Jumanne, 23 Februari 2016

NGUVU ILIYOPO KATIKA UTULIVU



NGUVU ILIYOPO KATIKA UTULIVU


Wepesi wa macho sio uzito wa mizizi!

Usione mti umetulia tu ukadhani ni rahisi nitauangusha! Usipokuwa makini unaweza kuchukua miaka mingi pasipo kupata jibu…….na kubaki na swali pasipo muafaka kuwa mti huu hivi utaanguka lini?

Iko misemo mingi mizuri na ya kushawishi masikio ya watu na kivutio cha macho ya watu na kuna wakati mwingine misemo/methali hizo zinakuwa na uhalisia katika jamii yetu mathalani harakaharaka haina Baraka, polepole ndio mwendo, mvumilivu ula mbivu na nyingine nyingi na zote ziki husisha  hali sahihi katika kuamua maamuzi yoyote na nyingi zikilandana na methali hii fikiri kabla ya kutenda bado ikilalia sehemu inayoitwa tatua jambo katika njia muafaka na sio kwa kukulupuka.

Ndomana maamuzi ya vijana wengi hayathaminiki kama ya wazee kwani haya maamuzi yana aminika kuwa ndani yake hakuna umakini kama ya wazee na pia yana amini kuwa hayajakomaa au hoja zao hazina shibe/mshiko kwa kiufupi hoja zao hazina uhalisia katika maisha wanaoishi na moja ya sifa kubwa ambayo inaaminiwa sana na maamuzi ya wazee ni kuwa na hekima yanaangalia mbali sana, japo pamoja na hayo kunaweza kuwa na kasoro katika upande wa mawazo ua wazee mathalani yakawa ni mawazo yasioendana na mabadiliko ya sasa( mawazo mgando) bila shaka iliutambue hili unahitaji mawazo mapana yaani mawazo yenye utafiti wa uhakika.

Japo kuna mazingira mengine maamuzi ya haraka yanahitajika na hasa katika jambo la haraka linalohitajika utatuzi wa haraka mathali katika vita bila shaka hapo maamuzi ya haraka na yenye akili yanahitajika sana ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuweza kuwa salama na hata kuleta ushindi kwani utambue kuwa makosa yako ndio fursa ya mwenzako!

Na kubaliana kabisa kuwa unaweza kuwa katika hali ya utulivu lakini bado unaweza usiamue jambo la maana kutokana na sababu mbalimbali migandamizo ya mawazo(stress), mshauri wako, nguvu za hisia zako na hasa pindi unaposhindwa  kuzitawala.

Pamoja na hayo nipende kusema kuwa maamuzi sahihi na yenye utendaji wa nguvu kubwa pamoja na kishindo yanayoweza kuleta mabadiliko makubwa ya ajabu sana kusababisha mafanikio makubwa katika maisha yako!

Mwanzo 1:2 Nayo nchi ilikuwa ukiwa, tena utupu, na giza lilikuwa juu ya uso wa vilindi    vya maji; Roho ya Mungu ikatulia juu ya uso wa maji.

                 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.

Tunaona katika utulivu wa Roho ya Mungu ndio ilikuwa ni hatua ya kwanza ya Mungu kabla ya uumbaji wa kitu chochote japo dunia haikuwa na sura nzuri wala muonekano usio faa, lakini katika utulivu ndani yake ilikuwako nguvu ya kuleta mageuza ambayo ndio imefanya sisi wanadamu tuweze kukaa na kuona fahari ya dunia tuliyonayo.

Tunaona Mungu anatumia siri kuu katika utulivu kufanya mambo makuu atuoni Mungu akiamua tu jambo kwa sababu lipo tu na anaweza kuliamua tu maadamu anayo nafasi na uwezo huo bali alitulia katika hali ya kujua mwisho kabla ya mwanzo na katika hilo tunaona Mungu kushindwa hakutajwi kwake…………….ndomana mwisho tunaona akisema 

Mwanzo 1:31 Mungu akaona kila kitu alichokifanya, na tazama, ni chema sana………

Ukweli Mungu anatufundisha siri kubwa hapa na inadhihirika katika hali ya ushindi wake katika kila alichokifanya!

Kiubinadamu hali hii inakuwa ngumu sana unaweza ona mtu kuwa ni mtulivu sana katika muonekano wan je lakini ukweli ndani anafurukuta moto unaotaka kulipuka kwa hiyo muda wowote unaweza kulipuka ni sawa sawa na dumu la petro kupita  mahali ambapo moto unaweka na dumu  likiwa wazi.

Katika mambo yote ningependa kusema utulivu uliobeba akili ya kutosha na dhamira njema ni jambo muhimu sana katika maisha yako kama mkristo inawezekana watu wakakuona unachelewa sana, niseme ni bora wakuone unachelewa sana kuliko uwai badala ya kutengeneza ukajikuta unaharibu.
Nikubaliane kusema ukweli hasira wakati mwingi isipoongozwa na akili iliyo sahihi mwisho wake ni uharibifu au mtokeo yake yakawa chini ya kiwango au hali inayotakiwa.

Niseme utulivu wa kibinadamu hauna matokeo mazuri kwani ni kweli unaweza ukatoa maamuzi ya kuangalia kesho lakini uhakika wa hiyo kesho kuwa sawa na unavyosema au anavyoamini lakini uko utulivu wa kimbingu ambao ukiiwaza kesho kamwe haiwezi kuwa tofauti na vile alivyowaza kwani yeye anaitwa jana leo kesho hata milele na neno lake hakuna kinachoweza kutengua.

Isaya 55:10 Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;
             11 ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma

Anavyosema ndivyo inavyokuwa na sio kitu kingine!

Umaana wako mbele za Mungu unaanza pale utakapoamua kumbeba Mungu!

Imeandaliwa na: 

Cothey Nelson…………………………………………….0764 018535

BARIKIWA!

Jumanne, 16 Februari 2016

UNAPENDA NINI KWA MTU?



UNAPENDA NINI KWA MTU?


Kupenda kwa jina rahisi nimelipa kuwa ni kifungo huru kwa maana hakuna mtu anakuja kukulazimisha kuwa sasa unahitaji kuingia huku, bali inakuwa ni kwa utashi wako na akili zako timamu pamoja na msukumo mkali wa hisia zako bila kusahau ikisaidiwa na ndoto zako katika maisha yako.

Japo siku hizi kiukweli ni ngumu kutofautisha kiukweli yupi anakupenda kweli au upendo wake sio wa kweli na kuna wakati mwingine unaweza fikiri kirahisi kuwa huyu mtu kwa namna anavyonitendea naona hapa kuna upendo wa kweli lakini muda si mfupi unaweza kubadilisha maneno yako kwa kuona tofauti na akili yako ilivyoamini mwanzo nakuona kama uko ndotoni au katika mawazo yalikuamisha kuwa ndio huyu kweli au mwingine kwa namna alivyobadilika hasa katika utendaji wake uliouona mwanzo na wa sasa unao ushuhudia.

Katika hali ya kawaida tunaposema KUPENDA tunasema ni haki ya  tu na sio wajibu wa mtu hivyo unahiari ndani yake kuwa naweza kupenda au nisipende kwani hakuna mahakama au jela utapelekwa kwakua wewe umekiuka kifungu cha kupenda kanakwamba ni wajibu na wewe ukuutekeleza zaidi sana utaweza kujikita na kuamini kuwa hili ni jambo la ubinafsi wa mtu! Na sio swala la kushurutishwa.

Tukiingia katika uwanja wa kupenda kuna vitu na viona hapo kupenda kunaweza kuzaliwa kutokana na muonekano wa ndani au muonekano wan je, na muonekano wan je ni rahisi tu kuona lakini muonekano wa ndani ni ngumu kuona kwa haraka haraka.

Ni maswali ndani yangu? 

►aina kazi uliyonayo ndio ina amua aina ya mwenzi kuwa naye?

►muonekano ulionao ndio unaweza kuamua aina ya mwenzi kuwa nae?

►kipato ulichonacho ndicho kina amua aina ya mwenzi kuwa naye?

►ni kweli mwenzi mzuri utoka katika familia yenye maadili mazuri?

►na nikipimo gani unachotumia kugundu mtu huyu ametoka katika familia yenye maadili bora?

►ni kweli umri ni kigenzo au ni kikwanzo katika mausiano katika ndoa?

►je! Ni kweli muonekano wa mtu uweza kusadifu tabia ya mtu?

Haya ni baadhi ya maswali yaliyo ndani katika kichwa changu ni kijaribu kutafuta kwa umakini uhalisia wa hali hii ni kweli iko hivyo na usawa wa mambo haya na ubora wake.

Basi tukirudi katika mada yetu kuwa UNAPENDA NINI KWA MTU najua wewe sio chizi wa kupendapenda hovyohovyo hata kama umechelewa kuwa na mwenzi na pia hata chizi naye anachagua sio kila mtu uweza kumtupia takataka bali kwa wale atakao wachagua.

Ningependa kuongelea muonekano wa ndani?
Hali hii unaweza kumtambua mtu katika kuongea na mwitikio katika katika changamoto anazozikabili, wako wengi uweza kuvutiwa namna  mtu anavyokuwa kimya anaposemwa vibaya basi hali hiyo uweza kupelekea kuwa ikitokea mtu huyu akiwa mwenzi wangu basi bila shaka atanisikiliza mahitaji yangu na kunifanyia sawa ninavyopenda na hatimae tutaishi maisha ya raha mstarehe na hapo ikawa chanzo cha mausiano.

Napia ninapoongelea muonekano wa ndani wa ndani uwa naongelea rutuba ambayo mtu aliyonayo ndani yake ambayo pindi inapotoka inaweza kuwa ustawi wa watu wengi na wengi waka mea kutokana na rutuba toka kwa mtu.

Ni kweli hali ya ndani ya mtu imekuwa kivutio kwa wengi pasipo kujua ili uweze kumjua mtu vizuri unahitaji kuchukua muda katika kuishi nae ukaona kwa undani tabia kujua hii ndio halisi au sio halisi watu wengine wamekuwa wakigundua baada ya kufanya maamuzi tayari na kujikuta kuingia katika shimo lisiloweza  toa uwezekana  wa kutoka inategemea na imani yako.

Si katai mtu kuvutiwa kwa mtu katika hali mbalimbali mathalani mcheshi, mkarimu, mwenye upendo, mwenye huruma na hata busara ningependa kusema kuwa binadamu kama huyo wako wengi japo kiukweli natambua kuwa hakuna mfanano wowote wa utendaji wao.

Kwa dunia ya sasa muonekano wa ndani ushawishi wake ni mkubwa lakini ukweli unaweza kuwa sio sahihi kwani mtu anaweza kuficha makucha kwa muda lakini mwisho akayachia baada ya kuishi kama mke na mme.maumivu yake uyasikiage kwa mwingine kwani yakikuta utaona afadhali moto wa jehanamu japo ujawai kuona wala kuhuhisi kuliko kuishi na mtu aliyachia makucha mara tu baada ya kuingia ndani.

Niseme ulimwengu wa wapendao ni ulimwengu unaobadilika kwa kasi kubwa lakini ushindi wako unategemea uwezo wa nguvu uelewa wa mambo hayo na ungamaniko la kweli kati yako na Mungu.

Ushauri wangu kwako..USIMPENDE MTU ZAIDI YA KUYAPENDA MAONGOZI YA MUNGU!

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson…………………………………………..0764 018535

Jumanne, 9 Februari 2016

USIISUMBIKIE KESHO



USIISUMBIKIE KESHO

 Kila mtu utamani sana kuwa na kesho,na sio bora kesho tu bali kesho nzuri yenye ushawishi na mvuto kwa wengine na iliyobeba maswali yake ya leo mathalani kuwa na nyumba, maisha yenye furaha na mwenzi sahihi na mengine mengi….. kwa hakika ni kitu kizuri kwa mtu yeyote mwenye akili njema sana ni lazima awaze mambo kama haya kwakua ndiko huko anakoelekea ……….na unaweza kuwa katika hali njema sasa kwa maana mke mwema, watoto wazuri nyumba nzuri na bila shaka na usafiri wa maana lakini bado utahitaji kuona kesho yako ikiwa njema sana kuliko leo, naamini bado utamani kuona ustawi watoto wako katika elimu, mali na kuishi maisha ambayo yatampendeza Mungu kulingana na imani yako na matarajio yako binafsi kwa kusema hivyo ni seme kesho inatofautiana kulingana na leo yako uko katika hatua ipi?.

Sio ajabu kuona watu wakichukua maamuzi ya kuhatarisha maisha mara baada ya kuona mwanga hafifu au giza katika kesho yao unaweza kukuta mtu anaingia katika shughuli ambazo zita hatarisha maisha yake na hata kupelekea ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha yake lakini dhamira yake ni kuilinda kesho yake au kuifanya kesho iliyo na manufaa kwake,

Ukitaka kumtambua mtu katika upande mwingine basi ukute mtu anaona njia iliyo bora katika kufikia kesho yake lakini wewe ukasimama na kuwa kizuizi katika njia yake, hapo utaweza kuona namna mtu huyu anavyoweza kuziruhusu hisia zake kuchukua nafasi katika utendaji wake na hatimae akachukua nafasi hata ya kukudhuru katika sehemu kubwa katika maisha yako

Ninapozungumzia kuwa usisumbukie keshi uwa sina maana kuwa usifanye kazi au  uridhike tu au uridhike katika hatua ya maisha uliyofikia ila nazungumzia usijaribu kuilazimisha kesho yako kuwa kama unavyotaka bali iache kesho ijitengeneze kisha nawe uingie kuikabili

Mathayo 6:30 Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba

Mungu apingani na wewe kujishughulisha katika maisha yako bali inakuwa katika mazingira magumu pindi pale mtu anaanza kuona umuhimu wa kesho yake hata kuliko Mungu, na anakuwa yuko tayari kufanya chochote ili mradi asikose kitu ambacho anakiwaza kuwa ni cha maana katika kesho yake pasipo kujua uweza Mungu unaweza ukamtosheleza na kumpa ustawi ulio bora kuliko kile ambacho anacho fikiria.

Wako watu walioacha imani zao kwa kuona kesho inaingiliwa na mwingine mathalani mtu alikuwa na mchumba wake na baadae wakaachana na kisha akamuona na mtu mwingine basi hapo uweza kuzaliwa kisirani kisicho koma na bila shaka furaha yake inakuwa ni maumivu ya mwenzake, wako watu wanachukua maamuzi na kusahau kuwa wameokoka na maisha mtu aliyeokoka anatakiwa aishi vipi badala yake anakumbuka baada ya kutimiza hazma yake inawezekana katika kumdhulu au jambo lingine.

Watu wengi wamekuwa wakihama makanisa kwa kuona hapa kesho yangu imeingiliwa na mtu mwingine mathalani alikuwa anajiona kuwa anastahili kuwa na nafasi fulani kanisani lakini akaona ile nafasi imechukuliwa na mtu mwingine na hivyo kuona hapo kuna hujuma imefanyika basi na kuona hakuna la maana sana hapa na ukaanza kuona kama vile thamani yake imekwisha potea na kuona bora aende mbali ajiondoe na aibu au kuona kama umeshuka kiroho kwa wewe kukosa nafasi hiyo.

Mathayo 6:34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake

Ni jambo la kawaida sana pindi utakapoanza kuipigania kesho kwa nguvu na kujitahidi sana bila shaka uovu utaanza kukunyemelea na kutaka kukumeza kwa ndipo hapo shetani uweza kukupa akili nyingine ya haraka katika kufanikisha lile kusudi lililo ndani ya moyo wako, atakupa akili yake kama aliyo mpa eva pale bustanini

Mwanzo 3:1Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana    Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?
2 Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula;
3 lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse, msije mkafa.
4 Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa,

►Yalikuwa maneno machache lakini yaliweza kuupindua ufahamu wa eva na atimae kuangukia sehemu isiyo salama katika maisha yake!

Ukikaa katika nafasi yako ambayo Mungu amekuweka kesho sio swala la kukunyima raha bali ni swala la kufurahia na kuamini kuwa itakuwa tu kwakua Mungu atakuweka hapo!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………….0764 018535

Jumanne, 2 Februari 2016

HAIKUWA RAHISI



HAIKUWA RAHISI
 Ukitaka kuona mtu anaongea na maneno hayaeleweki, na ukitaka kuona mtu anaongea maneno ambayo hayaishi, ukitaka kuona mtu analia pasipo kupigwa wala kukasalishwa, ukitaka kuona mtu anagalagala chini pasipo kuangalia chini panausafi kiasi gani,ukitaka kuona mtu anashikwa kigugumizi cha ghafla na mwisho uweza kutamka neno hili HAIKUWA RAHISI!

 Hili neno kwa kawaida linatamkwa mwisho wa jambo au wa safari na hasa jambo hilo linapokuwa na mwisho mwema au ushindi wa kishindo! Na kwa kawaida kinachofuata hapo ni pumziko la moyo na hali hii inaweza kujitokeza katika hali ya mwilini kwa namna mtu anavyo shusha pumzi na kusema kwa kweli HAIKUWA RAHISI napingine anaweza kusema HAKIKA MUNGU AMETUSAIDIA.

Na pengine hili  neno linatamkwa baada ya mtu kupitia changamoto katika maisha yake yawezekana magonjwa, mateso,kuchelewa kuolewa (kadiri ya ufahamu wa mtu),misukosuko ya mahusiano,kunyimwa haki zake na pengine hata kukosa kazi kwa muda mrefu, na ukubali kuwa changamoto zinatofautiana na pindi mtu mmoja anapotokea akutie moyo….bila shaka unaweza kuamini kuwa nami Mungu atanikumbuka na hatimae nitakuwa katika nafasi iliyo bora zaidi ambayo itafanya ni mwabudu Mungu kwa raha zaidi kuliko kitu kingine chochote.

Japo kuna wakati katika maisha unaweza kuishi na usione kama kuna haja ya kumshukuru Mungu na kuzidi kumwamini kwakua unaweza usiuone ushindi kwa namna ya akili ya kimwili niseme tu kuwa ipo nguvu kubwa sana kwa wewe kumuona Mungu katika kila hatua unayofikia na sio manung’uniko kwani manung’uniko sio sehemu yako bali unahitajika kuona nguvu na uweza wa Mungu kuhusika katika maisha yako.

Hauhitaji kuona makubwa sana na ndio uone kuwa haikuwa rahisi na mengine ukaona kuwa ni ya kawaida tu, kubwa ni kutambua kuwa katika yote unahitaji kuona uwezo wa Mungu katika kukutoa mahali fulani na kukupeleka katika hatua nyingine kwa maana hiyo usisubiri upone kwenye ajali, magonjwa makubwa na ndio uone kuwa uweza wa Mungu la hasha jifunze kushukuru Mungu kwakua yeye anapenda kushukuriwa sana.

Yoshua 4:24  watu wote wa duniani wapate kujua mkono wa Bwana, ya kuwa ni mkono wenye uweza, ili wamche Bwana, Mungu wenu, milele.

Na ni kweli Mungu anafanya jambo ili kuhakikisha kuwa yeye aonekane  na sio kitu kingine na pia anafanya yote ili wewe ujisikie vizuri na watu wamuone Mungu katika hali nyingine na ya kiupekee zaidi kupitia wewe.

Kwa kusema ukweli mtu yeyote anayefanya kazi,anayesoma na shughuli zingine upenda kufikia hatua ambayo itakayomluhusu kusema kuwa mimi kuwa hapa au kuwa hivi HAIKUWA RAHISI na hivyo upata sababu au heshima ya kumwabudu Mungu zaidi na kumshukuru sana kwa kuwa ana amini ni Mungu pamoja na yeye ameweza kufika hatua aliyoifikia( mwenye akili njema).
Japo siwezi kukataa kuwa kuna wakati unaweza kuona sasa yamekwisha ukamshukuru Mungu sana lakini ukumbuke kwamba maadamu unaishi jua kila jambo kuna majira yake kuna majira ya kucheka na majira ya kulia na kadharika sawa na neno la Mungu linavyosema…………
Japo furaha/huzuni ya jana haitakuwa sawa na furaha/huzuni ya leo.

Mhubiri 3:1 Kwa kila jambo kuna majira yake, Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu.

Ndivyo hivyo ilivyo Mungu ajawai kukosea na kamwe hatakosea kama alivyosema ndivyo itakavyo kuwa kwa kuwa yeye analokusudi lililokamili kwa ajili ya kusudi lake…..mathalani unaweza kuona mtu baada ya kumaliza hatua fulani katika maisha yake anaweza kufanya sherehe kubwa katika hali njema tu kuwa Mungu amemsaidia mathalani mwanafunzi wa chuo anapohitimu anakuwa na furaha sana lakini hajajua kile kitakachofuata wakati mwingine anaweza kukaa mtaani bila kazi na ikamfikia hata kuwaza hivi kwa nini nilifanya sherehe katika baada ya kuhitimu hatua fulani ya elimu.

HAIKUWA RAHISI inapaswa kuwa ni lugha yako kwakua utakuwa ukimuona Mungu akikuvusha siku baada ya siku kadili ufahamu utakapozidi kumuona Mungu katika kufanana na Mungu kwa namna alivyotaka tuwe.

Waefeso 4:13 hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

Imeandaliwa na;

Cothey  Nelson……………………………………………………………………0764 018535