Jumatano, 27 Agosti 2014

NAFASI YA SAUTI YA MUNGU



NAFASI  YA  SAUTI  YA  MUNGU  NDANI  YA  MAISHA  YAKO;



Kila utekelezaji wa sauti yoyote maishani mwako inabebwa na nafasi ya huyu mtu kwako unamuelewaje! 

Nafasi yake kwako! Kwakua kila neno linakuwa na uzito likitegemea limetoka katika kinywa cha nani mathalani neno la daktari aliwezi kuwa na uzito ulio sawa na neno la rafiki yako au adui yako,jirani hama mtumishi wa Mungu yeyote.

Uzito wa utekelezaji unategemea sana yeye ni nani kwako?

Umaana wa mtu utegemea namna unavyolitekeleza neno au sauti yake katika maisha yako hapo ndipo udhihirisho kuwa umemuelewa, unampenda na unamthamini tena katika utendaji ambao yeye amekusudia.

Ndani ya dunia tuliyonayo uwa tunasikia sauti mbalimbali zipo zilizo na matumaini mema katika maisha yetu na pia zipo zenye zinaleta shida katika moyo. Hakuna jambo linaweza kwenda pasipo mgongano wa sauti mbalimbali zenye kukuonyesha mwanga katika jambo ambalo unalopitia.

Kila sauti uwa inakuwa imebeba dhima fulani,lengo katika kutimiza kusudi lake,kutoelewa sauti kunapelekea kushindwa kupata kuelewa kile ulichotakiwa kukipata lakini pindi utakapoelewa basi hapo unakuwa na nafasi ya kupata yale yote unayotakiwa kuyapata.

I samweli 3:1-11

Wakati samweli anaandaliwa katika utumishi japo alikuwa anaishi katika nyumba ya Mungu lakini hakuitambua sauti ya Mungu na pindi alipoitikia sauti na kuiza kusikiliza ndipo alipotambua kuwa ni Mungu anazungumza nae.

Kila sauti unayoisikia inakuwa ina nguvu ya ushawishi katika utekelezaji wa jambo fulani na pindi utakapoipa nafasi basi yale makusudi yake ndipo yatakapotimia mathalani roho ya hofu utakapoikubali basi hapo ni wazi hofu itatawala katika maisha yako.

NAFASI YA SAUTI YA MUNGU NI UKOMBOZI WA MAISHA YAKO;

Kutoka 14:1-14

Japo kuna mchanganyo mkubwa ambao tunaona kwa Musa ulikuwa ukivuta huku na huku katika kushawishi kuchukua maamuzi kinyume na sauti ya Mungu. Hapo ndipo ishara kubwa ya kuonyesha nani ananguvu kwako.

Tunaona Musa anafanikiwa kuleta ukombozi juu ya maisha yake na israel kwa ujumla mara baada ya kuweza kuvuka bahari ya shamu kwa mkono wa bwana.

Siri kubwa hapa tunaona Musa aliipa nafasi kubwa sauti ya Mungu kuliko kishindo cha wamisri walipokuwa wanakuja, makelele ya israel kutaka kumlaumu Musa na kelele za bahari katika mawimbi yake, yote katika kumtisha Musa dhidi ya kuisikiliza sauti ya Mungu! Lakini bado Musa alitia bidii katika sauti ya Mungu.



Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com

Alhamisi, 21 Agosti 2014

HOFU YA MUNGU



HOFU YA MUNGU;




Ni hofu ya Mungu pekee inayokuwezesha kuishi maisha ya furaha, ushindi,nguvu na ujasiri. Haya maisha hayana kuigiza wala hayana mkumbo ni maisha yanayo jitambua na kuona fahari ya kweli ya maisha pamoja na Mungu.

Japo neno hili watu wamelitafsiri vibaya kutokana na namna lilivyo HOFU lenye maana ya kuogopa, kutisha kushangaza hata kustajabisha, hivyo watu uhusianisha neno hili na hali yao na Mungu katika kumuogopa sana 

Mungu kanakwamba mtu katili, anatisha, hanahuruma na hali hii utaikuta pale watu wanapoenda kanisani wanakuwa wapole sana na wenye unyenyekevu wa nje. Na sio hapo tu bali hata katika misiba watu huwa na hali ya ukimya sana wanatulia kila mtu akiwa muogopa Mungu kama kitu ambacho huwezi kushinadana nacho.

Ndani ya biblia neno hili HOFU YA MUNGU(KUMCHA MUNGU) limepewa nafasi kubwa sana kiasi kwamba mtu yeyote ambaye anamcha Mungu amekuwa ana nafasi ya pekee na Mungu kama ishara kubwa mtu anampenda Mungu, anamjua Mungu na anaishi kwa matakwa ya Mungu tu.                             

  Ayubu 1:1

Napia tunaona Mungu vile asivyopendezwa na mtu ambaye hamchi yeye, hivyonishara ya kwamba kwa tu ambaye anamcha yeye basi anakuawa na nafasi nzuri kwa Mungu
                                         
                                                       Warumi 3:18
Japo kuwa sio wote lakini wengi wao wamekuwa katika kutimiza taratibu za binadamu zinazo muhusu Mungu, na kwakufanya hivyo wamepata kibali kwa watu na watu kuwaita kuwa ni wanamcha Mungu.

Na watu wengi wamekuwa wakisumbuliwa sana kuona/kupata maana ya neno hili KUMCHA MUNGU ilivyo halisi.

-kwa maana ya kumcha Mungu zipo maaana nyingi lakini hizi ni maana kama msingi katika kukupa mwanga tayari kutembea na Mungu.

i.ni kutembea katika maisha yako huku ukitambua na kuthamini uwepo wake pamoja nawe!

Ni vile unafanya kwakua unampenda na kuona kuwa fahari yako ni Mungu kujisikia vizuri katika uwepo.

Hii ni nidhamu popote ambayo unafanya kwakua unamtambua na kumuheshimu Mungu na sio kitu kingine.

Mwanzo 39:9(b)( ni vizuri usome sura nzima)

………..nifanye ubaya huu mkubwa nimkose Mungu wangu!

Siku zote unajiona mbele za Mungu na wala sio mbele za watu kutokutekeleza kwako si vile unaogopa watu bali ni vile UNAMUHESHIMU MUNGU!

Ni nidhamu binafsi iliyo nzuri na yenye udhihirisho wa kweli kweli unamoenda Mungu na unaheshiu uhusiano wenu.


ii.ni kutembea katika maisha yako huku ukiwa ni kivutio na furahisho la moyo wa Mungu!

Mtazamo wa maisha yako kwa Mungu yakaonekane kuwa ni burudiko katika moyo wake maisha yako yakaonyeshe yanamuelewa Mungu, na kumthamini Mungu katika utekelezaji na sio hisia tu.

Furaha yako inajengwa na furaha ya Mungu ndani yako na sio jambo lingine…..FURAHA YA BWANA NDIO NGUVU YAKO!



Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                                                                                                                                      

KILA LA KHERI…………..RAFIKI


Jumatatu, 18 Agosti 2014

UPWEKE



UPWEKE;



Yesu alisema…..sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu tena.(yohana 14:18)

Hili ni neno ambalo linahusiana sana na neno KUPOTEZA, palipo kupoteza pana ukiwa basi panapelekea kushamiri kwa upweke. Katika moja ya janga linalotishia sana katika ulimwengu ni upweke ni neno lenye herufi chache sana lakini ni neno lenye nguvu sana na katika utendaji wake uwa matokeo yake uwa makubwa.

Upweke ni vile unavyofikiri na sio vile ilivyo kwakua vile ilivyo inategemea vile akili yako inavyoamini na kukubaliana na sio mazingira yenyewe.

Hili si neno zuri au jambo zuri kusikia au kuona mtu amekuwa mpweke au hali hii imekukuta wewe binafsi kwani hali inayotesa na kama kifungo ambacho haujui utatoka lini.(kina kuwa kama kifungo cha maisha)

Upweke uwa ni matokeo ya kupoteza mtu(kufariki),lengo kutotimia(matarajio yako kwenda sivyo) au kupungua katika hali fulani ambayo umekuwa ukizoea kutendewa mathalani unaweza ukaishi na mtu kwa namna mtu alivyo badilika mpaka unaona unaishi katika hali ya upweke.

Hii hali haibishi hodi(maana haitaji ujiandae kwanza) wala haingalii maskini au tajiri vilevile haingalii mrembo au sio mrembo kwa kifupi hakuna kitu kinahusiana na jambo hili uwa kina mkuta yeyote na kwa mahali popote haijalishi ni wakati wa kufurahi au wa kuuzunika.

Ni wazi mahali palipo na upweke lazima pacha wake wawepo MOYO ULIOSHUKA, AKILI ILIYOKOSA MWELEKEO NA UKOSEFU WA RAHA NDANI YA MOYO.

Japo jambo hili limekuwa likitokea watu wengi na umekuwa ukishuudia na pengine hata kuwatia moyo lakini tambua litakapo kukuta alina uzoefu au ufundi bali linatesa na lina maumivu ambayo haujawai kuyasikia mpaka pale utakapo kumbana na hali hiyo uso kwa uso ndipo utatambua makali yake na ukatiri wake na hapo ndipo utaweza kutambua kwanini watu hali hii inapowatokea uzimia, ujinyonga,kujiua au wengine kuishi maisha ambayo ukuyategemea hapo awali mathalani ulevi, umalaya hata uvutaji wa bangi kutokana kuondokana na upweke.

Wakati mwingine watu hali hii inapowakuta uchukua maamuzi mabaya kutokana na mtazamo ambao wanaona mathalani aibu ndio umenifika,maringo yangu yamefika mwisho,heshima yangu imeondoka,faraja yangu haipo tena,sasa mateso yanakuwa maisha yangu na mwingine uweza sema furaha/fahari yangu haipo tena.

Unapokuwa na fahari yoyote kama vile nyumba nzuri magari ya kifahari na mali nyingine za kuvutia na za ajabu lakini pindi unapokumbwa na hali hii ya upweke utaona wafungwa walio gerezani wana nafuu kuliko wewe kwani kipindi hiki kinaondoa fahari yote unayofikiri itakuwa ya maana kwako.

Ni vizuri kutambua kuwa hii ni hatua kama zilizovyo hatua nyingine kama wewe hauta achwa mpweke basi wewe utawaacha wapweke ndugu zako, rafiki na wakupendao au uwapendao.

Japo hali yoyote inaweza kutokea si semi ujiandae kwa hilo kwani hakuna mtu anajiandaa katika kuishi ya upweke na pindi unapotokea unaweza kuwa tofauti ya vile ulivyofikiria mathalani unaweka insurance ya nyumba au gari basi anakufa mtu upendaye ambaye ukuweza kutegemea wala kufikiria.

Hakuna maneno ya mtu ambayo yakaondoa upweke ndani yako wala “kampani” ya mtu bali hapo itakuwa ni vigumu kwako kujielewa na hata kuelewa watu.

Hakuna suluhisho lingine zaidi………..

MUNGU NDANI YAKO……………………

Yeye anaitwa Mungu wa amani basi na akupe amani!!

Anaitwa Mungu mwenye nguvu basi na akutie nguvu!!

Anaitwa Mungu wa faraja basi na afariji moyo wako!!

Anaitwa Mungu wa kibali basi na akupe kibali tena!!


  Imeandaliwa na ;                                                                                                          
                    
                         Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com




Ijumaa, 15 Agosti 2014

NGUVU YA MUUNGANIKO



NGUVU YA MUUNGANIKO




Wewe uko vile inategemea sana na nini ulichoungamanika nacho kwakua kile ulichoungamanika ndicho kina kutengeneza wewe,wakati mwingine tunajirahumu sisi kumbe yote yanatutokea kulingana na kile ulichoungamanika. Maisha ya ushindi furaha na ukombozi kwa ujumla yanategemea sana kile ulichoungamanika.

