Jumanne, 29 Septemba 2015

UNASIKIA NINI?



UNASIKIA NINI?



 “ kama wakisikia na kunitumikia, watapisha siku zao katika kufanikiwa na miaka yao katika furaha” Ayubu 36:11

Ikiwa neno la Mungu(biblia) limetoa kipaumbele sana katika kusikia kama chanzo cha ustawi na ubora wetu basi hakuna shaka jambo hili ni muhimu sana na linatakiwa lipewe nafasi ya kutosha sana ili tuweze kuona matunda yake.

Swali?
Unasikia nini? Na uko na nani? Na huyo ni nani? Yaani anajua nini? Na anafanya nini? Na anapenda nini? Na kwanini uko karibu yake? Na unapenda kitu gani kutoka kwake? Na unafikiri ni sahihi katika kutumia muda wako kuwa nae!

Utendaji wa mwanadamu moja inabebwa na kuchukuliwa katika kiasi kikubwa ni kusikia mtu awezi kuwa tofauti kama ajambiwa maneno ya tofauti na basi utakuwa wa kawaida kama tu ukiambiwa maneno ya kawaida na ukayapokea kuona wewe ni sehemu wa hayo maneno.

Kikawaida mtu upenda kusikia jambo ambalo masikio yake yatapenda kusikia na hatimae kuleta kuleta furaha katika moyo wake na jambo hilo hata liwe linamgharimu kiasi gani kama kipo kwenye uwezo wake basi hata tumia njia yeyote ili mradi tu aisikie hiyo habari.

Kusikia ni jambo zuri ila inategemea nini unasikia na kwa nani? Unasikia kwakua matokeo yake yanaweza kuwa makubwa hata ukashindwa kuelewa kwanini nilifanya vile au niliamua vile lakini kwa vile ulivyosikia na kuamini.

Naamini maamuzi yako katika kusikia yanategemea sana upeo wa ufahamu wako katika jambo hilo ikiwa huna upeo wowote kuhusu jambo hilo unakuwa na shauku ya kujua zaidi na utekelezaji wake pasipo kujua hili ni jambo sahihi kwa mimi kuwa katika kufikia hatua hii.

Ningependa ujue kuwa jambo lolote unalolisikia jua lina nafasi katika maisha yako kwa kadili kila siku unavyosikia na ndivyo inavyozidi kujijenga na kama nyumba kadili unavyojenga basi unaongeza hatua katika kukamilisha nyumba hiyo na utakavyoendelea basi hapana shaka kunakipindi utafikia lile hitimisho.

Watu wengi wamejikuta katika matatizo makubwa kutokana na kusikia sehemu (chanzo) kisicho sahihi na hatimae kujikuta katika mazingira magumu kama kufiwa, kuachwa na hata kuteseka maisha yake…. Ni kweli kama unataka kulinda afya yako basi hauna budi kuwa makini sana na kile unachokisia kwani kinaweza kukuongezea hofu au mashaka na hatimae kujikita kudumbukia katika shimo ambalo litaleta majuto katika maisha yako.

Watu wengi waliofanikiwa walikuwa wangalifu sana na jinsi walivyosikia katika kusikia kunakuwa na nguvu ya utendaji na hata walishundwa kufanikiwa walichangiwa sana na namna walivyosikia na hatua waliochukua.

Wako watu walikuwa watu wazuri sana lakini kutoka na kusikia kusiko na chanzo sahihi basi wamejikuta wakiuchukua maamuzi ambayo mwisho wamekuwa wakilia mathalani mwanafunzi alikuwa na tabia nzuri lakini baada ya kukutana na  marafiki zake wakampa habari isiyo sahihi nae akajikuta anadumbikia huko na hatimae anaishia kupata ukimwi au mimba. Pia wako watu walio kuwa wakifanya kazi pamoja lakini kutokana na ushirika na wenzake akajikuta kusikiliza sana na kuwaamini wenzake hatimae akajikuta anakosa kazi na wenzake wanaendelea na kazi.

Sio mbaya kusikia lakini nini unasikia ni muhimu sana na kwa nani unasikia nalo ni muhimu zaidi……. Kwakua tendo lolote unaloliamua linamchango katika maisha yako katika upande wa faida na upande wa hasara.

Unapomsikiliza mtu na kukuacha njia ya panda uwa nafasi ya kutengeneza hawezi kukusaidia zaidi sana anaweza kukuona wewe ni mjinga usio jitambua! Hivyo aibu inakuwa kwako na familia yako na yeye anakuwa na maisha yake.

Kuna watu wanashangaza sana unakuta mtu anashawishika na kukubaliana na kufanya jambo hilohilo na kuona madhara yake baadae unakuta tena amejikuta palapale…………mathalani mabinti unakuta kapata mimba ya kwanza kwa kudanganywa na baada ya muda kidogo unakuta ana mimba nyingine.

UPEO WA UFAHAMU ndio kinga tosha katika kukuepusha na jambo lolote unalo lisikia katika kulipa nafasi katika utendaji katika maisha yako.

Kama unajipenda sana basi haun budi kuongeza upeo wa kuyaelewa mambo katika fahamu zako ili uwe salama  na sio kuishia kuupendezesha mwili na kujikuta ukidumbukia katika mtego hulehule wa siku zote katika maisha yako.

UNAJIPENDEZA MWILI NA KUUTUNZA BASI HAKIKISHA PIA UFAHAMU WAKO UNAPENDEZA NA KUNG’AA KATIKA KUKUPA USHINDI KATIKA CHANGAMOTO ZINAZO KUKABILI.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson………………………………………………0764 018535

Jumatano, 23 Septemba 2015

UBABE WA KANUNI



KANUNI


 Unapoona mbegu inawekwa na kuchipua katika ardhi hapo wewe unajifunza nini? Na unapoona yai la kuku na baadae kutoa kifaranga na hapo unajifunza nini? Na pindi unapoona mchana unakuwa usiku je! Hapo unajifunza nini? Na pia unapoona bahari ikipungua maji na baadae yakiongezeka wewe hapo unaelewa nini?..............sina shaka kichwani mwako kuna majibu mengi ambayo hayana ushawishi wa ulimi katika kutamkwa kwakua hakuna uthibitisho wa masikio toka nje!

Kiufupi hapo nazungumzia KANUNI AU UTARATIBU AMBAO MUNGU AMEUWEKA DUNIANI na kamwe hakuna binadamu anaweza kutengua pasipo idhini yake yani kufanya tofauti na alivyoamuru yeye.

Unaweza ukachezea vitu vyote na bado ukawa salama au ukaweza kurekebisha lakini kamwe sio KANUNI na unaweza kuwadanganya watu maelfu lakini kamwe uwezi kudanganya kanuni au kufanya tofauti na kanuni na ukapata jibu lililo sahihi…………. hata hesabu ni muhimu uielewe KANUNI na kuifuata ndipo upate jibu lililo sahihi tofauti na hapo kosa hapo ni haki yako.

Katika dunia kila kitu kina kanuni yake ili uweze kukipata na kamwe uwezi kuchanganya kanuni na bado ukategemea kupata kile kilichosawa na kanuni hiyo, na kubaliana kabisa kwamba kuna kanuni za Mbingu na kuna kanuni za dunia japo kwa kiasi kikubwa yeye aliyeweka kanuni za Mbingu ndie aliye wapa wanadamu neema ya kuweka kanuni za duniani.

Kama ilivyo darasani watu wengi sana wanakosa hususa somo la hesabu kwasababu hawajui kanuni ndivyo watu wengi wanaangukia sehemu mbaya kutokana na sababu kuu mbili moja hawaijui kanuni au hawaifuati kanuni na pengine  hawajaielewa kanuni. Pia Kanuni inaweza kuwa ni moja lakini jibu likachelewa kupatika kutokana na wepesi wa ufahamu wa mtu.

Niseme tu unaweza kuwashawishi maelfu wawe upande wako lakini kamwe uwezi kuishawishi kanuni ikafuata upande wako tofauti na asili yake, ni ukweli utafanya lakini utakesha pasipo matunda yake au sawa na ile nguvu uliyoitumia.

Unaweza ukafanya jambo watu wote wakakufichia hilo jambo lisijulikane na mtu mwingine zaidi ya wale waliokuona au walio shiriki lakini kamwe hauwezi kuificha kanuni isifanye kazi yake mathalani unaweza ukafanya mapenzi na mtu na kwa bahati ukashika mimba(msichana) lakini utaki watu wajue kuwa ulishiriki ilo tendo na hivyo ukatumia kila njia ili isijulikane lakini mwisho kanuni ikichukua na nafasi na mtoto akaanza kuumbika ndani yako bila shaka kwa mtu mwenye akili nzuri ambaye hata waza mawazo ya kutoa mimba basi itajulikana tu kutokana na muonekano mpya wa mwili wako.

Niseme kama kuna mtu ambaye hana huruma kabisa basi huyo anaitwa KANUNI kwani yeye ajui huyu ni adui wala rafiki bali yeye ufanya sawa inavyotakiwa pasipo kuhofia kitu chochote na ukitaka kuabika nenda tofauti na kanuni alafu ujifiche katika nafasi uliyo nayo uone jinsi kanuni itakavyo kukuabisha  na kukuweka hadharani kila kitu pasipo kujali nani anakuheshimu au hakuheshimu.

Unapomwangalia mtumishi wa Mungu Daudi alipotembea na mke wa mtu alijaribu kuficha kila hali lakini kanuni haikumuacha ikamfichua na kumgharimu kwa kile alichokifanya pasipo kujali yeye alikuwa ni chaguo la Mungu au la wanadamu.

Ukitaka kuwa mtu unayeenda sawa na hali stahiki basi haunabudi kuipenda KANUNI na kuifuata katika ufahamu ulio sahihi, ukifanya kanuni kuwa ni rafiki yako bila shaka wengi watakufuata kwakua kanuni ikikuweka mahali fulani kamwe hakuna mtu atakaye kushusha.

