UMAKINI
WA AJABU,
UMAKINI unaweza sema ni
hali ya akili yako, macho yako na hisia zako zote kuelekea katika kile
unachoelekezwa katika kuelewa au kukifanya….kwa lengo kiwe sehemu ya maisha
yako, kwa maana nyingine umakini upelekea akili yako kula chakula chake katika
hali stahiki yaani maarifa.
Katika hali ya dunia ya
sasa neno Umakini limekuwa likitumwa kutokana na matokeo Fulani yaliyotokea
mathalani ukifanya vizuri jambo lolote au mtihani watu watasema alikuwa makini
sana katika kuzingatia katika yote aliyoelekezwa na watu wengine watasema
alikuwa ni mwanafuzi au mtu msikivu mwenye kuzingatia yote aliyofundishwa
LAKINI itokee upande wa pili ya kushindwa jambo Fulani watu watasema mimi
niliona mwenendo wake kwa vile ulivyokuwa nilijua matokeo yake yatakuwa haya na
wengine watasema yote hatayasiokuwa ya kweli wengine watasema alikuwa MZEMBE!
Lakini litakuja mtu mzembe yukoje na mtu aliye makini yukoje na ni kweli wote
walio makini ndio wanauwezo kufanya vizuri hili ni swali tu!
Si katai kweli umakini
ni chanzo kimoja katika kufanikiwa au kufanikisha jambo moja ambalo
umelikusudia, kwani umakini unakupa utaratibu ambao utaoheshimu na kuzingatia
japo kuwa unaweza kuweka mwenyewe kutokana maarifa uliyonayo. Na siku zote
chanzo cha kuwa makini ni lazima kuwe na lengo na hatua za kufikia hilo lengo.
Katika umakini kuna
kitu ambacho uwa kinasahaulika sana kuwa umakini haukamiliki bila UTAYARI maana palipo na
utayari basi hapo panautekelezaji ambao mwisho wake uleta matunda ambayo watu
utegemea sana baada ya kuungamanishwa na BIDII ambavyo ubeba juhudi na
uvumilivu katika kutimiza jambo ambalo liko mbele yake katika mazingira yeyote
katika kutimiza lile ambalo limebebwa ndani yake,
Lazima ujue kwamba
umakini ujengwa na utayari baada ya kukubali ndani ya akili yake…hapo ndipo
unaweza kusema huyu ni makini sana kwakua tayari dalili za utekelezaji zimeanza
kuchipua lakini umakini wa kusikiliza pekee yake sio kigezo cha kutosha cha
kusema mtu huyu yuko makini kwani anaweza badilika wakati wowote na kitu
kingine wakati wote.
Umakini ujengwa na mtazamo wa Yule unaye msikiliza na
namna akili yako inavyomtafsiri kutokana alivyo kwako namna anavyokuona na
namna unavyomuona, nguvu ya maarifa
uliyonayo ambayo yatakupa kuendelea kusikiliza ua kuacha kusikiliza na upendo wako kwa Mungu inayokupa nguvu
katika kumsikiliza mtu wa aina yeyote ili mradi kukipata kile ambacho
unachokitaka na kusudi au azma yako
katika kufanikisha jambo Fulani katika maisha yako.
Imeandaliwa
na;
Cothey
Nelson…………………………………..0764 018535
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni