Jumamosi, 28 Machi 2015
VILE ULIVYO
VILE
ULIVYO;
Vile
ulivyo ndio utofauti wa wewe na mwingine na huo utofauti
upo katika utendaji, mawazo, maamuzi na nguvu ya kutafsiri na hata muonekano.
Ukweli katika swala ambalo Mungu amelifanya na wanadamu wengi wanamshangaa sana
Mungu, ni utofauti uliopo kwa wanadamu kwa wanadamu kua japo wako wengi lakini
bado inakuwa ni rahisi kuwatofautisha kati ya mtu na mtu………… katika maeneo
ambao watu wanamuona Mungu kuwa ni mweza wa yote kwa utofauti watu katika kujiona utofauti wao
wenyewe.
Utofauti wa mtu na mtu
hiki ni kitu kizuri kwani inachangia kuona radha tofauti tofauti ya watu na
hivyo kuifurahia sana dunia katika utofauti huo japo sio wote wanafurahia huo
utofauti kwani wako watu wenye hali ya ubinafsi wanapenda wao wenyewe
wajitangulize pasipo kuangalia upande mwingine……….niseme kama mwili ili uweze
kuwa vizuri unahitaji kuwa na utofauti wa viungo japo vyote ni viungo kuna
mikono,miguu,masikio na kadhalika(n.k) lakini vyote ni vya muhimu sana hasa
kwakua vyote vinatambua kazi yake kwani kazi ya mikono haiwezi kufanywa na
miguu au kazi ya tumbo ikafanywa na mikono hivyo vyote vinategemeana na
vinahitajiana japo wewe mwanadamu unaweza ukavipa baadhi ya viungo heshima sana
lakini viko ambavyo havionekani mathalani MOYO lakini huyu ndio mwezeshaji wa
mambo mengine yaendelee kufanya kazi yake.
Moja ya watu kushindwa
kufika mbali kutoishi vile walivyo hivyokujikuta kuyafanya mambo ambayo sio
kazi yao nakufanya mambo ya kuwa magumu sana na wengine kumsingizia Mungu
anipendi kumbe sio kweli…….lakini utofauti ambao Mungu ameuachilia kwa kila
binadamu unakazi yake katika kufanikisha kusudi lake.
Ni seme wazi ili
ufanikiwe au ufanikishe katika yale yanayo kukabili ni muhimu uishi maisha yako
katika mwelekeo wa ishara ya uhalisi wako, wako wengi wanashindwa si kwasababu
wanavipangamizi vingi la asha! ni kwa vile tu hawajaamua kuwa vile walivyo bali
amekuwa akiishi kwa kufuata yale wengine wanafanya. Kama watu wote wange weka
juhudi katika kutengeza gari tu basi ndege zingetoka wapi? Au meli zingetoka
wapi? Ni wazi ule uwezo ulipewa na Mungu ukiutumia basi unaweza ukakupa matunda
ambayo unapaswa kuwa nayo…..ziko hazina ambazo Mungu ameweka ndani ili uweze
kuzitumia katika kuleta ufumbuzi katika dunia ya sasa.
Mazingira magumu……. hii
moja ya sababu ambayo inakuwa ni kikwazo katika kuonyesha au kutembea vile
alivyo kwa sababu hakuna urahisi wa mazingira au usaidizi wa mazingira katika
kufanikisha lile unalolikusudia, ni seme wazi ukianza kupiga mahesabu ya
gharama kama ujaanza kazi yenyewe basi itakuwa ndicho kikwazo cha kwanza katika
kufikia malengo yako na hakuna mtu aliweza kufanikiwa kama tu aliogopa gharama.
Lazima uchukulie kwamba
wewe ndie unatengeneza misingi wa wengine kufuata hivyo maumivu yako ni kwa
ajili ya ustawi wa wengine, kila ataye endeleza hawezi kukusahau kwani alama
yako itabaki hapo siku zote.
Muda wa kutambulika……swala
lakutambulika lisiwe kichwani mwako japo ndicho chanzo cha kukua na
kuongezeka(kufahamika), kwakua unafanya kitu ambacho kiko ndani yako yeye
aliyekiweka atakitambulisha na kukiweka hadharani na kuachilia kiu ya watu
kukitafuta na inaweza kuanza kwa mtu mmoja halafu kikaenea sehemu kubwa tofauti
na unavyofikiria.
Unapoamua kuitoa hazina
ya Mungu ambayo ameiweka ndani yako acha maswala
ya kujitanguliza au ubinafsi au mimi kwanza tamani kuona lile kusudi au
lile jambo unalolifanya kuwafikia watu na kuona ile fahari watu wanaifurahia na
kuipokea………kujulikana na kupata fedha hiyo sio kazi yako yuko anaye thamini
kile unachokifanya.
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………..0764 018535
Ijumaa, 20 Machi 2015
UTAMBULISHO WA KIMBINGU
UTAMBULISHO
WA KIMBINGU
Swala sio utambulisho
tu! bali unatambulishwaje? Wewe kama nani na katika hadhi unayostahili!
Ndani ya dunia ya sasa
kumekuwa na shida sana kwa baadhi ya watu kuwepo mahali Fulani alafu
wasitambulishwe kama anavyotaka japo pia wako watu ambao hawana shida sana
katika utambulisho,.wako watu wanaghaili kwenda mahali Fulani au kujuta kwa
sababu ya kutotambulishwa vile wanavyotaka,wako watu wanaanza kuchukiana na
kisilani kisa ametambulishwa ki kawaida sana kwahiyo mojamoja ufikiri ni dharau.
Uko urafiki na kushirikiana
kumekuja pale tu baada ya mtu kutambulishwa vizuri na pengine hata kupewa sifa
ambayo hakustahili na hivyo kujenga undugu na mashirikiano ya muda kulingana na
shughuli yenyewe, japo kutambulishwa hakuongezi hela wala hakupunguzi hela
lakini ni kitu cha kawaida tu ni kama kitu cha kutambulika na sio maana
nyingine ukiwa katika hali hii basi kama umesahaulika kutambulishwa bado
utakuwa na amani kwa kua unajua kama binadamu ni hali ya kawaida kupitiwa
lakini kisiwe chanzo cha maamuzi yasiyostahili.
Kila utambulisho
unakazi yake katika mazingira husika,na ina aminika kila hadhi ina heshima yake
mathalani bosi na mfanyakazi kila mtu anautambulisho wake na unanafasi yake,iko
raha ya dunia pindi dunia inapokutambulisha katika nafasi mbalimbali mathalani
rais,waziri,boss na hata manager kuna haki utazikosana kama usipotambulishwa
katika nafasi unayostahili kwakua heshima ya dunia utaikosa lakini endapo
ukatambulishwa basi utayapata yale unayopaswa kuyapata.
Ni kitu kizuri sana kwa
mtu anayestahili heshima basi na apewe heshima kutokana na hadhi aliyokuwa nayo.
UTAMBULISHO
WA KIMBINGU
Kuna utambulisho ambao
unatisha na unashangaza umebebwa na umesimamiwa na Mungu mwenyewe na sauti yake
inapotokea ardhi na mbingu vinatia muhuri kuwa vinashikilia katika kutekeleza
katika Mungu alichokisema, huu ni utambulisho wa kudumu kwani utambulisho
wowote unaweza kuwepo na kuonekana kama kama yeye aliye kutambulisha akiwepo
lakini utambulisho wa kimbingu ni utambulisho ambao hauna mwisho wala kikomo.
Uwezi kutambulishwa
bila kujitambua!!!
Mungu akujidhihirisha kwa watu ili mradi walikuwa
wanamtumikia bali yeye ujidhihirisha kwa Yule ambaye anatembea katika nafasi
yake kikamilifu.
Paulo
anasema……….Mungu alipoona vema kumdhihirisha mwanawe ndani yangu!
Haya aliyasema akiwa ameshakubali wito wake na
kuanza kutendea kazi na hivyo akaona namna Mungu alivyo jidhihirisha katika
utendaji wake wote na hakuna aliloshindwa.
Lazima utambue na nafasi yake kwanza na kuipa nafasi
katika utendaji wa hiyo na nafasi ili Mungu achilie kitu ambacho
kitaadhihirisha kile unachofanya sio kwa ajili yako bali ni Mungu mwenyewe
anahusika hivyo atajidhihirisha kujionyesha.
Watu wengi wanatumia muda mwingi kutamani na kuiga
na kujifanya kuwa sasa Mungu amejidhihirisha kwao lakini jua kwamba halisi na
kisicho halisi kitajulikana tu baada ya muda Fulani, kwa kilicho halisi
kitadumu kwakua ndicho kilichopo na kitakuwepo….kwa kusema hivi ni sema kwamba
udhihirisho unajitosheleza na walio rohoni tu ndio watakao utambua.
Wako watu wanapopata nafasi za juu kazini wanafikiri
Mungu ame wakumbuka hivyo kuonyesha kuwa Mungu amejitambulisha kwao lakini
mwisho watu hao wamejikuta wakitembea na bosi zao na mwisho kuwa mbaya zaidi
mathalani familia zao kuvunjika na magonjwa kushamiri katika miili yao.( sio
kila jambo jema linalokuja kwako limebeba hatma njema katika maisha yako)
Lakini utambilisho wa mbingu hauna hatima mbaya…..
kwani umejaa manufaa ya rohoni na mwilini kwa ukamilifu………..na hautaji
ujipendekeze ili ujidhihirisha bali ni wewe kutembea katika nafasi yako
aliyokupa halafu yeye atakutambulisha tu!
Imeandaliwa
na ;
Cothey Nelson………………………………………..0764 018535
Alhamisi, 12 Machi 2015
UMAKINI WA FAIDA
UMAKINI
WA AJABU,
UMAKINI unaweza sema ni
hali ya akili yako, macho yako na hisia zako zote kuelekea katika kile
unachoelekezwa katika kuelewa au kukifanya….kwa lengo kiwe sehemu ya maisha
yako, kwa maana nyingine umakini upelekea akili yako kula chakula chake katika
hali stahiki yaani maarifa.
Katika hali ya dunia ya
sasa neno Umakini limekuwa likitumwa kutokana na matokeo Fulani yaliyotokea
mathalani ukifanya vizuri jambo lolote au mtihani watu watasema alikuwa makini
sana katika kuzingatia katika yote aliyoelekezwa na watu wengine watasema
alikuwa ni mwanafuzi au mtu msikivu mwenye kuzingatia yote aliyofundishwa
LAKINI itokee upande wa pili ya kushindwa jambo Fulani watu watasema mimi
niliona mwenendo wake kwa vile ulivyokuwa nilijua matokeo yake yatakuwa haya na
wengine watasema yote hatayasiokuwa ya kweli wengine watasema alikuwa MZEMBE!
Lakini litakuja mtu mzembe yukoje na mtu aliye makini yukoje na ni kweli wote
walio makini ndio wanauwezo kufanya vizuri hili ni swali tu!
Si katai kweli umakini
ni chanzo kimoja katika kufanikiwa au kufanikisha jambo moja ambalo
umelikusudia, kwani umakini unakupa utaratibu ambao utaoheshimu na kuzingatia
japo kuwa unaweza kuweka mwenyewe kutokana maarifa uliyonayo. Na siku zote
chanzo cha kuwa makini ni lazima kuwe na lengo na hatua za kufikia hilo lengo.
Katika umakini kuna
kitu ambacho uwa kinasahaulika sana kuwa umakini haukamiliki bila UTAYARI maana palipo na
utayari basi hapo panautekelezaji ambao mwisho wake uleta matunda ambayo watu
utegemea sana baada ya kuungamanishwa na BIDII ambavyo ubeba juhudi na
uvumilivu katika kutimiza jambo ambalo liko mbele yake katika mazingira yeyote
katika kutimiza lile ambalo limebebwa ndani yake,
Lazima ujue kwamba
umakini ujengwa na utayari baada ya kukubali ndani ya akili yake…hapo ndipo
unaweza kusema huyu ni makini sana kwakua tayari dalili za utekelezaji zimeanza
kuchipua lakini umakini wa kusikiliza pekee yake sio kigezo cha kutosha cha
kusema mtu huyu yuko makini kwani anaweza badilika wakati wowote na kitu
kingine wakati wote.
Umakini ujengwa na mtazamo wa Yule unaye msikiliza na
namna akili yako inavyomtafsiri kutokana alivyo kwako namna anavyokuona na
namna unavyomuona, nguvu ya maarifa
uliyonayo ambayo yatakupa kuendelea kusikiliza ua kuacha kusikiliza na upendo wako kwa Mungu inayokupa nguvu
katika kumsikiliza mtu wa aina yeyote ili mradi kukipata kile ambacho
unachokitaka na kusudi au azma yako
katika kufanikisha jambo Fulani katika maisha yako.
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson…………………………………..0764 018535
Jumamosi, 7 Machi 2015
MUONEKANO
MUONEKANO;
Katika DUNIA ya leo
kama kuna vitu vinapewa kipaumbele basi muonekano wa mtu utakuwa una nafasi ya
kipekee sana, kwakua inaaminika namna unavyoonekana ndivyo heshima utakayoipata
hivyo kila mtu ujitaidi kufanya sawa na uwezo wake alionao kuhakikisha anakuwa
na muonekano unaovutia wako wanatumia fedha zao kununua madawa na mafuta aina
mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wana kuwa na muonekano mzuri na wako wanatumia mizizi ya miti au matunda
mathalani palachichi na mangine mengi na wengi wanafanya hivi ili kuhakikisha
kuwa wanakuwa na ngozi yenye afya inayo nawiri na kivutio kwa watu wote.
Jambo hili mwanzo
lilikuwa likishamiri sana kwa wanawake sana lakini sasa kumekuwa na mwamko
mkubwa kwa wanaume katika kutunza ngozi zao mithili ya mwanamke anavyotunza
ngozi yake na yote hayo ni katika kuwa maridadi kutokana na hilo ziko sabuni
zinazo amasishwa katika matumizi ili kutunza ngozi.
Ngozi inapokuwa haina
mvuto hiyo inakuwa simanzi sana kwa mtu husika hasa kwa mwanamke… furaha ya
ubora wa ngozi yake inakuwa haipo tena na wakati wote ujitaidi sana kutafuta
ufumbuzi wa tatizo hilo, kutafuta habari zinazousiana na tatizo alilonalo, hali
hii ni mbali na hali ya mtu kutaka kujichubua au kubadilisha ngozi yake.
Sas hivu si ajabu wa
mtu anayejua jinsi ya kutunza ngozi yake kuwa na marafiki wengi na wote hao katika
kufanikisha kila mtu katika lengo lake
kuwa ngozi yenye ubora iliyonawiri kwa ajili ya kumfanya kuwa kama mtu ambaye
anamuona anamuonekano ulio mzuri.
Ili ni jambo jema sana
lakini limekuwa ni moja ya janga katika jamii husika ndani ya jamii moja
wamekuwa wenye kujua kutunza ngozi na wako ambao hajui jinsi ya kutunza ngozi (
hawajitambui) na watu kuachana na wapenzi wao kwakua wameshindwa kuwa tunza
katika kuwafanya kuwa ngozi iliyo bora, hivyo pamekuwa na vikundi
tofautitofauti kulingana na hadhi ya ngozi zao.
Imeiibuka kasumba mbaya
kuwa mwenye ngozi nzuri basi huyo ana uwezo mzuri wa kiuchumi na yeye ambaye
ana ngozi ilidhoofika basi uchumi wake wake ni wa chini japo hali hii si ya
kweli lakini hali hii imepekea kuchukua maamuzi ambayo yataathiri maisha yako
ya baadae mathalani kuingia kwenye tabia za wizi,uongo na mengine mengi.
Nami na kubaliana
kabisa kuwa na ngozi yenye afya hiyo ni haki yako na kawaida ngozi nzuri
ujengwa na vitu vingi moja wapo ni MOYO WENYE FURAHA, pamoja na kuridhika. Ni
wazi pindi utakaposhindwa kuwa na moyo uliokunjuka hata ngozi yako inakuwa ina
makunyazi ambayo yatapoteza ubora wa ngozi yako japo sio wote wenye ngozi nzuri
mioyo yao imekunjuka ila kwa asilimia kubwa wale ambao mioyo imekunjamana basi
ngozi zao ufabaa na mambo mengine kama vile changamoto za maisha uyatima, kukosa
haki kushindwa kutimiza azma yako uliyoikusudia.
Japo umaridadi uficha
umaskini niseme tu! MUONEKANO WAKISASA NI MATOKEO YA TEKNOLOJIA NA SIO MPANGO
WA MUNGU, usikubali kuondoa utu kwa sababu ya muonekano na wala usiondoe utu
kwa mtu kwa sababu ya muonekano…………Mungu angalii muonekano bali MOYO ULIOMBEBA
YEYE.
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson……………………………………0764 018535
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)