MKRISTO AZALIWI BALI ANAANDALIWA;
Ni kawaida mtu uweza kurithi tabia toka kwa wazazi
na hata muonekano wa namna ya kutembea,kusema na namna nyingine nyingi. Lakini sio swala la mkristo
Swala hili alina uhusiano ulioko kati ya damu na Mungu bali ni roho ya mwanadamu na Mungu
hivyo sio swala la kulichukulia katika kawaida.
Ni kweli mtu iliafike duniani ni lazima azaliwe
tukiachana na Adamu na Eva ambao ndio mama na baba wa wanadamu wote hapa
duniani.
Hii ni kauli ambayo inawezakuibua maswali mengi
kuhusu vipi kwa mtu ambaye alizaliwa katika familia ya baba na mama wote ni kristo, ukweli ni kwamba mkristo sio
swala la kurithishana na wimbi la watu wengi.
Japo unaweza kuzaliwa katika familia ya kikristo
haina maana ya wewe kuwa ni mkristo uamuzi wa kuwa mkristo au kutokua mkristo.
Hili swala aliendi kwa mkumbo bali linahitaji maamuzi ambayo yanatokea baada ya
kuelewa kwa ufasaha zaidi.
Kwa maana nyingine ukristo ni kujitambua mwenyewe na
kumtambua Mungu kwa uhalisia wake.
Kwa kusema hivyo unaweza kutoka kwenye familia
yoyote halafu bado ukawa wa maana zaidi kama tu utakubali na kuwa tayari kwa
atengenezo hayo.
Sio swala ambalo unaweza kulichukulia katika hali ya
kawaida bali ni swala lililo na latofauti sana lenye nguvu sana wala alina
mfano wake.
Hivyo hauhitaji kujivunia kwa kutoka kwenye familia
inayo mwamini Mungu bali furahia kwakua wewe binafsi una mwamini Mungu.
Mungu anapokuangalia wewe uwa angalii kuwa wazazi
wako kuwa ni watu wanamna gani ili akufanyie kitu kwako japo anaweza kubariki
au kulaani kizazi cha kwanza hadi cha tatu.
Ili ufike kule Mungu anapotaka ufike ahitaji kuona
wazazi wako wamefanya nini bali ina kuangalia wewe kwakua wewe ndio hatma yako
mwenyewe.
I wafalme 6:12
Ni vizuri kuwa utambue kwamba Mungu ahitaji
ukoo/familia bali waliopo ndani ya familia kila mmoja na nafsi yake.
Mungu haitaji kuona fahari kwa watu wengine bali
anahitaji wewe binafsi ili aone fahari kupitia wewe na sio kitu kingine.
Wako watu wengi wamekuwa wa kiishi maisha ya kawaida
sana kwa kutegemea ukristo walio karibu nao mathalani utakuta watu hawaombi
wakitegemea wako watu ambao wataomba kwa ajili yao na kufanya mambo ya mtu
husika kwenda vizuri.
Kama kuna jambo ambalo ni maumivu ya Mungu ni kuona
wewe unaangalia wengine wakati yeye anakuangalia wewe kwakua ubora wako unakuwa
furaha kwa wengine au unakuwa ni nguvu kwa wengine.
Unapotegemea ulipotoka panauelewa kuhusu Mungu
ukaelemea hapo pasipo kujua Mungu anakuangalia wewe binafsi unaweza kushangaa
pindi tu YESU atakapo kuja utaona majabu yake na hapo utaanza kuona kuwa Mungu
ana angalia ukoo au familia au kitu gani hasa.
Biblia inasema,…..mwana hata uchukua uovu wa mama au
baba wala baba au mama hata chukua uovu wa mwana.
……..watakua wawili mmoja atachukuliwa mwingine
ataachwa.
Hizi kauli zote utaziona kwa uhakika pindi pale
kristo atakapo lichukua kanisa lake kwa macho yako utayaona mambo hayo kwa
uwazi wake.
Ni vizuri usisubiri hiki kipindi mpaka kitakapofika
ndipo uanze kujuta au kujilaumu bali ni utambue kuwa mkristo anayo nafasi ya
kuandaliwa/kutengenezwa akawa mkristo aliye sahihi mwenye hatari katika ufalme
wa giza.
Wokovu ni kati yako na Mungu na Mungu ananamna ya
kukuandaa ili wewe usifanane na Yule wala wale bali ufanane na yeye kwa namna
yake.
Tambua mtu kama wewe hajatokea wala hatatokea bali
ni wewe uko peke yako hivyo lazima ufanye mambo ambayo yatakutofautisha wewe na
watu wengine.
Mungu hanamfano wake bali ana utendaji wake wake kwa
mtu aliye tayari ili kupitia huyo haweze kumuona au ajionyeshe yeye alivyo
kupitia mtu husika.
Haijalishi umezaliwa wapi la muhimu kukumbuka ni
kweli umefanyika vile Mungu anapenda akuone wewe ukitoa chapa yake katika
ulimwengu wa sasa.
II wakorintho 5:17
Uhuru wa Mungu kwako katika kukutumia ni vile tu
ambavyo utampa uhuru wa kutosha kwa yeye kukuandaa kwa ajili ya kazi yake. Penda
yeye akufurahie wewe ili aone fahari kwake kwa kua yeye amekutengeneza.
Unapokuwa tayari Mungu yuko zaidi ya utayari kwa
ajili ya kukufanya kuwa kiumbe cha ajabu ambazo ataonyesha maajabu yake kupitia
wewe.
imeandaliwa na;
Nelson, Cothey – 0764 018
535 or cotheyn@yahoo.com
KILA LA KHERI…………..RAFIKI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni