Jumanne, 27 Oktoba 2015

NENO LA KINYWA



NENO LA KINYWA


Wako watu katika dunia ya leo wamekuwa machizi, wamekosa mwelekeo,wanashindwa kuzaa,maisha hayasongi, hawajielewi maisha yanavyokwenda zaidi ya kuona miaka inakatika tu! Lakini yote haya yanaweza kusababishwa na NENO LA KINYWA.

Na ni ukweli usiopingika kuwa wako watu wanafika mbali kutokana na neno linalotoka kinywani, wanapokea uponyaji,wananawiri  na kushamiri kwasababu ya NENO LA KINYWA, na ukumbuke kuwa neno  lenye misingi ya kweli uwa linadumu siku zote ata kama mtamkaji wa hilo neno amesha fariki au hayupo tena lakini lile neno linaweza kuishi na kumshikilia au kuwashikilia. Kwa kusema hivyo unaweza ukamkimbia mtu na kuama sehemu nyingine lakini kamwe hauwezi kulikimbia neno linatoka kinywani mwake.

Na ukumbuke kuwa neno alikuachi kwasababu umeteseka sana au umelia sana bali linaondoka au kukuacha kutokana na kubadilisha mfumo au mtu kuja kulitengua hilo neno alilolitamka. Naweza kusema moja ya laana mbaya ni laana zinatokana na neno lenye uhalisi(sababu za kweli) , mathalanii mtu anaweza kusema kwamba kama hauta mweshimu mzazi wako basi hautatoka katika maisha haya mabovu unayoishi sasa na kweli iwe ujamuheshimu mzazi wako basi laaana hiyo itakuwa maisha yako.

Ujenzi wa maisha ya rohoni katika upande wa GIZA na NURU uwa yanajengwa au kuumbwa kupitia neno la kinywa cha mtu husika au kunenewa na mtu ambaye moyo wake umemlizia au haujamlizia, na mwisho hayo maneno tutayaona ya kidhihirika katika ulimwengu wa mwili.

Ni kweli neno la kinywa chako linakuwa na nguvu sawasawa na hadhina iliyoko ndani yako lakini sio tofauti na kile kilichomo ndani yako, japo kuna vitu viwili kuna kuwa na hadhina katika moyo wako na kuliamini lile neno unalolitumia kuwa lina nguvu na linaweza kufanya kazi.

Kinywa chako lazima kiwe ni kisima kinachotoa maji matamu ambayo mtu akiyanywa atataka kunywa hayo maji na pindi atakapo kunywa hayo maji basi yatajenga afya katika maisha yake na sio kumdhuru katika afya yake, japo watu wengi tumekuwa tukishindwa kujitambua kwamba kwa uhakika sisi ni watu tulibeba aina gani ya maji kutokana na mchanganyo wa maji matamu na machungu.

Uwezi kuwa katikati alafu ukawa na nguvu kubwa lakini pindi utakapo kuwa katika upande mmoja unaoeleweka ndio nguvu itakuwa ya uhakika maana Mungu katika neno lake anasema ukiwa vugu vugu nitakutapika kwakua kila upande unagharama zake na una mambo yake hivyo pasipo kujua kuwa unahitaji kuwa na nguvu moja ambayo nitawezesha maisha yako.

Ni ukweli kwamba ukombozi wa kinywa usihanishwa kwa karibu na ukombozi wa mawazo na fikra kwa ujumla wake kwakua tuna jua katika fikra kunajenga au kunatoa tafsiri ya mambo na hatimae ndio kunazaliwa na tamko(maneno ya kinywa).

Siku zote siraha ambayo ni hatari ufichwa na kuwa katika uangalifu wa hali ya juu sana kwasababu inaaminika kuwa ni siraha ya ushindi na inatumika katika mazingira muafaka na sio kila wakati na kila mahali, hivyo lazima utambue kuwa kinywa ni siraha ya ushindi na hatari sana basi inapaswa kuitunza kujilinda kuhakikisha inatumika katika mazingira muafaka ilikuleta matokeo sahihi.

Nikweli mtua anaweza akaongea mengi lakini yako maneno yalibeba athari katika maisha ya mtu husika na katika hayo unaweza kuona ni ngumu kutoka hapo ulipo, hivyousikubali kuishi maisha ambayo kila mtu ataweza kuona anasababu ya kunenea neno baya katika maisha yako.

Kila neno linalotamkwa katika maisha yako linakuwa na nguvu pindi tu litakapopata nafasi!!!
Imeandaliwa na;

Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535

Jumanne, 20 Oktoba 2015

BADO UNAYO NAFASI



BADO UNAYO NAFASI

 Maumivu ya mtu yanaongezeka sana sio kukosa nafasi tu bali pindi anapotambua kuwa hakuna nafasi nyingine ya kuweza kufanikiwa tena!

Haijarishi upo katika kipindi kigumu kipi elimu,kazi,mausiano au huduma jibu langu kwako ni kusema kuwa  BADO UNAYO NAFASI!

Machozi ya mtu unaweza kuyaona hapa katika hatua hii pindi mtu anapo ona sasa sina nafasi tena kinachopaswa sasa niangalia kitu kingine kabisa.

Ni jambo kubwa na ni mateso pindi unapogundua kuwa katika mtu mliyependana sana inawezekana alikuwa rafiki tu au mchumba na hata mke pindi inapojua sasa ndio mwisho wa mausiano yangu naye katika maisha yako!

 Kinacho wa umiza watu wengi sio kukosa katika yale wanayoyatarajia tu bali ni kuona kuwa hawana uwezekano tena kuyapata yale waliokuwa wakitarajia! Ndo mana mtu anaweza kulia mara mbili kwakumkosa mtu anaye mpenda na kuwa hata onana nae tena hivi vinakuwa ni vilio viwili katika moyo wa mtu.

Ni kitu kizuri pindi unaposikia kuwa bado unayo nafasi kwakua unajua kuwa kumbe naweza fanya kitu bora au kizuri zaidi kwakua ninayo nafasi tena!

Kutoona nafasi tena kunaweza kusababishwa na namna unavyojiona au mazingira au hali halisi inayoonekana mathalani binti anaona umri unaenda na mwili unazidi kuwa katika hali ya uzee basi nafsi yake inaweza kusema sasa nitakufa bila mume wala mtoto. Kitu ambacho wanawake wanalia sio tu kupoteza watoto au kutoshika mimba kwa sababu mfumo wa kimwili kutokuwa sawa bali maumivu hayo yanazidi pindi anapopewa jibu kuwa hakuna uwezekano wa yeye kushika mimba au kupata mtoto.

Katika hali hii na maumivu haya mtu uweza kujikuta kufanya maamuzi ambayo kiukweli yanaweza kusababisha matatizo katika maisha yake na sio kuleta pumziko au suluhisho la kudumu katika maisha yake.

Niseme katika yote bado unayo nafasi ya kufanya lolote  na kufika popote na kuwa yeyote, la msingi tu limepata kibali kwa Mungu na kwa neema zake basi unaweza kuwa mtu wa tofauti sana, niseme watu wengi wanalia kwasababu maarifa yao yameshafika kikomo hivyo anakuwa anajibu linguine zaidi ya kusema SAWA! Lakini kumbuka kuwa maarifa yako sio ya Mungu.

Ni seme kuwa watu wengi wanafika katika hatua hii kwasababu wanakuwa wanalazimisha mambo yao yaweze kufanikiwa kwa maarifa yao kwa mawazo yao na mwisho inavyokuwa tofauti basi hapo kilio kinachukua nafasi na kilio kinakuwa na nafasi kubwa na hali ya mtu kupenda kuwa katika hali ya mwenyewe tu! Upweke uzaliwa hapo.

Niseme katika maisha jambo baya sana ni kikwazo katika maisha ya watu wengi ni kuona ubaya aliotendewa kuliko wajibu wake sikuzote ubaya unapozidi wajibu wako basi kinachofauta hapo ni maumivu na mateso na kujikataa.

Jua anayeweza kukupa raha sio mchungaji, mpenzi au wazazi wala watoto ni kweli wanaweza kukupa furaha furaha tu! Lakini sio raha kama chimbuko la matumaini katika maisha yako ya sasa naya baadae.

Niseme tu kweli yanayotokea yanaweza kuwa mshangao kwako au surprise lakini sio mshangao kwa Mungu kwakua hakuna jipya kwa Mungu hivyo unachopaswa kuona kama bado huko kwa Mungu basi ujue yeye atarekebisha tu na utakuwa salama.

Ni vizuri kuwa na mipango mizuri katika maisha tulionayo yaani kuwa na mke au mume mzuri na mengine mengi lakini pindi Mungu anapoingilia ili kuyaboresha usiwe kikwazo kwake katika kukusaidia kuyafanya kuwa katika mtazamo wake Mungu uliojaa matumaini ya kweli.

Usikubali kuonekana sawa na vile watu wanavyo kuona kuwa umeshindwa au umeaibika au hauwezi tena yaani usiishi katika mtazamo wa watu bali kubali kuishi katika mtazamo wa Mungu mwenyewe anaeijua kesho yako na kuitunza kwa ajili yako.

Niseme tu hakuna mtu anamwamini Mungu katika hali sahihi akawa ana kesho mbaya hayupo hii inakuwa ni fikra zetu tu na hofu za maisha kikubwa ni kumwamini Mungu katika kila hatua….kwakua Mungu anafanya jambo kwa Yule anaye mwamini.

Unahaja ya kuchoka maana Mungu ajachoka, unahaja ya kushindwa maana Mungu ajashindwa kufanya jambo litakalo leta mwanga katika maisha yako.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………..0764 018535


Jumanne, 13 Oktoba 2015

TULIZO LA MOYO



TULIZO LA MOYO


  Kuna vitu vingi ukikosa unaweza ukavumilia na maisha ya kaendelea lakini kamwe sio tulizo la Moyo, nimeona watu wengi wakifikia maamuzi mbalimbali kwasababu la kukosa tulizo la moyo!!!

Ni kwli mtu unaweza ukakosa fedha,watoto,elimu na mengine mengi lakini bado maisha ya kaendelea japo katika hali ya kuvumilia na baadae ukazoea, lakini kamwe sio tulizo la moyo kwani katika hali hii moyo unakuwa haujielewi maana hauna furaha, ujui ufanye nini au usifanye nini? Unaweza kukaa ukaona bora usimamame na hata ukisimama bado utaona haitoshi unaweza ukaona bora ukimbie na hata ukikimbia bado utaona haitoshi utaona bora utambae na utamaliza mambo yote lakini kamwe hauta weza kupata jibu la swali la moyo wako!

Najua hali hii sio ya wote kwakua wako watu wanaweza wakaishi maisha ambayo hayaleti burudiko au tulizo katika moyo  lakini bado akaona wacha maisha yaendelee maana nitavumilia na baadae ndio yatakuwa maisha yangu.

Niseme mtu anayeishi katika hali hii ukweli anaishi maisha ya utumwa na ya ukiwa japo anaweza kuwa na mali nyingi familia bora iliyoelimika na maendeleo .

Kitu pekee kinachoweza kuleta tulizo la moyo ni SEHEMU SAHIHI

Nje ya hapo uwezi kuwa na tulizo la moyo, kwakua unaweza kuwa sehemu nzuri inayopendeza macho na inayofurahisha na kugusa hisia zako lakini isiwe sehemu sahihi!

Kwa kawaida ukuaji wa binadamu ili uweze kwenda katika ubora wake kila jambo lina wakati wake pindi mtoto anapozaliwa sehemu sahihi kwake ni mikononi mwa mama yake japo anaweza kulelewa katika taasisi na hata watu wengine tofauti na ndugu zake na kila hatua atayopiga ina sehemu yake sahihi mathalani katika mfumo wa elimu kuna hatua anayotakiwa kuwa  shule ya awali na baadae kuingia chuo kikuu.

