Ijumaa, 27 Aprili 2018

MUNGU HAONGWI




Moja ya kitu kinachoweza kukuonyesha kuwa wewe ni wakisasa ni uwezo mkubwa wa kupata fursa pasipo kujali hizo fursa unazipataje? ( unatoa rushwa au hautoi ).

Imekuwa ni mtindo wa kisasa na kukubalika kwa haraka kama sio kwa wepesi katika jamii kwa kundi la watu fulani, vitu vingi ili uvipate utahitaji lazima ulainishe viwe rahisi kuvipata au kuvimeza, ndomana kukaibuka na misemo mingi iliyo na maana iliyo wazi au imejificha kama vile, ili ule lazima nawe uliwe, mtaka cha uvunguni sharti ainame, ukitaka……………..penyeza rupia, ukipenda boga  penda na ua lake na misemo mingi yote ni katika kujirahisishia ili mambo yako yaende.

Imekuwa ni kawaida kana kwamba ni mafuta kwenye gari kwakuwa gari aliwezi kwenda pasipo mafuta ndivyo imekuwa bila ya kuongwa au kuonga maisha hayaendi sawa, hivyo ndomana mtu akitaka kitu/mtu ( msichana au mvulana ) lazima aonge kama njia ya rahisi ya kupata uhitaji wake sio hilo tu hata mtu akitaka kazi anaweza kuweka uwezekano wa kutoa ongo na hii imeenda mbali kidogo hata unapotaka ( haki yako ) utoshangaa mtu akitoa ongo au kudai/akitaka ongo.

Imekuwa kwenye akili ya watu kiasi kwamba mtu akipata huduma/ kitu pasipo kutoa ongo uweza kupata wasiwasi na kujiuliza hii hali/jambo linawezekana vipi? Kwa hiyo anapotoa hivyo uweza kujisikia vizuri na kupata uhakika zaidi kuwa hicho kitu atakipata au ni chake.

Hali hii imetawala na kuzidi mpaka inatisha na kuonekana ni kitu cha kawaida na kufanya rangi nyeusi kuonekana nyeupe, kitu ambacho si halali sasa kimehalalishwa.

Naam hali hii imefunika macho ya watu mpaka kuona mtindo huu unaweza kutumiwa hata kwa Mungu.
Pindi mtu anapokuwa na shida au uhitaji unaenda na kitu kwa Mungu, ukitazamia jicho la Mungu likuone huruma na kunyosha mambo yako na hivyo hali hii imepelekea hata watumishi kushawishiwa na kuona njia rahisi ya kuwapata watu na fedha ni kubuni utaratibu fulani kwa kuwatoza hela kwa kila tatizo na ukubwa wa tatizo ndio wingi wa hela na kushawishi hata kusema ili utoke kwenye shida/tabu yako ni lazima utoe kitu.

Sauli “ bwana upendezwa na dhabiu kuliko kuitii sauti ya bwana”

I samweli 15:22 Naye Samweli akasema, je! Bwana huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu Sawasawa na kuitii sauti ya Bwana? Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu, Na kusikia kuliko mafuta ya beberu.

Ni muhimu kutambua sio utaratibu wa Mungu kuwa lazima utoe pesa ili upokee bali anataka maisha yako kwa ujumla umpe yeye…………………..japo na kubaliana kabisa Roho mt. anaweza kukugusa utoe kitu ili uweze kutoka katika shida/maangamizi yako.

Hii hali ya kutoa ili upokee pasipo kujua unapokea unatakiwa kupokea nini? Hali hii ni hatari sana katika maisha yako na Mungu, kwa maana usipoiona au kupata vile ulivyotegemea kuacha wokovu ni jambo linaloweza kutokea wakati wowote.

Ni muhimu uhitaji wako kwa Mungu ujengwe katika PENZI ( itokee au isitokee ) isikupe shida ili mradi penzi lipo usiwe na hofu ustawi utakuwepo tu.

Usipende sana kuwa makini katika kuona uhitaji wako unatatuliwa bali elekeza umakini wako katika penzi lenu linakuwa siku kwa siku.

Ndani ya penzi kuna kukidhi mahitaji yenu pasipo msukumo wa nje yenu ( kila mmoja uwajibika kwa ajili ya mwenzake ) wala hakuna kutegemeana/ kutegeana.

Kunatofauti kubwa kati ya kuomba kukidhi uhitaji wako ukiwa ndani ya penzi na inje ya penzi.

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson……………………………………………….. 0764 018535

Ijumaa, 13 Aprili 2018

UJANA WANGU UNAPOTEA!





Neno kupotea au kupoteza limekuwa na picha tofauti tofauti katika vichwa vya watu: wako watu baada ya kupoteza wamekuwa na furaha sana na wengine wamekuwa na huzuni sana ikitegemea nini ulichopoteza na umuhimu wa hicho kitu kilichopotea,

Mathalani kama ulikuwa na kitu ambacho kilikuwa ni teso kwako kinapoondoka/ kupotea furaha inachukua nafasi lakini kama jambo ulilokuwa unalipenda na kulitegemea hama kulitarajia kuwa bora zaidi katika majira yajayo alafu likaondoka bila shaka huzuni na mateso yata tawala kwako.

***************************************************************************
Lakini tunapozungumzia UJANA WANGU UNAPOTEA! Hii hali imebeba sura moja tu kwa mtu mwenye akili timamu, hile namna ya utendaji / muonekano kama kijana unakosa nguvu ( inakuwa haipo ).

Unapokuwa kijana unakuwa na hali iliyojaa uhuru binafsi katika mwenendo unaopelekea kuupoteza ujana wako au kuufanya kuwa wa kuheshimika au kutamanika.

Ni muhimu kutambua, hakuna mtu anaweza kuupoteza ujana wako ila wewe binafsi, na unaweza kuupoteza ujana wako kwa kujua hama kutokujua.

Ujana ni hatua ya msingi sana katika maisha ya mwanadamu hivyo unapofanikiwa kuitendea haki itapelekea hatua bora katika maisha yako.

Na ikumbukwe kwamba ukishindwa kuyafanya mambo unayopaswa kuyafanya unapokuwa kijana jua ni ngumu kuyafanya katika hatua nyingine katika maisha yako kwakua kila hatua ina mambo yake.

Kwa hiyo kama kitu cha kuwa makini sana hama cha kuzingatia basi hakikisha ujana wako haupotei kwa gharama yoyote.

Wako watu wanajilaumu katika maisha yao kwakuwa walipewa ushauri  na watu walio wazidi umri katika kipindi chao cha ujana lakini walikosa kuzingatia na hatimaye yakawa kuta mambo ambayo hawakutegemea yawakute.

Sio kila kitu ambacho unaona watu wengi wanafanya hasa katika rika la ujana basi nawe ufanye ili mradi tu usionekane uko nyuma ya wakati.

Kuna mambo ya ujana ambayo ukiyafanya yataziba fulsa zako za mbele hata kama mwanzoni wakati unafanya hilo jambo wenzako walikuwa wanakushangilia.

Pia kuna mambo ukiyafanya yanaweza kukupelekea kushindwa kufanya mambo mengine mathalani unapokuwa na mtoto katika njia isiyo halali kwa Mungu, tayari unakuwa na wajibu juu ya mtoto na tayari kuanza kuwajibika kwa huyo mtoto kiakili, kimwili ( nguvu ) na hata uchumi wako na hata kama ulikuwa na mpango mzuri kiasi gani utategemea kwanza ustawi wa mtoto wako.

Kila jambo lipo tu ili mradi unaishi kwa wakati wake utapata.

TUNZA UJANA WAKO UFAIDI MATUNDA YAKE!

INAITWA SIKU! BARIKIWA

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………………….. 0764 018535