Jumanne, 27 Juni 2017

SURA YANGU



SURA YANGU


Moja ya kitu kinacho dhihirisha huyu mtu anajipenda ni muonekano wake! 

Na kitu kimoja wapo kinachozingatiwa sana katika muonekano ni sura hama kwa jina jingine uweza kuitwa RECEIPTION (Mapokezi), ni seme swala la muonekano mzuri uwa alina jinsia wanaume au wanawake wote upenda kuwa na muonekano mzuri na zaidi unao vutia.

Na ni rahisi mtu akasahau kusafisha miguu yake kuliko sura yake, kwa maana sio rahisi kukuta mtu amewekeza sana kufanya miguu yake ing’ae na kuacha sura yake ifubae na huku ana amani zote na pengine aseme “nafanya hivi kwasababu mimi naipenda sana miguu yangu kuliko sura yangu” na huku ana uwezo wa kufanya vyote.

Ila kwa kiasi kikubwa unaweza kukuta mtu anapenda sura yake, miguu yake pamoja na ngozi yake ili kukamilisha muonekano mzuri ulio kivutio kwa wengi na kuwa faraja kwake! Na muonekano wa mtu utegemea uchumi wa mtu, na aina ya ngozi aliyonayo ( maana kuna baadhi ya ngozi hata utumie mafuta, matunda uongeze na mazoezi bado haibadiliki).

Mbali na hayo pia sura ya mtu utumika kutambua hisia za mtu, kwaku mwangalia pana uwezekano wa kutambua hali ya mtu kama amekasirika hama anafuraha au anacho ongea ana kimaanisha hama feki na wengine wana neema zaidi pindi wanapo mwangalia mtu uweza kutambua kuwa huyu amekula hama ajala japo anaweza asimsaidie hiyo hela ya kula,

Pia muonekano wa mtu ukihusishwa na sura uweza kutambua chimbuko la mtu/ asili ya mtu husika aliko tokea na wengine kwaku mwangalia sura yake uweza kukadilia miaka ya mtu husika………SURA YANGU!

Katika hali ya kawaida jambo baya linapo mpata mtu utoshangaa maneno haya aki yasema…..nitaiweka wapi sura yangu! Inawezekana amefanya yeye hama limetokea miongoni mwa familia yake mathalani mwanae aliyekuwa anajivunia kwamba anapenda shule matokeo yake ya mtihani kapata daraja ziro (0)

Kikawaida jambo lolote zuri unapolifanya utapenda watu walijue na hapo utatembea kifua mbele alikadhalika jambo baya linapokutokea hutapenda lijulikane na watu wengi, na muda mwingi hutapenda uonekane na watu. Japo wakati mwingine unashindwa kutambua unaweza ukajifunza  kupitia kukosea na sio kujilaumu na mwisho kukata tamaa.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………0764 018535

Jumanne, 20 Juni 2017

UNAWEZA.



UNAWEZA


Katika maneno ambayo watu wengi upenda kusikia wakiambiwa mojawapo ni hili neno, na unaweza kuona tabasamu na changamko katika sura ya mtu pindi anaposikia neno…UNAWEZA,

Unaweza kufanya misuli na mishipa iliyo kuwa katika hali ya kusinyaa ikawa imara, unaweza kukatisha kisima cha machozi katika macho, unaweza kufungua mlango wa moyo wa mtu uliofungwa kwa muda mwingi naam unaweza kurejesha usingizi wa mtu uliotaka kupotea, unaweza fanya mtu aliyefunga mlango kwa hofu kubwa ndani yake lakini ukakuta anafungua mlango na kutoka nje kwa ujasiri pindi atakaposikia sauti ikimwambia……..UNAWEZA!

Hili neno UNAWEZA linaweza  kukosa umuhimu wake kwa wakati fulani ila kuna wakati utaona fahari yake kuliko chochote, hii naweza fananisha na mtu anapokuwa mzima uwa haoni umuhimu wa dawa hivyo anaweza pita katika duka la madawa na kuona kama aina fulani ya duka linalo uza bidhaa fulani zisizo na tija kwake, lakini pindi ikatokea unaumwa ukapewa orodha ya dawa kwa ajili ya afya yake  hapo ndipo utakapoona duka la dawa kama lulu unayo hitaji isivyo kawaida……….hivyo kila neno lina majira/wakati wake ili kudhihirisha umaana wake!

