Ijumaa, 20 Machi 2015

UTAMBULISHO WA KIMBINGU




UTAMBULISHO WA KIMBINGU



Swala sio utambulisho tu! bali unatambulishwaje? Wewe kama nani na katika hadhi unayostahili!
Ndani ya dunia ya sasa kumekuwa na shida sana kwa baadhi ya watu kuwepo mahali Fulani alafu wasitambulishwe kama anavyotaka japo pia wako watu ambao hawana shida sana katika utambulisho,.wako watu wanaghaili kwenda mahali Fulani au kujuta kwa sababu ya kutotambulishwa vile wanavyotaka,wako watu wanaanza kuchukiana na kisilani kisa ametambulishwa ki kawaida sana kwahiyo mojamoja ufikiri ni dharau.

Uko urafiki na kushirikiana kumekuja pale tu baada ya mtu kutambulishwa vizuri na pengine hata kupewa sifa ambayo hakustahili na hivyo kujenga undugu na mashirikiano ya muda kulingana na shughuli yenyewe, japo kutambulishwa hakuongezi hela wala hakupunguzi hela lakini ni kitu cha kawaida tu ni kama kitu cha kutambulika na sio maana nyingine ukiwa katika hali hii basi kama umesahaulika kutambulishwa bado utakuwa na amani kwa kua unajua kama binadamu ni hali ya kawaida kupitiwa lakini kisiwe chanzo cha maamuzi yasiyostahili.

Kila utambulisho unakazi yake katika mazingira husika,na ina aminika kila hadhi ina heshima yake mathalani bosi na mfanyakazi kila mtu anautambulisho wake na unanafasi yake,iko raha ya dunia pindi dunia inapokutambulisha katika nafasi mbalimbali mathalani rais,waziri,boss na hata manager kuna haki utazikosana kama usipotambulishwa katika nafasi unayostahili kwakua heshima ya dunia utaikosa lakini endapo ukatambulishwa basi utayapata yale unayopaswa kuyapata.

Ni kitu kizuri sana kwa mtu anayestahili heshima basi na apewe heshima kutokana na hadhi aliyokuwa nayo.

UTAMBULISHO WA KIMBINGU
Kuna utambulisho ambao unatisha na unashangaza umebebwa na umesimamiwa na Mungu mwenyewe na sauti yake inapotokea ardhi na mbingu vinatia muhuri kuwa vinashikilia katika kutekeleza katika Mungu alichokisema, huu ni utambulisho wa kudumu kwani utambulisho wowote unaweza kuwepo na kuonekana kama kama yeye aliye kutambulisha akiwepo lakini utambulisho wa kimbingu ni utambulisho ambao hauna mwisho wala kikomo.

Uwezi kutambulishwa bila kujitambua!!!
Mungu akujidhihirisha kwa watu ili mradi walikuwa wanamtumikia bali yeye ujidhihirisha kwa Yule ambaye anatembea katika nafasi yake kikamilifu.

Paulo anasema……….Mungu alipoona vema kumdhihirisha mwanawe ndani yangu!
Haya aliyasema akiwa ameshakubali wito wake na kuanza kutendea kazi na hivyo akaona namna Mungu alivyo jidhihirisha katika utendaji wake wote na hakuna aliloshindwa.

Lazima utambue na nafasi yake kwanza na kuipa nafasi katika utendaji wa hiyo na nafasi ili Mungu achilie kitu ambacho kitaadhihirisha kile unachofanya sio kwa ajili yako bali ni Mungu mwenyewe anahusika hivyo atajidhihirisha kujionyesha.

Watu wengi wanatumia muda mwingi kutamani na kuiga na kujifanya kuwa sasa Mungu amejidhihirisha kwao lakini jua kwamba halisi na kisicho halisi kitajulikana tu baada ya muda Fulani, kwa kilicho halisi kitadumu kwakua ndicho kilichopo na kitakuwepo….kwa kusema hivi ni sema kwamba udhihirisho unajitosheleza na walio rohoni tu ndio watakao utambua.

Wako watu wanapopata nafasi za juu kazini wanafikiri Mungu ame wakumbuka hivyo kuonyesha kuwa Mungu amejitambulisha kwao lakini mwisho watu hao wamejikuta wakitembea na bosi zao na mwisho kuwa mbaya zaidi mathalani familia zao kuvunjika na magonjwa kushamiri katika miili yao.( sio kila jambo jema linalokuja kwako limebeba hatma njema katika maisha yako)

Lakini utambilisho wa mbingu hauna hatima mbaya….. kwani umejaa manufaa ya rohoni na mwilini kwa ukamilifu………..na hautaji ujipendekeze ili ujidhihirisha bali ni wewe kutembea katika nafasi yako aliyokupa halafu yeye atakutambulisha tu!

Imeandaliwa na ;
Cothey  Nelson………………………………………..0764 018535

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni