Jumanne, 27 Agosti 2013

uko wapi UPENDO wa kweli?(where is true love)



UPENDO;
 
Si neno geni masikioni mwa watu wengi hili neno PENDO,kwakua kama ujawai sema basi umeshaambiwa na kama ujaambiwa basi umesha sikia sehemu fulani au toka kwa mtu mmoja akizungumza na mwezake  hivyo si neno geni kwako.

Ukweli upendo ni asili ya Mungu mwenyewe kwakua ndani yake ndiko kuna asili ya neno ya UPENDO, mbali na yeye hakuna kupenda kwa maana ya Mungu bali kuna kupenda kwa maana yetu. Hali hii uweza kupotea mara kikatokea kitu kingine kikachukua nafasi basi hali ya kupenda upotea.
Tatizo kubwa mtu anapo kwambia ninakupenda huwa amalizii kuwa huo upendo ni wa muda gani huwa haiko wazi unakuta yale yote ambayo mmeahidiana yana katishwa na kukuta anakwambia umefikia mwisho au unaona vitendo vinavyoashiria mwisho.

Kwa namna hiyo watu wameshaliondoa thamani ya neno  NAKUPENDA kiasi kwamba mtu anaweza kukwambia asubuhi nakupenda halafu jioni akasema nimeghairi, inaweza ikakusumbua baada ya kutendwa sana unaweza kuona sasa ni kawaida hivyo halitashtua sana moyo wako.
Kwa namna hii watu wamekaa katika mausiano kwa tahadhari kubwa sana wakijiweka sawa kwa lolote kutokea. Hivyo uhuru katika kuhusiano umepungua sana kwani imekuwa ikileta majanga katika moyo wake.
Japo kunachangamato za neno hili UPENDO kukosa thamani yake katika dunia ya sasa lakini bado jambo hili lina hitajika sana kwakua katika hili mambo mengi mazuri ufanyika.
Maisha au uhusiano wowote wenye hali ya upendo ndani yake ni mahala ambapo unapenda kuwepo siku zote. Kwa hakika UPENDO ulitakiwa kuwa msingi wa jumuhia,familia na mahusiano yoyote ili kuleta radha ya mausiano hayo.
Lakini upendo wa siku hizi umekuwa ni wakujisikia tu,wakuwaza tu pasipo kujua upendo ni zaidi ya kujisikia au kufikiri.


Ki ukweli hali hii imepotea kiasi kwamba watu wamekosa kuona mahala penye upendo wa kweli lakini hali hii imebakia katika maneno,nyimbo na masimulizi tu yasiyo kuwa na msingi wowote.
Imefika kipindi cha kuwa watu wanatafuta namna ya kuishi pasipo kupendwa au kupenda kwa namna alivyotenda katika mausiano mbalimbali.
Neno hili limekuwa likiambatanishwa na mambo yasiofaa ambayo yamekuwa kikwazo katika jamii inayotuzunguka kwa kiasi kikubwa usemi huu uwa na nguvu PENDA UNAPO PENDEKA. 

 
Hili neno lina nguvu sana kama likibebwa kwa namna yake katika ukamilifu wake ili kuleta dhima iliyokusudiwa.
UPENDO ni namna moyo wako unavyozungumza na sio wewe unavyosema au watu wanavyozungumza.


Mitazamo tofauti ya dunia ya sasa kuhusu UPENDO;
                       