Usijiwekee mipaka katika utendaji wako ila la msingi ujue jambo limekuja kwako kwa namna yake jua hilo jambo limejipima na likaona linatosha kuja kwako, likabili linaweza kukuvusha na kukupeleka katika hatua ya kuweza zaidi.

Ukijiwekea mipaka katika kuweza itakujengea hofu na hatimaye kushindwa kujifunza zaidi na mwishowe kujiona kutoweza ndio maisha yako.

UNAWEZA  linapaswa kuwa ni neno linalo tawala moyo wako ili kudhihirisha imani yako kwa Mungu ili naye aone utayari wako na kuonyesha ukuu wake!

Katika biblia kuna mtu mmoja ninge penda tumwangalie anaitwa DAUDI, karibu……………………….
1 Samweli 17: 45 Ndipo Daudi akamwambia yule Mfilisti, Wewe unanijia mimi na upanga, na fumo, na mkuki, bali mimi ninakujia wewe kwa jina la Bwana wa majeshi, Mungu wa majeshi ya Israeli uliowatukana.
                        46 Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.

                      47 Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.

                     48 Ikawa, hapo Mfilisti alipojiinua, akaenda akamkaribia Daudi, ndipo Daudi naye akapiga mbio, akalikimbilia jeshi ili akutane na yule Mfilisti.

                     49 Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.

                    50 Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.

                    51 Ndipo Daudi akapiga mbio, akasimama juu ya Mfilisti, akautwaa upanga wake, akaufuta alani mwake, akamwua, akamkata kichwa kwa upanga huo. Nao Wafilisti walipoona ya kuwa shujaa wao amekufa, wakakimbia.

Ni vizuri sana kuambiwa kuwa unaweza lakini ni vizuri zaidi kujiona unaweza kama daudi alivyojiona anaweza  japokuwa alikutana na vipingamizi vingi lakini namna alivyojiona kuwa “ninaweza kuleta heshima katika Israeli” akuweza kuruhusu ile namna anavyojiona ipotee kwasababu ya watu waliopinga mtazamo wake.

ANAITWA MUNGU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………………..0764 018535

Jumanne, 13 Juni 2017

MASIKIO YA WENGI



MASIKIO YA WENGI



Siku zote nguvu ya mtu ya kusema inakuwa pale utakapoona mtu/watu wanakusikia na wakati mwingine umakini wao unaweza kukushawishi kusema zaidi,

Uwa inakosa maana zaidi pale utakapo tumia nguvu kubwa kuongea, wakati hakuna anaye kusikiliza kwa jina jepesi wanaweza kukuita chizi kama hautakuwa unafanya mazoezi ya kuimba hama maigizo. (kwa maana rahisi raha ya kusema ni kusikilizwa)

Maana ya kuwa na sikio ni kusikia, japo unapoona sikio sio lazima huyo mtu awe anasikia kwani anaweza kuwa kiziwi lakini akakuangalia kana kwamba anasikia lakini sivyo!

Katika dunia imekuwa ni fahari ya mtu kusema na watu wengi! Imefika kipindi cha mtu kupata heshima kutokana na watu anaozungumza nao kama ni watu wachache au wengi heshima yake itabebwa sawa na watu anao waongoza, japo sina uhakika kama ni sawa!

Imekuwa ni changamoto kwa watu kutaka kuongea katika idadi kubwa ya watu na sio kwa maana ya kuwasaidia bali kutaka heshima au umaarufu, na amini ni mwalimu tu anapenda wanafunzi wachache ili aweze kuwa mudu vizuri na sio wengi ikawa shida kuwa mudu.

Imefikia kipindi kujua mahali penye watu wengi basi hapo ndio penye ubora, mathalani katika kikombe cha babu watu wengi walienda uko wakijiamini kuwa ndio suruhu ya matatizo yao! Lakini ukweli anaujua mwenyewe baada ya kunywa kikombe cha babu na kuona matokeo yake,

Hii imeenda mbali kidogo watu wengi upenda kuwa na mtu anayejulikana sana hama kusikilizwa na watu wengi  wakiwa wana amini kuwa ukikaa na waridi basi nawe utanukia. Japo ni ukweli kila mtu upenda kusikilizwa.

Upaswi kushangaa pindi mtu anapotaka kuchukua maamuzi fulani uwa ni lazima atafute maoni ya watu kuona hichi kitu ninachotaka kukifanya kuwa ni sahihi au la! Niseme tu jambo hili linakuwa la maana sana kama maamuzi yanayo husu kundi la watu lakini sio muhimu sana kutafuta ushahidi wa watu wengi katika jambo linalohusu ubinafsi wako linaweza kukugharimu ukaanza kutafuta nani wa kumlaumu.

MASIKIO YA WENGI! Imeathiri sana katika utendaji wa wengi;

Watu wamekuwa wakitumia nguvu kubwa ili mradi watu waendelee kumsikiliza kuliko kuwapatia ufumbuzi sahihi na wenye tija katika maisha yao,

Siku zote utakosa mwelekeo ulio sahihi kwakua wako watu watakuvutia huku na kule, wengine watapenda hiki na wengine watapenda kile kama utakuwa pale ili waendelee kukusikiliza utakosa kujua nini nifanye ili wote wafurahi maana utaki kuwapoteza.

INAITWA SIKU! BARIKIWA.
Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 6 Juni 2017

NITAIJUA BAADAE!

NITAIJUA BAADAE


Hakuna kitu kizuri kama kujua! Japo uzuri wa kujua unakamilika pale unapo jua na matokeo yake unapoyaona!

Kila mtu utamani kuwa na kesho nzuri lakini shida inakuja pale namna ya kuifikia hiyo kesho iliyo ndoto yako( iliyo beba kiu na shauku ya moyo wako)……… unaweza kukuta mwanafunzi alikuwa ana mipango yake labda baadae awe rubani, wakili, engineer, muhasibu, mwalimu na hata taaluma nyingine lakini mchakato  wake unaweza kubadilisha hiyo ndoto yake kutokana na matokeo ya kidato cha nne au cha sita kutokidhi vigezo vya kumwezesha kusoma masomo Fulani au taaluma aliyokusudia hama maamuzi binafsi, ukakuta muhasibu akawa mwalimu hama mwalimu akawa muhasibu,

Naam imekuwa ni rahisi kwa mtu kunung’unika, kughairi, kukasirika kwa jambo analolitegemea kushindwa kufanyika kwa muda alio upanga au namna alivyotaka mathalani unaweza kukuta mtu anaweza kujisikia vibaya kwa kuachwa na ndege na pindi akiwa kituoni analia na kusikitika pamoja na kumlaumu mtu anayedhani aliyesababisha hayo yatokee lakini ghafla akasikia ripoti kuwa ile ndege imelipuka…. Bila shaka ataondoka taratibu na kwenda sehemu ya mapumziko huku akimshukuru Mungu…..NITAIJUA BAADAE!

Wako watu wamegombana na kupelekea hata kuachana na wazazi wao, marafiki zao haya yote yanawezekana ni baada ya kutoa majibu binafsi katika kila tendo analofanyiwa hama analo hisi anafanyiwa na pindi ikatokea kuwa tofauti na uhalisia wa mawazo yake baadae ikapelekea majuto ya kudumu.

 Japo ni muhimu kutambua jambo kwanini hili limekuwa hivi au limekuwa vile lakini sio lazima kujisumbua sana ili mradi ujue tu! Unaweza kukuta mtu anasema kila jambo linalo nitokea uwa sili, silali mpaka nijue kinaga ubaga lakini yako mengi unahitaji ukubali tu kuwa UTAIJUA BAADAE SABABU YAKUTOKEA KWAKE.

Upaswi kukosa raha kwa jambo ambalo alina utatuzi uliobora au wenye tija katika ufalme wa Mungu maana huyo ndio ustawi katika maisha yako, 

Wafilipi 4:6 Msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Kuwa na wasiwasi kama hatima yako imeshikwa na watu wengine lakini kama iko mikononi mwa Mungu huna  haja ya kujitetea zaidi wewe simama katika nafasi yako, japo kuwa yako mengine yataonekana ni magumu kunyamaza kimya tambua kuyaruhusu yachanganye akili yako kunaweza kupelekea kuharibu hatima yako.

Kuongea sana akupelekei usalama wako kuwa mkubwa bali ufumbuzi sahihi upelekea usalama wako wan je na hata wa ndani kuwa wakutosha na kufanya uzidi kuwa bora katika utatuzi wako katika yote yaliyopo na yatakayo kuja.

INAITWA SIKU!BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………….0764 018535