Ijumaa, 16 Februari 2024

UZURI WA HATUA MPYA:

 



Kwa mzazi mwenye mapenzi ya kweli kwa mwanae uwa anakuwa na furaha kubwa katika kila mabadiliko yanayofanyika katika ukuaji wa mwanae mathalani kutoka hatua ya kulala kuanza hatua ya kukaa….na moja ya hatua inayompa furaha mzazi kuona mwanae ameanza kupiga hatua au kutembea, kwani hapo anaweza kuwa msaidizi wa mahitaji madogo madogo kwake kama vile kumtuma akachukue kitu fulani ndani ya nyumba hadi dukani.

Naam hatua mpya ni shauku ya waliowengi kwa maana inaaminika katika hatua mpya kuna maongezeko, pia tunaweza sema kama uzuri wa kujifungua japo kuna maumivu lakini tunaita ni uzuri kwa sababu ya matokeo yake, kupakata mwana…………na heshima katika jamii inayokuzunguka.

Ni kama mlizi anavyoingojea asubuhi kwa hali ya shauku ndivyo ilivyo kwa mtu anayengojea hatua inayofuata kwa makamio yote.

Ni kama uzuri wa kutimiza ndoto yako ambayo ulikuwa unaitamani siku nyingi, inapotimia inageuza siku yako na kuwa hali nyingine iliyo njema.

Hatua ya juu au mpya ni kitu kinachofurahiwa na kupendwa na watu wengi kwa kuwa wanaamini katika hatua mpya uweza kuamini hadhi zao na mambo mengine uweza kubadilika.

Ni kama mwanamke anavyotamani kupakata mtoto na wakati akitambua kipindi cha kujifungua ni kuweka maisha yake rehani lakini inabidi akubaliane nayo kwasababu ndio hatua ambayo jamii inataka aelekee huko kwa maana inaaminika kuwa baada ya ndoa ni furaha kuongezeka.

Ni kama mkulima akiwa na shauku ya kuona mavuno na kuyafurahia na ikiwa anatambua kuwa kuamua kulima ni kuweka fedha yake rehani kwa kuwa inaweza kukata na kumwacha katika ndoto isiyokucha na kubaki kujuta bora asingeamua kupanda au kuingia kwenye kilimo.

Bila shaka hatua mpya ni jambo zuri linaloleta furaha kwa mtu mmoja na familia pamoja na ukoo kwa ujumla, kwakuwa wana amini kwamba kama mmoja akitoka katika kufanikiwa basi ukoo utakuwa na sehemu ya kupumulia au unafuu.

Niseme tu kwenda hatua mpya sio jambo la mchezo au la kawaida kuna hali unaweza pitia  hata usijue mara ya mwisho kulala usingizi ilikuwa lini maana inawezekana kipindi hicho kikasababisha hali ya kukosa utulivu wa akili na mwili kwa kiasi kikubwa.

Unapotaka kwenda hatua mpya ukaangalia mchakato wake usipokuwa na dhamira ya dhati unaweza kukuta umeghairisha kuingia katika hatua mpya na sio kwamba upendi hatua mpya bali ni ugumu wa mchakato unaonekana katika akili yako.

“ petro alipoamua kutembea juu ya maji alipoangalia mawimbi shaka ikaingia ndani yake na hatimaye akaanza kuzama……….”

Mathayo 14:26 Wanafunzi walipomwona akienda juu ya bahari, wakafadhaika, wakisema, Ni kivuli; wakapiga yowe kwa hofu.

 27 Mara Yesu alinena, akawaambia, Jipeni moyo ni mimi; msiogope.

 28 Petro akamjibu, akasema, Bwana, ikiwa ni wewe, niamuru nije kwako juu ya maji.

 29 Akasema, Njoo. Petro akashuka chomboni, akaenda kwa miguu juu ya maji, ili kumwendea Yesu.

 30 Lakini alipouona upepo, akaogopa; akaanza kuzama, akapiga yowe, akisema, Bwana, niokoe.

 31 Mara Yesu akanyosha mkono wake, akamshika, akamwambia, Ewe mwenye imani haba, mbona uliona shaka?

Hatua mpya unaweza kuifananisha na ng’ambo iliyojaa mema kwa ajili yako lakini kuna mto inabidi uogelee ili ufike ng’ambo na ndani kuna mamba wa kali lakini kwa namna yoyote inabdi upite katikati ya hao wanyama ili uyafikie yale mema yako yaliyo ng’ambo.

Akili ya mkulima uwa naipenda kwasbabu uwa inaangalia matokeo kabla ya kuangalia mchakato utakao sababisha matokeo hali hiyo inafanya kuukabili mchakato wote katika hali zote ugumu na kujinyima ili mradi apate matokeo anayo yataka au yale aliyokuwa anayawaza na ikiwezekana hata zaidi ya yale aliyokuwa anayawaza.

Hauwezi kupata mavuno kama ujafuata mchakato mzima wa kukupelekea hayo mavuno, kama haupendi mchakato wake basi hauko tayari kupata mavuno, ni sawa sawa mwanafunzi anataka kupenda daraja la juu huku hayuko tayari kulipa gharama ya kusoma kwa bidii.

Ni shauku ya Mungu tuingie katika hatua mpya sio hatua ileile kwa kuwa unapodumu katika hatua ya awali kwa muda mwingi kuna baadhi ya mambo hutaweza kuyapata mpaka uingie katika hatua nyingine, kila hatua ina utukufu wake hivyo ili upate utukufu mwingine basi hakikisha unaingia katika hatua nyingine.

Isaiah 1:19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi;

Hatua mpya unaingia kwa kuikubali na kuitii sauti ya Mungu, pindi utakapo amua kuishi sawasawa na sauti yake pasipo kuangalia nini kinaendelea nawe au gharama utajikuta upo katika hatua nyingine wenye utukufu wake.

“ kama ukuweza kunizuiliwa mwanao……………..basi sasa kukubariki nitakubariki”

Mwanzo 22:16 akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema Bwana, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,

 17 katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki mlango wa adui zao;

 

INAITWA SIKU! BARIKIWA SANA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………………………..0764 018535