Jumatano, 14 Januari 2015

VITA YA MAISHA

NAPENDA VITA;



Nikiwa najua wazi kuwa katika vita kuna kushinda na kushindwa lakini pamoja na hayo yote ni seme wazi napenda sana vita, kwakua ni vita pekee inaweza kunionyesha na kunifuza yale yote ambayo kwa namna ya kawaida ni singeweza kuyaelewa na hata kuyamudu lakini kupitia vita inanipa kujielewa sana, kupata ufahamu mwingine katika yale ambayo yananizunguka.

Najua kwa uhalisia kabisa kuwa vita ni mbaya kwani inaweza kuleta maafa makubwa sana katika jamii yetu….bila shaka utakuwa njia ya panda lakini sisemi vita ya kutumia vifaa vya moto kama vile bunduki mabomu la asha bali na zungumzia vita katika mapambano ya kimaisha ya kila siku na vilevile na zungumzia namna ya kukabili yale yanayotaka kukukabili pasipo kupepesa macho kwani ukipepesa macho ni wazi utatoa mwanya kwa Yule anaye kukabili kuona amekushinda.

Lakini niseme wazi kuwa vita hii ya maisha katika kupambana kutokana na mapungufu tuliyonayo wengine elimu wanatakusoma lakini uwezeshwaji unakuwa haupo, wengine wanataka kujenga kutokana na kero za nyumba za kupanga lakini uchumi bado ni changamoto nyingine, mwingine kampata mke au mme lakini vile alivyotazamia kumbe sivyo na hata vijana kukicha wako katika mausiano lakini bado kusalitiwa na kutendewa ndivyo sivyo katika ulimwengu wa kimapenzi nao umeshika kasi uwa watu hawaoni wapi kuna uwafadhali,

Katika vita hii wako watu wanaamua kujinyonga, kuachana na habari za kimausiano na wengine kuamua kuishi maisha wasiyoyataka laity wangekuwa na uwezo wangeomba wajengewe dunia ya kwao ili waishi huko pasipo buguza yoyote hile na wengi wao wanaishi kwakua amua kuwa na kinyongo katika moyo wao na wale walio tumiwa katika kufanyika kuwa jaka la moyo ndani yao.

Hautaji kuambiwa na mtu bali nikile kinachoendelea ndani yako kinachokuweka njia mbili za mkato kati ya kushoto au kulia yote yanabebwa na wewe na hivyo kusababisha kuwa ni vita kali pamoaja na mashindano yasiyoisha.

Pamoja na changamoto zote hizo katika vita unayokukabili bali tambua kuikabili ndio njia pekee katika kukufanikisha kwenda katika ustawi mwingine lakini tujiulize jambo moja je!inakabili vita katika maarifa yapi? Katika nguvu ipi? Na katika uimara upi? Mambo yote haya ni ya muhimu sana kwani katika hayo ndio uweza kukutambulisha pamoja na kukupa uhakika wa kushinda ua kushindwa.

Ni vizuri kutambua vita ipo kwakusudi lake hivyo wewe kulitambua kusudi la vita ni moja ya ufahamu wako kuweka katika njia ya ushindi pasipo udhihirisho katika ulimwengu wa macho yako, lazima utambue vita imebeba kusudi la Mungu na sio uonevu kama unaweza ukachukulia kirahisi tu.
Bali vyote vimebebwa na kusudi la Mungu haijalishi katika macho yako yamebeba makusudi gani lakini asili yake imebeba utukufu na ustawi wako usio elezeka wala usio beba tafsiri ilipata kibali kwa mwanadamu.

Na muhimu uwe mtu katika kujiandaa na vita wakati wote katika ufahamu wako na wala sio katika mazingira ya hofu bali katika mazingira yalibeba matumaini na uhakika pasipo kukata tama.

Ni ukweli ulio wazi sio wewe unayepigana bali ni Mungu mwenyewe anapigana wewe unawakilisha tu lakini vita haipigani kwa ajili ya kutaka kukumaliza bali ni kutakuua kile kilicho ndani yako ambacho kwa hicho kina kuwa ni tatizo katika utawala wao, ni seme wazi hautaji kuiogopa vita au kuikimbia kwakua kazi yako katika vita ni kufuata maelekezo tu na wala sio jambo jingine………….kwakua yeye MUNGU naujua mwisho wako kabla ya mwanzo kuanza!

