Ijumaa, 21 Machi 2014

AMANI ADIMU



AMANI ISIYO NA MIPAKA,

Amani yangu na wapa sio kama ulimwengu utoavyo…….yesu alisema!

AMANI katika maisha ya mtu yeyote ,kwa mwanadamu hiki ni zaidi ya kuwa na chochote mathalani watoto, mme au mke na hata kazi na amini hakuna madini yoyote hapa duniani yanayoweza chukua thamani ya amani ndani moyo wa mtu, ni kweli kuna wakati unaweza usione maana wa jambo lolote au mtu yeyote lakini si kama AMANI.Na unaweza kuwa na chochote lakini kama hauna AMANI utoshelevu wa hicho kitu akita kuwa na maana sana zaidi kwakua kinacholeta radha katika yote ni AMANI, wakati mwingine tunaweza fananisha AMANI kama chumvi katika chakula chochote unaweza ukaweka kila kitu lakini kama chumvi haipo jua hapo hakuna radha utakayoipata kwa ukamilifu.

Amani kama angekuwa mtu basi watu wote wangependa kuwa rafiki yao wa dhati kwani watu wote wanahitaji amani hata kama mchawi,jambazi,chizi na wengine wengi wanahitaji amani na wanapenda maisha yao yote yatawaliwe na amani.kutokana na mtazamo huu watu wengi wamekuwa wa kikiri kuwa haiwezekani kama mwanadamu kutawaliwa na amani wakati wote ungalipo hapa duniani kwani wanaamini hapa duniani sio mahali salama sana kwani kuna kukasilishwa,kuumizwa na hata kudhurumiwa hivyo watu wamekubaliana  kuwa na amani iliyo na mipaka.

Watu wengi tumekuwa tukiishi na amani kanakwamba ni haki yake kutokea halafu ikatoweka tumekubaliana na hali hii hivyo tumeona mtu kuishi pasipo amani ni jambo la kawaida, na mtu kuwa mahali fulani au kufanya jambo fulani pasipo amani basi panakuwa na mgawanyiko ulio katika mwili na akili kwa maana hii akili na mwili vinakosa ushirikiano kamilifu basi kwa hali hii mtu uweza kujigawa pasipo ridhaa yao binafsi.

Ningependa utambue kuwa amani ni haki yako ya kudumu na wala sio ya muda fulani tu au yakutokea kwa majira fulani mathalani kipindi ambacho unazo pesa za kukidhi mahitaji yako kwa wakati wako huo na sio hilo tu bali pia au wakati ambao unahisi kupendwa na kila mmoja kwa kipindi fulani.Ni kweli tunakuwa na mfano wa amani lakini sio amani yenyewe kwa kuwa kila amani huwa kuna shina au misingi yake ambayo haiwezi kubomolewa na chochote kile. Imkuwa si ajabu mtu kusema asubui nilikuwa na amani yangu ghafla imetoweka sijui kwanini? Au mtu akisema maneno haya…. mimi nilikuwa na amani zangu lakini ulipokuja tu amani yote imetoweka, amani sio kitu cha kufikirika tu ambacho kinaishia kwenye akili ni zaidi ya hapo kwani kina nguvu na uwezo mkubwa wa kumtawala mtu.

Wana amani nyingi waipendayo sheria ya bwana wala hakuna la kuwa kwaza….”

Hivyo ukifikia hatua ya kukwazika basi hiyo amani ya kweli haipo ndani yako kwa ukamilifu wake.
Wako watu wakijishughulisha na mambo fulani au kiburudisho fulani ili mradi aweze kusikia amani ndani ya moyo wake…..lakini muda mwingi imekuwa sivyo kama alivyotegemea!!!!!!

Amani za watu wengi zimekuwa ni za vipindi fulani kiasi kwamba watu uweza kusema kwamba je! Kwenye msiba kunauwezekano kuwa na amani hasa kwa mtu unaye mpenda au aliyekaribu kweli unaweza kuendelea amani iendelee kutawala ya moyo wako.Ninapozungumzia amani na zungumzia zaidi ya kuwa na furaha au utulivu huwa amani haijaishia hapo bali imepitiliza zaidi ndani sana na hakuna kipimo chake.

