Jumanne, 29 Desemba 2015

URAFIKI NA MUNGU: SWALI LISILO NA JIBU!

URAFIKI NA MUNGU: SWALI LISILO NA JIBU!: SWALI LISILO NA JIBU  Mwanzo 41:8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na    watu wo...

SWALI LISILO NA JIBU!



SWALI LISILO NA JIBU

 Mwanzo 41:8 Hata asubuhi roho yake ikafadhaika; akapeleka watu kuwaita waganga wote wa Misri, na   watu wote wenye hekima walioko. Farao akawahadithia ndoto yake, wala hakuna aliyeweza kumfasiria Farao mambo hayo.

KARIBU……………………….!!
Kwa mwalimu mwenye mapenzi mema na wanafunzi wake pindi inapotokea ametunga mtihani na baadhi ya maswali au swali pakatokea makosa kwa kutumia busara weza kutoa alama za bure katika hilo swali au maswali!

Na tukiingia katika maisha ya kila siku kuna mambo mengine yanakutokea katika maisha yako yanaweza kuwa magumu sana lakini pindi huo  ugumu utakapokuwa sio wakudumu/baada ya kupata jibu basi tunaita ni changamoto ya kitambo lakini pindi jambo hilo litakaposababisha akili yako kukosa mwelekeo mwingine tunaita jambo lilikosa jibu na hatimae uweza kupelekea akili kufika mwisho! Sikatai katika hali ya kisomi na hata ya kikawaida(kijamii)  katika maswali yako yenye majibu na yako yasiyo na majibu na maswali haya kwa jina lingine uweza kuitwa maswali yenye utata!au yaliyoshindikana.

►Hivi kwanini niko hapa na wala sio kule?Hivi kwa nini nilizaliwa huku na sikuzaliwa kule? Hivi kwanini nilikutana na huyu na wala sikukutana na Yule? kwanini napenda hiki na sipendi kile kile? Na hivi kwanini sikuwaza vile ni kawaza hivi? Hivi ni kwanini nilitamani vile wala sikutamani hivi?………………………………!!!

Hivi kwanini niliishia pale sikuishia hapa? Hivi kwanini niliomba hivi sikuomba vile? Hivi kwanini naomba hivi na wala siombi vile? Hivi kwanini nachoka hivi na wala sichoki vile?.............................................!!!

Haya yote ni aina ya maswali ambayo mwanadamu mwenye akili timam lazima ajiiulize na wakati mwingine uweza kuijiuliza hivi mimi nimemkosea Mungu kitu gani mpaka ni kawa hivi nilivyo leo au nilivyoleo mimi binafsi nilifanya jambo gani? Lakini wengi uweza kujijibu majibu yaliyo kawaida ya wanadamu na mengine kukosa majibu kabisa lakini wengi watasema ni neema ya Mungu! Hasa katika hali njema.

Ni wazi tu kuwa jibu la kujipa mwenyewe kutokana na ukawaida wa wengi unakuwa na nguvu pale tu utakapoona jibu ulilolipata ni sawa na ulivyofikiria lakini pindi itakapo kuwa kinyume na vile ulivyokusudia ndipo hapo akili inakosa mwegemeo na kuanza kuyumbayumba kwakukosa mwelekeo uliothabiti katika kushikiria.

Japo na kubaliana kabisa jambo lolote zuri uzaliwa katika wazo na baadae kupelekea utekelezaji na pindi utakapokuwa ukiwaza kuna maswali yatakuwa yakiibuka na yote ni katika kukusaidia namna ya kuteleza lile wazo ulilokuwa nalo katika mkakati wako uliokuwa nao. Katika hilo unaweza kuwa na maswali yakapata jibu na mengine yakakosa jibu kutokana na  imani iliyondani yako au kutokana na mawazo ya watu yaliyo katika hali ya kusikika au kuandikikwa.

Na pindi utakapo fikia kipindi cha swali kukosa jibu hapo uwezekano wakufanya jambo lisilopaswa ni mkubwa sana au kufanya jambo nje ya matarajio yako au katika mipango yako kuwa kufanyika kuwa tofauti, kuna wakati unaweza fikiri kuwa unalo jibu sahihi lakini pindi utakaposhindwa kufanikiwa basi litakuwa swali lisilo na jibu mathalani mtu anaweza kuhisi kuwa anaumwa ugonjwa wakichwa na bila wasiwasi akaenda duka la dawa na kununua dawa lakini pindi hiyo dawa ikashindwa kutibu kichwa chake ndipo hapo ataanza kuona ugumu wa swala linalo mkabili na kuanza kutumia muda wake na fedha zake katika kushughulikia tatizo linalo mkabali katika kila kona na pindi jitihada zake zitakapofika mwisho pasipo mwelekeo wa kupata nafuu hapo bila shaka itazaliwa swali lililokosa jibu!

Ni jambo linaloleta huzuni sana pindi unapotambua swali ulilonalo limekosa jibu kwa maana nyingine kama ni mwanafunzi basi hapo kosa ni haki yako na kama ni maisha basi yanaweza kuwa na mwelekeo mwingine na anaweza asiupende au upande mbaya.

Kunakuwa ni wakati mgumu sana kwa mtu pindi anapokuwa na wakati ambao haoni jibu sahihi, wako watu wajiingiza katika ulevi uliopitiliza, wengine wanakuwa makahaba, wengine wanakuwa na maisha ya upweke na hata mwingine kufikia hatua ya kujiua.

Katika kipindi hiki hata profesa/ata watu wenye  uweza mkubwa la kusaidia jamii lakini unaweza kuta  kufanya jambo ambalo kwa hakika ukilisikia hutaweza kuamini kama ndiyo yeye amefanya jambo hilo na hata kushindwa kujua kwa nini amefikia hatua hii, wako watu wanafika hatua ya kuuana kwa sababu amefikiria sana lakini bado amekosa jibu hasa la kujibu moyo wake na moyo wake ukatulia.

Unaweza kuwa na mtu mwenye heshima katika kijiji/mtaa wako lakini baada ya maswali yako kukosa jibu unaweza ukakuta kafanya jambo ambalo hata chizi hawezi kufanya jambo hilo na watu wote kubaki kushangaa lakini yote ni matokeo ya swali lako kukosa jibu!

►Swali lililokosa jibu ni mateso ya akili na ni usumbufu wa moyo na zaidi sana adhabu katika maisha yako!

*Mwisho wa swali hili ni mpaka pale utakapotambua Mungu ni mkubwa na mpana sana katika maisha yako na hapo akili yako itakapoelewa kuwa kweli uwezo wa Mungu hauna kipimo chake anaweza fanya jambo lolote wakati wowote na katika mazingira yoyote!

*Hapa ndipo sehemu sahihi ya kusema acha Mungu aitwe Mungu kwakua unakuwa umemuona katika maisha yako na sio habari ya kusikia kwa mtu na ni mahali ambapo akili yako inapata funzo jingine na kupata hatua nyingine!

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………………0764 018535

Jumanne, 22 Desemba 2015

MUNGU HAKOSEI



MUNGU HAKOSEI



Hili swala sio la kusikia tu ukaishia hapo bali ni hali  halisi ya moyo wako kukwambia kuwa Mungu hakosei kwa uthibitisho wa Roho mtakatifu ndani yako. Japo ni kweli kukosea ni sifa ya binadamu lakini sio sifa ya Mungu na pindi utakapo amua kwa dhati kumbeba Mungu itakuwa si rahisi kwa wewe kukosea kwani uwezo wa Mungu utakuwa umekufunika katika hali ya kukuwezesha.

Ni rahisi kumshukuru Mungu katika jambo jema alilokutendea na pia ni rahisi kunung’unika katika jambo baya ambalo litakalo kupata! Katika maisha yako ya kila siku ni vizuri utambue kwamba kosa lako sio kosa la Mungu na pia kushindwa kwako sio kushindwa kwa Mungu.
Ni kweli kama binadamu mabaya yanaweza kukukabili lakini hapo sio fursa ya kuona kuwa Mungu amekosea kwa wewe kupitia hali ngumu japo wakati mwingine unaweza kuona mambo yamekuandama ukaanza kufikiri na kusema Mungu anioni.

Hili ni neno kwa namna ya uhalisia wake unaweza sema AMEN kweli Mungu ajawai kukosea na kamwe hatakosea kwakua kazi zake ni kamilifu, na kunakipindi unaweza kuwa njia panda kujua huyu ni kweli Mungu wa huruma kweli au ! na wakati mwingine unaweza kusema katika jambo hili Mungu ajakutendea haki kwa maana nyingine amekuonea!

Ukweli uponyaji wa hatua hii unahitaji sana ufahamu wako kuweza kumwelewa Mungu kwa namna ya kimungu tu! Zaidi ya hapo ukweli hautaweza kuona ukamilifu wa Mungu katika kila jambo linalokutokea kwani unaweza kuyumbishwa kama upepo huku na huko.

Ni maisha mengine utaanza kuishi pindi utakapoweka kwenye ufahamu wako kuwa Mungu ajawai kukosea na hata kosea hata kama jambo lolote likikukuta haijarishi jambo hilo ni baya kiasi gani? Niseme tu kuna maisha watu wengi wanaishi katika mateso na dhiki na kugandamizwa pasipo kujua kuwa uwa Mungu hakoseibali wanaishia kulalamika, wako watu wanaishi maisha yasiyo ya kwao kutokana mioyo yao imejaa lawama kuhusu Mungu kwa kuona anaruhusu mabaya katika maisha yake siku zote.

Matokeo ya watu kuona Mungu anakosea matunda yake kama ifuatavyo,wako watu hawana tena imani ya ukristo walionao wamekuwa hawaoni maana ya kwenda kanisani, hata thamani ya mchungaji na kuona nafasi yake haipo katika kanisa, mtu huyu amejawa na lawama maisha yake yote…….mtu huyu hana maombi zaidi ya malalamiko, hana maneno mazuri ya Mungu zaidi ya kulaumu. Zaburi 36:3 “Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.”

Ni kweli hauwezi kuwa mtu wa tofauti kama tu ufahamu wako umejawa na hali ya kuona Mungu anakosea itakuwa ni kizingiti kitachoshika maisha yako na mbaya zaidi kitasambazaa hata kwa watoto wako huzuni  yako haitakuwa kwako tu bali hata kwa wale watakao kufuata wata beba msalaba wako.

Waebrania 11:6 “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao”.
Napindi utakapo tambua kuwa Mungu hakosei hapo itakuhakikishia ushindi wa kimungu katika yale yanayokukabili kwakua katika dogo utakapo ona uweza wa Mungu bila shaka Mungu naye atakushangaza kukufanyia makubwa zaidi ……….hii tunaiona pale yesu walipo pewa mikate mitano na samaki wawili yesu alishukuru kwa kile kilichopo na Mungu akaanza kukizidisha sawa na uhitaji uliokuwepo,

Mathayo 14:19 “Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi, wanafunzi wakawapa makutano”

Napenda kusema kwa kiasi kikubwa utendaji wa Mungu utegemea sana na vile unavyomuona au mwamini, imani yako ndio kigezo kikubwa katika kuhakikisha kunautendaji wa kimbingu ndo mana biblia inasema kuwa pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu…( waebrania 11:6).

Luka 17:6 “Bwana akasema, Kama mngekuwa na imani kiasi cha chembe ya haradali, mngeuambia mkuyu huu, Ng'oka, ukapandwe baharini, nao ungewatii”

Hivyo ufahamu wako unaweza kuleta giza katika maisha yako au nuru katika maisha yako kutokana mtazamo wako usio sahihi kuhusu Mungu, ukomboe ufahamu wako katika kuimarisha kumjua 
Mungu katika njia iliyo sahihi nasio ya kujifariji tu! Pasipokuwa na  muelekeo ulio sawa.

Japo kweli kila jambo linalotokea linakuwa na sababu yake mengine nikutaka kujua ubora wa imani yako ulionayo kwa Mungu,mengine ni kukumbusha katika utumishi ulio sahihi, kurejea kwa toba mbele za Mungu na mengine mengi ambayo Mungu anaweza kukupa tafsiri yake.

Kuna aina mbili ya maisha kati ya maisha ya kumuona Mungu anakosea na kuona Mungu hakosei kila maisha yana namna yake ya kuishi na matokeo yake, hivyo usikubali kuishi maisha ya kuona Mungu anakosea kwani utaweza kuwa na imani potofu, ugumu wa moyo na kutokuwa tayari katika kumtumikia Mungu kwa ukamilifu.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson………………………………………………………………0764 018535

Jumanne, 8 Desemba 2015

HAIJUI KESHO YAKO



HAIJUI KESHO YAKO


 Yako maneno ambayo hayasauliki wala kufutika katika maisha ya mtu kirahisi hata kama hayo maneno ajayahifadhi katika moyo wake mathalani HAUTA FIKA, UTANIKUMBUKA, UTAIONA DUNIA, UTAKUJA KWA MAGOTI, HAUTA PONA, UMEFIKA MWISHO, UTAJUTA, SINILISEMA,UMEKWISHA.

Pia yako matendo ambayo mtu akikufanyia uwezi kusahau na hasa yakiwa yana ashiria mwisho wa hatua katika maisha yako yanaweza kuweka alama katika maisha yake na kutia hofu katika maisha yako, lakini.pindi unapotambua kuwa hakuna mtu anaijua kesho yako hii ni siraha kubwa sana kwa wewe kushinda kwakua utatumia muda mzuri katika kufanikisha lile kusudi ambalo Mungu amelikwa ndani yako kuliko kuangalia mwitikio wa kile unachokifanya au kile unachokiangalia kukifanya.

 Hakuna kitu kizuri kama mtu unayepigana nawe kutojua chanzo cha nguvu zako…..tukimwangalia daudi alipokuwa akimkabili goliati, goliati alimdharau daudi kutokana na kutojua chanzo,asili ya nguvu zake au kujiamini kwake na hapo ndipo chanzo cha kushindwa kwa goliati na laiti goliati angelijua chanzo cha nguvu zake daudi asinge thubutu kupambana nae.

Nikutoe tu hofu katika kila jambo unalolikabili jua kwamba kama mtu ajui kesho yako tambua kuwa kufika ni lazima kwakua njia yako ni upofu kwa wengine hivyo kamwe hawawezi kuzuia kwa ukamilifu japo anaweza kuzani kuwa anaziba njia lakini ukweli unabaki njia yako inakuwa iko wazi kwa ajili ya Mungu kukufikisha.

Unapoona ukombozi wa mwanadamu, yesu alipokuja duniani katika kuleta ukombozi kwa mwanadamu ambaye yeye aliwapenda sana…….. lakini shetani alijua kwa kuhakikisha yesu anapotea ulimwenguni kwa haraka ili aendelee katika kutawala dunia lakini akujua kuwa haraka yake katika kumpoteza yesu kumbe ndio hatarisha maisha yake katika utawala wake duniani.

Unahaja ya kuweka kisirani kwa mtu wala kisasi kwa lolote linalo kukabili kwakua yeye Mungu alianza kukupa nuru katika duniani atakufikisha kule unakotakiwa kufika kwakua yeye ndio anajua njia ya kukufikisha kule unakotakiwa kufika, lakini sumu kwako inaweza kutokea pindi ukaona katika mwisho wako ni sawa na  neno la mtu na ukaanza kujipanga katika kukabiliana na ushindani  na mtu huyu pasipo kuweka mwelekeo wako kwa Mungu tu hapa kushindwa au kuchelewa ni haki yako.

Niseme tu kuwa kushindwa kufika kesho yako ni wewe mwenyewe na sio kitu kingine japo vikwazo vinatokea ni kawaida tu na sio uone kuwa Mungu hana upendo na wewe kutokana na  yale yanayokukabili, lazima ujifunze kitu kimoja kukaa mahali ambapo unaonekana hauna kibali kwa wote lakini namna ya kuishi hapo ndio msingi mzuri wa kuinuka kwako au wakishindwa kwako. 

Usiwe mwepesi wa kukimbia katika kila mazingira yanayokukabili………mwangalia daudi alipokaa na Esau wakati akiwa hana kibali kwa mfalme Esau lakini alitambua namna ya kukaa nae.

Na hali ya mtu kutojua kesho yako haina maana sasa kuanza kudharau wenzako na kuona hawana mchango wowote katika maisha yako jua hili litakuwa kikwazo kwako na sio tumaini kwako na inaweza kusababisha kushindwa kule unakotakiwa kufika, sikuzote unyenyekevu na upole pamoja mshikamano wa wewe na Mungu na kuthamini kwa wengine kuliko wewe binafsi uwe dira ya maisha yako.

Nikukumbushe kuwa thamani yako inategemea sana na namna ya unavyowathamini wengine kwakua Mungu anataka KUMPENDA JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO fanya jambo kwa uelewa na katika hali ya uelewa uliosahihi na sio kwa hofu isiyotokana na Mungu.

Imeandaliwa na;

Cothey  Nelson…………………………..0764 018535

BARIKIWA NDUGU!!!

Jumanne, 1 Desemba 2015

MAPENZI YA MUNGU



MAPENZI YA MUNGU




Hili neno MAPENZI sio jambo la kushangaza katika ulimwengu wa leo lakini kubwa zaidi ni namna linavyopewa nafasi katika dunia ya leo, kimekuwa kama kitu cha mpito tu kwani leo unaweza kuwa na mapenzi na huyu na bila wasiwasi kesho ukawa na mapenzi na mwingine na huku moyo wako ukiwa umejaa ujasiri wote pasipo uwoga wowote na mbaya zaidi unaweza kujisifia kuwa hali hiyo ndio ukisasa wenyewe imekuwa hivyo kwa muda……mathalani ya mlo asubui utakunywa chai na maandazi na jioni unaweza kuamua kula wali na dagaa sawa sawa na uwezo wa uchumi wa mtu na maamuzi ya mtu.

Niseme tu kuwa chezea mapenzi yoyote kati yako na wanyama, jirani na hata rafiki lakini sio mapenzi ya Mungu katika maisha yako, niseme haya mapenzi hayabadilishwi kirahisikirahisi leo utaamua kuwa na mapenzi na Mungu kesho utaki tena kuwa na mapenzi alafu baadae kidogo ukaamua kurudi tena kuwa na mapenzi na Mungu.

MAPENZI YA MUNGU!
Hiki ni kitu kingine kwani kinausisha maumivu ya mwili na mateso ya nafsi katika kutimiza matakwa au mapenzi ya Mungu, ni wazi pindi utakapo amua kuanza kuyaishi haya mapenzi ya Mungu kwa ukamilifu bila shaka utaanza kuliona penzi la Mungu likiidhihirika kwa upya katika maisha yako likitofautisha maisha yako na watu wengine.

Penzi la Mungu kuliishi sio jambo la kufikirika tu kumbuka yesu katika kutimiza matakwa ya baba yake ili mgharim mateso ya mwili wake ndomana nafsi yake iliteseka sana kwa kuona kile kitakachompata katika kutimiza lile neno ambalo Mungu mwenyewe alilo liongea pale bustanini eden kuwa uzao wa mwanamke utakuponda kichwa nyoka.

Ni wazi pindi utakapoanza kutekeleza mapenzi ya Mungu lazima yako yavunjike kama ilivyo kawaida unapotaka kutekeleza mapenzi ya mtu lazima yako ya teketee ili utoe fursa katika kutekeleza mapenzi ya mwingine, na kamwe hauwezi kutekeleza mapenzi yako huku unatekeleza mapenzi ya mwingine kwa ufasaha zaidi.

Moja ya sumu kubwa katika ushirika wa watu wowote ni hali ya kushindwa kuteleza matakwa ya mwingine, watu wengi wanaachana kuona kwamba huyu mchumba,rafiki,ndugu niliye naye amejaa maslai binafsi yeye anajali maisha yake zaidi kuliko maisha ya mwingine hivyo sioni sababu ya mimi kuendelea nae.

Hata katika biblia amri ngumu ambayo watu wengi watakayoshindwa ni KUMPENDA JIRANI YAKO KAMA NAFSI YAKO hii inaweza kubaki katika maandiko tu na wala neno hili lisitoke na kuwa na athari au kuwa halisi katika maisha tunayoishi.

Niseme pindi unaposikia MAPENZI YA MUNGU huu ni jumla ya mambo ya Mungu ambayo yamebebwa au yanabebwa na mtu mwenye ufahamu kamili ambao unajua unafanya kitu gani? Na kamwe hajali hasara zake kuwa ni kikwazo katika kufanikisha kile kitu ambacho Mungu anakitaka toka kwake, kwa maana nyingine mtu huyu hayuko tayari kumfurahisha MTU au YEYE mwenyewe zaidi ya kukamilisha kile ambacho Mungu anataka akikamilishe kwa ufasaha zaidi.

Furaha yake ni kuona lile lililokuwa penzi la Mungu kwake linakamilika tena katika mafanikio makubwa pasipo hata kuacha chembe ya kitu chochote kutotimia, na kwa maana hiyo usingizi wake unakuja baada ya kuona la Mungu limesha timia.

Niseme tu wazi hauwezi kujiita kuwa unafanya mapenzi ya Mungu kwakua unafahamika kanisani vizuri na mchungaji au waumini wenzako bali ni vile nafsi yako inavyo kushuhudia na sio lazima uwe mtakatifu sana bali kuwa halisi mbele za Mungu kuwa ndio wewe hakuna mbadala hali hii inabidi ujifahamu wewe binafsi.

Pia kutembea katika karama au huduma yoyote ambayo Mungu amekupa hichi sio kigenzo cha kuonyesha sasa wewe unatembea katika mapenzi ya Mungu, kwani unaweza kufanya ubadhilifu na bado ukatembea katika karama za rohoni kwani Mungu ameziachilia kwa kusudi lake kwa ajili ya kufanyika baraka kwa watu wengine lakini sio kwako.

Kuna hasara kubwa kufanya mambo ya kimungu pasipo kutembea katika mapenzi ya Mungu unaweza kupoteza uzima wa Mungu ndani yako na kule unakotarajia kwenda yaani mbinguni, jali sana utendaji wako katika mapenzi ya Mungu kuliko sifa za watu katika maisha yako.


Imeandaliwa na ;

Cothey Nelson……………………………………………………………….0764 018535