Jumanne, 23 Mei 2017

NGUVU YA UKIRI



NGUVU YA UKIRI


Tunapozungumzia ukiri hii ni zaidi ya kusema, pindi utakapo kuwa na furaha hama huzuni!
Unaweza ukaongea maneno mengi kwa misisimko najazba pamoja na maamuzi ya dhati yasiyo usisha moyo katika ufahamu ulio mkamilifu hapo hakuna NGUVU YA UKIRI

Ni muhimu kujua ukiri wako unaongoza maisha yako katika mema hama mabaya, muda mwingi mtu anapo kuwa katika hali ngumu katika maisha yake uwa moyo wa mtu huyu unazungumza mambo mengi wakati mwingine anaweza kujuta hama kujilaumu sana.

Yako mambo yanapotokea hasa katika upande hasi watu wengi uweza kujiapiza na kusema maneno mazito mathalani mtu uweza kusema katika maisha yangu sitakaa na kuzungumza nae kwa namna alivyo nitenda hakika sitakaa nisahau! Uwa maneno ya namna hii mara nyingi uambatana na hasira na wakati mwingine hasira zikisha poa uweza kubadilika hama kuendeleza na msimamo wako,

Sio kila ukiri una nguvu, bali ukiri unao maanisha ukibebwa na mizizi ya moyo na ufahamu kamili.
Nazungumzia ule ukiri unaoweza kukutenga wewe na furaha hama amani yako na hata kusababisha afya ya mtu kudhoofika, akili kudumaa na hata kusababisha mahusiano kufa na kupelekea mtu kuishi maisha ya upweke.

Moja ya njia ya kutambua ukiri wako ni badiliko la dhati katika mfumo wa maisha yako; unaweza kukuta pindi mtu atakapo kutana na mtu hama baadhi ya watu utakuta ana badilika kabisa, ata kama anataka kununua bidhaa yuko tayari aache pesa zote dukani kuliko kuonana na mtu huyo hama kundi hilo, dalili kubwa ya ukiri ni hali ya kutofanya yale uliyo yazoea kuyafanya.

Ni muhimu kutambu atupaswi kuchukua maamuzi au ukiri kutokana na tendo ulilofanyiwa ujapendezewa bali katika yote iruhusu AMANI YA KRISTO, ichukue nafasi katika maamuzi yako.
Uwa na amini kila maamuzi ya mtu yanayo ambatana na ukiri ulio na makusudi ya kuleta unafuu wa nafsi ya mtu na amani ya kufikirika lakini muda unapozidi kwenda ndio utatambua ukweli kuhusu maamuzi uliyo yachukua, na ikumbukwe kuwa baadhi ya maamuzi yanaenda na muda ukisha amua neema yakurekebisha inaweza isiwepo tena.

Ni muhimu kutambua kuwa kila ukiri unao ambatana  na maamuzi una matokeo yake unapoamua jambo uwe tayari gharama utakazo zibeba hivyo kila ukiri unaoufanya utoe muda mzuri wa kujiandaa kwa gharama za matokeo yake. 

Kila ukiri ujue una matokeo kwako na kwa mwingine hama jamii husika na matokeo mazuri hama mabaya utegemea na vyanzo vya maamuzi vilivyo pelekea ukiri, imekuwa ni rahisi sana mtu kudumu katika maamuzi ya ukiri yaliyo jengwa na maumivu,hasira na husuda kuliko maamuzi yanayo ambatana kujenga kesho yake mathalani maamuzi nakujiapiza kusema nitasoma neno la Mungu na kuliishi kwa uaminifu na kwa gharama yoyote.

Katika yote hakikisha ukiri wako unakuwa na FAIDA KWA MUNGU katika gharama yoyote haijarishi nafsi yako itakuwa na maumivu kiasi gani? MUNGU ATAKUPA RAHA.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………………..0764 018535

Jumanne, 16 Mei 2017

UKIMTUMIKIA ATAKUTUNZA

UKIMTUMIKIA ATAKUTUNZA


Yohana 15:2 Kila tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na kila tawi lizaalo hulisafisha, ili lizidi kuzaa.

Katika kitu ambacho Mungu ataona fahari juu yako ni KUMTUMIKA, maana gharama nyingi Mungu anaingia juu yako, yote ni kuhakikisha unakuwa huru katika kumtumikia yeye na zaidi sana unakua na kuongezeka katika utumishi wako juu yako.

Moja ya jambo la msingi sana unapoamu kuyatoa maisha yako ili kutumika kwa ajili ya Mungu tu yeye mwenyewe uku safisha hama kwa lugha rahisi ukufanya kuwa bora ili uzidi kutumika katika namna anavyotaka na ukupa neema yake kuhakikisha unatumika kwa furaha.

Katika jambo la kuzingatia pindi unapoamua kwa dhati katika utumishi wako mbele za Mungu tegemea kutunzwa na yeye tena kwa namna yake kwakua unapoamua kwa dhati kumtumikia nay eye ana amua kukustawisha katika njia zake.

Mathayo 6:26 Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao?

                    27 Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja?
                    28 Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti

                     29 nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo.

                    30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba?

                    31 Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini?

                    32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

                   33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.

Moja neema ambayo Mungu anahiachilia pindi unapo amua kumtumikia Mungu ni hali ya kutoishia njiani wala kuchoka hama kukata tamaa, bali siku zote Mungu ukupa nguvu mpya ili uzidi kuleta faida katika ufalme wake,

Japo nakubaliana kutumika mbele za Mungu sio kitu rahisi ndomana wapo wanafanya kazi ya Mungu katika mafanikio na wengine wakibwaga manyanga( kukimbia huduma) kutokana na sababu mbalimbali lakini bado atabaki kuwa Mungu na kuzidi kutumikiwa katika viwango vyake.

Kutumika ni jambo jema hasa unapotumika katika hali ya kupenda na utayari maana utalifanya katika ufanisi na uhodari mkubwa hilo kusudi ulilopewa! 

Niseme tu, tatizo sio kutumika tu bali namna unavyo tumika mbele za Mungu ina maana kubwa lazima ujiulize mapenzi yako kwake yanaongezeka hama yana pungua…maana ni muhimu unapotumika kwa Mungu uone deni likiongezeka siku zote kwa ajili yake tu,

Ili uweze kumtumikia Mungu katika namna anavyotaka uwezi kujitenga na KUMJUA MUNGU! Kwakua hapo ndipo  panazaliwa utofauti aliye imara na asiye imara…kwakua unapo wekeza katika KUMJUA MUNGU, ndipo hapo uweza kuwa imara na kuona Mungu akikutunza zaidi ya kuona makucha ya shetani.

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………….0764 018535

Jumanne, 9 Mei 2017

RAHA ISIYO NA MIPAKA



RAHA ISIYO NA MIPAKA



Naomba kuuliza hivi kunatofauti ya raha na furaha? Na furaha ndio inaleta raha hama raha ndio inaleta furaha? Karibu sana tutafakari pamoja!

Furaha na raha ni vitu muhimu sana katika maisha ya mwanadamu  kwa ujumla wake na hasa katika upande wa afya na hata kufanya ngozi yako kukunjuka na kunawiri a.k.a kuwa na mvuto,

Katika ulimwengu wa kila mtu utafuta kufanya jambo litakalo mpa raha na wala sio mzigo wala mateso katika mawazo yake, yanaweza kuwa kusoma, kufanya kazi hama kuoa au kuolewa na mengine mengi lakini ukweli katika kutimiza  lengo lako mwisho kunaweza kuwa raha hama majuto pamoja na hayo lakini bado maisha yanaendelea.

Wako watu wanajitahidi kulinda furaha zao, wako na wengine wanatafuta kuwa na furaha na wengine wamechagua kuishi maisha yasiyo na furaha zaidi ya kuridhika tu, na kuona ili mradi miaka inaenda basi hakuna  cha maana zaidi ya pumzi anayoitumia.

Niseme kuishi katika vita kali na bado ukawa raha ndani yako japo ina aminika mahali penye vita hapo hapana raha kwa sababu hakuna utulivu….Niseme tu panapo kuwa na vita sio wote wanakuwa hawana raha bali uko upande japokuwa unapambana unajua utashinda tu kutokana na uwezo mkubwa walionao dhidi ya adui yao,

Tatizo ya furaha hauwezi kununua japo kuna uwezekano kujifanya kuwa na furaha kana kwamba umeajiriwa katika kitengo cha mapokezi hivyo wakati wote inabidi uonyeshe tabasamu haijalishi unayo furaha hama hauna ili mradi mwisho wa mwezi paeleweke na zaidi sana ili kibarua kisiote nyasi.

Upaswi kuwa furaha kwakua uko kazini hama kwasababu ya kutunza afya yako bali kwasababu ulikusudiwa kuwa furaha na raha tangu ujatoka tumboni mwa mama yako na ulikusudiwa kuwa uishi maisha ya furaha kwa maana ni haki yako,

Mungu anatazamia uwe na furaha wakati wote haijalishi uko katika hali gani na maana Mungu ni zaidi ya baba kwa kuwa yeye anaijua kesho yako ambalo ni fumbo la wanadamu wengi,

Ili uwe na raha isiyo na mipaka kuna mambo ya kutambua;
i.uelewa sahihi kuhusu furaha
wako watu wana amini wasipo kuwa na furaha katika jambo linalo watatiza wana amini watakapo sikiliza muziki wa aina Fulani basi hapo furaha itarejea, wengine wana amini wakienda disko watachangamka, wengine wana amini wakienda beach watapata pumziko la akili na njia nyingine nyingi.

Ni muhimu kutambua lolote unalopitia si kigezo cha kuondoa furaha yako na tambua funguo ya kuruhusu huzuni ingie na raha iondoke iko katika himaya yako…
Ni kweli unaweza sema ni gumu lakini wewe si wa kwanza, lazima utambue kuwa kila jambo linakusudi lake lakini sio kuondoa furaha ndani yako.

ii.uwezesho Mungu katika kutunza furaha ndani yako
wataalamu (wanasaikolojia,washauri) wanapo shindwa kuona njia nyingine ya kukuwezesha kuwa na furaha ndipo hapo Mungu ujidhihirisha kuwa yeye yuko juu ya vyote na hakuna kinacho mshinda,

Ni muhimu kutambua mambo mengi yanayo tukabili wakati mwingine uonekana ni mazito lakini katika uwezesho wake furaha na raha itazidi kutawala mioyoni mwetu.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na: 

Cothey Nelson…………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 2 Mei 2017

UHURU WA NAFSI



UHURU WA NAFSI


Moja ya vitu ambavyo binadamu anavyo vipenda katika utendaji wake ni kuwa huru!
Kuna kipindi kinafika pindi mtu anapokosa uhuru wake uwa chakula, pesa na mali vinakosa maana kwake…anaweza kujiona kama asiye na hadhi yoyote kwa maana haoni maana ya kuwa navyo maana anakosa uhuru wa nafsi ambao ndio msingi mkubwa wa maisha yake.

Natambua kuna uhuru wa aina nyingi mathalani uhuru wa akili yako! Uhuru wa mwili wako! Tukiachia mbali uhuru wanchi, na huku tukiwa na tafsiri fupi kuhusu neno UHURU kwa maana hali kufanya mambo pasipo na kuingiliwa/ hama shinikizo lolote la nje bali lililobebwa na utashi wa mtu/nchi husika. 

Twende mbele na kurudi kama kuna vitu bora ukiachana na uhai basi uhuru wa nafsi ni kitu bora maana hapo ndipo unaweza kuanza kuyafurahia maisha binafsi, na kudumu kwa mambo mengi unayo yafanya utegemea sana nafsi ilivyo kuwa huru.

Japokuwa sio kitu rahisi kufanya jambo lilibebwa na uhuru wa nafsi wakati wote kwakua nafsi inaweza kukutuma kufanya jambo ambalo ni kinyume utaratibu uliozoeleka na jamii husika, sasa wewe kwa kuogopa hilo ukawa unaumia tu kwa ndani.

Usitegemee pindi utakapo amua kufanya jambo linalo tokana na uhuru wa nafsi  yako watu wote watalipenda hama kuliunga mkono tambua kila mtu ana nafsi yake na yuko huru kufanya yale anayo yaona kuwa ni sawa machoni pake hivyo nawe tia bidii katika yako ili mradi tu yamebeba nia njema.
Mtu anaye heshimu uhuru na nafsi yake uwa haogopi itakuwaje? Gharama zake ni kubwa kiasi gani? Bali uamini atafanikisha tu na upenda kufanya jambo lake kwa ubora wake na sio bora limefanyika tu.

Hakuna shaka maumivu yanakuwa katika maeneo mengi mathalani ndoa kwasababu mtu ameingia sio kwa uhuru wa nafsi yako bali kwa ushawishi wanje yaani marafiki hama vitu vinavyoonekana na mwisho migogoro na mateso yakawa ndio maisha.

Kuna maumivu makali pindi utakapo fanya jambo nje ya uhuru wa nafsi yako na kisha matokeo ya kawa mabaya zaidi na kukuacha na msongo wa mawazo usio na mwisho.

Ni muhimu kutambua kila mtu alikuja akiwa na utashi wa nafsi yake hivyo huna haja kuangalia nani atafurahi hama kuchukia tambua kuwa wewe ndio mwenye dhamana ya maisha yako kuyajenga hama kuyabomoa siku zote watu usubiria matunda yakionekana mazuri mbona watakuheshimu na pindi yasipo onekana hata uliwafurahisha kiasi gani bado watakusema tu na kukukebei.

Iboreshe nafsi yako kuwa yenye maamuzi ya maana kwa wewe KUMJUA MUNGU ili ikupeleke katika maamuzi yakayo jenga hatima yako na sio kuiharibu.

Maisha yanaanza kuwa na maana pindi nafsi yako inapoanza kutembea katika uhuru wake!

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………………..0764 018535