Ijumaa, 23 Machi 2018

UJANA WANGU THAMANI YANGU!




Katika kila hatua ya ukuaji wa mwanadamu  kuna umuhimu wake na faida yake naam na upekee wake. Maana kwa kila hatua uumbaji unafanyika na muhimu zaidi kila hatua inategemea hatua nyingine mathalani hauwezi toka mchanga ukawa kijana kuna vitu havitakuwa sawa katika mwili wako!

Japo kila hatua ina maana yake ila ujana una utofauti wake unaoashiria hama kuwa kivutio kwa wengi hata wengi wao upelekea kusema “ Laiti ningelikuwa kijana” lakini sio rahisi kusikia mtu akisema “ Laiti ningelikuwa mtoto” japo hiyo nayo inawezekana.

Ndani ya dunia wako watu wazima waki ufurahia utu uzima wao na wengine wakiishia kujilaumu tu kutokana na namna walivyo kitumia kipindi chao cha ujana.

Kipindi hiki cha ujana kimekuwa ni kipindi cha shauku na uhitaji wa kujua mengi maana uwezo wa kuyaelewa mambo unakuwa ni mkubwa na kuyabeba japo inategemea kijana mwenyewe…… inakuwa sawa  na mtu aliyetoka kijijini na kuingia mjini kwahiyo kila kitu anashangaa na kustaajabu.

Kuna asilimia kubwa sana kwa kitu hama wewe binafsi ukijiweka katika mtazamo ulio sahihi na ukiuambatanisha katika utendaji basi watu wengine watafuata mtazamo wako, kwa kuwa mtazamo wako utapelekea utendaji wako.

Moja ya kauli ninayo ipenda na yenye ukweli ndani yake ni hii “ unapojipa thamani wengine wataiona thamani yako “ Na ni muhimu kutambua kuwa thamani haiji hivi hivi tu unahitaji uwe na maamuzi na dhamira ya dhati katika kuheshimu uthamani wako.

Haijarishi unajivunia ujana wako kiasi gani kama kuna mambo ukishindwa kuyazingatia unaweza kupoteza thamani ya ujana wako haijarishi utakuwa unajua hama haujui “ kwa kuwa maneno matupu sio njia sahihi ya kuonyesha una uthamini ujana wako”

Katika kipindi hiki unaweza jikuta unaingia au unatamani kwenda katika hatua nyingine usiyoijua hasa uhitaji wake na pindi unapoingia uko ghafla ( muda si mrefu ) ukatamani kutoka nje!

Unahitajika kuishi katika nafasi ya ujana kiasi kwamba yeye aliyekupa ( Mungu ) aone fahari na kujisikia vyema na kuona sababu ya kukupa hatua hiyo ya ujana.

Kuna mambo ambayo unapaswa kufanya unapokuwa kijana na kuna mambo ambayo haupaswi kabisa kuyafanya unapokuwa katika hatua hiyo kwakuwa inaweza kujenga msingi mbaya/ mzuri katika hatua unayoifuata.

Ni hatua ambayo mwili na akili vinakuwa katika hali iliyo njema katika wepesi wa kutenda, kuna kipindi kitafika uta itamani hatua hiyo lakini muda utakuwa umeshapita na mwili hauta kuwa tayari kuendana na kasi hiyo.

Unahitaji utumie ujana wako vizuri pasipo kutamani hatua nyingine kwakua kila hatua itakuja kwa wakati wake maadam majira yake yakifika . ( Hauhitaji kuulazimisha usingizi ili ulale bali majira yake yakifika na mwili ukiwa tayari basi utaona ukichukua nafasi ).

Ni muhimu katika maisha ya ujana;

i.                    Uishi kwa kujifunza vitu vingi vyenye mchango katika maisha yako ( positive ).

ii.                  Uishi uku ukijua kipindi hicho kikisha pita akijirudii tena.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………. 0764 018535