Ni napozungumzia sehemu sahihi na zungumzia sehemu ambayo itakayokupa mwanga katika maisha yako uliojaa ushindi na ubora na ushujaa na mwendo wenye kishindo ulio jaa mamlaka. Na ninapozungumzia sehemu hapa na zungumzia ni zaidi ya nyumba nzuri iliyo jaa malumalu na kumetameta au aina ya kanisa ambayo iliyojaa nguvu ya Mungu au yenye taratibu zenye kuheshimika na kukubalika katika nchi.

Sina tatizo na nyumba nzuri, kanisa lako nzuri bali ninashida na tulizo la moyo wako kweli lipo? niseme kusema kunatofauti kati ya matumaini ya akili na tulizo la moyo na niseme tu kwamba hakuna mtu ataleta tulizo la moyo wako zaidi ya Mungu mwenyewe katika moyo wako kwani katika yeye ndio linapatika tulizo la kudumu.

Unaweza kuwa sehemu yoyote hata iwe bora kiasi gani lakini ukweli kwamba kama tulizo alipo hata kama ikiwaje na kamwe tulizo la moyo aliwekewi katika kutamkiwa bali linachipuka ndani yako!

Unaweza kuwa sehemu sahihi katika mazingira lakini usipo itambua nafasi ya Mungu katika maisha yako iliyojaa kwa ukamilifu utaweza kufanya jambo sahihi.

N.B; tulizo alitegemei namna unavyokaa na mtu wa Mungu vizuri tu bali namna unavyokaa na Mungu vizuri kwani yeye ndio mtoaji tulizo la Moyo kwako na mtumishi wake,

Kwakua hivi sasa watu wamekuwa makini sana namna ya kukaa na mtu wa Mungu kuliko namna ya kukaa na Mungu na watu wa namna hii wamekuwa wakiangukia katika maumivu makali kwakua walimuamini Mtumishi wa Mungu kama Mungu mwenyewe!

Sisemi usiwasikilize watumishi ambao Mungu amewaweka uwaheshimu sana kwakua Mungu amewaweka kwa kusudi lake na Mungu anawaheshimu sana maana amesema mwenyewe…..mtu akinitumikia nami nitamuheshimu,

Kubwa sana nataka kusema ni muhimu kutambua nafasi ya mtumishi wa Mungu na Mungu mwenyewe ili ufanye jambo katika ustawi mzuri wa maisha yako.

Sehemu sahihi ya kukaa wakati mwingi kwa macho haya ya nyama inaweza isivutie bali sehemu nzuri na kuvutia lakini niseme sehemu sahihi ni mahali wewe ulipo na Mungu

Nasio mahali ambapo watu wengi wanakimbilia na kupasifia bali ni mahali ambapo Mungu anakuwa tulizo la moyo wako na sio mazingira au maneno ya mtu yenye ushawishi au yenye kutisha , kwakua hakuna mwenye hatima ya maisha yako zaidi ya Mungu mwenyewe yeye mwenye kujua kabla ujatoka duniani na baada ya kutoka yeye anaijua hatima yako na kujua namna ya kukufikisha.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson…………………………………………………………0764 018535

SEHEMU SAHIHI KATIKA HATIMA NJEMA!!

Jumanne, 6 Oktoba 2015

TAFSIRI YA JICHO



NGUVU YA JICHO


Japo mwili wa binadamu una viungo vingi na kila kiungo kina umuhimu wake na hiyo inatokana na kazi yake katika kuendesha gurudumu la mwili. Lakini mimi nimeona bora ni zungumzie jicho kama moja ya kiungo chenye umuhimu wa kipekee katika mwili japo si zaidi ya viungo vingine.

Tunapozungumzia jicho kila mtu anatambua umuhimu wake kwani kupitia macho unaweza kufanya uchaguzi, kufurahi na kujisikia vizuri na hata kutambua hisia za mtu kwako.  Naweza kusema jicho ni moja nyenzo ambayo imetumika katika watu kufanya maamuzi.

Hivyo Jicho  linasafishwa, linatunzwa na linatengenezwa ili liwe na muonekano unaofahaa ili liweze kufanya kazi inayopaswa…….!

