MUONEKANO;
Katika DUNIA ya leo
kama kuna vitu vinapewa kipaumbele basi muonekano wa mtu utakuwa una nafasi ya
kipekee sana, kwakua inaaminika namna unavyoonekana ndivyo heshima utakayoipata
hivyo kila mtu ujitaidi kufanya sawa na uwezo wake alionao kuhakikisha anakuwa
na muonekano unaovutia wako wanatumia fedha zao kununua madawa na mafuta aina
mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wana kuwa na muonekano mzuri na wako wanatumia mizizi ya miti au matunda
mathalani palachichi na mangine mengi na wengi wanafanya hivi ili kuhakikisha
kuwa wanakuwa na ngozi yenye afya inayo nawiri na kivutio kwa watu wote.
Jambo hili mwanzo
lilikuwa likishamiri sana kwa wanawake sana lakini sasa kumekuwa na mwamko
mkubwa kwa wanaume katika kutunza ngozi zao mithili ya mwanamke anavyotunza
ngozi yake na yote hayo ni katika kuwa maridadi kutokana na hilo ziko sabuni
zinazo amasishwa katika matumizi ili kutunza ngozi.
Ngozi inapokuwa haina
mvuto hiyo inakuwa simanzi sana kwa mtu husika hasa kwa mwanamke… furaha ya
ubora wa ngozi yake inakuwa haipo tena na wakati wote ujitaidi sana kutafuta
ufumbuzi wa tatizo hilo, kutafuta habari zinazousiana na tatizo alilonalo, hali
hii ni mbali na hali ya mtu kutaka kujichubua au kubadilisha ngozi yake.
Sas hivu si ajabu wa
mtu anayejua jinsi ya kutunza ngozi yake kuwa na marafiki wengi na wote hao katika
kufanikisha kila mtu katika lengo lake
kuwa ngozi yenye ubora iliyonawiri kwa ajili ya kumfanya kuwa kama mtu ambaye
anamuona anamuonekano ulio mzuri.
Ili ni jambo jema sana
lakini limekuwa ni moja ya janga katika jamii husika ndani ya jamii moja
wamekuwa wenye kujua kutunza ngozi na wako ambao hajui jinsi ya kutunza ngozi (
hawajitambui) na watu kuachana na wapenzi wao kwakua wameshindwa kuwa tunza
katika kuwafanya kuwa ngozi iliyo bora, hivyo pamekuwa na vikundi
tofautitofauti kulingana na hadhi ya ngozi zao.
Imeiibuka kasumba mbaya
kuwa mwenye ngozi nzuri basi huyo ana uwezo mzuri wa kiuchumi na yeye ambaye
ana ngozi ilidhoofika basi uchumi wake wake ni wa chini japo hali hii si ya
kweli lakini hali hii imepekea kuchukua maamuzi ambayo yataathiri maisha yako
ya baadae mathalani kuingia kwenye tabia za wizi,uongo na mengine mengi.
Nami na kubaliana
kabisa kuwa na ngozi yenye afya hiyo ni haki yako na kawaida ngozi nzuri
ujengwa na vitu vingi moja wapo ni MOYO WENYE FURAHA, pamoja na kuridhika. Ni
wazi pindi utakaposhindwa kuwa na moyo uliokunjuka hata ngozi yako inakuwa ina
makunyazi ambayo yatapoteza ubora wa ngozi yako japo sio wote wenye ngozi nzuri
mioyo yao imekunjuka ila kwa asilimia kubwa wale ambao mioyo imekunjamana basi
ngozi zao ufabaa na mambo mengine kama vile changamoto za maisha uyatima, kukosa
haki kushindwa kutimiza azma yako uliyoikusudia.
Japo umaridadi uficha
umaskini niseme tu! MUONEKANO WAKISASA NI MATOKEO YA TEKNOLOJIA NA SIO MPANGO
WA MUNGU, usikubali kuondoa utu kwa sababu ya muonekano na wala usiondoe utu
kwa mtu kwa sababu ya muonekano…………Mungu angalii muonekano bali MOYO ULIOMBEBA
YEYE.
Imeandaliwa na;
Cothey
Nelson……………………………………0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni