Jumanne, 31 Mei 2016

GOD'S PROMISE



AHADI YA MUNGU


Kama kuna kitu ambacho utakiwi kuweka mashaka atachembe!...wala moyo wako kushuka chini na hata fahamu kupoteza muelekeo ni hiki kitu kinaitwa AHADI YA MUNGU! Nitangulie kusema tu maadamu unaishi ndani ya dunia hii jua ahadi ya Mungu juu ya maisha yako ipo kama isingelikuwepo isinge likuwa ya maana ya wewe kuwepo duniani, hivyo uhitaji kuomba ahadi ya Mungu jua zipo na zitakuja kwa namna yake kutokana na mfumo na utaratibu wake.

Yeremia 1:5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.

Haya ni maneno ya Mungu yanaishi na yana nguvu mpaka leo! Ni akili yako ni kutambua tu.
Ni pende kusema tu ahadi ziko nyingi…..ziko zinazo toka kwa wanadamu, miungu na MUNGU lakini kamwe haziwezi kufanana lakini nikubaliane tu kuwa kila ahadi ina taratibu zake na ili uzipate ahadi zake basi hauna budi uzifuate hizo kanuni zake kwakua ndani ya taratibu zake huko ndiko ahadi upitia.

Najua yako malengo mengi ya ahadi lakini mimi niseme malengo machache tu:
i.                    Kufanya uwe na furaha
ii.                  Kufanya uzidi kuimarika pasipo kuchoka
iii.                Kudumu katika mwenendo mzuri
iv.                Kufanya usahau mengine na kuweka bidii katika jambo husika

Nikubaliane tu ahadi imetumika sana katika maeneo mbalimbali mathalani ofisini bosi anaweza kukuambia ukiifanya vizuri kazi hii kuna zawadi nitakupa au kukuongeza kima cha mshahara wako na nyingine nyingi, katika familia wazazi wengi wamekuwa waki waahidi sana watoto wao zawadi ilikuwafanya watoto  wasome kwa bidii au wabadilike kutoka katika tabia fulani ambayo wazazi/mzazi afurahishwi nayo.

Nipende kusema tu kuwa ahadi ya Mungu juu ya maisha yako ni zaidi ya kukopa salio katika mitandao ya mawasiliano (voda,tigo,zantel,airtel) na pindi utakapoongeza salio kwa njia ya kawaida utaona meseji watakayokuandikia “asante kwa kurudisha deni lako” japo kuwa tunaona ni mtandao uliotengenezwa na hiyo program kuanza kufanya kazi…..lakini ahadi ya Mungu kumbukumbu  yake ni zaidi ya hapo kamwe haiwezi kuwa rahisi kusahaulika!

Ahadi za Mungu ni nyingi katika maisha yako na katika mwendo wako na Mungu bila shaka utaona mambo mengi wala usijue haya mambo mbona sikuyajua wala sikuwai kumuomba bali yatakuja kwakua yeye kama baba anajua wajibu wake kwako na atatoa kwakua  hilo ni jukumu lake.

Mathayo 6: 32 Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote.

Na wakati mwingine unaweza kujua baadhi ya ahadi ya Mungu katika maisha yako, Ni ukweli usiopingika kuwa hivi ni vitu viwili tofauti sana kati ya kutambua ahadi ambayo Mungu amekuwaidi na kuipata ahadi hiyo, kwani kuna mchakato mrefu sana(majira sahihi) na hapo ndipo kuna kuwa ni kipindi kizuri cha kupima PENZI LAKO kwa Mungu.

Warumi  4:18 Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ili apate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.
             19 Yeye asiyekuwa dhaifu wa imani, alifikiri hali ya mwili wake uliokuwa umekwisha kufa, (akiwa amekwisha kupata umri wa kama miaka mia), na hali ya kufa ya tumbo lake Sara.
             20 Lakini akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa imani, akimtukuza Mungu;
             21 huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoahidi.

Tunaona ibraham japo Mungu mwenyewe alimuahidi lakini alihitaji kutiwa nguvu na Mungu mwenyewe ili kuifikia ahadi yake.

Kama nilivvosema hapo awali kuwa kila mtu maadamu uko duniani unayo ahadi ya Mungu katika maisha yako hasa mtu uliye okoka unapata kibali kuishi katika maisha yanayoambata na ahadi ya Mungu kwa asilimia mia, lakini kutokana na mabadiliko ya dunia imekuwa ni changamoto sana acha mbali na sayansi na teknolojia bali hasa injiri ya sasa imekuwa ikiwapa watu njia fupi katika kuwapatia mapumziko ya shida zao mathalani maombezi kwa wagonjwa kwa namna ya kimwili fedha imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa.

Pamoja na hilo wa kristo wengi wanashindwa kudumu katika imani zao za kweli kutokana na misingi waliyo ibeba sio imara imara zaidi.

Mathayo 7: 24 Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba;
                      25 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, isianguke; kwa maana misingi yake imewekwa juu ya mwamba.
                     26 Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga;
                      27 mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, pepo zikavuma, zikaipiga nyumba ile, ikaanguka; nalo anguko lake likawa kubwa

Nipende kusema ahadi ya Mungu ni amina na kweli na kamwe awezi kusahau ila uzidi kudumu katika yeye kwa majira yake atakutoa na kuchomoza!

Sina maneno mengi zaidi ya kusema!

Ayubu 22:21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson………………………………….0764 018535

BARIKIWA SANA RAFIKI

Jumanne, 24 Mei 2016

ACHA IPITE



ACHA IPITE



Kibinadamu uwa atupendi mazuri yapite…… bali tunaomba usiku na mchana kuwa mambo mazuri yazidi kuwepo sikuzote wala yasikome kamwe lakini katika upande wa mambo mabaya tunapenda yaondoke haraka sana yaani kufumba na kufumbua hilo jambo liwe limetoweka kabisa.

Unaweza ukawa katika eneo ambalo kwa kipindi fulani kukawa na hewa nzuri sana na nafsi yako pamoja na mwili wako ikapafurahia sana lakini kama hiyo hali ya hewa ni ya kipindi tu bila shaka itaondoka atakama utakuwa umeipenda kiasi gani! Mbali na hali ya hewa pia kuna hatua katika mwanadamu inayojulikana kama hatua ya ujana ambayo wanadamu wengi wanaipenda sana lakini kwa uhakika ujue tu kuwa kipindi hicho uwezi kudumu nacho siku zote ahijarishi ataukifanya mazoezi kiasi gani ili kuutunza ujana wako bado mwili utakataa tu! Unaweza ulikuwa na mtu ambaye uliye mpenda sana, kumuheshimu na kumthamini lakini usiopingika kuwa kuna majira mtaachana tu kwa kupenda au kutopenda! Unaweza kuipenda siku kwa namna ilivyokuwa na usiitamini ata usiku uingie lakini kwa kutamani kwako usiku usiingie ni kweli hautaingia ni swali jepesi.

Wako watu wengi sana wamekuwa katika hali mbaya sana pindi wanapokuta kuna kitu alichokipenda sana na kuona sasa kimeshatoweka na hakuna la kufanya uweza kuugua ugonjwa wa kichaa, shinikizo la moyo na wengine ufika mbali sana hata kutaka kujiua kwa kuona kile alichokipenda au alichojivunia akipo tena hivyo ana amini sasa aibu imesha mfika na hakuna njia nyingine ya kurejesha furaha yake.

Acha ipite inaweza kuwa katika hali ya kukosa  au kufukuzwa kazi, kupoteza rafiki, mpenzi, na hata ndugu! Kinachoweza kuwatengisha katika kuachishwa au kuachana mathalani kusafiri kwenda mbali sana ambako kumuona si rahisi tena au kufungwa jera kwa muda wa miaka mingi kiasi kwamba uhuru wako hautakuwepo tena.

Isaya 40:8 Majani yakauka, ua lanyauka; Bali neno la Mungu wetu litasimama milele.

Najua kwa uhalisia ni ngumu katika kuyaruhusu mambo mazuri kupita japo ingekuwa ni amri yako usingeweza kukubali hali hiyo itokee lakini mambo mengi kutokana na asili yake ni lazima yapotee tu…..aijalishi unapenda au haupendi.

Na sio mbaya kujua kama kitu kilikuja basi pasipo shaka kitatoweka tu ila shida inakuja pale kutojua  ni wakati gani hiki nilichonacho kitatoweka na je! Utakuwa radhi pindi kitu kitakapo toweka. Najua kuna mambo mengi yanapotoka kwako hasa yale uliyo yapenda na kuyawekea malengo mazuri uwa moyo wako unakuwa katika hali ya chini.

Niseme kuna kuwa na wakati mzur(jicho jingine) katika kuacha hali kwanza kutoweka na hatimae kuchipuka katika hali nzuri, wakati watu wameinuka sana pale walipoamua kuachana na vitu vya awali na wakati mwingine ilikuwa katika hali ya maumivu lakini mwisho wake ulikuwa bora kuliko mwanzo wake.

Na katika kipindi cha kuacha kitu kipite usipokuwa makini unaweza ongeza maadui kuliko marafiki na kuwa mbali hata watu wale ambao ulikuwa unawaona kuwa ni watu wazuri ukaanza kugeuza moyo wako na kuwapa mtazamo mwingine.

Najua inaweza kuwa ngumu au kuchukua muda katika kukubali kuwa imesha tokea na imeshakuwa na hapo kukubali kuwa imeshatokea kutokana na majira yaliyopo sasa lakini bado yule aliyenikutanisha au aliyenipa nafasi bado yuko anawezafanya makubwa kuliko vile ninavyowaza na kuhofia sasa itakuwaje? Mbona hivi au nitakamilishaje ndoto zangu usihofu aliyeweka ndoto atazitimiza tu kwa namna yoyote maana ameziweka kwa ajili yake na kusudi lake kamwe aliwezi kuzuiliwa kamwe.

Lazima utambue ukubwa wa Mungu wako na Upendo wake usio kuwa na mipaka wala kizuizi chochote kwani bila yeye hakuna kilichofanyika na ndani kuna kushamiri na ubora usio koma kwakua ndani yake asili ya kuzalisha vitu vikubwa vikafanya mwisho ukawa mkubwa kuliko mwanzo.

AMINI MUNGU HAKOSEI WALA ACHELEWI!

Imeandaliwa:

Cothey  Nelson………………………………………….0764 018535

Jumanne, 10 Mei 2016

NJE YA AKILI YANGU!



NJE YA AKILI



1 Wafalme 4:29 Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.

Binadamu utambuliwa na hata kuheshimiwa kutokana na matumizi ya akili yake, kwani watu wengi wamesaidia na kuwa wa maana katika jamii kutokana na matumizi mazuri ya akili au hali ya kuiruhusu uweza wa Mungu kufanya kazi kupitia akili zao na hatimae kuvumbua vitu mbalimbali na mwisho kuzaliwa MTAALAM au mtu aliyebobea jambo fulani na kulielewa zaidi katika jambo fulani.

Zaburi 36:3 Maneno ya kinywa chake ni uovu na hila, Ameacha kuwa na akili na kutenda mema.

Mithali 12:8 Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili zake; Bali mwenye moyo wa ukaidi atadharauliwa

Kwa mtu ambaye anaonekana hana matumizi sahihi ya akili yake basi uweza kuitwa chizi, kwa maana hana matumizi sahihi ya akili yake binafsi……kwa maana nyingine mtu anayefanya jambo ambalo ni hasara maana alina faida katika jamii yake zaidi ya hasara basi uitwa chizi lakini kwa mtu anayefanya jambo ambalo sio la kawaida katika jamii husika ambalo likazalisha tija katika jamii husika uitwa mtaalam.

Zaburi 49:20 Mwanadamu mwenye heshima, iwapo hana akili, Amefanana na wanyama wapoteao.

Matumizi ya akili yaliyo sahihi ni kitendawili kilicho na maswali mengi katika kutaka na kujua hivi ni nini maana ya matumizi sahihi ya akili na namjuaje mtu aliye na matumizi sahihi ya akili mathalani ukiweza kurudisha akili yako katika enzi za NUHU ukajichukua nawe ukawa mmoja wa wananchi waliokuwa wanaishi mahali ambapo nuhu yupo ni kweli ungekubaliana na Nuhu kuwa kile anachojenga kina maana kweli na kita wasaidia kweli jamii husika……..anajenga safina wakati katika jamii husika hakuna historia ya mvua na mbaya zaidi safina kubwa sana, katika elimu ya kibiashara tunasema high demand = high supply…….kwa maana rahisi mahitaji ya bidhaa basi yaendane na usambazaji wa bidhaa, kwa maana halisi katika harakati za Nuhu hazikuwa sawa kutokana hapakuwa na uhitaji wa safina kwakua watu walikuwa hawaijui mvua.

Kwa maana hiyo wakati mwingine katika mwanzo wa jambo unaweza usijue kama mtu kama huyu  hichi anachofanya kweli ana matumizi sahihi ya akili kweli? Lakini jibu la uhakika linaweza kuja pale mara tu ile picha iliyokuwa katika kichwa chake au hazma iliyokuwa katika moyo wake itakapokamilika na kuona picha inayoonekana au matunda ya kile anachokifanya mathalani mtu anatengeza dawa na kuanza kuponya maisha ya watu.

Utofauti wa jambo lazima uanzie kwenye utofauti wa akili kwa maana akili inapokuwa tofauti basi bila shaka utendaji utakuwa tofauti na kuwa tofauti katika jamii husika…. Na bila shaka wako watakao kukubali na wapo ambao hawatakukubali ila wanaweza kukubali baadae.

Nje akili ya kiubinadamu hichi ndicho kitu kitakachokutambulisha wewe na kukuweka katika alama katika jamii yako na kubaki katika fahamu za watu kuwa kitu fulani kilifanywa na mtu na kiliwasaidia watu wengi hivyo mioyo yao itabaki na shukrani kwa tendo ulilolifanya.

Uvumbuzi unapokuwa umetokea kwa namna yake bila shaka hata matokeo yake yatakuwa ya jinsi yake kwakua kila uvumbuzi wajambo unaubora wake, na sio lazima ufanye makubwa sana yakasababisha pawepo na mshangao mkubwa ni kitu chochote ambacho kitaleta manufaa katika jamii husika kwa kiwango chochote kile.

Hauhitaji uwe na nafasi kubwa sana ili uweze kufanya makubwa zaidi unahitaji kuwa na nafasi ndogo ili ufanye yaliyo makubwa sana, kwa kuwa utendaji wa jambo na matokeo utegemea sana na mipango iliyothabiti na sio nafasi kubwa.

Ili uweze kuimarika mahali popote ulipo unahitaji sana upate ufumbuzi sahihi katika mazingira husika kwa kutumia mapana ya akili yako, kwakua akili yako ni hazina tosha inayoweza kuyafanya yale katika namna macho pekee hayawezi kutendeka.

Ni muhimu kutambua kuwa utofauti wako utegemea sana na utofauti wa akili yako kwakua ndani ya akili yako ndiko kuna zaliwa utendaji ulio na nguvu na wenye mafanikio.

Imeandaliwa na:

Cothey Nelson…………………………………..0764 018535

Jumanne, 3 Mei 2016

IPENDE FURAHA YAKO



IPENDE FURAHA YAKO



Furaha ipo kwa ajili yako na sio wewe uwe kwa ajili ya furaha!

Furaha haina uchaguzi wake bali wewe ndio mwenye mamlamka na hiyo furaha…..ni kutambua tu kuwa wewe ndio mwenye kauli ya mwisho katika kuitawala furaha yako na wala sio kitu kingine.

Hakikisha hakuna jambo katika maisha yako lenye kauli au lenye nguvu katika kuiondoa furaha katika maisha yako iwe kuchekwa, kusemwa, kuhisiwa vibaya au kutothaminika ni vizuri kutambua furaha ni zaidi ya hapo au ni zaidi ya hayo.

Moja ya kipenzi cha wengi katika dunia ya sasa ni FURAHA na kwa kawaida furaha uwa ni rafiki wa moyo kwa kua moyo ukifurahi basi na sura itachangamka na hatimae mwili mzima utakuwa unakuwa katika hali iliyo njema katika kuondoa makunyazi yake.

Na nzuri zaidi sana kila mtu ana changamko la moyo binafsi wala aliingiliani na mtu mwingine ndomana unaweza kukuta huyu analia na huyu anacheka, hapa kuna msiba na huku kuna harusi kwa kila mtu anakuwa na upande wake, bila shaka natambua au kukubaliana katika mwendelezo wa furaha unategemea sana msingi wa furaha yako wako watu furaha imebebwa na msingi wa kazi nzuri au usafiri mzuri na mangine mengi.

Nakubaliana kwa asilimia zote ufanisi mwingi katika utendaji ubebwa na moyo wenye furaha kwa kuwa moyo wa furaha utengeneza utulivu wa akili na upelekea ufanisi wa utendaji na hatimae uzalisha ubora na tija katika jambo husika.

Katika ulimwengu wa sasa kuwa na furaha ni jambo la kawaida lakini katika kudumu furaha imekuwa ni shida kwakua watu kuto kutambua misingi sahihi ya kuwa na furaha hivyo inakuwa kama mfa maji maji aishi kutapatapa hivyo watu wanaishi kama nguruwe leo una muosha na baadae anajichafua.

Nipende kusema kuna kuwa na furaha iliyo na asilimia 0%,20%,40% n.k lakini furaha ya kudumu katika maisha ya sasa inawezekana kama ukitambua msingi sahihi wa furaha yako, kubwa zaidi lazima uipende furaha yako na ujue wewe binafsi unahitaji furaha yako siku zote maana ni haki yako na Mungu anataka uwe na furaha wakati wote.

Wako watu wamejiwekea kuwa furaha sio maisha yao bali uja kwa kipindi fulani na kuondoka hivyo kutokuwa na furaha anaona ni jambo la kawaida kuona anastahili kutokuwa na furaha na wala ashangai yeye kutokuwa na furaha kwa kua ana amini kuwa furaha ni swala la kitambo tu.

Ni tatizo kubwa zaidi kwa mtu anaishi pasipo furaha kwani watu wa namna hii kuchukua maamuzi ambayo yata hatarisha maisha yake ni jambo la kawaida mathalani ujambazi, ukahaba, ukatiri na hata kujifikiria kujiua niseme mtu aliyekosa furaha uwa aogopi kujitoa mwanga na kuhatarisha maisha yake, ukifuatalia vizuri utakuta watu wengi wanafanya maamuzi magumu ya kuhatarisha maisha yao  na hata ya jamii husika ni watu walioumizwa au waliokosa furaha.

Ishara nzuri ya kuipenda furaha yako ni kuituza na kutotaka ipotee kwa haraka katika maisha yako kwani ndani ya furaha kuna ubora katika maamuzi husika yenye tija na manufaa katika jamii yako kwa ujumla kwakua ndani ya furaha ya kweli hakuna ubinafsi unaotawala ndani yake hivyo utafanya kuwa ni kitu cha Baraka na cha maana sana.

Niseme unahitaji kuwa na furaha katika maisha yako katika hali zote njema na sio njema katika muonekano wa macho ya nyama, lakini bado furaha yako inakuwa imetuzwa na Mungu mwenyewe kwa kuwa ndani yake kunatumaini lisilo na sababu linaibuka ndani yako lenye kuonyesha njia na ustawi usio na mashaka katika hazima yako iliyo njema.

Hatuhitaji furaha ili tufurahi tu bali tunahitaji furaha ili tuweze kufanya mambo katika hali iliyosahihi isiyo jaa kisilani wala chuki yeyote kwani nje ya furaha ya kweli kushindwa ni swala la kawaida.
Hakikisha furaha yako hauwiruhusu itoke katika maisha yako kwakua mwenye uwezo wa kuiruhusu furaha itoke ni wewe na kuimiliki ni wewe kwani iko chini ya himaya yako. Ni vizuri utambue kuwa furaha haipo kwa kitambo ipo katika maisha yako yote.

Wafilipi 4:4 Furahini katika Bwana sikuzote; tena nasema, Furahini.

Imeandaliwa na:
Cothey Nelson…………………………………………………0764 018535