AMANI= MATUMAINI  + ULINZI

Hii ndio tafsiri yangu ya neno Amani katika hili neno lazima pawepo na muambatano wa matumaini na ulinzi kwa kile unachokitumaini kuwa utakipa au kifikia.Mambo haya matatu uwa yanaenda pamoja na ndio yanakamilishana yote kwa ubora sana.

Amani ubebwa na matumaini yaliyo ndani yako yanayolindwa na katika kufanikisha jambo, hivyo shina la matumaini linategemea liko wapi au limebebwa na nini? Na je uhakika wa kufikia katika yale unayoyaendea.Tunapozunguzia ulinzi uwatunatoa maana ambayo inalandana na Imani-kitu kinachokupa uhakika.Katika yote utayoyapitia amani haiwezi kuondoka kwa sababu imebebwa na vitu hivyo viwili vilivyo na ukamilisho kwa ufasaha.

Ukiwa katika misingi hii lazima itakuwa inachipuka kwa wakati wote katika hali mbalimbali iliyo ngumu au nzito unakuwa na AMANI ISIYO NA MIPAKA ambayo inachipuka ndani yako na kukupa busara katika maamuzi siku baada ya siku,kama ukiwa na amani ya kipindi tu ya ushawishi wa mwili hauwezifika mbali kwakua ni ngumu kushamiri na kuwa na uimara wa nyakati zote.

Lazima uwe na amani ambayo hakuna kinachoweza kuondoa iwe mchumba, rafiki, ndugu au wazazi bali inakuwa imeshirikiwa na nguvu ya mbingu ndani yako ambayo yeye aliyoiweka ndio mwenye uwezo wa kuiondoa na hakuna wa kuiondoa zaidi yake ukiona amani inaondolewa tu jua haijajikita katika misingi ya matumaini pamoja na ulinzi(imani).

Amani isipo kuwepo ni wazi mahala hapo uwezi ukadumu na vilevile amani isipokuwepo mahali hapo hauwezi ukapafurahia na pakaleta burudiko ndani ya moyo wako.

Usiwe na amani isiyoimarika bali yenye mabadiliko siku baada ya siku,amani inatabia ya kuongezeka pale ambapo shida inapokuwa kubwa huwa aipungui kama kawaida ya mambo ya dunia yalivyokuwa.hivyo amani yako inapotoweka pale ambapo mambo yanapokukabili basi ujue hiyo amani ujaipokea kwa kristo bali inafanana na hile ambayo kristo anaiachilia kwa watu wake.

Uwa amani hii ambayo Mungu anapoiachilia haitaji huichochee bali ipo inatawala nakutembea katika mwili mzima una kuwa mtu wa kicheko wa furaha na mawazo yaliyotulia yenye mwelekeo katika mwelekeo uliosahihi katika mwelekeo ulio na ulinzi wa ki Mungu katika kuyafanikisha yale yote yaliyo matumaini yako.
Na haiwezekani ukawa na amani ya namna hii kwa kuombewa au kutabiriwa bali katika kuliruhusu neno la Mungu katika mwili wako mzima kwa uhakika na kukufanya vile linavyotaka katika kiwango chake na sio katika fikra zako bali katika akili ya hilo neno kwa utoshelevu wake. “Mjue sana Mungu ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujiaa…    Ayubu 22:21

Hauwezi kufanikiwa katika huduma yako na mambo mengine ya kuinua ufalme wa Mungu kama tu una amani yenye mipaka(amani yenye kawaida ya dunia) kwakua yenye sio kamilifu kumudu kila hali itayojitokeza lakini amani ambayo haina mipaka hakuna jambo lililowa tokea au litakalotokea likamtingisha mtu wa namna hii.

Amani hii uwa uenda pamoja na ujasiri kwakua amani hii ndani yake hakuna hofu ndani bali inakuwa ni amani yenye uhakika kwa kila kile kilichokusudiwa kwa kua hii ni amani iliyo kuu kuliko amani yoyote(shwari kuu).Vilevile amani hiihaendani na utashi wa mwili ndani yake hakuna asila,chuki,kisasi wala dharau. Hii ni amani iliyombeba Mungu kwa utoshelevu wake hivyo matunda yaliyo ndani ya Mungu ndiyo yaliyo ndani ya amani hii katika ubora wake, kwa maana nyingine amani hii inaongozwa na Roho kwa utoshelevu wake uliosahihi zaidi hatua za Roho mtakatifu ndio hatua zake.

Vilevile amani inaenda pamoja sana na pendo la kristo uwa vinashikama pamoja sana kwakua amani ufanyakazi mahali penye pendo la Mungu kwa utoshelevu kwakua amani hii imebeba dhima ya kuujenga ufalme wake,kwakua amani yake inakuwa kwa ajili yake na sio jambo lingine.

Amani hii pia inatiwa nguvu na macho yako ya rohoni baada ya kutiwa nguvu ili kuona kama vile Mungu anavyoona na tumani lizaliwe hapo na wala sio mahala pengine kwa kua macho ya Mungu yamebeba ulinzi wa Mungu na utoshelevu wake.Na utulivu na maamuzi yenye misingi iliyo bora yanatokana sana na AMANI ISIYO NA MIPAKA!

Amani hii haina uhusiano na akili ya kibinadamu kwakua haijashikamanishwa na mwili bali na roho iliyojaa Mungu. ukiona unaihusisha na akili jua hiyo sio amani iliyombeba kristo bali itakuwa imebeba kitu kingine!



Imeandaliwa na ;
                      
                 Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                  
                Katiti, James       - 0713 398 042 orjames.adili19@gmail.com                                                 


KUWA NAYO AWE NAWE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Jumamosi, 8 Machi 2014

UHURU WAKO



UHURU WA MWANADAMU

Mwanadamu katika sifa nyingi alizonazo mojawapo ni UHURU. Japo kila rika uhuru uwa unaanza kuwa unamipaka mwisho unakuwa hauna mipaka, kufanya vile uonavyo vyema na sio vile jamii inavyotazamia bali ni kile unachojisikia katika matakwa yako.

Na kila mtu kila anauheshimu uhuru wake ndomana yuko tayari kuulinda uhuru wake kwa gharama yeyote ili mradi tu anaendelea kuwa uhuru, na wakati mwingine ukitaka kujua huyu ni nani anafanya nini basi mwingilie katika uhuru wake basi hapo utajua namna mtu anavyodhihirisha yeye ni nani, hama mtu mwenye asila kali, mstaharabu au mnafiki na mengine mengi. Uhuru wa mtu tunaweza sema ni almasi ya mtu kwakua ni kitu ambacho mtu anajivunia kuwa ni mali ya mtu binafsi. Kila mtu mtu upenda kuheshimiwa kwa uhuru wake hivyo upelekea mtu au umlazimu mtu huyo kuheshimu watu wengine.

Na katika kutumia uhuru wa mtu binafsi basi uweza kupeleka mahala pa zuri saaana au pabaya saaana lakini yote yamebebwa na uhuru mtu binafsi na ni kawaida kuona kama umemuheshimu mtu ni kuheshimu uhuru wake na sio jambo linguine kwakua kila jambo ufanywa katika mistari iliyo bebwa na msingi wa uhuru wa mtu binafsi.hakuna kitu kinachoweza kumfurahisha mtu kama kile ambacho umekifanya kwa uhuru wako halafu ukafanikiwa na vilevile hakuna kitu kama hiki ambacho mtu uweza kujisikitikia sana kama jambo alilolifanya kwa uhuru wake halafu likaleta uharibifu ndani ya maisha yake.

Uhuru wa mwanadamu umegawanyika katika sehemu kuu tatu;

  i.uhuru wa kujimiliki binafsi

 ii.uhuru wa kumilikiwa na nje ya ubinafsi

 iii.uhuru wa kumilikiwa na Mungu
 


I.UHURU WA KUJIMILIKI BINAFSI

Hiii ni hatua ambayo mtu uwa nayo/ufikia mara baada kutoka kwenye himaya ya wazazi huwa na uhuru wa nafsi katika kufanya yale ya ujazayo moyo wake pasipo kuuhusisha kitu kingine kutokea kikaleta shida katika maamuzi yake. Hali hii uwa inkuwa sauti ya muhusika kuwa na nguvu zaidi ya jambo jingine na hii ni hatua nzuri kwa kuwa unawe kuvunja mipaka ya zaidi unavyofahamu kwakua uhuru ulio ndani yako unakusukuma kufanya jambo fulani kutokana na uhuru ulionao basi uwa unakupa wepesi kufanya jambo hilo katika moyo wa kujaribu katika kufanya vyema.

Ni uhuru wa kujisikiliza sana wewe binafsi kuliko kingine hivyo wakati mwingine uweza kufanya jambo ambalo hautajali wengine watachukulia katika namna gani katika hali chanya au hasi.hii ni hatua inayoweza leta msukuma nakupelekea mtu katika kufanikisha jambo ambalo watu wengine hawakuweza kulifanikisha.
Japo hatua hii inamazuri mengi lakini katika upande mwingine mbele za Mungu hii hatua ni kikwazo kikubwa sana katika kufanisha mpango wa Mungu hapa duniani kwa vile anavyoona upingamiza unaotokana na umiliki wako binafsi( kujimiliki binafsi). Ni hali ambayo Mungu inampa ugumu katika utendaji wake kwani lolote atakalo kukwambia lazima kwanza lipate kibali kwenye uhuru binafsi halafu litendeke hivyo kama tu alitapatakibali katika uhuru ubinafsi halitaweza tendeka, na jambo lolote linapopita katika uhuru wa nafsi basi nafsi uhesabu kugharimika kwake katika jambo hilo hivyo ikiona kuna kugharimika sana kuliko kufaidika basi uweza kulizuia hilo jambo lisiweze kutendeka kabisa na hivyo kuwa kikwazo cha mpango wa Mungu hapa duniani. Uhuru huu wakati mwingine upelekea hali ya kujiamini sana kuliko kawaida na kupelekea kuchukua maamuzi ambayo yataleta picha nzuri katika nafsi yake na sio katika upande mwingine wowote. 

Pia hali uweza kukupelekea kushindwa kukaa na watu wengine hata mbele za Mungu ikawa kikwazo kikubwa sana. Katika hii hatua unaweza kujiweka kipaumbele kiasi kwamba hata utawajali wachungaji,wazazi hata ndugu zake hali hii inatokea sana katika jamii katika kutafuta kitu ambacho kitanufaisha nafsi yako kuliko chochote.

II.UHURU WA KUMILIKIWA NA NJE YA UBINAFSI

Na hali hii inawezajengwa na ushawishi wa atu au wa vitu au utashi wa mtu binafsi pia hii ni hali inayofuata mara baada ya umiliki wa nafsi hali ya kuwa sauti yako kuwa na nguvu lakini hatua hii ni hali ya kitu kingine kuwa na nguvu zaidi ya nafsi yako hivyo sauti ya nafsi ya nafsi yako haina nguvu sana kama vitu vingine hali hii uchelewesha katika kuchukua maamuzi au kuchukua maamuzi pasipo ridhaa ya nafsi kamili. Na hali ndio iko katika maisha ya watu wengi kwani wengi wanauliza marafiki,shemeji na hata wazazi katika kuchukua maamuzi Fulani na mgawanyiko wake
    
 a)kitu; gari, mti au mlima
   
 b)mwenzi; mke au mume
  
  c)wazazi

mtu anaweza kuruhusu vitu vingine viweze kuwa na sauti katika maisha ya mtu husika kwa kukosa kwa yale uliyoyakusudia. mtu anakuwa ametawaliwa zaidi ya maamuzi yake binafsi kwakua ndani ya nafsi yake hakuna utoshelevu ulio sahihi katika kuchukua maamuzi. Na hali hii ya kutoridhika katika kuitosheleza nafsi yake, uweza mfanya mtu sio jambo jambo rahisi katika kuchukua maamuzi kwakua upima gharama zake kwa mapana sana na hata yasiyowezekana kutokea anaweza kutoa uwezekano mkubwa wakutokea  ndani yake kuna hali isiyo shwari. Na hali hii upelekea mtu hali ya kutokua rahisi katika kuridhika na hali moja na hivyo mtu huyu uweza kukosa msimamo wa namna ya kufanya kwa usahihi wa jambo husika, hali hii sio inamtesa mtu husika bali hata jambo lenyewe na pia kwa lile ambalo linasubiliwa na hata kwa wanao lisubiria jambo hilo kwakua inawezekana kuchelewa kwao ndio upelekea maumivu kuzidi kushamiri katika maisha ya watu hao. Japo watu wengi wanaamini kuwa katika kuchanganya mawazo mengi kunaleta majibu yaliyo bora mimi na kataa kwani kwanza lazima uweze na hali ya binafsi ya kile unachokiamini ndicho uweze kushirikiana na wengine ili uweze kupata kitu kitachoboresha na kuimarisha katika kile ulichokiamini.
Hali hii pia ni kikwazo mbele za Mungu kwani kijambo ambalo Mungu atakwambia lazima uweze kulipeleka katika mizani ili jibu sahihi hii ni hatari sana kwani kuna mambo mengine ulivyoeleweshwa wewe ni tofauti na wengine wanavyoelewa. Sauli katika kufuata ushauri wa watu wengine zaidi ya agizo alilopewa na Mungu vilevile adamu katika kutekeleza sauti ya mke wake kuliko lile agizo alilopewa na Mungu.  kwa maana hii ni jambo hili linahitaji misuli katika maamuzi yasioweza kuingiliwa lakini yawe sahihi. Haya yote ni sawa kwa kauli ya ubinadamu lakini yamekuwa kikwazo kikubwa katika utendaji wa Mungu ndani ya maisha ya mwanadamu kwakushauliana hata yasiyo takiwa kushauriwa, ni muhimu uweze kujishauri kabla ya kushauriwa.

III.UHURU WA KUMILIKIWA NA MUNGU

Hili Mungu akumiliki anahitaji uhuru wa mtu binfsi au utayari wa mmilikiwa na hichi ndicho kilio cha Mungu kwa wanadamu na ndio hatua hii ambayo Mungu anatamani tuwe hapo ili yale makusudi yake yaweze kujidhihirisha kwa ukamilifu ndani ya maisha yetu, kwa hakika dunia vile tulivyo ni matokeo ya kupoteza uhuru wa Mungu ndani ya maisha yao watu wamekuwa na nguvu katika maisha yao na hata ubinafsi wao umekuwa na kiasi cha juu kuliko jambo lolote.

Katika maisha na Mungu kama hiki kisipokuwa na nguvu inayostahili jua kwamba hakuna jambo unalolifanya likawa na la maana sana kwa Mungu hiki kama ukipuuzia jambo hakuna ustahivu unaotakiwa . kwa maelezo ya haya Mungu anatafuta mtu atakaye mwabudu katika roho na kweli na sio waenda kanisani au wafuata mkumbo ni kweli unapenda uhuru binafsi lakini hata Mungu anahitaji atumie uhuru wako ndani yako wewe kama hekalu la Mungu mluhusu yeye afanye kwa raha zake ndani yako ili azidi kuona fahari juu yako,

Ni vizuri kwenda kwenye msingi wake na sio ya yeye ndio kusudi kuu analolitaka ndani yenu ndomana anasema mimi ni Mungu mwenye wivu usiwe na mungu mwingine ila mimi hichi ndicho Mungu anataka kwa mwanadamu ili uweze kuwa baba yake nawe uwe wake, na pasipo hilo sahau tu Mungu kudhihirika kwa ukamilifu. Kwakua anajua pindi atapokuwa akizifanya kazi zake ndani yako hauta inuka kiburi wala kujiona wewe ni mtu saaaana kuliko wengine lakini tunakuwa KRISTO.

Imeandaliwa na ;
                     Nelson, Cothey – 0764 018 535 or cotheyn@yahoo.com
                    Katiti, James       - 0713 398 042 or james.adili19@gmail.com



KILA LA KHERI…………..RAFIKI