Jumanne, 26 Septemba 2017

JASHO LA MAAMUZI.






Ubora hama uzuri wa maamuzi haupo kwenye kusema “ sasa nimeamua” la hasha! bali ni namna unavyoenenda baada ya maamuzi ni jambo la msingi kwani yanayoweza kukupa raha hama majuto!

Inawezekana ikawa rahisi kuamua maamuzi fulani katika maisha yako kwa lengo zuri tu la kuleta raha katika moyo wako lakini jasho linaweza kukutoka pindi utakapoanza kuyaishi hayo maamuzi…… Na inasemekana maisha ya mwanadamu yamebebwa na maamuzi na maisha yake yanadhihirisha maamuzi aliyo yachagua, na ikatokea mtu akasema mimi sina maamuzi katika hili kwa maana hali ya kutofanya jambo, basi hayo nayo ni maamuzi japo mtu anaweza asijue kwa yeye kuamua kuishi mtindo fulani katika maisha yake nayo ni maamuzi na hata wakati mwingine anaweza asijue.

Japo katika dunia ya sasa unaweza usishangae kuona mtu ndani ya siku amekuwa na mawazo mengi yanayoweza kupelekea maamuzi mathalani mtu aliyekuumiza au kukuuzi unaweza kuwaza mengi kama vile sijui ni mchunie tu! Au nimpe dozi! Hama nimpige mkwala/biti zito, au ni mwaribie katika mambo yake au nimfanyie kitu ambacho hata kaa akisahau ( kiweke alama katika maisha yake) na mengine mengi yako mengi mawazo yanayo sukuma kuchukua maamuzi na sababu zake.

Ukitaka kuona usumbufu wa moyo wa mtu wa hali ya juu, ni pale jambo linalo mkabili likakosa majibu katika akili likazaa teso la moyo usumbufu wake unaweza kuwa mkubwa zaidi ya uchungu wa mjamzito maana hapo panakuwa apakaliki, apaliki, mate hayamezeki, hofu + msongo wa mawazo( stress) inakuwa ni maisha yako yasiyo rasmi.

Wakati mwingine katika maamuzi uliyoyafanya nyuma unaweza kuona gharama hama kujigharimu kwingi kutokana  na maamuzi uliyoyafanya awali japo yako maamuzi ukisha chukua hatua ni ngumu kuyabadili bali yanaweza kukupelekea maisha yaliyo kosa furaha.

Ina aminika kuwa maamuzi yenye kukugharimu sana basi hayo ndio yenye faida katika maisha yako ndo maana watu usema “ No pain No gain” huu msemo utakuwa na maana sana kama tu umepata kitu ulicho sumbukia hama kukigharamia.

Kuna baadhi ya watu safari inapoanza kuwa ngumu uweza kusema “ Laiti ningelijua kesho”  kwa maana rahisi jambo hili limekuwa tofauti na vile alivyofikiria hama kuamini hivyo jasho jembamba linapoanza kumtoka na kutamani dunia ibadili majira yake labda utapata ahueni.

Unaweza kukuta mtu ameamua kuwa peke yake muda mwingi au muda mwingi anaangalia video au simu na wengine ujitahidi kufanya mambo yatakayo leta furaha hama kuchangamsha moyo wake na yote anafanya sio hobby au fun bali ni kujaribu kupunguza ugumu na uzito unao mkabili kutokana na maamuzi uliyoyafanya.

Ni bora uchukue muda kusema Ndiyo au Hapana kuliko kuyatamka haya maneno pasipo kuwa tayari kubeba gharama zinazotokana na maneno hayo, jiandae vizuri akili, hisia na mtazamo wako katika jambo lolote unaloliendea.

Muhimu kutambua mafanikio na kutofanikiwa kwa jambo unalolikabili linakutegemea wewe sio mtu mwingine ( sio rafiki, ndugu, mzazi), hivyo matokeo yoyote yatakayo kukabili wewe ndio mwajibikaji pekee.

Jasho linalotokana na maamuzi ni jambo jema kwani ni ishara kubwa kuwa maamuzi umedhamiria sio ya kukulupuka!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………0764 018535

Jumanne, 12 Septemba 2017

NGUVU YA UELEWA




Kwa kiasi kikubwa udhihirisho wa uelewa wa mtu uone katika utendaji………unaweza kukuta huyu ana dhira na mwingine anaendelea, huyu anajinyonga na mwingine anakula chakula, huyu anachukia na mwingine anatabasamu, huyu kavurugwa na huyu anafanya mazoezi katika kuimarisha afya yake, huyu amesusa kula na mwingine anakunywa juice kwa raha zake…….na mengine mengi yanayotokea katika ulimwengu wa sasa!

Na inawezakana kuwa jambo ni moja lililowatokea watu wawili, familia na hata kundi la watu lakini namna yakuchukulia ni tofauti hasa inategemea na UELEWA WA MTU HUSIKA inawezekana familia moja ikatokea wapo waliofanya vizuri katika elimu na wengine awakuweza kufanya vizuri, ikatokea yule miongoni aliyefanya vibaya akaanza kujisikia vibaya na kuona kuwa tumaini alipo tena, asipo pata upendo kwa wenzake usishangae akawa chizi hama kujinyonga.

Pia inaweza kutokea kwa mama ( mwanamke) aliyefiwa na mme wake, na mara baada ya msiba kuisha ndugu wa marehemu mume wake wakaja na kuchukua na kumtoa katika nyumba ya marehemu mume wake yeye na watoto wake, uwezi kushangaa kumkuta huyu mwanamke anaweza kuwa mnyonge na kwenda kuishi katika maisha ambayo akupaswa kuyaishi lakini kwa mwanamke mwenye UELEWA hana hofu ahitaji kutiwa moyo bali anajua hatua gani za kufuata na hatimaye kupata haki yake.

Yako matukio mengi yanayo mtokea mtu kwa namna yake yote yanawezekana kutatulika hama kushindikana yanategemea uelewa sahihi juu ya jambo alilonalo, unaweza kukuta mtu wakati mwingi anafuraha tu ukafikiri katika maisha yake hakuna vikwazo vinavyo mkabili ukweli vikwazo vipo ili mradi unaishi lakini uwekezaji wake maarifa anapata ufumbuzi wa kila jambo analokumbana nalo na baada ya kushinda amani yake inaongezeka.

Usalama wa moyo wako utegemea sana uwezo wa uelewa wako yaani mapana na marefu ya uelewa wako, kumbuka uelewa mdogo ndio wingi wa mateso yako kwahiyo kutafuta kuelewa mambo kwa mapana yake ni kujiongezea usalama binafsi na kurahisisha utekelezaji wa utaratibu wa maisha yako.
Moja ya kiashiria kuwa unajipenda ni kutafuta amani na usalama na njia sahihi ni kutafuta uelewa utakao sukuma ndoto yako na kuanza kuchanua siku baada ya siku……kwa hiyo ukiona mtu anatafuta kuelewa mambo ya msingi basi ujue anajipenda! 

Na nzuri zaidi usipojipenda ni ngumu watu wengine wa kukupenda zaidi ya kukuonea huruma tu, ongeza uelewa ili uongeze ushindi katika maisha yako.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………………………….0764 018535