                                 I.hakuna maana ya kupenda pasipo kupendwa.
Huwa hatuangalii jambo kwa namna stahiki bali ni vile tunavyoona sisi tunavyo amini sisi na kila tendo tuna itafsiri kwa lugha/maana yetu.
Ni kweli unapo pendwa hapo nawe upenda sana lakini haujui kwa namna gani mtu yule anakupenda kwa nini anakupenda.
Msingi wetu mkubwa umekuwa kwa vile anvyo nipenda na mimi nita muonyesha hayo mapenzi kuwa kikisha anafurahia uwepo wangu.
Na mahali ambapo unaona ishara ya kutopendwa hapo utafuta namna gani kuwa mbali na mazingira hayo kwani unahisi lolote laweza kukutokea.
Tutambue sio kila mahali unapo pendwa basi unaweza kufanikiwa vile unavyofikiri na sio kila unapochukiwa unaweza kutofanikiwa, wakati wowote na majira yoyote mambo yanaweza badilika yale mazuri kwako yakawa mabaya na yale mabaya yakawa mazuri.
Hali hii ni tatizo katika jamii kubwa tuliyo nayo kwani mausiano pindi yanaposhuka watu utafuta namna kuachana zaidi na sio namna ya kutafuta namna ya kurejesha.

                      
                              II.nini alichonacho ambacho kitanifaidisha mimi!
Kwa hiyo upendo wangu unajengwa kile kitu alicho nacho kwa uwepo wako na mtu huyo utegemea sana uwepo wa kitu hicho hicho kitu hicho kikipotea basi upoteza.
Ni kweli unapo uhusiana na mtu lazima kutakuwa na mbadilishano wa vitu lakini tambua kuwa mbadilishano wa vitu sio msingi wa maisha yenu bali ni vitu vinavyoboresha urafiki/mausiano yenu.
Hali hii inapokuweka unakuwa ni mausiano ya tahadhari sana inakuwa kama mtu anayesubiria mzigo maana fulani akisha upata halafu haende zake/haendelee na maisha yake.
Watu wenye uhusiano huu wanakuwa na hali ya utegemezi mmoja kuliko mwingine hali hii uhishia mahala ambapo si salama sana.
Kama hauna kitu ambacho kitamfaidia mwingine mtu wa namna hiyo hawezi kukaa nawe kwani kile anachokitaka ajakipata.
Huu sio msingi wa kuwa na mausiano na mtu lakini katika dunia ya sasa imekuwa ndicho chanzo cha kufamiana, ulikuwa haumuheshimu wala hautambui maana halikuwa si kitu kwako lakini baada ya kuwa na kitu sasa thamani yake ikawa. Uhusiano ulioshikamana na maslahi haya uwa kunatokea na uharibufu mkubwa.
Ni vizuri kutamani mambo toka kwa mwenzako ukjifunza na yeye akakuelewa kuliko kwenda kwake ukawa mnafiki halafu mwisho ukawa mbaya.

             
                           
                           III.nimepungukiwa na nini mpaka ni mpende!
Unaweza kushangaa kwanini mtu anaweza kusema maneno kama haya  hii inatokana na mambo matatu makubwa, KUTENDWA,KIBURI NA KUKOSA UELEWA.
Mambo haya yote yanaweza kumfanya mtu kuwa katika nafasi ya kusema maneno hayo. Hii yote inaonyesha jinsi tulivyopoteza misingi ya UPENDO.
Kwa hakika hali ilivyo uadui utakuwa ndio  urafiki maana kama mnaishi kwa tahadhari basi hamna tofauti na maadui ambao wanamendeana.

Jamii ya watu wa namna hii ni hatari sana kwakua upolomoka katika maangamizi makubwa kwani wanajiamini kana kwamba duniani unaweza kuishi pasipo kuwa na UPENDO.
Ni kweli kila mtu anayo nafasi ya kujitengenezea maisha yake kwa namna yake lakini jamii bado unahitaji hakuna njia ya kukwepa kama usipo wahitaji leo basi utawahitaji baadae.
Hivyo mtu anapokuwa katika hali hii si vyema kumuhukumu kwakua haujui kitu gani kimeleta hali aliyokuwa nayo. Ila inakuwa shida pale tu kwa mtu husika asipotaka kukubali kuwa wazi.
Mtu uweza sema nisipokuwa nae kwani nitakufa na maneno mengi ya kejeli yanayofanana na hayo usikusumbue kama kuna giza jua kuna mwanga muda si mrefu kitajulikana.

         Prepared by ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                     Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com

                                      Kila la kheri,rafiki……….”