Jumanne, 21 Februari 2017

KUJIKWAA SIO MWISHO WA SAFARI BALI NI NAMNA NYINGINE YA KUJIFUNZA!

NAMNA NYINGINE

Katika dunia ya sasa utendaji wa mambo mengi umerahishwa sana, unaweza kufanya kitu kwa njia mbalimbali kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo maendeleo ya sayansi na teknolojia, hali ya hewa, aina ya kitu/ jambo husika.

Katika kufanya jambo moja, kunaweza kuwa kwa njia nyingi sana lakini shabaha inawezakuwa ni moja kwa wote….. kama vile wote wanaweza kuwa na nia/mwelekeo mmoja lakini kila mtu anaweza kutumia njia yake na mwisho wote wakajikuta wamekutana sehemu moja, japo wakati mwingine utofauti wanjia ya kutumia utegemea sana wapi umetokea hivyo mahali ulipotokea unaweza kukupa mwelekeo ambao ni tofauti na mwingine,

Tukiangalia katika uwasilishaji wa habari unaweza kutumia njia nyingi kutokana na uwezo wako na uelewako kama sio umahiri wako unaweza kuwasilisha habari kupitia njia za mitandao fb, twitter n.k au kutumia media mathalani radio, tv japokuwa njia ni tofauti lakini inawezakana kuwa ni habari moja inayowasilishwa kwa njia nyingi.

Vilevile wako wataalamu wanaweza kuwasilisha ujumbe kwa namna mbalimbali mathalani kwa njia ya picha, kinyago hama kwa njia ya maandishi lakini unaweza kukuta wote wanawasilisha jambo moja inawezekana kuwa hali ya siasa nchini, ubora wa kitu, tuuthamini utamaduni wetu ,umuhimu wa amani hama tuyatunze mazingira na mengine mengi.

Japo watu kuamua kutumia namna nyingine katika kufanya jambo kunaweza kuwa kwa nia njema hama la! Kwakua wapo watu kwakuwa hawapatani na mwenzao hivyo uweza kutumia namna nyingine kuonyesha kuwa akubaliani, 

Nakubaliana kuwa wakati mwingine katika kufanya jambo moja kunaweza weza kuibuka kwa namna mbalimbali katika kulitekeleza jambo moja na pengine hiyo njia ikaleta matokeo mazuri na kwa haraka mathalani ujumbe unaweza kutumia simu kuwasilishwa sehemu husika kuliko kutumia barua kutuma kwa mtu inaweza chukua muda kulingana na umbali, hama kutoka katika matumizi ya jembe kwenda kutumia trekta.

NAMNA NYINGINE!

Tumeona watu wakikubali hama kukataa kutokana na kupata namna nyingine katika kufanya jambo, wazo jingine, nia nyingine, maamuzi mengine katika kufanya jambo unaweza kukuta mtu alishauriwa ilikupunguza unene lazima upunguze kula na baada ya kupata wazo hama ushauri mwingine inawezekana kufanya mazoezi tu,anaweza kuacha njia moja na kuingia katika njia nyingine hama kutumia njia zote inategemea halmashauri ya ubongo wake.

Wako wako watu wameshindwa kwenda mbali/ kupata kile wanachokitaka  kwa sababu ya kukosa kutambua njia nyingine katika utatuzi wa jambo………mathalani kilimo unaweza kukuta mkulima analima apati mazao ya kutosha sawa na vile anavyotegemea kwa kukosa njia nyingine uweza kujikuta akaghairi kulima kabisa badala ya kutafuta namna nyingine ya kilimo chenye tija, hama kupata uelewa kuhusu namna ya kuitunza ardhi ili iweze kuwa na rutuba na hatimaye aweze kupata mazao anayoyataka.

Ni kweli unaweza kuwa unaomba sana na unasoma Neno la Mungu, unapoona hakuna mpenyo katika yale unayoyafanya lazima utafute namna nyingine ili maombi na Neno liwe na faida katika maisha yako na sio dawa kuacha kwakua umefanya kwa muda mrefu na hakuna matokeo unayo yategemea maana kila jambo kuna namna namna yake yakulifanya tena kulingana na wakati na uhitaji uliopo sawa na Roho mtakatifu atakavyokuagiza,

Upaswi kukariri kuwa ukimsikia mtu anacheka basi anafuraha wako watu wanavyolia ukiwasikia kwa mbali unaweza fikiri wanacheka,

Upaswi kuweka imani mbali na Neno la Mungu kwakua unaweza kukuta mtu ana amini kuwa akiuza maembe Tabora basi yatatoka kwakua rafiki yake alipeleka maembe roli zima yote yakaisha anaamini na yeye akipeleka yake yataisha pasipo kujua ule ulikuwa msimu gani?