Kile ulichoungamanika ndicho kinacho kutengeneza wewe vile ulivyo,uwezi kuwa tofauti na kile ulichoungamanika nacho, hivyo ukitaka kujikomboa pale ulipo kwanza jikwamue na muungamaniko ulionao ili ujiungamanishe na kitu kingine.Kila muungamaniko wowote unaleta furaha,kujiamini na hata kuwa na mategemeo yasiyo koma yaliyo na uhakika, watu wanakuwa na kujiamini sana pindi wanatambua wana muungamaniko mzuri na mtu wa ngazi anajua atapata nafasi mzuri kuyafikia mazuri.

Kwa mfano mtu ambaye ana muungamaniko na mkuu wa kituo cha polisi uwa yuko na ujasiri mwingi hata anapokamatwa au mipango yake kuzuiliwa anajiamini kwa kuwa kuna mtu akiwasiliana nae mambo yanakuwa sawa.

Mnaweza kuwa wote mnamatatizo yanafanana lakini kila mtu atatoka hapo kutokana na muungamaniko,mathalani wanafunzi wanamaliza chuo wakiwa wamefanikiwa stashahada na shahada mbalimbali lakini kutoka/kupata kazi hapo inategemea umeunganika na watu walio katika nafasi zipi? Watu ulioungamanika ndio wanaweza kukupa kile kitu walichonacho na kama hawawezi kukupa kitu ambacho hawana.

Hivyo tunaweza kuona kwamba wapo mtu wanateseka  sasa sio kwamba hawana akili au hawana vigezo vya kukuwezesha kuwa na nafasi nzuri katika kazi na hatimae kuwa na maisha bora.

HAKUNA MUUNGANIKO WENYE MAANA SANA MBALI NA MUNGU NDANI YA MAISHA YAKO,

Katika muungamaniko huu wa wewe na Mungu vilevile utegemea namna ilivyoungamanika ndivyo itakavyo kuwa, namna mlivyoungamanishwa vizuri ndivyo utakavyo kuwa vizuri,Kuwa na muungamaniko na watu wengi sio mbaya kwakua katika maisha tuliyonayo tunawahitaji watu kwa kiasi kikubwa kwa kuwa wao wanakutegemea wewe na wewe unawategemea hivyo sote tunategemea ni kama vule viungo katika mwili wa binadamu vyote vina umuhimu wake na hakuna kiungo chenye maana sana kuliko kingine japo kwa haraka haraka unaweza kuona kiungo Fulani ndicho cha maana lakini sio kweli mathalani unaweza sema tumbo ni muhumu sana kwa kua linatunza chakula na hatimae kupelekea mwili mzima kuwa nguvu lakini mdomo ukifunga usipitishe chakula hapo ndipo unaweza kutambua kuwa kunakutegemeana

 Watu wanapenda kuunganishwa katika shughuli mbalimabali ili mradi tu  aweze kufanikisha hazma yake.

Mtu anaye kuungamanisha halafu ukaweka matumaini yote kwa mtu huyo ni wazi utafika kipindi ambacho utajuta hata kwanini umeunganishwa katika kazi hile au sehemu hiyo.

Ni kweli Mungu anatumia watu katika kutenda hapa duniani lakini haina maana kutoithamini nafasi yake katika maisha yako na ukampa alie kusaidia.

Ni vizuri kutambua misaada yaweza kutokea popote ila upande wa Mungu yuko mwenyewe na ana njia zake za kumpata bila hivyo uwezi kupata.

Mbali na Mungu muungamaniko wowote mwisho wake ni AIBU tu hakuna usalama mwingine.

Ni vizuri utamfute Mungu kwanza halafu yeye akuungamainishe basi hapo utakuwa salama ila ukijiungamanisha mwisho itakupelekea maumivu lakini Mungu yeye ajuaeye moyo wa kila mtu atakuungamanisha na mtu naye atafanyika Baraka na wala sio jeraha la moyo.


            Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
               

KILA LA KHERI…………..RAFIKI