HAKUNA ALIYE MBABE MBELE YA KANUNI
Imeandaliwa na:

Cothey Nelson……………………………………………………0764 018535

Jumatano, 16 Septemba 2015

HATUA YA MWISHO



HATUA YA MWISHO


 Mwisho wa safari ndicho chanzo sahihi kwa mtu kuwa na furaha au huzuni………..na zungumzia mwisho uliobeba hitimisho jema lenye matumaini mema, unapoangalia kule ulikotoka na kule unakoelekea ndipo panaweza kutoa hali yako ya furaha au huzuni. Na kuna mambo ambayo unaweza usijue huu ndio mwisho au ndio mwanzo………mathalani Samson alipoojitoa kwa ajili ya ndugu zake Israel ila kifo chake akikuwa na tafsiri sahihi katika ufahamu wa ndugu zake ila baada ya kifo basi tafsiri sahihi ikajitokeza baada ya kuona adui zao hawapo tena.

Ni nguvu na ni faraja ya pekee isiyoweza kufutika katika moyo wako katika majeraha na mateso katika maisha yako pindi unapoona au kufikia hitimisho lililobeba ndoto zako katika maisha ya ustawi wako.

Hitimisho nzuri ni kitu pekee kinachoweza kufuta macho yanayolia ndani moyo wa mtu na ni dawa inayotibu majeraha ya moyo wako. Na ni nguvu inayokupa fursa ya kuendelea mbele pasipo kuchoka………….!

Hiki ni kipindi ambacho afya ya mwili uweza kurejea katika maisha yako tena kwa kasi isiyo ya mfano na watu wengi kuanza kurejea tena kwako tena katika hali ya kuona umuhimu kwa namna nyingine isiyoelezeka………!

Katika hatua hii wako watu wanaweza kufanya jambo ambalo kwa hakika akuwai kufanya katika maisha yako au kuzidisha katika hali isiyo ya kawaida matahalani mtu anaweza kusema kwa furaha niliyokuwa nayo leo na amua kulala nje na haikuwa mzoea yake na wala sio kwa sababu nyingine bali kwa lile burudiko katika maisha ya mtu husika.

Uwa ni vizuri sana pindi unapoanza safari au jambo huku ukiwa na furaha lakini hiyo furaha italeta maana kwako na kwa wengine yaani jamii inayokuzunguka kama mwisho wako utakufanya uwe na furaha mara dufu yaani kuliko mwanzo lakini pindi mwisho utakuwa ni wa huzuni bila shaka wewe binafsi utaona kwanini ulikuwa na furaha mwanzo wa safari na hata watu wanokuzunguka hawataona kwanini wewe ulikuwa unacheka wakati mwisho wa safari umekuweka katika mazingira mabaya, …….jamii inaweza kuwa na maswali mengi lakini bila shaka wewe kwako yazidi kwakua kile ulichokitegemea hakikua sawa na ulivyotegemea.

Laiti tungekuwa tunajua mwisho kabla mwanzo basi mambo mengi tunayofanya kipindi cha mwanzo au cha awali tusingeyafanya kabisa au kuyapunguza.

Napenda kusema kuwa furaha ya maana sana ni mwisho uliobeba hatma njema katika maisha yako inayotoa mwanga na matumaini yaliyobeba usalama wa kesho yako. Siku zote watu wanapenda kuona taabu zao za leo zisiendelee kesho ndomana wanasema mchumia juani ulia kivulini wakiwa wana maana kabisa baada ya dhiki ni faraja!!

Hatua ya mwisho ni kipenzi cha watu wengi……..hata katika stori yoyote mtu anapobaini kuwa mwisho wa hiyo stori hauta furahisha moyo wake huwa hana haja ya kusikiliza hiyo stori kwakua haivutii kuendelea kusikiliza baada ya kubaini au kundua mwisho wa hiyo stori hauta ufurahisha moyo wake.

Unaweza kumkuta mtu anavumilia katika mazingira hatari au magumu na hata kushindwa kujua kwanini mtu anajisumbua kwanini asiache tu akafanya mambo yenye maana kubwa lakini pamoja na wewe kuona hivyo utakuta mtu bado anaendelea na uwa anaongeza bidii sana pindi anapoona kuwa mwisho wa jambo lake au safari yake utakuwa ni matumaini au mwanzo mzuri wa watu wengine.

Hatua ya mwisho ni jambo zuri sana kwani linakuwa ni hitimisho la mwendo mzima wa maisha yako na ndio kitu pekee kinachoweza kufuta maumivu yote ya nyuma na kukupa mwanga mwingine katika maisha yako…………niseme wazi kama kunakitu ambacho kitakufuta machozi na simanzi katika yote uliyopita ni kuona mwisho wenye ushuhuda au uliobeba ustawi uliojitosheleza katika ubora na uzuri.

Imeandaliwa na;

Cothey Nelson…………………………………………………………………..0764 018535