Jumamosi, 6 Septemba 2014

ILI KUPATA LAZIMA UPOTEZE



ILI KUPATA LAZIMA UPOTEZE!!!





I wakorintho 9:24-25

…………na kila ashindanaye katika mchezo hujizuia katika yote.

I wakorintho 9:26-27
…………bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe nikiisha kuwahubiri wengine; mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa.

Katika dunia tuliyonayo mambo mengi tunayoyaona kuna watu wamepoteza vitu vingi sana na wewe unafurahia matokeo ya watu kupoteza mathalani wako watu wamepoteza muda wao,uhai wao, nguvu zao na ufahamu wao.

Katika ujumbe huu neno hili kupoteza nimelitua katika mawanda mbalimbali mathalani hali ya kutoa kwa ujumla wake fedha, nguvu na muda katika lililo jema, matendo ya kujigharimu kwa ajili ya wengine katika hali njema.

Ni jambo la kushangaza sana watu wengi wanapenda kupata sana lakini hawako tayari kupoteza pasipo kujua wakati mwingi msingi wa kupata ni kupoteza. Kwa mkristo yeyote aliye wa kweli lazima kanuni hii haiweke katika utendaji wake ilikupata ya rohoni lazima uyapoteze ya mwilini!

Pamoja na hayo lazima ujue kwamba unapoteza nini na kwa namna gani unapoteza haya yote ni muhimu sana ili uweze kufanikisha yale ambayo unatakiwa, na kuna siri kubwa sana katika kupoteza kwani hali hii ni inaashiria kutoa kitu kimoja ili kiingie kitu kingine, na kawaida kinatoka kitu kidogo na kuingia kitu kikubwa.

Ni kweli yako maumivu makubwa sana katika kupoteza(kutoa) lakini hayo maumivu yatazimishwa baada ya kupata(gain) hii ipo wazi hata pindi mkulima anapofanya kazi uwa vitu vingi anavipoteza nguvu, fedha na mangine mengi lakini mwisho anakuwa na furaha kupita ile ya awali baada ya kupata.

Watu wengi ujizuia sana ili wasipoteze hasa kitu ambacho wanachokipenda sana kwakua hawajui nini kitatokea baada ya hapo lakini ni vizuri ujue kwamba kujuzuia kupoteza wakati mwingi ni kujizuia kupata.

Yesu alisema….inanibidi mimi niondoke ili aje huyu Roho mtakatifu atakaye wafundisha na kuwa kukumbusha yote!

Japo yesu alikuwepo duniani katika lengo la ukombozi na pindi alipomaliza ili mlazimu aondoke japo watu wengine wanamwitaji azidi kuwa nao, lakini yeye alitambua kuwa ni vizuri yeye aondoke aje huyo Roho atakayekamilisha.

Lazima akili yako ikubaliane kuwa kuna mambo mengine ni muhimu kupoteza ili uweze kuwa katika namna nyingine hata kama itakugharimu kwa muda fulani kwani ni muhimu ugharimike leo kwa pumziko la kesho kuliko kinyume chake.

Kupoteza ni tabia ya Mungu mwenyewe yesu alisema….nautoa uhai wangu kisha nita utwaa tena na baada ya kutoa uhai wake na kurejea tena hawezi kuwa vilevile alivyokuwa vile alivyokuwa awali.

Usitegemee kuwa mkubwa sana kama ukiwa hauna tabia ya kupoteza(kutoa na kusahau) kwakua vile unavyo jigharimu ndivyo utakavyo stawi ( kujigharimu katika akili njema-maarifa sahihi) na kama hauta weza jambo hili hawezi kuwa sawa na mtu unayemtamani, kwakua ipo siri kubwa katika kupoteza na kusahau kabisa.

Usipendelee kushangaa tu vitu vilivyotokana na watu katika kupoteza na wakawa watofauti bali ata wewe unaweza kujiunga nao katika kupoteza kuliko kwema kwa hatua njema ya maisha yako.

Pia katika kupoteza lazima uwe tayari kutoeleweka na watu wengine wanaweza uonekana kama wana kuhurumia sana bali kumbe ndipo wana kuangamiza.




Imeandaliwa na ;
                    
                                Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com                     



Alhamisi, 4 Septemba 2014

IN THE DARKNESS



KATIKA GIZA KUNA KUSTAWI;


(Secrete in the darkness)>siri iliyondani ya giza

Ni dhana iliyokosa mvuto/uhalisia wa kawaida kusema kuwa katika giza kuna uwezo wa kustawi

Je! Katika mji huu atatoka mkombozi…. Japo ilikuwa kama haiwezekani lakini ukweli katika hali hiyo ya mshangao na ndipo mkombozi alipotokea.

Ni hali ya kawaida kuwa katika giza kuna mambo mabaya yanatukia yakutisha na hata ya kufedheesha 
ambayo hayakubaliki katika jamii yetu pamoja na mambo hayo napenda utambue giza ni majira na hivyo utegemea sana mtumiaji na sio usiku wenyewe.

Tumekuwa tukishuhudia wachawi wakitenda kazi nyakati za usiku (giza) na ikisemekana kuwa hawa ni wana wa giza hivyo ufanya mambo katika giza ili kuonyesha uasilia wake. Pia yako matukio kama ujambazi usemekana sana ufanyika wakati wa usiku kuliko mchana.

Lakini na penda kusema hakuna wakati mzuri kama wakati wa giza!!! Huu ni wakati vitu vingi uimarika na kuwa bora na tishio sana

Yesu! Alikuwa anaomba sana usiku kuliko mchana…….japo alikuwa anauwezo kuomba popote na muda wowote na anga likapisha maombi yake kwenda yanakotakiwa.

Giza ni kipindi kizuri sana kwani ni kipindi kinachoashiria nuru inakaribia pasipo giza kuondoka basi nuru haiwezi kutokea.

Ni kweli katika muonekano mzuri hamna mtu angependa kufanya mambo yake usiku kwani wana amini usiku ndio muda mzuri wa kupuzika kwa ajili ya kesho kwa ajili ya kuendelea na shughuli nyingine……….lakini pamoja na hayo sio wote wana kuwa katika usiku na wanapata fulsa ya kuiona kesho namna vile wanavyotegemea.

Giza ni hali ambayo unaweza ukawa unamategemeo lakini bado ukawa na mashaka kwakua hiyo kesho haiko mikononi mwako.

Hichi ni kipindi unaweza kuona jambo lako haliwezekani au hauta weza kulifikia kwakua kila dakika unaona giza tu wala haoni mwanga ukitokea kwa haraka kama vile unavyotegemea.

Unapokuwa katika kipindi hiki ni wazi unaweza kujiona unaweza kuisi kama sio kuona uko wewe na usiku tu na wala hakuna mtu mwingine aliye pembeni yako.

Hichi ni kipindi usipo kuwa makini sana unaweza ukatamini kujiua au kutomea machoni pa watu na kamwe usionekane lakini yote hayo ni kwasababu tu giza limekutana. Na penda sana hichi ni kipindi cha kuzidi kuimarika sana na kuwa na nguvu sana.

Kweli katika kipindi watu wengi wanaweza kupata ugonjwa wa moyo kwa namna ulivyolipokea jambo likakuingiza katika usiku wako, japo na kubali giza ni mahali panapotisha sana na kwa kifupi akupendezi kwa kuwa uwapo huko hakuna furaha yoyote inayo zaliwa na mwili ikawa na mwendelezo usio koma.

Ikitokea kama bado haujauingia usiku/giza basi jua bado hautaweza kuona fahari ya dunia na kusema nimeijua dunia na watu wake pamoja na mambo yake. Kwa binadamu yeyote lazima aingie gizani lakini utatokaje inategemea sana uwezo wa uelewa wa akili yako pamoja na wepesi wa kubadilika  sawa katika mwelekeo unakotakiwa.

Hakuna nguvu iliyoimarika sana isiyozuiliwa kama nguvu inayozaliwa katika giza kwakua nguvu inayozaliwa hapo inakuwa imebeba ujasiri zaidi, uhalisi wake, kwakua kipindi hiki akili yako in aona giza tu hakuna mwanga ambao unaweza kutokea.



Imeandaliwa na ;                                                                                                                   
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com