Jumamosi, 6 Aprili 2019

LIACHE KUSUDI LIVUTE MAMBO YAKE:



Ni jambo la fahari kwa mtu pindi anapofanya jambo akatambua kwanini anafanya hivyo au jambo hilo! Na litakuwa ni jambo la kushangaza kwa mtu awe anatia bidii sana na uku asijue kwanini anafanya hivyo.

Ni ukweli usiopingika pindi utakapoamua kulitumikia kusudi basi haki inayoambatana na hilo kusudi udhihirika au uweza kulipata.

Na ni jambo linakuwa gumu pindi utakapoanza kulitumikia kusudi uku ukiwa na matarajio yako ambayo ayaletwi na kusudi mathalani mtu unaweza ukajikuta katika shughuli za uvuvi lakini itakuwa ngumu kama moja ya kusudi lako ni kuvua swala mkubwa badala ya samaki.

Unapolitumikia kusudi uku akili yako ina mtazamo wako mbali na kusudi lilivyo ni ngumu kudumu na hilo kusudi au kuendelea na kusudi mathalani utakuta mtu anajitoa sana katika shughuli fulani akitegemea labda atapata pesa lakini pindi inapokuwa kinyume na matarajio utoshangaa kesho katoa udhuru wa kutoendelea na shughuli hiyo.

Biblia inasema “ hakuna aendaye vitani kwa gharama zake mwenyewe “.
1 Wakorintho 9:7 Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi?

Kusudi lenyewe linajua linahitaji nini ili liweze kudhihirika kwa hiyo ni muhimu ulitambue hilo na utoe nafasi lenyewe liite yaliyo yake sio swala la utendaji wa akili yako usio na uvuvio wake.
Ni muhimu kutambua kusudi lenyewe linaona kuliko macho ya nyama yanayoona, linajua chimbuko lake na hatima yake.

Uwezi kuchoka kama ukikubaliana na kusudi katika yale unayoyataka, kwa maana lenyewe kusudi linajua uhitaji wake.

Usipende kuishi katika maslahi yako pindi unapolitumikia kusudi bali ishi kwa matakwa ya kusudi bila shaka lenyewe litakutunza kukuimarisha maana ndilo matokeo au makusudi yake pindi utakapoamua kuishi katika hilo.

Kama unahitaji kuona fahari na ustawi wa familia na ukoo pamoja na watoto bila kusahau na wajukuu wako basi hunabudi kulitumikia kusudi ambalo Mungu ameliweka ndani yako.
Uzuri wa kusudi “ ukilitumikia nalo litakutumikia ila ukiliacha litakubwaga mazima “!

Nje ya kusudi uwezi kuona fahari ya wewe kuwepo duniani, kitu pekee ambacho kilicho mshawishi Mungu akuruhusu uje duniani ni kwa sababu ya hilo kusudi mbali na hilo hakuna kitu kingine.

Usiwe mjuaji sana katika kusudi maana utalitumia kwa namna yako ( kulitaka likutumikie baada ya wewe kulitumikia ) kwakuwa lenyewe lilivyoachiliwa linamaelekezo yote bali wewe kuwa mnyenyekevu na umakini wa kulisikiliza hapo utakua salama.

“ kuyapenda maisha yako ni kulipenda kusudi lililowekwa ndani yako “

INAITWA SIKU! BARIKIWA.

Imeandaliwa na:

Cothey  Nelson…………………………………………….0764 018535