VILE
ULIVYO;
Vile
ulivyo ndio utofauti wa wewe na mwingine na huo utofauti
upo katika utendaji, mawazo, maamuzi na nguvu ya kutafsiri na hata muonekano.
Ukweli katika swala ambalo Mungu amelifanya na wanadamu wengi wanamshangaa sana
Mungu, ni utofauti uliopo kwa wanadamu kwa wanadamu kua japo wako wengi lakini
bado inakuwa ni rahisi kuwatofautisha kati ya mtu na mtu………… katika maeneo
ambao watu wanamuona Mungu kuwa ni mweza wa yote kwa utofauti watu katika kujiona utofauti wao
wenyewe.
Utofauti wa mtu na mtu
hiki ni kitu kizuri kwani inachangia kuona radha tofauti tofauti ya watu na
hivyo kuifurahia sana dunia katika utofauti huo japo sio wote wanafurahia huo
utofauti kwani wako watu wenye hali ya ubinafsi wanapenda wao wenyewe
wajitangulize pasipo kuangalia upande mwingine……….niseme kama mwili ili uweze
kuwa vizuri unahitaji kuwa na utofauti wa viungo japo vyote ni viungo kuna
mikono,miguu,masikio na kadhalika(n.k) lakini vyote ni vya muhimu sana hasa
kwakua vyote vinatambua kazi yake kwani kazi ya mikono haiwezi kufanywa na
miguu au kazi ya tumbo ikafanywa na mikono hivyo vyote vinategemeana na
vinahitajiana japo wewe mwanadamu unaweza ukavipa baadhi ya viungo heshima sana
lakini viko ambavyo havionekani mathalani MOYO lakini huyu ndio mwezeshaji wa
mambo mengine yaendelee kufanya kazi yake.
Moja ya watu kushindwa
kufika mbali kutoishi vile walivyo hivyokujikuta kuyafanya mambo ambayo sio
kazi yao nakufanya mambo ya kuwa magumu sana na wengine kumsingizia Mungu
anipendi kumbe sio kweli…….lakini utofauti ambao Mungu ameuachilia kwa kila
binadamu unakazi yake katika kufanikisha kusudi lake.
Ni seme wazi ili
ufanikiwe au ufanikishe katika yale yanayo kukabili ni muhimu uishi maisha yako
katika mwelekeo wa ishara ya uhalisi wako, wako wengi wanashindwa si kwasababu
wanavipangamizi vingi la asha! ni kwa vile tu hawajaamua kuwa vile walivyo bali
amekuwa akiishi kwa kufuata yale wengine wanafanya. Kama watu wote wange weka
juhudi katika kutengeza gari tu basi ndege zingetoka wapi? Au meli zingetoka
wapi? Ni wazi ule uwezo ulipewa na Mungu ukiutumia basi unaweza ukakupa matunda
ambayo unapaswa kuwa nayo…..ziko hazina ambazo Mungu ameweka ndani ili uweze
kuzitumia katika kuleta ufumbuzi katika dunia ya sasa.
Mazingira magumu……. hii
moja ya sababu ambayo inakuwa ni kikwazo katika kuonyesha au kutembea vile
alivyo kwa sababu hakuna urahisi wa mazingira au usaidizi wa mazingira katika
kufanikisha lile unalolikusudia, ni seme wazi ukianza kupiga mahesabu ya
gharama kama ujaanza kazi yenyewe basi itakuwa ndicho kikwazo cha kwanza katika
kufikia malengo yako na hakuna mtu aliweza kufanikiwa kama tu aliogopa gharama.
Lazima uchukulie kwamba
wewe ndie unatengeneza misingi wa wengine kufuata hivyo maumivu yako ni kwa
ajili ya ustawi wa wengine, kila ataye endeleza hawezi kukusahau kwani alama
yako itabaki hapo siku zote.
Muda wa kutambulika……swala
lakutambulika lisiwe kichwani mwako japo ndicho chanzo cha kukua na
kuongezeka(kufahamika), kwakua unafanya kitu ambacho kiko ndani yako yeye
aliyekiweka atakitambulisha na kukiweka hadharani na kuachilia kiu ya watu
kukitafuta na inaweza kuanza kwa mtu mmoja halafu kikaenea sehemu kubwa tofauti
na unavyofikiria.
Unapoamua kuitoa hazina
ya Mungu ambayo ameiweka ndani yako acha maswala
ya kujitanguliza au ubinafsi au mimi kwanza tamani kuona lile kusudi au
lile jambo unalolifanya kuwafikia watu na kuona ile fahari watu wanaifurahia na
kuipokea………kujulikana na kupata fedha hiyo sio kazi yako yuko anaye thamini
kile unachokifanya.
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni