Alhamisi, 31 Julai 2014

USALAMA WA AKILI



ULINZI WA AKILI YAKO;



Unapoona huyu amekuwa wa kwanza na huyu wa mwisho, unapoona ona huyu kajenga na huyu kapanga, wote wana virusi vya ukimwi huyu anaishi kwa uhuru na huyu anaishi kama kifungoni, huyu ana afya na huyu hana afya, huyu ndoa yake inaimarika zaidi katika changamoto na mwingine ndoa yake imevunjika, wakati mwingine huyu anaomba kwa uchungu na huyu anaomba kwa furaha yote haya yana jumuisha matumizi ya akili.

Akili inaitaji afya njema mbali na mwili japo wengi hawawezi kukupongeza unapokuwa na afya ya akili kuliko ya mwili, lakini ukweli ni kwamba akili inahitaji afya ili iweze kutekeleza utendaji wake kwa ufasaha pasipo upingamizi wowote kama vile ili utembee vizuri kuwa na mwili ulio vizuri lakini katika yote akili isipo kuwa na afya njema kuna shida itatokea katika maisha.

Katika maisha ndani ya dunia ya leo tunaona umakini mkubwa unapewa namna ya kutunza mwili wako ili kujikinga na magonjwa yanayoweza kukuathiri na kuleta mateso katika mwili wako na hatimae kudhoofika, lakini ulinzi katika akili yako ni kitu cha msingi sana ambacho unahitajika sana ukipe kipaumbele

Kwa kiasi kikubwa sana mateso ya watu yanasababishwa na kukosa ulinzi katika akili yako mimi nilikuwa na rafiki yangu ambae matokeo hayakuwa mazuri japo hakutarajia alijipa moyo na maisha yakawa yanaendelea lakini maneno yasiyo faa yaliyokuwa yakisema juu yake kutokana na kutofanya vizuri katika matokeo yake ya kidato cha nne kuwa ni mzembe, mbona ndugu wengine walifaulu haya maneno yalikuwa yakijirudia kichwani mwake hatimae mwisho wake akapata ugonjwa wa akili na mpaka sasa anaendelea na matibabu muhimbili.

Ni akili pekee inayoweza kukutambulisha kuwa uko wapi na unafanya nini au una hali gani? Majibu yote yanatokana na akili sio masikio au kitu chochote, na ni jambo la kawaida mtu anaweza akakusuma ukadondoka na baadae ukarudi  tena katika hali ya kawaida lakini pindi tu utakaposhindwa kuweka ulinzi katika akili yako kuna maneno mengine unayoambiwa yanaweza sababisha shinikizo kubwa katika maisha yako.( kutokana na maneno na sio matendo/kitendo).

Kile kinachokubalika katika akili yako ndicho kinachopelekea utekelezaji, wako watu waliojinyinga kutokana na maneno tu au waliokimbia na hata kujitenga na jamii zao kutokana na maneno tu yaliyoweza athiri akili yake kwa kiasi kikubwa,mathalani baba yako anakwambia neno gumu(nimekuchoka sasa unaweza kwenda, umenichefua sina radhi nawe au najuta kwanini nimekulea) haya ni maneno ambayo yanaweza kuathiri akili yako kwa kiasi kikubwa hata ukakosa maana ya jambo lolote zuri linaloendelea katika maisha yako.(kama kweli unajipenda basi hauna budi kuulinda akili yako isi haribiwe na majanga mbalimbali) na ni vizuri utambue kuwa kila mtu anaakili yake hivyo kila mtu anawajibika kuilinda akili yake na sio ya mtu mwingine.

Akili ni ufunguo unaoweza ruhusu jambo liingie katika moyo na jambo lisiingie katika moyo kwa maana uamuzi wa jambo hili limebebwa na akili na sio jambo lingine.

Hakuna kitu kizuri kama kufanya jambo katika akili iliyotulia kwa maana inaleta ufasaha na umairi katika utendaji wako, na akili isipotulia inapelekea mwili kukosa ufanisi na umairi wake katika utendaji wako ni bora uishi katika utumwa wa mwili kuliko kuwa mtumwa wa akili unakuwa zaidi ya kichaa,teja au mtu asiye jitambua.

Kila kitu ilikiedelee kuwa bora na cha maana sana hakina budi kitunzwe katika hali stahiki na isiyo na mwendelezo usiofaa, hivyo akili ni kitu muhimu sana tunaona watu wakiheshimika kutokana na namna wanavyotumia akili yao na wako watu ambao wanazalaurika kutokana na matumizi ya akili zao.

Nailindaje akili yangu?

Kila mtu upenda kuona ustawi wa akili yake siku baada ya siku ila japokuwa ili akili iweze kustawi na kuwa bora siku hadi siku kupenda pekee yake au kutamani haisaidii sana bali ni lazima utambue kuwa ni nalo tatizo hili na ni wajibu wangu kuhakikisha akili yangu inastawi kwa kutambua kuwa ustawi wa akili yako ndio ustawi wako.

I.umakini katika kile unachokisikia

Unasikia nini kinaweza kukutengeneza nawe ukawa vile sawa na unachokisikia, ni seme wazi sio kila unayo yapenda basi yanaleta afya katika akili yako bali ni yale yaliyoshihi ambayo unatkiwa kuyasikia kwa ufasaha ili kuimarisha ufahamu wako kuhusu Mungu.
Wakrito tumekuwa huru kusikia kitu chochote pasipo kujua matokeo yake na pindi matokeo yake yanapokuwa mabaya tunajiraumu au kurahumu watu wengine pasipo kujua kuwa ni zao ya kile tunachopenda kusikia.
Yesu alisema;…..jiangalieni sana jinsi msikiavyo!!!!!
Namna unavyosikia ni muhimu sana kwakua kinakujaza na hatimae inaweza kukupeleka sawa na maneno hayo yanavyotaka.

II.changamko la kweli ndani ya moyo wako(furaha isiyo na mipaka)

Biblia inasema;…changamko la moyo ni dawa ya mifupa!!!
Hakikisha furaha inakuwa ni maisha yako katika ajira yote ahuitaji kuogopa bali unahitaji kuzidi katika kumwamini Mungu pasipo kuchoka wala kukata tamaa.
   I wathesalonike 5: 16-18
Kwa kila jambo linalokutokea jifunze kumuona Mungu sana kuliko zaidi kuliko shetani maana ndivyo Mungu anataka uone.
Tamani kuona furaha yako ikawa nguvu katika maisha yako na hata wengine utakiwi kuchoka katika kuzidi kumwamini Mungu.


Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com


MUNGU AKUBARIKI SANA……….!!!!!!!!!!

Jumanne, 29 Julai 2014

MKRISTO AZALIWI BALI ANATENGENEZWA



 MKRISTO AZALIWI BALI ANAANDALIWA;



Ni kawaida mtu uweza kurithi tabia toka kwa wazazi na hata muonekano wa namna ya kutembea,kusema na namna nyingine nyingi. Lakini sio swala la mkristo

Swala hili alina uhusiano ulioko kati ya damu  na Mungu bali ni roho ya mwanadamu na Mungu hivyo sio swala la kulichukulia katika kawaida.

Ni kweli mtu iliafike duniani ni lazima azaliwe tukiachana na Adamu na Eva ambao ndio mama na baba wa wanadamu wote hapa duniani.

Hii ni kauli ambayo inawezakuibua maswali mengi kuhusu vipi kwa mtu ambaye alizaliwa katika familia ya baba na mama  wote ni kristo, ukweli ni kwamba mkristo sio swala la kurithishana na wimbi la watu wengi.
Japo unaweza kuzaliwa katika familia ya kikristo haina maana ya wewe kuwa ni mkristo uamuzi wa kuwa mkristo au kutokua mkristo. Hili swala aliendi kwa mkumbo bali linahitaji maamuzi ambayo yanatokea baada ya kuelewa kwa ufasaha zaidi.

Kwa maana nyingine ukristo ni kujitambua mwenyewe na kumtambua Mungu kwa uhalisia wake.

Kwa kusema hivyo unaweza kutoka kwenye familia yoyote halafu bado ukawa wa maana zaidi kama tu utakubali na kuwa tayari kwa atengenezo hayo.

Sio swala ambalo unaweza kulichukulia katika hali ya kawaida bali ni swala lililo na latofauti sana lenye nguvu sana wala alina mfano wake.

Hivyo hauhitaji kujivunia kwa kutoka kwenye familia inayo mwamini Mungu bali furahia kwakua wewe binafsi una mwamini Mungu.

Mungu anapokuangalia wewe uwa angalii kuwa wazazi wako kuwa ni watu wanamna gani ili akufanyie kitu kwako japo anaweza kubariki au kulaani kizazi cha kwanza hadi cha tatu.

Ili ufike kule Mungu anapotaka ufike ahitaji kuona wazazi wako wamefanya nini bali ina kuangalia wewe kwakua wewe ndio hatma yako mwenyewe.

I wafalme 6:12

Ni vizuri kuwa utambue kwamba Mungu ahitaji ukoo/familia bali waliopo ndani ya familia kila mmoja na nafsi yake.

Mungu haitaji kuona fahari kwa watu wengine bali anahitaji wewe binafsi ili aone fahari kupitia wewe na sio kitu kingine.

Wako watu wengi wamekuwa wa kiishi maisha ya kawaida sana kwa kutegemea ukristo walio karibu nao mathalani utakuta watu hawaombi wakitegemea wako watu ambao wataomba kwa ajili yao na kufanya mambo ya mtu husika kwenda vizuri.

Kama kuna jambo ambalo ni maumivu ya Mungu ni kuona wewe unaangalia wengine wakati yeye anakuangalia wewe kwakua ubora wako unakuwa furaha kwa wengine au unakuwa ni nguvu kwa wengine.

Unapotegemea ulipotoka panauelewa kuhusu Mungu ukaelemea hapo pasipo kujua Mungu anakuangalia wewe binafsi unaweza kushangaa pindi tu YESU atakapo kuja utaona majabu yake na hapo utaanza kuona kuwa Mungu ana angalia ukoo au familia au kitu gani hasa.

Biblia inasema,…..mwana hata uchukua uovu wa mama au baba wala baba au mama hata chukua uovu wa mwana.
……..watakua wawili mmoja atachukuliwa mwingine ataachwa.

Hizi kauli zote utaziona kwa uhakika pindi pale kristo atakapo lichukua kanisa lake kwa macho yako utayaona mambo hayo kwa uwazi wake.

Ni vizuri usisubiri hiki kipindi mpaka kitakapofika ndipo uanze kujuta au kujilaumu bali ni utambue kuwa mkristo anayo nafasi ya kuandaliwa/kutengenezwa akawa mkristo aliye sahihi mwenye hatari katika ufalme wa giza.

Wokovu ni kati yako na Mungu na Mungu ananamna ya kukuandaa ili wewe usifanane na Yule wala wale bali ufanane na yeye kwa namna yake.

Tambua mtu kama wewe hajatokea wala hatatokea bali ni wewe uko peke yako hivyo lazima ufanye mambo ambayo yatakutofautisha wewe na watu wengine.

Mungu hanamfano wake bali ana utendaji wake wake kwa mtu aliye tayari ili kupitia huyo haweze kumuona au ajionyeshe yeye alivyo kupitia mtu husika.

Haijalishi umezaliwa wapi la muhimu kukumbuka ni kweli umefanyika vile Mungu anapenda akuone wewe ukitoa chapa yake katika ulimwengu wa sasa.

II wakorintho 5:17

Uhuru wa Mungu kwako katika kukutumia ni vile tu ambavyo utampa uhuru wa kutosha kwa yeye kukuandaa kwa ajili ya kazi yake. Penda yeye akufurahie wewe ili aone fahari kwake kwa kua yeye amekutengeneza.

Unapokuwa tayari Mungu yuko zaidi ya utayari kwa ajili ya kukufanya kuwa kiumbe cha ajabu ambazo ataonyesha maajabu yake kupitia wewe.

imeandaliwa na;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
         

KILA LA KHERI…………..RAFIKI

Jumapili, 27 Julai 2014

NAFASI YA KUPOTEZA



NAFASI YA KUPOTEZA;

                                                                            


Hapa duniani katika mambo ambayo wanadamu wote wangeungana kwa pamoja katika kupiga vita ni kupoteza(loose) hakuna mtu anapenda kupoteza wala kutegemea kupoteza kwani katika kupoteza kumeleta maumivu mateso na ukiwa miongoni mwa watu wengi, hili neno ni neno ambalo alitarajiwi sana na watu wngi kutamkwa kwani ni neno ambalo aliinui moyo bali linafanya moyo kuwa chini.

Hata mfanyabiashara yeyote anapotoa mtaji wake uwa hatarajii kama kuna kupoteza kwakua ni matarajio yake katika kuongezeka, na hili neno la kupoteza uwa linatokea katika hali ya kujua au kutojua kulingana na hali iliyopo husika mathalani mtu anafanya shughuli pasipo na maarifa ya kutosha.
Japo katika kupoteza kuna husika sana na nini unapoteza ingawa yako mengine yakipotea yana kuwa na upande wa kukusaidia zaidi au kuudhihirisha ule uwezo ulionao na mengine yanaweza kuacha pengo ambalo litaweza kukusumbua kulingana na uelewa wako.

Unaweza ukajitaidi kuziba kila kona lakini kama kuna upande umehusahau huo upande utachangia katika upande wa kukurudisha nyuma mathalani unaweza kujenga nyumba nzuri sana lakini ukasahau kuweka mlango hivyo hali hii inaondoa usalama wa mali ulizonazo na kuruhusu wezi kuweza kuchukua mali zako na kupelekea kukurudisha nyuma jitiada zako katika kujiletea maendeleo.

Japo kila mtu upenda aendelee ila usipo iangalia mianya hiyo inayo sababisha usiendelee inaweza kukurudisha nyuma tofauti na ulivyofikiri.

Katika makanisa mengi hasa wale wanao mwamini Mungu wa kweli tena katika usahihi wamekuwa wanamalengo mazuri yenye kuinua ufalme wa Mungu na kuaibisha ufalme wa shetani………..
Yesu alisema…….juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo milango ya kuzimu haitalijenga. Uimara wa kanisa lake litajengwa katika misingi ya kristo mwenyewe ambacho hakuna cha kumshinda na hii aliidhihirisha pale alipotoka msalabani na kukaa katika ardhi siku mbili baadae ardhi ilimtapika kwa kua haikuweza kumzuia.

Lakini tunaona ndani ya kanisa la leo kunamambo ambayo hayasadifu maneno maneno haya kwa kua ndani ya kanisa la leo kuna udhihirisho mkubwa wa tabia za mwilini ,paulo anasema kama ninyi watu mnaenenda kwa kufuata mwili ninyi si watu watabia za mwilini ninyi…..

Ndani ya kanisa la leo kuna uasherati,uzinzi,uongo, ubinafsi, choyo, maslai binafsi na mengine mengi……….( wagalatia 5; 19-21).

Ili kanisa tuweze kupona hatuna budi kurudi katika misingi ya yesu tukiona na namna yeye alivyoishi na hatimae alishinda….!!!

I.ukamilisho wangu unamtegemea mwingine

Japo biblia inasema tunayaweza yote katika yeye atutiaye nguvu (wafilipi 4: 13) haina maana maisha ya peke yako tu yataleta kuyafanya yote. Hata yesu aliiwahitaji watu ili kuacha msingi wake uzidi kutawa katika dunia nzima.

Kama hauta tambua basi utakuwa ukipoteza atakama unatuia nguvu nyingi kiasi gani kwani hauwezi kuyafanya yote mwenyewe.

Japo kunawakati ambalo unaweza ukahisi naweza kufanya lolote hata bila ya kumwitaji mtu kutokana na vile unavyojiona lakini ukweli tunahitajiana tena kwa muda wote sio wa kipindi fulani tu. (wafilipi 2:3). Mathalani mtu mwenye hela anaweza jua kuwa anaweza fanya jambo lolote ila kuna mambo mengi atatambua kuwa mimi na hela zangu bado sijitoshelezi katika kujikamilisha. 

Kanisa ni kama mwili unategemeana mdomo ili kula una mtegemea mkono na tumbo linaitegemea. Ni kweli kuna wakati unaweza usivione vitu vikidhihirika katika muonekeno wako unaoutaka lakini katika yote tambua vyote vipo ila shida inakuja katika kuvitambua na kuvipa nafasi mathalani mtu asipotembea haina maana hana miguu kunawakati ana amua kuto tembea, na mtu asipo ongea haina maana hana mdomo au yeye ni bubu…………!!!

Hili ni tatizo ambalo linakuwa ni shida kwa watu wengi kuona kwamba wenyewe wanaweza tu maadamu wanafanya kazi pasipo kujali kuwa paulo anasema kuwa ….pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule.( 1wakorintho 12: 4-7 ) wote wanatenda kazi lakini katika namna mbalimbali kadili ya Mungu alivyojalia na sio nani zaidi. Mathalani katika ujenzi wa nyumba kunautendji kazi tofauti tofauti lakini wote wanakusudi moja tu kuwa nyumba isimame.


Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com


MTAMBUE MWINGINE NAYE AKUTAMBUE?

Ijumaa, 25 Julai 2014

FAHAMU NGUVU ILIYO KATIKA MIZIZI



UIMARA WA MIZIZI YENYE UBORA;

Mathayo 7: 24-27

Hapa atuzungumzii tu mizizi bali tunazungumzia iliyoimara iliyonauwezo umkubwa katika kukiwezesha kitu hicho kiendelee kua mahala pale.Ni jambo la kawaida kwa usalama wa mtu au kitu utegemea wapi umegemea au uwezi wa mtu anayekukinga, wako watu wanaitwa wanajeuri ya fedha,waliojizindika au wenyekujuana na watu wenye uwezo au mamlaka hivyo uona yuko salama katika vigezo hivyo.

Unapoona uimara wa kitu chochote kimedumu kwa muda mrefu tena katika mafanikio mafanikio makubwa jua kuna uimara katika utawala,hivyo unapoona maafa yoyote jua sio muonekano wa nje wa kitu bali ni vile ndani kulivyobomoka.uimara wa nje hauna shida sana bali unategemea sana uimara wa ndani( mtu anaweza akaharibika sana katika muonekano wa nje lakini kama ndani pakiwa na uimara basi kuendelea kupo lakini ndani pakiwa apaeleweki nje hata paking’ara vipi muda si mrefu mpolomoko utatokea muda si mrefu.

Mti unapokuwa umenyauka matawi lakini mizizi bado imara basi hapo panakuwa na matumaini ya matawi kustawi lakini ikitokea mizizi ikatwe basi tambua hapo matawi yatanyauka hata kama sasa yanaonekana yanaonekana yanavutia ila kwa sababu tu kinachofanya ustawi wa tawi na shina akipo basi kinachofuata hapo ni anguko la tawi.

Sipo hapa kuelezea sayansi ya mizizi kwenye mti la hasha! Bali niko hapa kuleta somo hili

UTENDAJI WA ROHO MTAKATIFU KATIKA MAISHA YA MWAMINI

Vile unavyoelewa utendaji wa Roho mtakatifu katika ufasaha mzuri ndivyo inakupa kibali na nguvu katika maisha ya ukristo. Utendaji(Operation) ya Roho mtakatifu ndio uimara wa mkristo pasipo hilo hauwezi ukawa na ukristo wenye nguvu na kibali kwa Mungu. Uwa ninapozungumzia nguvu na kibali kwa Mungu ni vitu viwili tofauti kwani uanapozungumzia nguvu ya Mungu inadhihirisha katika fundisho na hata kuponya wagonjwa lakini hivi vinauweza kosa kibali kwa Mungu, maisha yenye kabali kwa Mungu yanaweza yasiwe na kibali na watu ila hicho cha Mungu kimebeba utoshelevu ulio timilifu.

Utendaji huu hupo katika nguvu ya kumsikia Roho mtakatifu na kumwelewa ili kuleta utendaji wako ufanane au uwe sawasawa na yeye atakavyotaka sio vile unavyojisikia bali vile alivyopanga kwa kusudi lake.
Katika biblia Roho mtakatifu kapewa nafasi kubwa sana katika ulimwengu wa sasa yesu anasema naenda ili aje msaidizi ( yohana 15: 26-27).

Wote wanaoongozwa na Roho mtakatifu hao ndio Mungu uwatambua kama watu wake.                ( warumi 8: 14).

Watu wengi wanaposhindwa kuendelea mbele tu ni vile mizizi yao haina uchambuzi ulio imara katika Roho mtakatifu,kwani namna unavyo endelea kutumika na Roho mtakatifu ndivyo unavyozidi kuwa imara na kuimalika katika yeye kwani kumtambua Roho mtakatifu katika mapana zaidi ndio ushindi wa kuzidi kutembea nae pasipo.

Isaya 66: 2(b)

Mtu anaposhindwa kutembea katika maisha ya ushindi na hatimae kukata tamaa ni vile mizizi yake katika Roho mtakatifu sio imara yenye nguvu iliyojikita sio katika mazoea bali kwa hofu na kutetemeka mbele za Mungu siku zote.



Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com



NURU YA BWANA IKUANGAZE………………!!!