Imeandaliwa na;

                        Cothey Nelson…………………………………..0764018535

Jumamosi, 3 Januari 2015

MWAKA MPYA NI DENI LAKO NA MUNGU




MWAKA MPYA;



Kila mtu ujisikia vizuri anapotoka hatua moja kwenda hatua nyingine inaweza kuwa kiuchumi, kielimu na mengine mengi, na wako watu ufurahia sana wanapoona siku nyingine katika mwaka mwingine.........kwakua ukianza kuhesabu tangu mwaka ulipoanza mpaka unaisha ua unaishia unaweza  kusema kuwa Mungu amenisaidia japo wako watu hawaoni tofauti ya mwaka mmoja na mwingine.

Lakini pamoja na hayo niseme kuwa tunapozungumzia mwaka mpya ziko maana mbalimbali kutoka kwa mtu mmoja na mwingine lakini mwisho tunamalizia kusema ni majira mengine na kipindi kingine chenye mambo ambayo hatuwezi kuyajua mambo yataendelea vilevile au yatabadilika.

Ni kawaida kwa watu ifikapo mwisho wa mwaka ziko kabila zingine uenda kujumuika kwa pamoja katika kupeana habari na mambo yanaendeleaje! Na watu wengine uenda katika nyumba za ibada au mahali popote ambapo kuna panakusanyiko la watu wanaomwabudu au watuwasiomwabudu Mungu mathalani disko na sehemu zingine za starehe.

Hivyo niseme hatuiti mwaka mpya kwa kubadilika namba tu na namna akili yetu inavyoelewa kuwa ni kipindi kingine tu bali tunaona mwaka mpya kama fursa amabayo Mungu ametupa kwa kusudi lake na itakuwa ya maana sana kama tukitambua na kuanza utekelezaji.lakini watu usherekea tu na kuishia kushukuru pasipo kujua hilo ni deni ambalo Mungu ametupa ili tuliweze kulilipa ni kama katika biblia Mungu kuwapa talanta moja kupewa mbili na mwingine kupewa tano,hakuna maana ya kuwa na hizo talanta halafu ukamrudishia kana kwamba ulimtuuzia tu.

Unahitaji kuona mwaka mwingine kwa macho mengine hii ni zaidi ya kula na kunywa na kufurahi pamoja na kushukuru kwa Mungu kwa kuwa amekupa jambo la wewe kulifanya tambua Mungu ni mfanyabiashara anayeitaji faida sio kutimiza utaratibu tu. Bali hali hii ni zaidi ya kusema asante kwa Mungu.....kwakua Mungu alijua kuwa utafika na sio kufika tu bali pia kuna kzi ambayo utaifanya itayofanya Mungu mwaka mwingine kwa furaha kwakua umeutendea haki wakati ambao Mungu amekupa.

Ukweli dunia ya sasa Mungu anajuta kwanini watu wengi amewapa wakati mwingine lakini vile wanavyotumia haoni faida ya kuwapa huko wengine wanafanya vitendo vya uhalifu, ubadhilifu na vitendo ambavyo jamii inazidi kupoteza nguvu kazi inakuwa siku ya maasi na sio siku ya tathmini yako na Mungu katika wakati wote ulioenda na Mungu.

Tumia mwaka vizuri kiasi kwamba yeye aliyekupa mwaka azidi kuona fahari ya wewe kukupa miaka yote kwa furaha akuone ni mtumwa mwema na sio awe anakupa kwa sababu apendi usiangukie mikono isiyo salama. Usifurahie mwaka mpya kwakua wengine wanafurahi tu bali furahia kwakua unaenda kuzidi kuikabili ile kazi njema ambayo Mungu amekuamini nayo au ambayo atakuamini nayo, ona ni mwaka wa kujenga ufalme wa Mungu ili watu waone uzuri wa Mungu na umuhimu wa Mungu katika maisha yao.


Imeandaliwa na;
    

                               Cothey Nelson...........................................................0764 018535 


TATIZO SIO MWAKA BALI NI WEWE KUTAMBUA NYAKATI.