Sote tunajua kazi ya jicho iliyokuu kuwa ni kuona japo inakazi nyingine kama kuwa ni sehemu moja ambao mwili utumia katika kutoa taka zake, tunajua katika sehemu ambayo mojawapo inaumakini sana katika maisha ya mwanadamu basi ni jicho au macho…………..unaweza kuwa mtunzaji wa mwili wako lakini usipo tunza jicho lako na ikatokea jicho likapoteza nguvu yake ya kuona basi maana ya wewe kupendeza hutaiona bali itakuwa kwa wengine hivyo itakunyima uhuru wa wewe katika kuwa na changamko la kweli na kuamini kile wanachokisema kuwa ndicho kweli au sicho kweli.

Pindi unapokosa macho basi yako mambo mengi utakosa kupata radha iliyokamili kwakua utakuwa unaishia katika kutumia milango ya fahamu iliyobakia. Kwakusema hivi hakuna mtu namtenga au namdharau kwakua kila kiungo cha mwili ukikosa kunasuluba yake….lakini neema ya Mungu inatosha sana.

Ni jambo la kawaida kwa mtu ambaye aliyepoteza uwezo wa kuona au tunaita ulemavu wa macho mtu huyu anakuwa anatumia sana hisia na umakini katika kusikia (sikio), ni jambo jema kwakua ni njia iliyobaki kwa yeye katika kuleta uelewa wa mambo yanayoendelea katika ulimwengu wa yeye alipo,

Nipende kusema kuwa jicho ni moja njia inayotumika katika mawasiliano katika kuleta uwelewa wa mtu na mtu hivyo ni seme kuwa jicho linatafsiri kwakua linaweza weza kuonyesha hali ya kufurahi, hatari au hali ya kuvutiwa na hata hali ya kushawishi hizi ni kazi zisizo rasmi sana japo zinaongoza katika matumizi hasa kataika ulimwengu wa sasa wakiongozwa na vijana.

Ni pende kusema kuwa jicho linatoa tafsiri, majibu na lina ishara maalum katika kuonyesha kwendelea mbele au kubaki palepale au kuacha kabisa!!

Nipende kusema tafsiri ya jicho inabebwa na;

i.uelewa wa ufahamu wako

ii.imani yako kwa Mungu

iii.nafasi ya jambo lililotokea katika moyo wako

Ni kweli jambo linaweza kuwa ni moja lakini kila mtu pindi anapoliona anatoa tafsiri yake ilibebwa na macho yake katika hiyo tafsiri ndio inaweza kumpa kushinda au kushindwa………mathalani daudi wakati anaenda kumkabili goliati japo wote Israel walimuona na kila jicho la kila mmoja lilitoa tafsiri yake lakini daudi alipomuona naye macho yake yalitoa tafsiri yake ambayo kiukweli ilikuwa tofauti na tafsiri na watu wengine kutokana na uelewa kile kitu anachokiamini.

Uwezi kushinda kama macho yako hayajabeba tafsiri sahihi ya jambo linalokukabili kwa maana nyingine tafsiri ya macho yako katika jambo ambalo litakalo kukabili ndio limebeba kushindwa kwako au kushinda kwako.

Wengi wanatafsiri katika macho yao ambayo sio sahihi hazijaambatana na uelewa katika fahamu zao bali wao wana amini kwakua kilisha fanyika basi wanaamini hivyo na wala sio kitu kingine hivyo wanashindwa kubeba nguvu na ujasiri wa kudumu katika utendaji wao.

Macho yako yakikosa kukupa tafsiri basi ni rahisi kila kitu kiwe na nafasi katika maisha yako kwakua ujui kuwa hiki ni haki yako na kile si haki yako. Hakikisha macho yako yanakupa tafsiri ya Mungu kwa usahihi iliikupe kuyakabili mambo katika uvuvio na uweza wa Roho mtakatifu.

Unaweza kufa kabla ya wakati wako au kuishi katika hali ya mateso kwakuto kuwa na tafsiri ya macho yako katika jambo linalo kuzunguka,

Ukitafuta ushindi katika maisha yako lazima uwe na tafsiri iliyo sahihi katika kila linalokukabili!


Imeandaliwa na;

Cothey Nelson…………………………………………………0764 018535