Upaswi kukubali kushindwa kwa kuliona jambo limeshindikana bali tambua kila jambo lina njia zake katika utatuzi wake sio lazima utatue kwa njia moja hama kwa namna ulivyofikiria, kuna njia nyingi ni wewe kukubali kuitumia tu.

Ni vizuri ufahamu uwe umetengenezwa kutatua kila jambo litakalo kuja mbele yako na sio kukariri jambo moja namna ya kulitatua yakija mengine yanakuweka chini, kumbuka utatuzi wa jambo ndio unapelekea amani, ushujaa na zaidi sana kuzidi kumpenda Mungu.

KUJIKWAA SIO MWISHO WA SAFARI BALI NI NAMNA NYINGINE YA KUJIFUNZA!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 14 Februari 2017

UBORA WA MTU

UBORA WA MTU

Kuna dhana mbili zinazo kinzana kama sio kushabiriana UBORA /UMUHIMU

Ukweli ni makosa sana kufananisha umuhimu na ubora japo wakati mwingine kutokana ubora wa mtu uweza kupelekea umuhimu wake, kwa maana kama hakuna uhitaji wake/ umuhimu wake basi watu uweza kuona hapo hakuna UBORA wakati ubora siku zote uko ndani yake lakini umuhimu upo penye uhitaji tu.

Japo kuwa ubora wa mtu anakuwa nao mtu ndani yake lakini umuhimu wa mtu unaoneka pale atakapoonyesha utendaji wake, na wakati mwingine umuhimu wa kitu uonekana pale kinapokosekana, kwa hivyo yale mambo yake yanapokosa mbadala basi hapo ndipo uona nafasi yake.

Nipende kusema kuna wakati UMIHIMU wa kitu unaweza isha lakini sio ubora uliondani, kwakua ubora ni kitu alichokiweka Mungu ndani ya mtu kwa faida yake,

Ubora wa mtu ahuonekana katika muonekano wa mtu japo umuhimu wa mtu unaweza kutokana na muonekano mathalani mashindano ya urembo, model uwa wanapenda watu wenye umbo fulani lakini huo sio UBORA wa mtu.

Ubora wa mtu tunauona kwa Mungu pale alipo amua kumuachilia mwanae kipenzi kwa ajili ya mwanadamu!

UBORA WA MTU!

Kama mzazi pindi anapomwangalia mtoto wake uwa siku zote anamuona kuwa katika UBORA WAKE ( kwa mzazi mwenye akili) na sio kwa umuhimu wake, maana anajivunia yeye anajisifia yeye na fahari yake imebebwa na yeye,

Ndo mana Mungu alionyesha THAMANI/UBORA wa manadamu kwa kumtoa kipenzi chake, kwa maana rahisi tu kuwa Mungu alitoa kipenzi chake kwa ajili ya wapenzi wake, mwanadamu ulivyo kuwa bora ili mlazimu atoe kilicho bora,

Japo katika dunia ya sasa ubora wa mtu umekuwa ukichukuliwa katika hali isiyo sawa ndomana watu kuutoa uhai wa mwenzake kwa ajili ya maslai binafsi hawaoni shida, kumtoa kasoro mtu kana kwamba anaweza kumrekebisha, unaweza kukuta mtu anasema”mwangalie anamacho makubwa kama mguu wa tembo asingekuwa anayatoa maana yanatisha” mtu anaongea kwa ujasiri tena pengine wakitiana ujinga na mwenzao huku wanacheka kwa kebei.

Unaweza kukuta mtu anasema”huyu jamaa ombaomba yaani akikuona lazima akubomu ingefaa naye awe mgogo na aende Dodoma” watu wanasema tu kwa kuwa wamepewa kinywa cha kusema kwa hiyo wana kitumia vile wanavyoona na wala sio kama wanavyopaswa,

Pia unaweza kuta watu wanasema “ king’ang’anizi kaja yani akishiria jambo lake hata la uongo yani huyu mbishi  yani ruba anasubiri kwa ung’ang’anizi wake bora angekuwa super glue ingejulikana moja, mangi angeuza iishe”

Yako mengi lakini watu wako huru kana kwamba wanamjua mwanadamu kinagaubaga hama walikaa na Mungu wakati anamtengeza mtu au huyo jirani yake,

Marko 12:31 Na ya pili ndiyo hii, Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi.

Biblia imekosa lugha nzuri yakueleza ikasema kama unavyojiona na kujipenda, kujithamini basi fanya hivyo kwa mtu yeyote pasipo kujali unamjua hama umjui,

1 Yohana 4:20 Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona.

Lazima ujue hatima umeshika na wewe ila Mungu ndio muamuzi, sio kila hali aliyonayo mtu binafsi anaifurahia laiti ungeuona usiku wake namna macho yake yanavyolowesha mashuka yake usinge thubutu kuwaza tofauti na namna unavyopaswa kuwaza,

UBORA WAKO NA WAKE NI SIRI YA MUNGU!

ANAITWA MUNGU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………………..0764 018535

Jumanne, 7 Februari 2017

MISULI YA NDANI.

MISULI YA NDANI

Moja ya ushupavu wa mtu katika muonekano wa nje ni kuonekana kwa misuli ikitandaa katika sehemu ya mwili wake mathalani mikononi na hata miguuni.

Ina aminika kuwa pindi mtu atakapoanza kuonekana kuwa na misuli bila shaka watu watajua mtu huyu ameanza kufanya mazoezi na wengine watasema anataka kuimarisha mwili wake hama kutengeneza muonekano mzuri katika mwili,

 Japo inawezekana mtu kuamua maamuzi hayo ni baada ya kuona watu wakiwa na muonekano tofauti tofauti wa kupendeza kutokana na mazoezi wanayo yafanya, 

Japo ilikuwa na mwili ulioimara sio lazima utoke misuli kuna aina ya mwili misuli haionekani kwa nje kama wengine lakini mwili wake uko vizuri na tishio hata kwa wale wenye miili iliyotuna kifuani hama sehemu nyingine katika mwili wake.

Katika kutoa maana ya neon MISULI ningependa tujikite katika dhana ya UIMARA,

Kutoka hapo ndipo tunapata kuona watu wamewekeza hama wamesimamia wapi na kutoa picha inayojidhirirsha katika mienendo yao, katika hili wako watu uimara wa imani zao unakuja pale anaposikia shuhuda basi hapo ujenga imani kuwa kama imewezekana basi hata mimi itanitokea na pengine hata kujipa matumaini kama kwa mtu ametendewa wakati mwingine unaona kama wewe ulistahili zaidi basi una weka mkao wa wewe kutendewa

Wako wengine uimara wao wameweka katika  kufahamiana na watu wengi, wakijua kuwa kwakua wanafahamiana na watu basi wako salama hivyo shida yake itakuwa ni rahisi kutatuliwa kwa kuwa ana amini katika nguvu ya wengi hakuna kitu kitakacho mshikilia sana,

Wako wengine pia wamejiona kuwa wako salama na imara kwasababu wanafahamiana hama kujulikana na mchungaji hama watu waliokaribu hama mke mchungaji hivyo anaweza kujiachia na kufanya anachoona na kujiona yeye ana nafasi na kamwe hakuna ataye mtingisha kwakua ameshikwa na mihiri ya kanisa,

Pia wako wachache ambao misuli yao ya ndani imetengenezwa na neno la Mungu hama Mungu mwenyewe watu hawa wana muona Mungu kuwa ndio uimara wao, ushindi wao na ushupavu wao wana amini wanaweza fika popote kwakua waliye nao anaijua njia.

Misuli ya ndani uwa haiweki msingi wake katika yale yanayomkabili sasa bali hata yatakayo mkabili bado anaona atakuwa salama tu!

Daniel 3:16 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia   mfalme, Ee Nebukadreza, hamna haja kukujibu katika neno hili.

                17 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuru ile iwakayo moto; naye atatuokoa na mkono wako, Ee mfalme.

              18 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.

Ni watu huwa awaogopi kupoteza kitu chochote ili mradi wasimkose Mungu kama watumishi hawa shadraka, meshaki na Abednego walikuwa tayari ni bora kuangamia wakiwa mikononi mwa Mungu kuliko kuishi maisha yaliyo mbali na Mungu,

Watu wana mna hii Mungu uwatafuta ili aweze kujivunia na kuona fahari juu yao kwakua Mungu ujivunia katika kitu kilicho bora na sio kitu kilichopo tu,

Ili ufike mbali lazima uhakikishe misuli yako ya ndani inajengwa na kuimarishwa na NENO LA MUNGU kwa kulikubali hili neno utafanya Mungu mwenyewe ashughulike na wewe katika kukuhakikisha unakuwa bora na wa maana zaidi.

KUBALI KUWA FAIDA KWA MUNGU UPATE MATUNDA YAKE HAMA KUBALI KUWA FAIDA KWA WANADAMU UPATE HASARA ZAO!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………0764 018535

Cothey  Nelson……………………………………………0764 018535