Jumanne, 3 Machi 2015

USTAWI WANGU



USTAWI WANGU,



 Ni jambo la kuvutia na lakuleta burudiko katika MOYO kusikia neno hili USTAWI au kushamiri kwa jambo jema katika maisha yako. Katika hali ya kawaida sana si rahisi mtu kuelezea siri ya mafanikio yake au ustawi wake kwani ndani ya binadamu kuna neno au hali ya UMIMI. Japo ina weza kutokea kwa mtu kuelezea kile ambacho yeye kimemfanikisha kama ni kitu cha halali au anaona huyu ni mtu sahihi wa kumwambia jambo na katika kusudi maalum kamavile kumshawishi nae aende katika njia ambayo yeye yuko.


***Nawe kama rafiki yangu ninajaribu kushirikiana na wewe katika jambo hili jema likionyesha imani yangu,nguvu yangu,tegemeo langu na matumaini yangu kuhusu dira ya maisha yangu ya kila siku katika nafsi yangu.

Kutoka 19:5…biblia inasema
“sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kwelikweli, na kulishika agano langu,hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu”

Kuna nguvu siri kubwa sana katika kumsikia MUNGU kwani yeye ndie muunganishaji wa yote ambayo unayafikiri kuwa ni shida katika ufahamu wako,lakini yeye anaweza kukuungamanisha na mali,rafiki na hata maajabu ya dunia ila ni kwa ajili ya utukufu wa jina lake.

Napenda kusema na kukubali kumsikia Mungu sio jambo la kawaida wala lele mama kwani ni namna Mungu anakutoa katika utumwa na kukupeleka katika uhuru wake sawa na vile anavyotaka yeye katika mpango wake.

Yohana 8:32…biblia inasema
“tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru”

Hivyo hapa kuna mambo mawili kuna kuifamu kweli hali ya ufahamu kupata kuelewa neno la Mungu kwa kusudi maalum, kuwa huru kuwa nje ya migandamizo ya nguvu za giza na kuwa tahayari kwa kusudi la Mungu tu, na sio kitu kingine.

Swala kubwa watu wengi ukazania kufanikiwa lakini swali linakuja nani anayekufanikisha kwakua huyo ndie anaye beba hatima yako, hivyo usifurahie kwakua tu ninafanikiwa bali misingi na uwezesho wa wewe katika kufanikiwa ni jambo la msingi sana.

Kuna ustawi wa mwili na ustawi waroho vyote ni muhimu sana katika maisha ya mwanadamu yeyote, kwani kuwa hivyo ndio unakamilisha kusudi la wewe kuumbwa na kuleta tija ya wewe kuwepo duniani na kuyafaidi ya dunia na hata ya mbingu.

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………………0764 018535
BAKI NA MUNGU ACHA VYOTE!

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni