Jumanne, 7 Novemba 2017

URAFIKI NA NENO





Urafiki ni jambo linalopendeza sana katika maisha ya wengi, kwani hutashangaa kusikia mtu akijivunia sana mwenzake! Ukimuuliza vizuri kwanini unampamba sana na kujivunia sana mtu huyu bila shaka ataongea kwa bashasha uku akijiamini na kwa furaha akisema “ huyu ni rafiki yangu sana, yaani ninapo muona huyu atakama naumwa nitapona ghafla” naam hakuna kitu kizuri kama kuwa na mtu ukatambua yeye ana upendo wa dhati na wewe, unajisikia uko salama zaidi ya pepo.

Kwakua unatambua ndani ya urafiki wa kweli kuna kusikilizwa, kusaidiana, kurekebishana, kutunziana siri, kuchukuliana na zaidi kunakuwa na kifo cha ubinafsi (umimi) ambao watu wengi upenda sana kwakuwa kila mtu ujiona si bora kuliko mwenzake.

Karibu!!!
Ni rahisi kuwa rafiki wa watu waliookoka kanisani (ukitaka) kuliko kuwa na urafiki na mwenye kanisa ( Mungu) kwa kuwa kila urafiki una utaratibu wake.

Na ni rahisi/inawezekana kufahamiana na watu wengi mahali ulipo ( kanisani, kazini (ofisini) na hata mtaani kwako ) kuliko kuwafanya watu hao kuwa marafiki.

Na ishara kubwa ya urafiki wako na mtu ni namna anavyo husika na wewe kuhakikisha unakuwa katika hali nzuri unayotakiwa kuwa nayo wakati wote maana furaha yake inakamilika anapoiona furaha yako.

Na unapojua una urafiki na mtu ujipangi sana katika kumwambia kitu kilicho ujaza moyo wako na hata rafiki yako atakapo kusiliza hatakuwa makini na kile utakacho mwambia tu bali ataweka mkazo zaidi katika urafiki wenu maana huo ndio utakuwa msukumo wake katika kukutendea.

Urafiki na neon karibu sana!
Inawezekana ukapata neema kulifahamu neno la Mungu ( kuwa kimeandikwa nini? Na kwanini) na hapo ukajua kuwa Mungu anaweza mambo mengi ( kuinua, kuponya, kufariji na mengine mengi) mathalani ukasoma sehemu ambayo bahari ya shamu iligawanyika kwa uweza wa Mungu kupitia fimbo ya musa  lakini hilo neno likikosa shirika nawe (lisibadilishe akili yako na kugeuza mfumo wa maisha yako) unaweza usijue maana yaw ewe kuelewa.

Na watu wengi walioishia katika hatua hii utoshangaa kuona ameacha wokovu au analegalega katika wokovu ( wokovu usio na matunda).

Unapoamua kuwa na urafiki na neno hii ni kitu kingine ni zaidi ya wengi wanavyozungumza au kuamini bali ni namna ya kiungu inayo jidhihirisha kwako.

Kama ilivyo katika urafiki mwingine unavyokuwa huru kumwambia chochote au kumwachia kuyafanya yale ambayo wewe ungeyafanya….. hivyo unapokuwa na urafiki na neno ni muhimu pawe na uwezekano wa wewe kuyafanya yale ambayo neno la Mungu lingeyafanya hapa duniani.

Utofauti wa utendaji utapelekea kushindwa kuimarisha urafiki wenu, na mfanano wenu katika utendaji utafanya urafiki wenu kuimarika na kuaminika zaidi.

hauhitaji kujitangaza hama kujisifia kama wewe una urafiki na neno kwakuwa neno lenyewe litakutambulisha na kujivunia wewe hatimaye kupata heshima mathalani mtu anaposhika mimba hauhitaji kutangaza mtaa mzima yenyewe itajionyesha na watajua tu kuwa huu sio ugali.

Ukweli wokovu bila urafiki na neno (mwingiliano usioelezeka) ni ngumu kuona mkono wa Mungu kwa ukamilifu.

Yohana 15:7  Ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa.

Moja ya mwingiliano usioweza kukatika ni huu, na kwa maelezo mafupi huu muunganiko ndio asili yetu kwahiyo kinachofanyika ni sisi tunarejea katika muunganiko na sio tunaanza muunganiko.

Kadili mwingiliano unavyokuwa au urafiki utakapozidi kuongezeka ndipo hapo utaomba naye atasikia na atajua hitaji lako au ombi lako hata kabla kinywa chako akija tamka na sio kupiga makelele hama maombi ya kubahatisha.

Faida kubwa ya mwingiliano huu (urafiki na neno) akili zako hazita tumika sana bali maongozi ya Roho mtakatifu yatakuwa dira yako.

Ni maisha yenye raha na furaha ya kweli maana ndio maisha tuliyo kusudiwa na Mungu.

Nzuri kuliko yote, huu muunganiko au mwingiliano hauna mwisho ( expire date) ni wa milele.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………….0764 018535