Jumanne, 30 Desemba 2014

WIMBO WANGU!



USIYESHINDWA;




Ningependa hili NENO likawe wimbo wako, unaotawala akili yako na iliyopata nafasi katika moyo wako na udhihirisho mkuu katika maisha yako. Ni kweli tunamshukuru Mungu kutokana na namna tulivyoishi mwaka 2014 haijarishi ulikuwa upande upi kwako kama ulikuwa mwepesi au mzito katika yote bado tunamuona Mungu katika yote hasa yaliyo inje ya akili au uwezo wetu binafsi.

Naamini wapo watu katika dunia tuliyonayo watu hawaoni maana ya kumshukuru Mungu katika mwaka tunaomalizia kwa masuabu waliyo yapata na pia kuna wengine wananafasi kubwa katika kumshukuru Mungu katika mazingira ya wenye ufahamu na wasio na ufahamu unaomwezesha mtu katika kufanya jambo stahiki.

Siko hapa katika kuwaambia mfanye tathmini katika maisha yako zaidi sana ningependa uanze kuona katika muono mwingine wa kumwezesha Mungu aweze kujidhihirisha vile alivyo katika maisha yako. Hili ni neon ambalo mimi binafsi nalipenda sana kwani nimejifunza kumuona Mungu sana pindi ninapoamini kuwa yeye Mungu ajawai shindwa kutokana na muonekano wake ulivyo, japo kushindwa ni kibinadamu bali Mungu vile alivyo ajawai shindwa katika kutekeleza mpango wake.
Hili ni neno kwa watu wengi uanza kulitumia lakini kamwe hawawezi kumudu kulitumia kutokana na nguvu ya macho ya mwilini yaliyomkuta petro.........(asomaye na hafahamu).

Kweli neno hili likatoe nafasi iliyokubwa katika maisha yako na kuona fahari ya Mungu katika maisha pamoja nawe! Ni lazima umuone kuwa ashindwi ili aweze kukuwezesha katika kushinda kwasababu ukweli ni yeye anashinda kupitia wewe. Na hata kama umeshindwa mara nyingi sana lakini jua kwamba yeye Mungu ajawai kushindwa kamwe kwakua yeye ni zaidi ya chochote.........na macho yake hayawezi kuzuiliwa na chochote.

Ukweli kibinadamu kuna muda unachoka lakini tambua kitu kimoja kwamba Mungu katika uumbaji wake alikutana na mambo mengi lakini kamwe hakuona kile ambacho kinaweza kuwa ni changamoto kwake au kumzuilia yeye asiendelee na mpango wake. Vile alivyokuwa akifanya yote ndivyo hivyo ataweza kufanya yote kati ya yote yanayokukabili endapo tu ukimkubali katika maisha yako                       ( kumwamini ).

Unahitaji kumwelewa Mungu kwa mapana yake kwakua yeye jinsi alivyo anajitosheleza na hana kikwazo kwake ambacho kitamfanyaasiweze kukutosheleza zaidi sawa na uwitaji wako katika haya yote jambo kubwa ni KUMJUA MUNGU!

Lazima utofautishe kumjua Mungu na kujua habari za Mungu kwani kumjua Mungu sio kujua habari za Mungu kwakua kujua habari za Mungu hazitakusaidia zaidi sana ni kumjua Mungu mwenyewe, kwani katika yeye.

Kumjua Mungu ni namna unavyopata maongozi ya KImungu katika shughuli za kila siku kwakua tunajua kileunachojua ndicho unkiweka katika utendaji inaweza kuwa katika ujuzi mbalimbali mathalani upishi wa kisasa, namna ya kutumia bidhaa kwa ufanisi au kuendesha biashara zako kwa faida.

Kumjua Mungu akuishii kwenda kanisani tu bali MPASUKO WA UFAHAM ULIOJAA MUNGU.


Imeandaliwa na;
                          Cothey Nelson................................................................0764 018535

Jumatatu, 29 Desemba 2014

UKO WAPI USALAMA



UKO WAPI USALAMA;



Hichi ni kitu ambacho kila binadamu anahitaji kuwa nacho ili kumwezesha kuishi kwa furaha, maendeleo na amani katika maisha yake, na endapo usalama utakapo kosekana sahau kusikia maendeleo ya mtu husika au jamii kwa ujumla. Pia ni pende kusema wazi tu kuwa kuna usalama wan chi na usalama wa mtu binafsi na ni wazi nchi inaweza ikawa na usalama lakini watu wake wasiwe na usalama wa maisha yao na pia watu wanaweza wakawa na usalama lakini nchi ikawa katika hali tete..........unaweza kushangaa lakini kubwa ni hili hakuna la maana sana hapa duniani kama kuhakikishiwa usalama.

Ni jambo la kawaida kusikia watu wenye imani za kidini wakiliombea taifa lao amani na usalama, wakitumaini Mungu atawasaidia na wakati nao wakijitaidi kuimarisha vyombo vyao vya usalama LAKINI pamoja na hayo biblia yangu inasema yeye ailindae nyumba au nchi bila yeye ni kazi bure lakini Mungu akiilinda usalama wake ni wakudumu sana.....tuachane na hili tuje usalama ambao watu utafuta unapatikana wapi katika dunia tuliyonayo tuna waona watu wakitafutasana usalama wa mioyo yao kuliko wa miili yao, wapo watu walio mwamini Mungu wakitegemea kwake Mungu kuna usalama wa kudumu wamevumilia sana baadae wakaamua kuachana na imani zao za kumwamini 

Mungu wa kweli na kwenda katika imani zisizo za kweli.......... na katika kupata burudiko lao kwa muda basi baadae ikawa ni mateso na hata kuitukana imani yao.

Kuna usalama wa duniani ambao mara nyingi sana unaletwa na fedha katika kusukuma maisha ya mtu kujiimarisha kiusalama mathalani kununua vifaa vya moto , pistol au bunduki na wengine hata kuweka usalama wake kupitia walinzi na mitambo yakuona na pia kupitisha nyaya za umeme katika nyumba yake na usalama wa kimbingu huu ndio usalama ulio imara sana wa kwli uwa unatawala duniani hata mbinguni huu usalama ambao hauonekani kwa macho ya nyama ulio imara sana na kamwe hauwezi kukosea na hauwitaji matengenezo yoyote wala kubadilisha vifaa.


JE! KWANINI USALAMA WA MBINGU HAUWASADII WAKRISTO WA SASA?

Ninapozungumzia wakristo sina maana wote haiwasaidii bali na zungumzia wale watu ambao wanashindwa kudumu katika katika usalama wa kimbingu. Biblia inasema wazi katika siku za mwisho....... manabii wengi watajitokeza nao wakifanya ishara nyingi sana na kuwavuta walio wengi ya mkini hata wateule wa Mungu.

Ki ukweli matatizo yamekuwa mengi sana katika dunia tuliyonayo sasa na mabya zaidi haya matatizo yamewakumba wote wanampenda Mungu na wanaipenda dunia na utatuzi wa matatizo haya yamekuwa ni shida katika kijua ipi ni njia sahihi na ipi si njia sahihi pamekuwa na mvutano mkubwa sana......kiasi kwamba hata waliokuwa na imani thabiti wameanza kuteteleka hili si jambao ambalo Mungu analikusudia kuwa watu wake watoke chini ya mawanda yake ila shida nini?

Zipo sababu kuu mbili ambazo mimi naziona kama ni tatizo kwa watu waendao kanisani;

i.watu wengi wanaishi maisha yao na sio ya kristo

kwenda kanisani na kufanya mambo ya kikristo sio maana nzuri ya kukuita wewe ni mfuasi wa kristo bali jambo la muhimu sana ni namna gani moyo wako unavyo kwambia au unavyo kupa picha yako na Mungu ni nzuri au ni mbaya.
Kama kufanya mambo ya Mungu hata punda aliongea katika kutekeleza lile jambo ambalo Mungu alitaka kumwambia nabii wake, hivyo kwakutumika pale haina maana kuwa ataenda mbinguni katika matendo yake.
Lazima ujue maisha ya ukristo sio dini wala taratibu za mchungaji wako bali ni vile moyo wako unavyo kushuhudia kuwa wewe ni nani mbele za Mungu.............biblia inasema kama dhamiri yako haita kuhukumu una ujasiri mbele za Mungu.
Ni lazima ujue Mungu hakutuita ili kwamba tuwe watumishi wa watu bali tuwe watumishi wake kwa kusema hivi si zungumzii msiwaheshimu wazazi wa kiroho la asha bali fanya yote ukijua aliyekuita ni Mungu na wala si mtu.


ii.wakati na jambo lake (majira)

usiishi maadamu siku zinaenda tu au siku zipo bali tambua ulikuwa ulizaliwa na sasa uko hatua hiyo nab ado unaelekea hatua nyingine. Usipoutambua wakati jua wakati utakukumbusha kwa namna yake yenyewe.

Yesu alitoa mfano huu kulikuwa na watu kumi wako kati yao waliweka mafuta ya kutosha na wengine mafuta hayakuwa tosha sio kama walinyimwa bali ni vile mtazamo wao ulivyokuwa kuona mambo kilahisi hata kabla bwana harusi kuja wale waliobeba mafuta machache waliisha nabado safari ni ndefu.........jua kama kweli umeamua kumjaza Mungu tumia wakati huo vizuri ili usije wakati huo ukaja kukusumbua.

Unapopata wakati wa kusoma neon basi lisome sana na unapopata nafasi ya kuomba basi omba sana vilevile nafasi  ya kutumika basi tumika.........ni kama mwanafunzi anapokuwa akisoma katika kujiandaa na mtihani wake ili hakikishe anafanya vizuri ndivyo unaye mwamini Mungu kufanya hivyo. Mwanafunzi mjinga ujiandaa mahali ambapo mtihani umeshawadia.............maandalizi mabaya upelekea matokeo mabaya.


Usimlahumu mtu bali lahumu sana matumizi ya wakati ulionao!!!


Imeandaliwa na;
      

               Cothey Nelson.......................................................0764 018535

Ijumaa, 19 Desemba 2014

NAFASI YA MUNGU




KUITAMBUA NAFASI YA MUNGU;





Unaweza ukaishi na mtu vizuri katika kushikiliana nae kwa kila kitu lakini pindi utakaposhindwa kuitambua nafasi yake, hauwezi kupata kwa utoshelevu wote yaliyo ndani ya mtu unaye kaa siku zote. Mtu kutambua nafasi yako katika maisha yako hiki ni kitu cha maana sana kuliko chochote kwani pindi mtu anapotambuliwa katika nafasi aliyonayo basi hapo anakuwa zaidi hata ya kumpa almasi yoyote au chochote ambacho utaona cha maana katika maisha yako.

Ninapozungumzia kuitambua nafasi ya Mungu katika maisha yako uwa ninazungumzia swala zima unaishije naye na Mungu katika maisha yako yeye ana nafasi gani katika ngazi hipi anasikilizwa na katika mambo yapi asikilizwi! Kuitambua nafasi ya Mungu ili sio swala la akili tu au lakujua na kujibu mtihani tu bali hili ni swala zima namna unavyomfanya Mungu kuwa nguvu katika maisha yako au kiongozi,dira na njia katika maisha yako tena wakati wote pasipo kuangalia haya ni majira gani au ni wakati gani au niko na nani!

Ukweli ninapozungumzia swala zima uwasizungumzii swala la kutoa Dhaka kamili, kuomba au kusoma neon hata kutii taratibu za ibada na kuaminiwa na mchungaji wako ni zaidi ya hapo kwani mahali ambapo Mungu anahusika katika maswali ya maisha yako kwa ujumla akibebwa na moyo wako ulio mjaa yeye kwa ukamilifu.

Kawaida hakuna mtu atafurahi kwakua anaishi na mtu bali furaha ya mtu ipo mahali ambapo anajua nafasi inathaminika kupewa nafasi iliyokamilifu tena katika ubora wake............biblia inasema watu wawili wataendaji kama hawajapatana.

Mungu afurahi tu kwasababu tu unamtumikia yeye kwa kawaida ya utaratibu katika maisha yako bali yeye uangalia sana jinsi gani unampa nafasi katika maisha yako, pindi atakapo tambua kuwa yeye umempa nafasi katika maisha yako basi kila jambo ukalo lifanya litapata kibali katika Mungu.
Mungu ashawishiki kwa vitu ambavyo unaweza kumpa Mungu katika kuonyesha unampenda zaidi ya kumpa nafasi ya kweli katika maisha yako ndicho kitu cha maana sana kwake kuliko chochote...............samweli ana mwambia sauli je! Mungu anapendezwa na sadaka ya kuteketezwa kuliko sauti yake!!!!!!!!!!!!!

Mathayo 7:21-24..................sio wote wasemao bwana bwana watakao ingia katika ufalme wa Mungu bali ni yeye afanye mapenzi yangu.....wengine watakuja kwangu na kusema bwana atukutoa kwa jina lako au kutoa unabii bali nitawajibu siwajui nyinyi kamwe ondokeni ninyi mtendao maovu!!!!!!!!!!! Itakuwa siku ya kilio na kusaga meno.

Hakuna mtu atayependa kuona kazi anayo ifanya harafu ikawa haina maana yeyote.............paulo anasema nisije nikaubiri wengi halafu mimi mwenyewe ni kawa mtu wa kukataliwa.......hata Mungu afurahi wala ategemei ila ni wewe unasababisha mazingira haya yatokee.

Hili jambo lazima ulipe kipaumbele sana kuliko jambo kwani kama hauta litilia mkazo linaweza kuleta madhara katika maisha yako ambayo ukuwa kuyategemea wala kuwaza kwa kuwa kila tendo lina malipo yako.


Imeandaliwa na:
      

                                Cothey Nelson.......................................................................0764 018535





MUNGU AFURAHISHWI KWA VITU BALI NAFASI ULIYOMPA KATIKA MAISHA YAKO!!!!!

Jumanne, 16 Desemba 2014

MATESO YA FEDHA





UTUMWA WA FEDHA;





Unaweza kuwa adui wa dunia nzima lakini kamwe hauwezi kuwa adui wa fedha, fedha kila mtu ni rafiki yake na laiti tungetoa nafasi ya watu kuchagua rafiki na fedha angekuwa ni mmoja kati ya hao watakao chaguliwa basi sina shaka watu wengi wangeenda upande wa fedha,kwa kusema hivi sina maana yakusema kuwa fedha ni mbaya bali na zungumzia swala zima la utumwa unausiana na fedha........ni jambo la kawaida kusikia mtu ametoloka au amekimbia kutoka sehemu moja na kwenda sehemu nyingine kwa sababu ya fedha na sikuacha mbali uchumba na sasa unavunjika kwa sababu ya tatizo la fedha.


Usipokua makini sana utaona jambo kama la mzaa fulani lakini ni kifungo kikubwa ambacho kweli kinapoteza watu katika familia, watu kuharibu miili yao kwa sababu ya utumwa wa kifedha.................!

Si pingani na fedha hata mimi naipenda sana fedha kwani katika maisha yangu fedha ina sehemu fulani japo sio kubwa kwani mimi naweza ishi bila fedha ila fedha haiwezi kuishi bila mimi, kwasababu fedha imemkuta mwanadamu na yeye ndiye aliitengeneza japo sasa hiyo fedha sasa ina mtawala binadamu kama hauamini basi tujongee pamoja katika ujumbe huu  pamoja katika kusoma......!


Ni kweli kiwango cha fedha ulichonacho ndicho kinachoamua uishi vipi yaani uvae nguo gani! Ule chakula gani! Uishi katika nyumba gani! Na hata usome katika shule ipi au chuo kipi..............unapokuwa na fedha haya mawazo yaliyokithiri katika fahamu za watanzania wengi yanapungua kama sikupotea kabisa.

Na vilevile unapokuwa kuwa na pesa inakupa hali ya kujiamini na hata kunawiri kwa wakati fulani japo watu wanasema fedha haiwezi kununua uzima au kukionga kifo mimi na sema fedha ni kitu kizuri kwani kuna wakati kinakupa heshima na kuwa na staa katika jamii yako na hata katika ukoo wako.

Pamoja na uzuri wote huo unaoletwa na fedha lakini tambua kichwa cha somo letu kinaitwa UTUMWA WA FEDHA sasa huu utumwa uko vipi na nitatambuaje kuwa sasa hapa fedha inanikosesha haki yangu .........kwakusema hivi sina maana watu wasitie bidii katika kuahakikisha wanapata mkate wao wa kila siku.

Ni seme kuwa hakuna kitu kibaya kama utumwa wa fedha kwani utapelekea umasikini ulikithiri, kifo na hata kuharibiwa mwili wako yaani ya mwili wako kukosa thamani ile ulio zaliwa nayo.
Mungu hafurahii hali ya sisi kuwa watumwa wa fedha bali ufurahi kuona sisi tumekuwa watumwa wa kristo japo yesu anasema.............si waiti tena watumwa bali ninyi ni marafiki hili ni neno ambalo limebeba moyo wangu lakini sasa hivi imekuwa ni tofauti kabisa na vile ilivyopangwa.

Biblia inasema uwezi kuwa mtumwa wa mwa bwana wawili lazima utaacha kimoja na kuutumikia kingine hauwezi kutumikia fedha na MUNGU. Hii ni halisi sasa hivi utumwa uko kanisani na dunia nzima kwa wale ambao wamekumbwa na janga hili utakuta mtu yuko tayari kuua mtu ili apate fedha na ukatiri wowote ili mradi apate fedha tu.

Wako watu wengi sana wanakatisha ndoto zao kwasababu ya utumwa wa fedha  na mbaya sana wako watu wengi wanaiacha imani yao japo wanaenda kanisani, hili jambo si maumivu katika familia tu bali ni maumivu hata katika moyo wa Mungu.

Usifurahie tu kwasababu unafedha bali furahia kwasababu unamstakabadhi mzuri katika maisha yako yaliyo mjaa Mungu kwa ukamilifu. Tambua wakati haujirudi kwa sababu ukishapita umepita na mambo yake baliunaweza kujifurhisha tu lakini ukweli wakati utakuambia wenyewe wakati unalia au unacheka inakutegemea wewe.

Tambua fedha haina mahali pa kukupaleka isipo kuwa Yule aliyekujua tangu misingi ya dunia anayo hatima njema katika maisha.


KUITUMIKIA FEDHA NI SAWA NA KUMSALIMU MWANAO SHIKAMO............!!!

unaweza kukataa lakini ndicho unachokifanya pindi utakapoanza kuitumikia fedha ambayo imefanywa na mwanadamu, unaweza kujiona wewe kuwa ni wakisasa kumbe ndio unapoteza dira yako ambayo kwahiyo umelindwa na kuwepo unafikiri gharama zote Mungu amezingia kusudi uwe mtumishi wa fedha au wake.

THAMINI ASILI YAKO KWA WEWE KUMPENDA MUNGU KWA DHATI........!!!

Imeandaliwa na;
         


              Cothey Nelson..................................................................................0764 018535