KIFO
SALAMA
Kwa kusema hivi
sichochei au siamasishi watu kufa au kuchukua maamuzi ambayo yataathiri maisha
yako pamoja na ndugu zako au wapendwa wako.
KIFO SALAMA hii ni
dhana ambayo kwa harakaharaka inaweza kukupa shida kwakua sio neno jema au
nzuri pindi unapolisikia kifo kwakua jambo hili lina usiana sana na kuushusha
moyo wako na hasa katika wale uwapendao na inasemekana sana ili jambo ndicho
chanzo kikubwa cha machozi,huzuni na simanzi isiyokoma.
Pange kuwa ni mahali
ambapo panauchaguzi ingekuwa ni vigumu tu watu kuelekea huku hata kama panaweza
kuwa ni sehemu salama sana, lakini kasumba hii inajitokeza pale kwakua hakuna
mtu ambaye ameenda huko na kutuletea habari za huko ili nasi tupate kuziamini,
hivyo ni jambo lililobeba mashaka na huzuni iliyo kosa majibu.
Kwakuanza ni seme wazi
tu katika maaana ya juu juu tu au maana ya kwanza kuwa hakuna kifo kilichokuwa
salama endapo ukiwa kama hauna Mungu ndani ya maisha yako na sio kuudhuria
kanisani (kuokoka), kwakua baada ya kifo ni hukumu kwa watatifu lakini kwa wale
hawakufuata nuru ya Mungu mateso ni haki yao………….sikutishi ila naongea ukweli
tu kwani Mungu apingani na maneno yake kama alivyosema ndivyo anavyo maanisha
na ndivyo itakavyokuwa
Yohana 3:36 inasema,…. amwaminiye mwana yuna uzima wa
milele; asiyemwani mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
Usijali kwakua nafasi
unayo yakumpokea kristo ndani ya maisha yako na kuishi maisha yaliyo jaa
usalama.
Katika maana ya msingi
hasa…………KIFO SALAMA ni maamuzi salama amabayo yatafautisha yale uliyokuwa
ukiyafanya nay ale ambayo unapanga kuyafanya au unayoyafanya huu ni utofauti
mkubwa sana na hakuna utofauti mkubwa kama huu wa KIFO na UHAI haya ni maamuzi
amabayo unayachukua kwa ajili ya kutimiza ndoto yako kama vile maiti haisikii
kile kinachosemwa na watu ndivyo hivyo inakuwa katika maaamuzi yako yanayolenga
kujenga ufalme wa Mungu katika ubora wake kwa ujumla.
Unakuwa na maamuzi
amabayo unajiungamanisha na kule unakokwenda na sio kule unakotoka ni kama
maiti anakuwa muungamaniko na kule nako kwenda na sio kule anakotoka, lakini
hali hii ni tofauti kabisa watu wengi wanachukua maamuzi katika hali wakiwa
wanatoa nafasi ya hivyo inakuwa ni rahisi wa mtu kurudi nyuma kirahisi.
Na amini ni Ngumu kama
hali yenyewe ilivyo lakini ukijitambua na kumpa Mungu nafasi ambayo
anayostahili, kwakua wako watu waliofika kama vile walivyoagizwa….mfano mzuri
Nuhu…mwanzo 6: 22,..Ndivyo
alivyofanya Nuhu,sawa sawa na vyote alivyomwamuru Mungu, hivyo ndivyo
alivyofanya.
Ki ukwali haikuwa rahisi kwa Nuhu ni maelezo machache
lakini yaliyobeba kujitoa kidhabiu kwa kiasi kikubwa sana na siri kubwa ni
kwakua alikubali kufa( kifo chenye manufaa).
Paulo anasema……….si mimi ninayeishi bali ni kristo
akaaye ndani yangu!
………..jambo moja nitakalo
lifanya ni kulisahau ya nyuma na kuchuchumia ya mbele!
Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535
CHAGUA
MAAMUZI SAHIHI KWA USTAWI WAKO.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni