Jumanne, 14 Januari 2014

MAANA YA KIFO CHA YESU KWA MUNGU



KUFA  KWA YESU  HAIMAANISHI  KUWA MUNGU ALISHINDWA:
                                              
 
                                             Luka 24:19-26

Utendaji wa Mungu kwa namna nyingine avieleweki kwakua katika kila tendo huwa kuna kazi yake anaifanya ambayo unaweza usielewe lakini itakapoanza kutumika ndipo hapo utaanza kuona umuhimu wa hile hatua uliyopitia.

Pindi unapokuwa katika imaya ya Mungu usitegee kushindwa bali kuna kushinda japo zipo tafsiri mbili za hali ya kuonyesha kuwa umeshindwa ambazo ni kibinadamu na ya kimungu,

 Tafsiri ya kibinadamu ya kushindwa ni kukosa vitu vya dunia lakini kwa Mungu tafsiri ni kuvunjika kwa uhusiano kati yake na binadamu.

Hivi ni vitu viwili vyenye mtazamo tofauti kutokana na hatma yake ya Mungu mwisho wake ni UZIMA na ya kibinadamu mwisho wake ni MAUTI.

Katika mauti ya yesu kwa namna ya kibinadamu apakuwa na matumaini yoyote kuwa hatainuka na kuwa mshindi zaidi alivyokua awali.

Katika mauti na kukaa yesu ndani ya kaburi inatafsiri kubwa katika maisha ya mwamini haina maana ya ubatizo tu bali inamaana kubwa sana katika ulimwengu wa roho na wa mwili.

Ili ni tendo(yesu kukaa kaburi) ambalo kama mkristo atakapolipita unapoinuka hauwezi kama ulivyokuwa awali.

Na mahali utakapo kuwepo unahitaji nguvu ya Roho mtakatifu ikutoe mahali ulipo si kitu kingine hivyo usiruhu kitu kingine kiendelee ndani ya ufaham wako.

Japo watu wengi hawapendi kufa lakini ni muhimu kufa ili uibuke mwingine pasipo kufa hauwezi kufufuka tena katika hali iliyo bora kuliko awali.

-kama mbegu katika ardhi inahitajika ionze ili kwamba iweze kuzaa matunda mengi. Na nivizuri ujue kwamba hii hatua kama usipo ipitia usitegemee ukawa bora au wa maana sana kwani hiyo ndiyo njia na hakuna njia nyingine ikaleta mafanikio ya kudumu.

Na sio kwamba watu wanapenda kufa bali hii ni hatua ambayo Mungu ameiandaa mwenyewe kwa ajili ya kutung’alisha vizuri.

Unapofika hatua ukaogopa kufa basi jua hapo ulipo hautaweza kwenda mahali pazuri unapo fikiri wewe binafsi.

KUFA hii ni hatua ambayo mwili unapoteza utawala wake na roho ya Mungu ndani yako inaanza kuwa na nguvu katika maisha yako.

Mungu hawezi kutenda jambo ndani yako katika ukamilifu wake huku matendo ya mwili ya kawa na nguvu ndani yako.

Pindi utakapo kubali kufa basi hapo ndipo penye mchakato wa Mungu kutoa uhai wake na uzima kisha kuchukua unyonge wako na kukupatia vyake.

Hii hatua ni ya muhimu sana kwa inakuweka njia panda ujui nini kinafanyika kama mgonjwa aliye NUSU KAPUTI ni hatua ambayo unahitaji utulivu wa kumsikiliza Roho mtakatifu ili afanye ndani yako.

Ni kipindi ambacho Mungu anajifunua kwako kwa namna nyingine tena ambayo unaanza kumwelewa Mungu kwa namna tofauti kuliko ile ya awali.

Hapa penye udhihirisho kuwa umeamua kufuata yesu pasipo maslahi yoyote ya kibinadamu kwa maana hii umeamua kujikana kiukamilifu.

Hiyo ndiyo ishara pekee ambayo Mungu anaitaka kuiona kutoka kwako ili umdhihirishie kuwa  wewe  ukotayari kujigharimu kwa ajili yake.

Na nivizuri kutambua kwamba maumivu ya mwili ndio furaha ya roho na maumivu ya ya roho ndio furaha ya mwili. Unaishi kwa kufuata nini?

Usiogope kufa kwakua kufa ni darasa la roho yako na Mungu kama hautaki kufa basi jua kwamba hautaji darasa kati yako na Mungu.

Kufa haifurahishi katika mwili wa kibinadamu hivyo haishawi sana kupenda kufa bali ni vizuri kutambua kuwa kama hauto kufa kimwili basi utakufa kiroho. Lipi jema basi chagua katika hayo usalama au mauti.

Hakuna kitu kizuri kama kupitia kwenye mafunzo ili upate uelewa zaidi kwa ajili ya kufanya vitu katika ubora na nguvu zaidi.

Mtu yeyote alikubali kufa halafu akabaki vilevile jua kuwa hakumaliza kozi, kwakua mbegu haiwezi kufa halafu ikachupa pasipo uzidisho kama hajachipuka basi wadudu wamekula hiyo mbegu.

Usiogope kufa kwakua kifo si kwa ajili yako bali ni kwa ajili ya mwili wako ila ni kwafaida yako hivyo kama unatamani kufanikiwa basi tamani kufa.

Hakuna ustawi usio kuwa na mizizi na hakuna mizizi pasipo kuwa na mbegu iliyo kufa halafu ikaoza.

Kwa maana nyingine kutamani kufa ni kumtamani MUNGU. Hakuna maana ya kumtamani Mungu kama utaki kufuata yale anayo yataka.

Imeandaliwa na ;
                    
                    Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                 

                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com


                               

                                      “Naomba tuwatakie wakati mzuri……….”