa nafsi yake ilivyo mtuma. Na uchaguzi huu uwa haungalii mzazi rafiki au mpenzi bali umetawaliwa na utashi wa mtu husika akiwa katika hali ya kujiamini na akijua kile anachofanya ndicho sahihi na ndicho alichpaswa kufanywa hivyo apaswi kuingiliwa na mtu katika yale anayoamua kuyafanya kwakua anaamini ni sahihi sana kuliko ushauri mwingine wowote.

Haya ni maamuzi au uchaguzi uliotoka katika misuli ya ya moyo wa mtu na huku damu ikiwa ni shahidi kwa hilo kwa maana nyingine akiipa nguvu hali ya mwanadamu katika maamuzi aliyoyachukua kwakua kwa anaamini ni ka ajili ya pumziko la nafsi ambayo ikipata pumziko inakuwa ni burudiko kwao. Haya maamuzi hayafanani na mtu katika kuwa tayari katika kujitoa mwanga bali ni haya maamuzi yanafanywa hata watu wengine hawawezijua badala yake uona matokeo na hivyo ujua kuwa kumbe mtu huyu alikuwa anakuelekea huku hivyo upatwa na mshangao tu lakufanya alijulikani tena kwakua limeshatendeka hivyo wako watu watakao lia na wengine watahuzunika na wengine kutowatambua kuwa wana lia au wanahuzunika na wengine watakuwa wa kicheka kulingana na aina ya tukio na matokeo yake.

Katika hali hii ya uchaguzi mtu huwa haogopi kifo bali ujali ule uchaguzi aliouchukua kwa mwendo wake utegemea tu uchaguzi wake utakavyompeleka na sio jambo lingine mtu uweza kukabili kifo pasipo mashaka yeyote kwakua anatambua kuwa kifo sio kizuizi kwake kutokana na uchaguzi alioamua. Pindi utakapokutana nae mtu kama huyu ambaye ameshafanya uchaguzi wake kwa ukamilifu basi kuwa mwangalifu sana pindi unazungumza nae kwakua ni mtu ambaye anachokihitaji kwa wakati huo.

Mtu wa namna hii usitegemee hata siku moja hata kaa ajutie maamuzi yake/uchaguzi wake kwa kua katika kufanya jambo hilo alikuwa la siku moja bali mizizi ndani ya moyo wake umekuwa ukikua siku baada ya siku tena katika utaratibu wake mpaka akachukua maamuzi hayo tayari pamesha kuwa na majadiliano ya kutosha na tayari pamekuwa na mwingiliano ulio thabiti kwa kile alicho kiamua yaani nyama, damu, mifupa na hata misuli hivyo tendo linalo toka hapo linakuwa na kishindo kisicho kuwa cha kawaida ni zaidi ya anguko la mlima everist.
  

   Imeandaliwa na;
                 

                                    Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                




TUMIA NGUVU HII KATIKA KUJIIMARISHA NA SIO KUJIMALIZA,

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni