Jumanne, 13 Februari 2018

KUTEMWA AU KUKUBALIWA NA MFUMO!






MUSA ( kushindwa kuingia kanani japo alikusudiwa kuingia kanani)

Kumbukumbu la torati 34:1 Musa akapanda kutoka uwanda wa Moabu mpaka mlima Nebo,    hata kilele cha Pisga kukabili Yeriko. Bwana akamwonyesha nchi yote ya Gileadi hata Dani;

                                              2 na Naftali yote, na nchi ya Efraimu na Manase, na nchi yote ya Yuda,    mpaka  bahari ya magharibi;

                                              3 na Negebu, na uwanja wa bonde la Yeriko, mji wa mitende, hata mpaka Soari.

                                               4 Bwana akamwambia, Hii ndiyo nchi niliyowaapia Ibrahimu, na Isaka, na Yakobo, nikisema, Nitawapa wazao wako. Basi nimekuonyesha kwa macho yako, lakini hutavuka huko.

Swala sio kutembea na Mungu tu, namna unavyotembea naye ina maana kubwa sana unaweza kuimarisha ushirika wenu hama kuubomoa au kutengeneza mpasuko.

ELIMU ( unapokuwa katika mfumo wa elimu, unapoanza darasa la awali unakuwa na matarajio mengi lakini namna unavyoiendea ndoto yako mfumo unaweza kuruhusu uifike hama usiifike)
-          Sio wote waliofeli walikuwa hawana akili.

Watu wengi wamekuwa makini sana na upepo wa watu kuona wanavyosema ili kutaka kuwafurahisha na kusahau mfumo unaoendesha mambo. ( imekuwa ni rahisi watu kujaa sifa kuliko uhalisia)

KAZINI ( ofisini ), mfumo ukikukubali unaweza jikuta unadumu ofisini na hata kupanda daraja katika uongozi lakini mfumo usipo kukubali kukutema ni jambo lisilo pingika.

Kila kitu ili kiende kinahitaji mfumo fulani ( instruction-maelekezo ) unaweza kuwa rasmi au sio rasmi, chochote unachokiona katika ulimwengu huu jua kuna mfumo ndani yake unakiendesha!

Na ni rahisi kumpata mtu hama kumjua mtu endapo utajua mfumo wake ( mwenendo wake) na unaweza kufanya afurahie maisha yake au kuchukia.

Na vilevile ni rahisi kuishi na mtu endapo utajua/kujifunza mfumo wa maisha yake hama kumpeleka katika mfumo uliobora zaidi ambaye yeye ataumudu.

Na ni kawaida uhuru katika sehemu yeyote ulipo ahuhitaji kupretend ( kujifanyisha ) hama kujilazimisha bali tia bidii kuujua vizuri mfumo wa mahali ulipo.

Usipende sana kujulikana ili uwe maarufu tu haraka haraka bali tembea katika mfumo ili wenyewe ukutambulishe kwa wakati wake.

Kutembea katika mfumo wa Mungu unapoishi duniani!

2 Wafalme 20: 1 Siku hizo Hezekia akaugua, akawa katika hatari ya kufa. Isaya, nabii, mwana wa Amozi, akamjia akamwambia, Bwana asema hivi, Tengeza mambo ya nyumba yako; maana utakufa, wala hutapona.

 2 Basi Hezekia akajigeuza, akaelekeza uso wake ukutani, akamwomba Bwana akasema,

 3 Nakusihi, Bwana, ukumbuke sasa, jinsi nilivyokwenda mbele zako katika kweli na kwa moyo mkamilifu, na kutenda yaliyo mema machoni pako. Hezekia akalia sana sana.

 4 Ikawa, kabla Isaya hajatoka katika mji wa kati, neno la Bwana likamjia, kusema,

 5 Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.

 6 Tena, nitazizidisha siku zako, kiasi cha miaka kumi na mitano, nami nitakuokoa wewe, na mji huu, na mkono wa mfalme wa Ashuru, nami nitaulinda mji huu kwa ajili yangu, na kwa ajili ya Daudi, mtumishi wangu.

Kunakuwa na sababu rahisi ya Mungu kukuponya/kukutana na uhitaji wako pindi unapotembea katika mfumo wake.

Wakati mwingine Mungu anaweza asione maana ya kukufikisha katika kilele cha huduma yako kama tu unatembea nje ya mfumo wake, maana unaweza ukakosa kufaidi matunda ya huduma yako katika umilele.

Japo kuna uwezekano wa kufanya kusudi la Mungu na likawa na matokeo makubwa katika jamii yako lakini ukawa umelifanya nje mfumo wa Mungu kwa hiyo swala sio watu bali usalama wa roho yako.

Kuishi/kutembea katika mfumo wa Mungu uwa haina maana tu kuwa na maarifa katika huduma hama uzoefu ulionao katika huduma, kusoma neno hama kuomba sana BALI ni kuishi katika kusudi ambalo Mungu amekuumbia kwalo kana kwamba Mungu anaishi badala yako.

Ni muhimu Mungu anapokuona wewe duniani jinsi unavyowaza, unavyoenenda ajione yeye mwenyewe ( Ni kama Mungu anajiangalia kwenye kioo chake akuone wewe na yeye hakuna utofauti ).

INAITWA KESHO! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………. 0764 018535