Jumamosi, 28 Machi 2015

Living Water Centre Ministry Makuti Kawe Dar Es Salaam

Living Water Centre Ministry Makuti Kawe Dar Es Salaam

VILE ULIVYO



VILE ULIVYO;



     Vile ulivyo ndio utofauti wa wewe na mwingine na huo utofauti upo katika utendaji, mawazo, maamuzi na nguvu ya kutafsiri na hata muonekano. Ukweli katika swala ambalo Mungu amelifanya na wanadamu wengi wanamshangaa sana Mungu, ni utofauti uliopo kwa wanadamu kwa wanadamu kua japo wako wengi lakini bado inakuwa ni rahisi kuwatofautisha kati ya mtu na mtu………… katika maeneo ambao watu wanamuona Mungu kuwa ni mweza wa yote  kwa utofauti watu katika kujiona utofauti wao wenyewe.

 Utofauti wa mtu na mtu hiki ni kitu kizuri kwani inachangia kuona radha tofauti tofauti ya watu na hivyo kuifurahia sana dunia katika utofauti huo japo sio wote wanafurahia huo utofauti kwani wako watu wenye hali ya ubinafsi wanapenda wao wenyewe wajitangulize pasipo kuangalia upande mwingine……….niseme kama mwili ili uweze kuwa vizuri unahitaji kuwa na utofauti wa viungo japo vyote ni viungo kuna mikono,miguu,masikio na kadhalika(n.k) lakini vyote ni vya muhimu sana hasa kwakua vyote vinatambua kazi yake kwani kazi ya mikono haiwezi kufanywa na miguu au kazi ya tumbo ikafanywa na mikono hivyo vyote vinategemeana na vinahitajiana japo wewe mwanadamu unaweza ukavipa baadhi ya viungo heshima sana lakini viko ambavyo havionekani mathalani MOYO lakini huyu ndio mwezeshaji wa mambo mengine yaendelee kufanya kazi yake.

Moja ya watu kushindwa kufika mbali kutoishi vile walivyo hivyokujikuta kuyafanya mambo ambayo sio kazi yao nakufanya mambo ya kuwa magumu sana na wengine kumsingizia Mungu anipendi kumbe sio kweli…….lakini utofauti ambao Mungu ameuachilia kwa kila binadamu unakazi yake katika kufanikisha kusudi lake.

Ni seme wazi ili ufanikiwe au ufanikishe katika yale yanayo kukabili ni muhimu uishi maisha yako katika mwelekeo wa ishara ya uhalisi wako, wako wengi wanashindwa si kwasababu wanavipangamizi vingi la asha! ni kwa vile tu hawajaamua kuwa vile walivyo bali amekuwa akiishi kwa kufuata yale wengine wanafanya. Kama watu wote wange weka juhudi katika kutengeza gari tu basi ndege zingetoka wapi? Au meli zingetoka wapi? Ni wazi ule uwezo ulipewa na Mungu ukiutumia basi unaweza ukakupa matunda ambayo unapaswa kuwa nayo…..ziko hazina ambazo Mungu ameweka ndani ili uweze kuzitumia katika kuleta ufumbuzi katika dunia ya sasa.

Mazingira magumu……. hii moja ya sababu ambayo inakuwa ni kikwazo katika kuonyesha au kutembea vile alivyo kwa sababu hakuna urahisi wa mazingira au usaidizi wa mazingira katika kufanikisha lile unalolikusudia, ni seme wazi ukianza kupiga mahesabu ya gharama kama ujaanza kazi yenyewe basi itakuwa ndicho kikwazo cha kwanza katika kufikia malengo yako na hakuna mtu aliweza kufanikiwa kama tu aliogopa gharama.

Lazima uchukulie kwamba wewe ndie unatengeneza misingi wa wengine kufuata hivyo maumivu yako ni kwa ajili ya ustawi wa wengine, kila ataye endeleza hawezi kukusahau kwani alama yako itabaki hapo siku zote.

Muda wa kutambulika……swala lakutambulika lisiwe kichwani mwako japo ndicho chanzo cha kukua na kuongezeka(kufahamika), kwakua unafanya kitu ambacho kiko ndani yako yeye aliyekiweka atakitambulisha na kukiweka hadharani na kuachilia kiu ya watu kukitafuta na inaweza kuanza kwa mtu mmoja halafu kikaenea sehemu kubwa tofauti na unavyofikiria.
Unapoamua kuitoa hazina ya Mungu ambayo ameiweka ndani yako acha maswala ya kujitanguliza au ubinafsi au mimi kwanza tamani kuona lile kusudi au lile jambo unalolifanya kuwafikia watu na kuona ile fahari watu wanaifurahia na kuipokea………kujulikana na kupata fedha hiyo sio kazi yako yuko anaye thamini kile unachokifanya.

Imeandaliwa na;
Cothey  Nelson…………………………………..0764 018535

Ijumaa, 20 Machi 2015

UTAMBULISHO WA KIMBINGU




UTAMBULISHO WA KIMBINGU



Swala sio utambulisho tu! bali unatambulishwaje? Wewe kama nani na katika hadhi unayostahili!
Ndani ya dunia ya sasa kumekuwa na shida sana kwa baadhi ya watu kuwepo mahali Fulani alafu wasitambulishwe kama anavyotaka japo pia wako watu ambao hawana shida sana katika utambulisho,.wako watu wanaghaili kwenda mahali Fulani au kujuta kwa sababu ya kutotambulishwa vile wanavyotaka,wako watu wanaanza kuchukiana na kisilani kisa ametambulishwa ki kawaida sana kwahiyo mojamoja ufikiri ni dharau.

Uko urafiki na kushirikiana kumekuja pale tu baada ya mtu kutambulishwa vizuri na pengine hata kupewa sifa ambayo hakustahili na hivyo kujenga undugu na mashirikiano ya muda kulingana na shughuli yenyewe, japo kutambulishwa hakuongezi hela wala hakupunguzi hela lakini ni kitu cha kawaida tu ni kama kitu cha kutambulika na sio maana nyingine ukiwa katika hali hii basi kama umesahaulika kutambulishwa bado utakuwa na amani kwa kua unajua kama binadamu ni hali ya kawaida kupitiwa lakini kisiwe chanzo cha maamuzi yasiyostahili.

Kila utambulisho unakazi yake katika mazingira husika,na ina aminika kila hadhi ina heshima yake mathalani bosi na mfanyakazi kila mtu anautambulisho wake na unanafasi yake,iko raha ya dunia pindi dunia inapokutambulisha katika nafasi mbalimbali mathalani rais,waziri,boss na hata manager kuna haki utazikosana kama usipotambulishwa katika nafasi unayostahili kwakua heshima ya dunia utaikosa lakini endapo ukatambulishwa basi utayapata yale unayopaswa kuyapata.

Ni kitu kizuri sana kwa mtu anayestahili heshima basi na apewe heshima kutokana na hadhi aliyokuwa nayo.

UTAMBULISHO WA KIMBINGU
Kuna utambulisho ambao unatisha na unashangaza umebebwa na umesimamiwa na Mungu mwenyewe na sauti yake inapotokea ardhi na mbingu vinatia muhuri kuwa vinashikilia katika kutekeleza katika Mungu alichokisema, huu ni utambulisho wa kudumu kwani utambulisho wowote unaweza kuwepo na kuonekana kama kama yeye aliye kutambulisha akiwepo lakini utambulisho wa kimbingu ni utambulisho ambao hauna mwisho wala kikomo.

Uwezi kutambulishwa bila kujitambua!!!
Mungu akujidhihirisha kwa watu ili mradi walikuwa wanamtumikia bali yeye ujidhihirisha kwa Yule ambaye anatembea katika nafasi yake kikamilifu.

Paulo anasema……….Mungu alipoona vema kumdhihirisha mwanawe ndani yangu!
Haya aliyasema akiwa ameshakubali wito wake na kuanza kutendea kazi na hivyo akaona namna Mungu alivyo jidhihirisha katika utendaji wake wote na hakuna aliloshindwa.

Lazima utambue na nafasi yake kwanza na kuipa nafasi katika utendaji wa hiyo na nafasi ili Mungu achilie kitu ambacho kitaadhihirisha kile unachofanya sio kwa ajili yako bali ni Mungu mwenyewe anahusika hivyo atajidhihirisha kujionyesha.

Watu wengi wanatumia muda mwingi kutamani na kuiga na kujifanya kuwa sasa Mungu amejidhihirisha kwao lakini jua kwamba halisi na kisicho halisi kitajulikana tu baada ya muda Fulani, kwa kilicho halisi kitadumu kwakua ndicho kilichopo na kitakuwepo….kwa kusema hivi ni sema kwamba udhihirisho unajitosheleza na walio rohoni tu ndio watakao utambua.

Wako watu wanapopata nafasi za juu kazini wanafikiri Mungu ame wakumbuka hivyo kuonyesha kuwa Mungu amejitambulisha kwao lakini mwisho watu hao wamejikuta wakitembea na bosi zao na mwisho kuwa mbaya zaidi mathalani familia zao kuvunjika na magonjwa kushamiri katika miili yao.( sio kila jambo jema linalokuja kwako limebeba hatma njema katika maisha yako)

Lakini utambilisho wa mbingu hauna hatima mbaya….. kwani umejaa manufaa ya rohoni na mwilini kwa ukamilifu………..na hautaji ujipendekeze ili ujidhihirisha bali ni wewe kutembea katika nafasi yako aliyokupa halafu yeye atakutambulisha tu!

Imeandaliwa na ;
Cothey  Nelson………………………………………..0764 018535

Alhamisi, 12 Machi 2015

UMAKINI WA FAIDA



UMAKINI WA AJABU,



UMAKINI unaweza sema ni hali ya akili yako, macho yako na hisia zako zote kuelekea katika kile unachoelekezwa katika kuelewa au kukifanya….kwa lengo kiwe sehemu ya maisha yako, kwa maana nyingine umakini upelekea akili yako kula chakula chake katika hali stahiki yaani maarifa.

Katika hali ya dunia ya sasa neno Umakini limekuwa likitumwa kutokana na matokeo Fulani yaliyotokea mathalani ukifanya vizuri jambo lolote au mtihani watu watasema alikuwa makini sana katika kuzingatia katika yote aliyoelekezwa na watu wengine watasema alikuwa ni mwanafuzi au mtu msikivu mwenye kuzingatia yote aliyofundishwa LAKINI itokee upande wa pili ya kushindwa jambo Fulani watu watasema mimi niliona mwenendo wake kwa vile ulivyokuwa nilijua matokeo yake yatakuwa haya na wengine watasema yote hatayasiokuwa ya kweli wengine watasema alikuwa MZEMBE! Lakini litakuja mtu mzembe yukoje na mtu aliye makini yukoje na ni kweli wote walio makini ndio wanauwezo kufanya vizuri hili ni swali tu!

Si katai kweli umakini ni chanzo kimoja katika kufanikiwa au kufanikisha jambo moja ambalo umelikusudia, kwani umakini unakupa utaratibu ambao utaoheshimu na kuzingatia japo kuwa unaweza kuweka mwenyewe kutokana maarifa uliyonayo. Na siku zote chanzo cha kuwa makini ni lazima kuwe na lengo na hatua za kufikia hilo lengo.

Katika umakini kuna kitu ambacho uwa kinasahaulika sana kuwa umakini  haukamiliki bila UTAYARI maana palipo na utayari basi hapo panautekelezaji ambao mwisho wake uleta matunda ambayo watu utegemea sana baada ya kuungamanishwa na BIDII ambavyo ubeba juhudi na uvumilivu katika kutimiza jambo ambalo liko mbele yake katika mazingira yeyote katika kutimiza lile ambalo limebebwa ndani yake,

Lazima ujue kwamba umakini ujengwa na utayari baada ya kukubali ndani ya akili yake…hapo ndipo unaweza kusema huyu ni makini sana kwakua tayari dalili za utekelezaji zimeanza kuchipua lakini umakini wa kusikiliza pekee yake sio kigezo cha kutosha cha kusema mtu huyu yuko makini kwani anaweza badilika wakati wowote na kitu kingine wakati wote.

Umakini ujengwa na mtazamo wa Yule unaye msikiliza na namna akili yako inavyomtafsiri kutokana alivyo kwako namna anavyokuona na namna unavyomuona, nguvu ya maarifa uliyonayo ambayo yatakupa kuendelea kusikiliza ua kuacha kusikiliza na upendo wako kwa Mungu inayokupa nguvu katika kumsikiliza mtu wa aina yeyote ili mradi kukipata kile ambacho unachokitaka na kusudi au azma yako katika kufanikisha jambo Fulani katika maisha yako.

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson…………………………………..0764 018535


Jumamosi, 7 Machi 2015

MUONEKANO



MUONEKANO;



Katika DUNIA ya leo kama kuna vitu vinapewa kipaumbele basi muonekano wa mtu utakuwa una nafasi ya kipekee sana, kwakua inaaminika namna unavyoonekana ndivyo heshima utakayoipata hivyo kila mtu ujitaidi kufanya sawa na uwezo wake alionao kuhakikisha anakuwa na muonekano unaovutia wako wanatumia fedha zao kununua madawa na mafuta aina mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wana kuwa na muonekano mzuri na  wako wanatumia mizizi ya miti au matunda mathalani palachichi na mangine mengi na wengi wanafanya hivi ili kuhakikisha kuwa wanakuwa na ngozi yenye afya inayo nawiri na kivutio kwa watu wote.

Jambo hili mwanzo lilikuwa likishamiri sana kwa wanawake sana lakini sasa kumekuwa na mwamko mkubwa kwa wanaume katika kutunza ngozi zao mithili ya mwanamke anavyotunza ngozi yake na yote hayo ni katika kuwa maridadi kutokana na hilo ziko sabuni zinazo amasishwa katika matumizi ili kutunza ngozi.

Ngozi inapokuwa haina mvuto hiyo inakuwa simanzi sana kwa mtu husika hasa kwa mwanamke… furaha ya ubora wa ngozi yake inakuwa haipo tena na wakati wote ujitaidi sana kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo, kutafuta habari zinazousiana na tatizo alilonalo, hali hii ni mbali na hali ya mtu kutaka kujichubua au kubadilisha ngozi yake.

Sas hivu si ajabu wa mtu anayejua jinsi ya kutunza ngozi yake kuwa na marafiki wengi na wote hao katika kufanikisha kila mtu katika  lengo lake kuwa ngozi yenye ubora iliyonawiri kwa ajili ya kumfanya kuwa kama mtu ambaye anamuona anamuonekano ulio mzuri.

Ili ni jambo jema sana lakini limekuwa ni moja ya janga katika jamii husika ndani ya jamii moja wamekuwa wenye kujua kutunza ngozi na wako ambao hajui jinsi ya kutunza ngozi ( hawajitambui) na watu kuachana na wapenzi wao kwakua wameshindwa kuwa tunza katika kuwafanya kuwa ngozi iliyo bora, hivyo pamekuwa na vikundi tofautitofauti kulingana na hadhi ya ngozi zao.

Imeiibuka kasumba mbaya kuwa mwenye ngozi nzuri basi huyo ana uwezo mzuri wa kiuchumi na yeye ambaye ana ngozi ilidhoofika basi uchumi wake wake ni wa chini japo hali hii si ya kweli lakini hali hii imepekea kuchukua maamuzi ambayo yataathiri maisha yako ya baadae mathalani kuingia kwenye tabia za wizi,uongo na mengine mengi.

Nami na kubaliana kabisa kuwa na ngozi yenye afya hiyo ni haki yako na kawaida ngozi nzuri ujengwa na vitu vingi moja wapo ni MOYO WENYE FURAHA, pamoja na kuridhika. Ni wazi pindi utakaposhindwa kuwa na moyo uliokunjuka hata ngozi yako inakuwa ina makunyazi ambayo yatapoteza ubora wa ngozi yako japo sio wote wenye ngozi nzuri mioyo yao imekunjuka ila kwa asilimia kubwa wale ambao mioyo imekunjamana basi ngozi zao ufabaa na mambo mengine kama vile changamoto za maisha uyatima, kukosa haki kushindwa kutimiza azma yako uliyoikusudia.

Japo umaridadi uficha umaskini niseme tu! MUONEKANO WAKISASA NI MATOKEO YA TEKNOLOJIA NA SIO MPANGO WA MUNGU, usikubali kuondoa utu kwa sababu ya muonekano na wala usiondoe utu kwa mtu kwa sababu ya muonekano…………Mungu angalii muonekano bali MOYO ULIOMBEBA YEYE.

Imeandaliwa na;
Cothey Nelson……………………………………0764 018535