Jumanne, 28 Machi 2017

BABY FACE



SURA YA MTOTO

Moja ya furaha katika familia nyingi za waafrika ni watoto, imefikia kipindi kuwa ndoa inaweza kudumu sio kwasababu kuna mapenzi bali kwakua kuna watoto ambao ndio kiunganishi cha wana ndoa hao hivyo wanaweza kuendelea kuishi maadam Mungu amewajalia pumzi sio kwa maana ya mke na mme,

Kiafrika sio swala la kushangaza kuona ndoa imevunjika kwasababu ya kukosa mtoto japo kuwa na watoto hakuna maana ndoa haita vunjika! Sababu ziko nyingi sana ambazo wanadamu wanazo lakini sina uhakika sana kama Mungu anazitambua na kuhalalisha kuachana,

Kwahiyo mtoto katika familia ni kivutio, heshima, staha, majivuno na naamini pia ni sifa kwa mwanamke kuwa anazaa.

SURA YA MTOTO ni furaha ya wazazi hasa inapotokea mtoto anafanana na baba, na kwa upande mama kama yeye ni mwaminifu katika ndoa itapunguza maswali upande wa kiumeni, kwakua kufanana na baba maswali yanakuwa sio mengi lakini akifanana na mama maswali uweza kujitokeza.
Mama yeyote mwenye akili uwa awezi kujizuia pindi anapomuona mwanae anacheka/anafurahi bila shaka na yeye atakuwa na sura ya tabasamu lililoanzia moyoni na kwenda hadi kwenye muonekano wanje!

Katika dunia ya sasa wanawake wengi wamekuwa wakitamani sana vitu vya watoto utakuta wanaitana BABY FACE moja ya maana zao sura iliyo na muonekano mzuri usio na makunyanzi wala ma waa! Ngozi ili nawiri na kupendeza………………….mabinti wengi wamekua wakiambiana hivi wamekuwa wakijisikia vizuri hata kutamani kuendelea na kutumia mafuta hama lotion iliyomfanya mpaka asifiwe kuwa anakabebi face, bila shaka unapomtamkia binti kuwa anakabebi face anaweza kutamani kuwa rafiki yako kwakua umemsifia naye amejisikia vizuri na ni kawaida ya binadamu yeyote kupenda sifa mathalani una mwambia umefanya vizuri, umependeza, umetokelezea hama umefunika.

Hali hii imepelekea hata mabinti wengi kudanganyana kuambiana kuwa wana muonekano mzuri katika sura yake na huku wanamkejeli  unakuta yule binti kujisikia vizuri lakini baadae anapotambua kuwa walikuwa wana msanifu anaweza kujisikia vibaya sana!

KARIBU SANA!

Sura ya mtoto imebeba tafsiri nyingi sana kwa mama pindi anapomuona na kumwangalia anakumbuka mengi wakati mwingine anaweza kucheka peke yake hama kuhuzunika kutegemea mwegemeo wa kumbukumbu yake,

Katika hili napenda tujifunze kitu kimoja katika SURA YA MTOTO kwa maana kuna mfanano mkubwa wa kile anachokifanya kwa nje na kile kinachoendelea ndani, uwa hajui maana ya UNAFIKI, uwa anapotabasamu hama kucheka uwa ana maanisha hivyo………ndomana mtoto akiwa anaumwa utamuona katika sura yake namna ilivyopoa ucheshi wote umekwisha ( kwa mwenye hulka ya ucheshi) analia hovyohovyo tofauti na ilivyo kawaida yake.

Muonekano wa mtoto katika sura yake ndio kusudi la Mungu katika maisha yetu mbele zake na mbele za wanadamu, japo kwa sasa unaweza kukuta mtu anacheka sana lakini amaanishi kabisa kucheka, anakuwa zaidi ya wenye tasnia ya wachekeshaji.

Marko 10:15 Amin, nawaambieni, Ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa.

Mwenendo wa mtoto unaubariki sana moyo wa Mungu, anapo samehe  ana maanisha na anapopenda pia ana maanisha sura yake iliyobebwa na hisia zake uwa zinaonekana katika sura yake, hivyo upati shida kutambua hiki nilichokifanya nimemfurahisha hama nimemuhuzisha pindi utakapomuangalia katika uso wake utatambua ukweli usio kuwa na maswali lakini sio kwa watu wazima anaweza akacheka hadi jino la mwisho lakini hakuna la kweli hata mmoja siri iko ndani yake.

SURA YA MTOTO NDANI YA SURA YAKO NDIO FURAHA YA MUNGU!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:
Cothey  Nelson………………………………………………………….0764 018535

“Sura inayosadifu kilicho ndani ya moyo wa mtu”

Jumanne, 21 Machi 2017

AMANI YANGU!



AMANI YANGU!


Yohana 14:27 Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu  utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Tunakubaliana kuwa unapozungumzia AMANI ni mbali na kicheko, kufurahi hama tabasamu…… japo hivi vyote vinaweza kubebwa na amani, na sio lazima vikiwepo hivi ni dalili ya kutosha kuwa hapo pana amani,

Katika swala linalobeba ubinafsi kwa kiasi kikubwa ni hali hii inaitwa AMANI kwani unaweza kuwa watu zaidi 10000000 katika sehemu moja na wote mkaonekana wanafuraha, wanacheka na kucheza kwa pamoja lakini katika hali hiyo kila mtu anakuwa siri ya moyo wake ( mambo yanayoendelea ndani ya moyo wake) bila shaka wako watu wengine watakuwapo hapo lakini awana utulivu wa akili hata moyo yaani makazi ya AMANI,

Tafsiri rahisi ya kidunia hili neon amani ni hali ya moyo kukubaliana na hali iliyopo haijarishi wengine wanaonaje(kuridhika kunako pelekea kufurahia).

huwezi kutambua AMANI ya mtu kwa kuangalia muonekano wake namna alivyo vaa hama anavyoongea tu kwakua wapo wenye hulka ya kuchekesha sana (yani ukimuona tu unajisikia kufurahi) lakini siri ya moyo wake anaijua mwenyewe.

Tunakubaliana kuwa Amani isipokuwepo basi hapo  radha ya vitu inatoweka hata kama ni chakula chenye ubora gani? Hama gari lenye thamani kubwa kiasi gani ? hama nyumba yenye fahari kubwa kiasi gani kamwe hauta ona maana ya kuwa navyo kwakua kiunganishi chema kati ya moyo wako na vitu ulivyonavyo hakipo.

Napia unaweza kuwa na kitu hama mtu ambaye watu wote wakashindwa kupata tafsiri sahihi ya wewe kuwa naye inawezekana wakikuchukua wewe na yeye hama hivyo vitu ulivyonavyo hawaona kuwa ulitakiwa kuwa hapo/kuwa na mtu huyo lakini kwakua hivyo vitu viunganishwa na amani ya moyo wako wewe ndio unawashangaa hao watu kwakua wanawaza hivi kana kwamba wanaishi wao na wala sio mimi nabinafsi ndio ulichukua maamuzi kwa utashi wa akili yako na Uradhi wa mapenzi ya moyo wako.

Tafsiri rahisi ya dunia kuhusu Amani ni hali ya uhakika wa kitu chema,hivyo uishi katika matumaini na kujipa moyo kuwa ipo siku kile anachokitamani hama shauku nacho kitatimia kwa majira fulani lakini hali hii ni tofauti kwa mtu anayemwamini Mungu uwa anajua kwa sababu yuko na Mungu basi amani yake hipo Mungu ndio amani inayotawala ndani yake, hivyo matumaini yake hayako katika vitu bali yako ndani ya Mungu, ndiko amani yake iliko fichwa na iko salama.

Katika swala hili la AMANI uwa hakuna maombi yatakayoleta amani ndani ya maisha zaidi ya kuwa mbeba Amani aingie ndani yako aichie amani yako ipitayo akili zako na kukupa utatuzi katika maisha yanayo kukabili.

Uwa hakuna mwendelezo wa kudumu kama kuna kitu unafanya pasipo amani kwakua hauta kifurahia sana na lolote linaweza kutokea haijarishi umelipanga au la! Kwani kuwa na mtu hama kitu au kufanya shughuli yoyote pasipo kuwa na amani nayo hapo ni sawasawa na kutembea na mtu pasipo kunia mamoja hama kupata……. hivyo kila mtu utembea na akili yake mwenyewe hivyo hapo kuachana ni jambo linalowezekana tu! Hama kuacha shughuli unayoifanya.

Katika dunia utasikia sana watu wakisema “ mimi nailinda amani yangu” lakini ukweli amani hailindwi kwa namna unavyoweza fikiria bali mwenye asili ya amani anayeichupua katika mazingira yote haijarishi nini kimekukumba amani yake inazidi hilo jambo lakini kwakutumia akili ya kibinadamu yako mambo ambayo utashndwa kuyaimiri na hatimae ukakuta uko chini.

Ni muhimu kutambua Amani ni mali ya Mungu yaani inapatika katika himaya ya Mungu hivyo unahitaji wewe kuwa wa Mungu kweli hili amani yake iwe ndani yako na wala sio kuomba mchana na usiku, amani yake ikupe uwezo wa kumudu kila kishindo hatimae uweze kuwa bora katika kila kona.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….0764 018535

Jumatano, 15 Machi 2017

JANA SIO LEO JAPO ZOTE NI SIKU!



JANA SIO LEO JAPO ZOTE NI SIKU!


Utofauti wa kitu usichotegemea kuwa tofauti ndio usumbufu wa akili ya mtu!

Tukiangalia mfano wa mama aliye na mtoto mdogo pindi anapotambua chakula kile mtoto apendacho hama kinywaji kile mtoto atakacho hivyo kutoka na mapenzi makubwa kwa mtoto wake uhakikisha kile apendacho mwanae anampatia sawa na uwezo wake lakini pindi atakapo tambua mbona ajakifurahia vizuri hama ajachangamkia kama ilivyo kawaida yake hapo maswali kwa mama uweza kuibuka kwanini mwanangu ali vizuri kama jana je! Ana nini? Kipi kinamsumbua ndani yake? Hapo tofauti ya jana na leo unaweza kuiona,

Kinachomfanya mtu awe na maswali pindi atakapo kutana na mtu ni hile hali aliyoizoea kuona kuwa haipo tena hata kama kwa udogo maadamu kunatofauti basi ujua kuwa hii hali ni ya dalili mbaya/nzuri hivyo uweza kutoa chumba cha mawazo kuhusu hilo jambo na kutafuta kwanini huyu rafiki amekuwa tofauti inawezekana ni kwa sababu yangu hama yake mwenyewe hama upendo umekwisha hama unaelekea ukingoni,

Japo nakubaliana kabisa pindi unapoona utofauti wa hali yoyote kwa mtu au kitu bado uko una maamuzi ya kuweza kutafuta ufumbuzi hama kupotezea ukisema lolote na liwe tu! Kwani yeye ameshika pumzi yangu.

Pia na amini sio kila utofauti unaojitokeza unakuwa na utatuzi mmoja uko utofauti mwingine utaitaji upe nafasi kwanza na uko utofauti ambao unahitaji ukabili mapema kabla ujawa mkubwa ukashindwa kuupatia ufumbuzi pia uko utofauti ambao unahitaji kuupotezea maana wakati mwingine ukichukua nafasi ndani ya maisha yako utakuchelewesha kuyafanya mambo ya msingi hama kufanya mambo kwa ufanisi,

Naamini tatizo sio utofauti uliojitokeza bali kwanini utofauti umetokea? Jibu la hapo ndilo linaweza kuzaa moyo kuwa chini hama kuweza kuikabili hali hiyo iliyojitokeza.

Unaweza kuwa mtu kuwa hauna pesa kwa sasa lisiwe tatizo kwako kwakua labda kuna mahali umewekeza na unategemea kupata mrejesho mzuri tu kwa muda mfupi lakini inapotokea ukajikuta huna hela kutokana na matumizi mabaya hama umeibiwa na hauna akiba hapo jambo hilo linaweza kuleta shida,

Katika maisha ya mwanadamu kuna kipindi hama siku unazozipenda kiasi kwamba unatamani ziendelee tu maana zinaleta faraja sana katika maisha yako! Wakati mwingine unafikiria hivi jana nilifanya nini ikawa hivi ngoja na leo niongeze umakini labda itajirudia ile jana ukweli hali hii inakuwa njema sana pale hali ya jana inapojirudia lakini inakuwa mbaya sana ile hali ya jana inaposhindwa kijirudia kwa maana hapo ndipo maswali na kuchanganyikiwa kunaweza kuzaliwa,

Lakini inapotokea utofauti wa kitu ambacho ulikuwa unahisi kitabadilika hama kujua kabisa kitabadilika hapo inakuwa ni rahisi tu kwakua akili yako ilikuwa imesha jua mathalani nyama/samaki wabichi wasipo tunzwa kwenye friji katika mazingira ya joto bila shaka baada ya siku chache utakapoanza kusikia harufu hauta shtuka sana kwakua unajua uwezekano wa mboga hiyo kuharibika ni mkubwa kutokana na hali halisi.

Ndomana mtu mmoja anaweza kuwa katika pande mbili mkionana anacheka na mkiwa mbali anaanza kukuponda, mchana rafiki na usiku ni adui yako,

Ndomana unaweza kuwakuta watu jana walikuwa marafiki sana kiasi kwamba ilikuwa uweza kutabiri kuwa ipo siku watatengana au kuwa mbali lakini siku inafika unashangaa hivi leo mmekuwa hivi.

Usikubali kutembea kwa namna hilehile uliyoizoea hatakama ni nzuri lazima uandae akili yako kukabiliana na hali itakayokubali ili mradi USALAMA WAKO uzidi wala usipungue siku baada ya siku,

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………0764 018535

Jumatano, 1 Machi 2017

ISHARA KUBWA YA KUJIPENDA! PENDA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO.



THAMANI YA KITU KILICHOPOTEA!


Hili limekuwa tatizo la wanadamu wengi hasa waafrika kuona thamani ya kitu mara baada ya kutokuwepo tena……unaweza kuwa na chepeo/koleo likawepo tu nyumbani pasipo na uangalizi wowote kwa sababu uhitaji wake bado hivyo ukapoteza umakini juu ya hicho kifaa pindi kikatoweka kwa kuibiwa hama hali yoyote mathalani mvua na hapo pakatokea uhitaji wake ndipo uanza kulitafuta kwa bidii na kuuliza kila kona jamani mmenionea wapi kifaa changu maana nina kazi nacho na bila hicho hali itakuwa ngumu sana “naombeni mnisaidie”

Unaweza kuwa ukipendi kiungo kimoja wapo katika mwili wako mathalani kidole katika mguu wako kwa kuwa watu wanakisema kimekaa vibaya lakini siku mguu wako utakapoondolewa kwa sababu mbalimbali hapo ndipo utaona ubora na hauta ona kasoro yoyote ya kile kidole ambacho wengi waliona akikosawa,

Tumeona watu walioishi na kujisifia uzuri wao na baadae ulipopotea akaanza kuwa mpole na tambo/majivuno yote yakaisha pia wako walikuwa na pesa nyingi sana lakini baada ya kipindi pesa zikaisha akawa anakumbuka enzi zile alizokuwa na pesa sio hayo tu pia wako watu walikuwa wakimiliki madini ya gharama kubwa lakini muda hiyo biashara ikaondoka mikononi mwao na wakajikuta wakiwa katika hali mbaya sana na wengine baada ya kushindwa kuimiri maisha mapya tofauti na walivyo zoea wakajikuta wamekuwa chizi,

Katika maisha ya kawaida ya wanadamu kunakipindi unaishi na vitu/kitu kana kwamba unaishi nacho/navyo milele, ukajisahau na ukaona kuwa wewe tayari umeshafika hama umeshapata.
Naweza sema thamani ya kitu kilichopotea hakuna uwezo wa kukikisia ukapata hile thamani yake halisi kinachotakiwa kuwa nacho!

KARIBU!
Ujue kama mwanadamu kuna vitu ukivipoteza unaweza kupata mabadala wake na maisha yakaendelea mathalani vitu vilivyo nje ya wewe ukivipoteza na moyo uka chini kwa muda fulani lakini baadae ukapata mbadala basi furaha inaweza ikaendelea hama neema ya Mungu ikauwisha nafsi yako ikawa imara tena!

Lakini sio vitu vya ndani yako alivyoweka Mungu mwenyewe kwa kusudi lake ukashindwa kuvitendea ipasavyo na hatimaye vikashindwa kuleta faida kwa Mungu, hapo ugomvi wake unakuwa wewe na Mungu na hakuna kisingizio yeye ataelewa, labda jirani yako amepelekea  ukashindwa kukitendea kazi kile kilicho ndani yako, Mungu maadamu amekupa anajua kitafanya kazi japo kuwa wewe ndio muhusika mkuu wa kukiruhusu

-isije kama ya Adam na Eva kuwaza kusingiziana, badala ya kufuata maelekezo waliyopewa,
Mathayo 25:14 Maana ni mfano wa mtu atakaye kusafiri, aliwaita watumwa wake, akaweka kwao mali zake.
                    15 Akampa mmoja talanta tano, na mmoja talanta mbili, na mmoja talanta moja; kila mtu kwa kadiri ya uwezo wake; akasafiri.
                    16 Mara yule aliyepokea talanta tano akaenda, akafanya biashara nazo, akachuma faida talanta nyingine tano.
                    17 Vile vile na yule mwenye mbili, yeye naye akachuma nyingine mbili faida.
                    18 Lakini yule aliyepokea moja alikwenda akafukua chini, akaificha fedha ya bwana wake.
                    19 Baada ya siku nyingi akaja bwana wa watumwa wale, akafanya hesabu nao.
                    20 Akaja yule aliyepokea talanta tano, akaleta talanta nyingine tano, akisema, Bwana, uliweka kwangu talanta tano; tazama, talanta nyingine tano nilizopata faida.
                 21 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
                 22 Akaja na yule aliyepokea talanta mbili, akasema, Bwana, uliweka kwangu talanta mbili; tazama, talanta nyingine mbili nilizopata faida.
                 23 Bwana wake akamwambia, Vema, mtumwa mwema na mwaminifu; ulikuwa mwaminifu kwa machache, nitakuweka juu ya mengi; ingia katika furaha ya bwana wako.
                 24 Akaja na yule aliyepokea talanta moja, akasema, Bwana, nalitambua ya kuwa wewe u mtu mgumu, wavuna usipopanda, wakusanya usipotawanya;
                 25 basi nikaogopa, nikaenda nikaificha talanta yako katika ardhi; tazama, unayo iliyo yako.
                 26 Bwana wake akajibu, akamwambia, Wewe mtumwa mbaya na mlegevu, ulijua ya kuwa navuna nisipopanda, nakusanya nisipotawanya;
                 27 basi, ilikupasa kuiweka fedha yangu kwa watoao riba; nami nikija ningalipata iliyo yangu na faida yake.
                 28 Basi, mnyang'anyeni talanta hiyo, mpeni yule aliye nazo talanta kumi.
                 29 Kwa maana kila mwenye kitu atapewa, na kuongezewa tele; lakini asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang'anywa.
                 30 Na mtumwa yule asiyefaa, mtupeni mbali katika giza la nje; ndiko kutakuwako kilio na kusaga meno.
                  31 Hapo atakapokuja Mwana wa Adamu katika utukufu wake, na malaika watakatifu wote pamoja naye, ndipo atakapoketi katika kiti cha utukufu wake;

Ni kweli ukikosa mengine Mungu atakupa faraja lakini sio kusudi likiondolewa ndani yako hapo faraja ya Mungu inakosekana unakuwa mpweke hata kama unakila kitu ambacho ulifikiri kitaleta amani ndani ya maisha yako,

Niseme wazi kila jambo mtu analifanya anataka faida lakini ujue kuwa pasipo faida anaona hakuna maana ya kuendelea kulifanya,

Ni muhimu kuheshimu kitu ambacho Mungu ameweka ndani yako baada ya kuona unastahili kuwa nacho aijarishi ni kidogo hama kikubwa bado aliona unaweza kukifanyia kazi,

Na ukumbuke kuwa amehakikisha uwepo duniani na anakuhudumia kukufanya uendelee kuishi kwa sababu ya hilo, sawa na mtu aliye ajairiwa na kupewa nyumba, gari na mshahara kuna kusudi ambalo anatakiwa alitekeleze ili hiyo kampuni iweze kufaidika naye,

Mungu anashida na unaonekaje! Bali anashida na lile kusudi aliloweka ndani yako kuhakikisha kuwa linamletea faida aliyoitaka ndani yako.

ISHARA KUBWA YA KUJIPENDA! PENDA KUSUDI LA MUNGU NDANI YAKO.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….0764 018535